Na Lydia Churi- Mwanza
Mahakama ya Tanzania inakusudia
kuongeza idadi ya Majaji katika kanda yake ya Mwanza ili kuongeza
msukumo wa kumaliza kesi za mauaji kutokana na kanda hiyo kuongoza kwa
kuwa na kesi nyingi za mauaji nchi nzima.
Akizungumza wakati wa ziara yake
ya kukagua shughuli za kimahakama katika kanda ya Mwanza, Jaji Mkuu wa
Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amesema ataongeza idadi ya
majaji katika kanda hiyo ili kesi hizo za mauaji zimalizike kwa wakati.
Jaji Mkuu pia ameiagiza Mahakama
Kuu kanda ya Mwanza kuzipa msukumo maalum kesi za mauaji ili kuhakikisha
zinamalizika mapema na kupunguza mlundikano wa kesi katika mahakama za
Tanzania.
Awali akisoma taaarifa ya hali
halisi ya kesi katika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza, Jaji Mfawidhi wa
kanda hiyo Mheshimiwa Robert Makaramba alisema kanda ya Mwanza ndiyo
inayoongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji nchini ambapo hadi kufikia
Aprili mwaka huu kuna jumla ya kesi 512 za mauaji.
Pamoja na mkakati wa Jaji Mkuu
kuongeza idadi ya Majaji ili kumaliza kesi hizo, Jaji Mfawidhi wa kanda
ya Mwanza alisema wameshachambua kesi hizo za mauaji ambapo Jaji
Kiongozi pia aliahidi kuwaongezea jumla ya Majaji 11 ili waweze kusaidia
kusukuma kesi hizo.
Jaji Makaramba alisema kati ya
mwezi Juni na Julai jumla ya vikao 11 vinatarajiwa kukaa ili kusikiliza
kesi 123 zilizopangwa kusikilizwa. Alisema kati ya kesi hizo, 35 ni zile
zitakazosikilizwa kwa mara ya kwanza na kesi 88 ni zile
zitakazosikilizwa mpaka mwisho.
Alisema endapo vikao hivyo vitafanyika kama ilivyokusudiwa vitasaidia kupunguza kesi zilizopo mahakamani kwa miaka mingi.
Hadi kufikia mwezi April mwaka
huu, Mahakama Kuu kanda ya Mwanza ina jumla ya kesi 2771 za aina zote
zikiwemo zile za Madai ya kawaida, Madai ya Ardhi na za jinai. Ili
kuongeza kasi ya usikilizwaji wa kesi hizo, kila Jaji amepangiwa
kusikiliza kesi 346. Kanda hiyo ina Majaji nane (8).
Jaji Mkuu wa Tanzania ameanza
ziara katika kanda ya Mwanza inayohusisha mikoa ya Geita, Mwanza na Mara
ambapo atakagua shughuli mbalimbali za kimahakama katika kanda hiyo.
Zawadi Azania Bank Kids Run zatajwa
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la Riadhaa Tanzania (RT), Tullo Chambo
akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mbio maalum za watoto zijulikanazo Azania Bank Kids Runzitakazofanyika juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini. Kushoto ni Ofisa MasokoMwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea na kulia ni mratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday. (Na Mpiga Picha Wetu)
akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mbio maalum za watoto zijulikanazo Azania Bank Kids Runzitakazofanyika juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini. Kushoto ni Ofisa MasokoMwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea na kulia ni mratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday. (Na Mpiga Picha Wetu)
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
kuhusu mbio maalum za watoto zijulikanazo Azania Bank Kids Run
zitakazofanyika juni 5 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho la Riadhaa Tanzania (RT), Tullo Chambo.
………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
WADHAMINI wakuu wa Mbio za Watoto za Azania Bank Kids Run 2016, Benki ya
Azania, wametangaza zawadi za washindi wa mbio hizo zitakazofanyika viwanja vya
Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, Juni 5.
Azania, wametangaza zawadi za washindi wa mbio hizo zitakazofanyika viwanja vya
Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, Juni 5.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea,
alisema benki yake inajisikia fahari kuwekeza katika mbio hizo za watoto.
Michezo la Taifa (BMT), Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea,
alisema benki yake inajisikia fahari kuwekeza katika mbio hizo za watoto.
Alizitaja zawadi za mbio za kilomita 5 kuwa ni Sh. 200,000 kwa mshindi wa
kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa tatu,
wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na vya michezo.
kwanza, Sh. 150,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 100,000 kwa mshindi wa tatu,
wote wakitarajiwa pia kupata medali, begi lenye vifaa vya shule na vya michezo.
Jibrea alibainisha kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za Kilomita 2
atajinyakulia Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh.
50,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.
atajinyakulia Sh. 100,000, mshindi wa pili Sh. 75,000 na mshindi wa tatu Sh.
50,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo.
Katika mbio za Kilomita 1, Jibrea alitaja zawadi za washindi kuwa ni Sh.
75,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000 kwa
mshindi wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa vya
shule na michezo.
75,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 50,000 kwa mshindi wa pili na Sh. 40,000 kwa
mshindi wa tatu, ambao watapata zawadi ya ziada ya medali, begi lenye vifaa vya
shule na michezo.
“Pia washindi wa nne hadi wa 10 wa mbio hizo, watapata kifuta jasho cha Sh.
15,000, begi lenye vifaa vya shule na michezo. Nia ni kuwafanya watoto
watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano, na zawadi zote za fedha
taslimu tutawawekea kwenye akaunti tutakazowafungulia katika Benki ya Azania,”
alisema Jibrea.
15,000, begi lenye vifaa vya shule na michezo. Nia ni kuwafanya watoto
watakaoshiriki kutotoka bure mwishoni mwa mashindano, na zawadi zote za fedha
taslimu tutawawekea kwenye akaunti tutakazowafungulia katika Benki ya Azania,”
alisema Jibrea.
Ofisa huyo alifichua kilichowasukuma Azania Bank kudhamini mbio hizo kuwa
ni kurejesha sehemu ya pato lake kwa jamii, lakini pia kuwa sehemu ya
kuiwezesha jamii kujenga kizazi imara kinachoshiriki michezo kwa ustawi wa
taifa.
ni kurejesha sehemu ya pato lake kwa jamii, lakini pia kuwa sehemu ya
kuiwezesha jamii kujenga kizazi imara kinachoshiriki michezo kwa ustawi wa
taifa.
Kwa upande wake Mratibu wa Azania Bank Kids Run 2016, Wilhelm Gidabuday,
aliishukuru Azania Bank kwa kukubali kusapoti mbio hizo, na kuongeza kwamba kwa
kuwa msingi wa michezo yote ni mbio, basi anaamini Azania imewekeza mahali
sahihi.
aliishukuru Azania Bank kwa kukubali kusapoti mbio hizo, na kuongeza kwamba kwa
kuwa msingi wa michezo yote ni mbio, basi anaamini Azania imewekeza mahali
sahihi.
“Hakuna mchezo duniani usiohusisha mazoezi ya kukimbia ama usiohitaji
mshiriki kuwa na mbio, iwe soka, ngumi, tenisi, nk. Ndiyo kusema Azania
imefanya uamuzi sahihi na tunawaomba wazazi na walezi wawasajili watoto wao kwa
ada ya Sh. 2,000,” alisema.
mshiriki kuwa na mbio, iwe soka, ngumi, tenisi, nk. Ndiyo kusema Azania
imefanya uamuzi sahihi na tunawaomba wazazi na walezi wawasajili watoto wao kwa
ada ya Sh. 2,000,” alisema.
Alibainisha kuwa fomu za ushiriki zinapatikana katika matawi ya Azania Bank
popote jijini Dar es Salaam, ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),
pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji.
popote jijini Dar es Salaam, ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT),
pamoja na Ofisi za BMT zilizoko Samora Avenue katikati ya jiji.
TBL GROUP YALIPA KODI SHILINGI BILIONI 81
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin akisisitiza jambo kwa waandishi wa
habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni
hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya mwaka
huu,mkutano huo ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Ilala jijini
Dar es Salaam leo Mei 26,2016.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin akisisitiza jambo kwa waandishi wa
habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni
hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya mwaka
huu,mkutano huo ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Ilala jijini
Dar es Salaam leo Mei 26,2016.
Mwandishi
wa gazeti la The East Africa Kidanka Christopher akiuliza swali kwa
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin (hayupo pichani) kuhusiana
na uzalishaji wa pombe za asili , wakati wa mkutano na wandishi wa
habari wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi
cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya mwaka huu,mkutano huo
ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo
Mei 26,2016. \
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria katika
mkutano wa TBL Group , wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni
hiyo wakimsikiza kwa makini, Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto
Jarrin (hayupo pichni) wakati wa mkutano huo ulifanyika makao makuu ya
kampuni hiyo Ilala jijini Dar es Salaam, leo Mei 26 2016.\
Mtalamu
wa upishi wa vinywaji wa TBL Group (Techincal Brewer) Emanuel Sawa
akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya bia aina ya Castle Luger, jinsi
inavyozalishwa wakati walipotembelea kiwanda hicho mara baada ya
kumalizika kwa mkutano wa tathmini na waandishi hao
……………………………………………………………………………………………..
Kampuni ya TBL Group imelipa kodi ya mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 81 katika kipindi cha mwaka 2015.
Akitoa taarifa ya tathmini ya
utendaji wa kampuni ya mwaka uliopita kwa waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam leo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin pia
amebainisha kuwa mbali na kampuni kulipa kiasi hicho cha kodi pia
imekusanya kodi za serikali kiasi cha shilingi bilioni165 ikiwa ni kodi
ya mlaji (exercise duty) ,bilioni 114 ikiwa ni kodi ya ongezeko la
thamani (VAT) na bilioni 24 ikiwa ni malipo ya kodi nyinginezo ikiwemo
kodi ya PAYE.
TBL Group ni kampuni inayoongoza
kulipa kodi nchini ikiwa imechagia pato la serikali kwa njia ya kodi
kiasi cha shilingi Trilioni 2.3 katika kipindi cha miaka 10 “Kampuni
yetu imechangia maendeleo ya taifa kwa njia ya kukusanya na kulipa kodi
na mchango huo umekuwa ukitambuliwa na taasisi mbalimbali na kuitunukia
tuzo ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo imeitunukia tuzo
ya Mlipa kodi bora nchini kwa kipindi cha miaka mine mfululizo”.Alisema Jarrin.
TBL Group inajumuisha makampuni
ya- Tanzania Breweries Limited (TBL), Tanzania Distilleries Limited
(TDL) na Dar Brew Limited.Biashara kuu ya kampuni ni kuzalisha na
kuuza vinywaji ikiwemo bia za aina mbalimbali,vinywaji vikali na
vinywaji vya asili..
Jarrin alibainisha hayo wakati
akitoa ripoti ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha mwaka 2015 na
mikakati yake ya mbele katika kipindi cha mwaka 2016/17 kwa waandishi wa
habari “TBL Group itaendelea kuunga jitihada za serikali zakukuza
sekta ya viwanda nchini kwa kuendelea kujenga viwanda nchini na tangu
kampuni hiyo ibinafsishwe mwaka 1994,imekuwa ikiendelea kuwekeza na
tayari imewekeza Zaidi ya shilingi bilioni 150 kwa ajili ya kujenga
viwanda vilivyokuwepo awali uwa vya kisasa Zaidi kuendana a teknolojia
ya kisasa”
Kampuni inavyo viwanda 10 nchini
na miongoni wa viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na
Dar es Salaam vimetunukiwa tuzo mfululizo za kuwa viwanda bora katika
viwanda vinavyomilikiwa a kampuni mama ya SABMiller katika bara la
Afrika.TBL Mwanza na Mbeya vikiwa katika kundi la viwanda 10 na 15 kwa
ubora duniani.
Jarrin alisema biashara ya bia za kampuni ya TBL zinatawala soko kwa asilimia 78 nchini ikiwa inaongozwa na aina za bia za Safari, Kilimanjaro, Ndovu, Castle lager na Castle Lite .Pia kampuni inatengeneza mvinyo na vinywaji vikali maarufu vinavyotamba kwenye soko kwa asilimia 73 ambavyo ni – Konyagi, Valuer and Dodoma Wine – Kwa upande wa vinywaji vya asili vinywaji vyake vinatawala soko kwa asilimia 8 ambavyo ni – Chibuku and Nzagamba
– Utafiti uliofanywa na taasisi ya CanBack kuhusiana na matumizi ya
pombe za asili nchini umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili nchini
ni asilimia 50%
Jarrin aliendelea kueleza kuwa
TBL Group inaendelea kutoa mchango wa kukuza uchumi wa taifa kupitia
katika sekta ya uuzaji vinywaji ambayo imetoa ajira zaidi ya milioni 2
za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zinazoendelea kuwanufaisha
watanzania wa kada mbalimbali.Kwa upande wa sekta ya kilimo wakulima wa
zao la Shahiri Zaidi ya 3000 wamenufaika kupitia mpango wa kushirikiana
na kampuni.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha ongezeko
la uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka
lengo la matumizi na mahitaji ya kampuni.
Pia imebainishwa kuwa zaidi ya
wakulima 700 wananufaika na mpango wa kiwanda cha TDL wa kushirikiana
nao atika kilimo cha zabibu kinachoendeshwa katika vijiji vya Bihawana,
Mpunguzi,, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na
Mbalawala .Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu
wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture Training
and Research Center (MVTRC). Pia chini ya mpango huu watoto wa wakulima
wa zao la zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia mfuko
unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza.
Jarrin pia alibainisha kuwa
kampuni ya DarBrew imeweza kuleta mapinduzi ya uuzaji wa pombe za asili
nchini kwa kuwawezesha watumiaji kupata kinywaji cha Chibuku na Nzagamba
kikiwa kimefungwa kwa viwango mbalimbali na katika mazingira ya usafi
yanayolinda afya za watumiaji na hivi sasa imekuja na mkakati wa
kuwainua akina mama kimapato kupitia kuuza bidhaa zake unaojulikana kama
Chibuku Mamas ambao hadi kufikia sasa wanawake wapatao 130
wameishajiunga na mpango huu.
Kuhusu mtazamo wake wa hali ya
biashara ya kampuni kwa sasa Jarrin alisema sekta ya uuzaji wa vinywaji
inakabiliwa na changamoto mbalimbali mojawapo ni bei kubwa ya bia ambayo
watumiaji wake wengi wanashindwa kuimudu,kuwepo na vinywaji visivyo
katika mfumo rasmi wa ushindani katika soko,kukosekana kwa motisha
katika uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vinywaji nchini kwa kuwa
zinatozwa kodi kubwa ya zuio kuliko malighafi zinazotolewa nje ya nchi.
Alisema baadhi ya mambo
yanayostahili kufanyika katika uboreshaji wa sekta ili iendelee
kuchangia pato la taifa ni kupunguza kodi za malighafi zinazozalishwa
nchini kama kimea kinachotumika kutengeneza bia pia kulasimisha pombe za
asili ziende sambamba na vinywaji vya sili vinavyolipiwa kodi na
kuhakikisha vinywaji vya asili vinapatikana katika mazingira ya usafi “Pamoja
na changamoto nyingi zilizopo katika sekta hii tunaendelea kukabiliana
nazo na tumedhihirisha uwezo wetu kwa kuwa na viwanda vyenye ubora wa
hali ya juu nchini Tanzania”Alisema Jarrin
MISS TANZANIA USA AEESHA KAMARA ATEMBELEA HIGHLAND NURSERY SCHOOL, TABATA, JIJINI DAR
Miss
Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akigawa penseli, vikiwemo vitabu,
mabegi ya kubebea vitabu na vitu vingine mahitaji ya shule hiyo ya
vidudu ya Highland Nursery school iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam.
Vitu hivyo vilitolewa msaada na wadau kutoka Washington, DC.
Miss
Tanzania USA Pageant, Aeesha Kamara akigawa mabegi ya kubebea vitabu kwa
watoto wa Highland Nursery School ya Tabata jijini Dar es Salaam,
Miss Tanzania USA Pageant akiongea na watoto hao wa shule ya Highland Nursery School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Highalnd Nursery school wakiwemo walimu wao.
Watoto wakimsikiliza Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara (hayupo pichani) alipokua akiongea nao.
Watoto wakitega sikio kwa makini kumsikiliza Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara (hatyupo pichani) alipokua akiongea nao,
MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA MWANAHABARI MAKONGORO OGING’ KUZIKWA MKOANI MARA KESHO KUTWA.
Picha ya Mwanahabari Makongoro Oging’ enzi za uwai wake.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers alikokuwa akifanyia kazi
Makongoro Oging’, Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza
lenye lenye mwili wa marehemu Oging’ wakati wa kuagwa katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana Dar es Salaam mchana wa leo.
Mmiliki wa Blog ya Michuzi, Issa Michuzi akitoa heshima za kwa mwili wa marehemu.
Mhariri wa Habari wa Gazeti la Champion, Salehe Ali akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.
Waombolezaji wakiwa na huzuni wakati wa kuaga mwili wa mpendwa wao Makongoro.
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV. Samu Mahela akitoa heshima za mwisho.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF), Absalom Kibanda akiwa
kwenye shughuli hiyo ya kumuaga Makongoro Oging’
Ndugu yake na Makongoro Oging’ akilia wakati wa kumuaga mpendwa wake Makongoro.
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye uagaji wa mpendwa wao.
Uagaji ukiendelea.
Mtoto wa marehemu akimuaga baba yake ‘hakika ni huzuni kubwa’
Majane wa marehemu akiwa hajiwezi baada ya kumuaga mume wake.
Mhariri
wa habari wa gazeti la Uwazi alilokuwa akiandia marehemu Oging’ Elvan
Stambuli akilia kwa uchungu wakati wa kumuaga Makongoro.
Baba mlezi wa Makongoro Oging ambaye alimsomesha, akizungumza na wanahabari.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Makongoro kulipeleka kwenye gari kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda mkoani Mara. |
Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari.
Temeke yapiga marufuku ufanyaji wa mazoezi barabara kuu
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Halmashauri ya Manispaa ya
Temeke imepiga marufuku vikundi vya mazoezi vinavyofanya mazoezi
kwenye barabara kuu ya uwanja wa Taifa ili kuzuia foleni na ajali
za barabarani.
Tamko hilo limetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Afisa Habari wa Halmashauri hiyo, Joyce Msumba alipokua
akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu foleni ya magari
inayosababishwa na wachezaji wanaotumia barabara kuu ya Temeke kuelekea
uwanja wa Taifa.
“Halmashauri yetu imepiga
marufuku wachezaji wote wanaokimbia kuelekea uwanja wa Taifa kupitia
barabara kuu na badala yake wanatakiwa kutumia njia za waendao kwa miguu
(service road) zilizopo pembezoni mwa barabara kuu”,alisema Joyce.
Joyce aliongeza kuwa kila kundi
la wachezaji wana viongozi wao ambao walishapewa maelekezo na
Halmashauri juu ya suala hilo kwahiyo,viongozi hao wana wajibu wa
kuwasimamia wanamichezo wao.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni
wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Ndumukwa amewaomba wanamichezo hao
kuzingatia sheria za barabarani ili kuepusha ajali.
“Mara nyingi tunawaeleza
wanamichezo wazingatie sana sheria za barabarani pamoja na kutumia
bendera nyekundu kama alama ya kuashiria uwepo wao katika barabara ili
kuzuia ajali”,alisema Ndumukwa.
Makandarasi 4572 wafutiwa leseni nchini
Bodi
ya Usajili wa Makandarasi imefuta usajili wa jumla ya makandarasi 4572
kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Sheria ya Usajili wa Makandarasi ya
mwaka 1997.
Hayo yamebainishwa na Kaimu
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Bw. Rhoben Nkhori
wakati wa Mkutano wa Mashauriano wa CRB uliofanyika jijini Dar es Salaam
na kufunguliwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Bw. Nkhori amesema kuwa katika
jukumu la kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi, Bodi ilikagua miradi
2735. Katika miradi hiyo iliyokaguliwa, miradi 1873 sawa na asilimia
68.5 haikuwa na kasoro.
Ameongeza kuwa miradi mingine
ilikuwa na kasoro za kutofanywa na makandarasi waliosajiliwa,
kutozingatia usalama wa wafanyakazi, kutokuwa na bango wala uzio na
miradi kutosajiliwa. Kwa mujibu wa Bw. Nkhori miradi yote iliyopatikana
na upungufu wahusika walichukuliwa hatua mbali mbali kwa mujibu wa
sheria.
Aidha, Bwana Nkhori amesema kuwa
kwa mwaka jana, Bodi ilisajili miradi 3,172 yenye thamani ya shilingi
trilioni4.23. Katika miradi hii asilimia 44.4 ilifanywa na Makandarasi
wazawa na asilimia 55.6 ilifanywa na makandarasi wa kigeni.
Licha ya mafanikio hayo CRD
ilikumbana changamoto kadhaa ikiwemo kuwasilisha nyaraka za kugushi
wakati wa usajili hususani kadi za magari na mitambo, vyeti vya
wataalam, kutumia majina ya makandarasi kwa udanganyifu kwa kuuza vibao,
waendelezaji kutotoa taarifa sahihi za umiliki kwa Bodi na baadhi ya
makandarasi kushindwa kuwalipa wafanyakazi na vifaa vya ujenzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Bi Consolata Ngimbwa amemwomba Mhe. Rais
John Pombe Magufuli kuwapa kipaumbele Makandarasi wa humu nchini ili
kuwawezesha kiuchumi. “Mhe. Rais tunaomba utupe kipaumbele kwani sisi
tukipata hiyo miradi tutawekeza hapa nchi na kuongeza soko la
ajira,”alisema Bi Ngimbwa.
Katika hotuba yake ya ufunguzi,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
amesema serikali yake itawapa kipaumbele makandarasi wazawa lakini
akawataka wajipange na kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili
ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Mkutano huu pamoja na mamabo
mengine utajadili jinsi ya kuwajengea uwezo makandarasi nchini. Kauli
mbiu ya Mkutano huo ni “Juhudi za Makusudi za kukuza uwezo wa
makandarasi wazawa, changamoto na mustakhabali.”
Dawati la malalamiko kufanya kazi masaa 24 hospitali ya Mwananyamala.
Katibu
Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi katikati akiongea na waandishi wa habari
hawapo pichani katika hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50
kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika
hospitali ya Mwananyamala wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
Bw. Ally Hapi na wa kwanza kushoto ni katibu Tawala wa Mkoa Bi.
Theresia Mbando.
Katibu
Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi katikati akiongozana na Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni Bw. Ally Hapi na wa kwanza kulia na wa kwanza kushoto ni
katibu Tawala wa Mkoa Bi. Theresia Mbando kuelekea wodini kusalimia
wagonjwa wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka
kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika katika hospitali ya
Mwananyamala .
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi wa kwanza kushoto akimsikiliza
mmoja wa wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali ya Mwananyamala akitoa
kero zake kuhusu hospitali hiyo wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada
wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya pentekoste iliyofanyika
katika hospitalini hapo.
Wananchi
wakitoa malalamiko yao kuhusu huduma zinzotolewa Hospitali ya
Mwananyamala mbele ya Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi na Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi hawapo pichani wakati wa hafla fupi ya
kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya
pentekoste iliyofanyika katika hospitalini hapo.
Wananchi
wakitoa malalamiko yao kuhusu huduma zinzotolewa Hospitali ya
Mwananyamala mbele ya Katibu Mkuu kiongozi Dkt. John Kijazi na Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Bw. Ally Hapi hawapo pichani wakati wa hafla fupi ya
kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka kwa Umoja wa Makanisa ya
pentekoste iliyofanyika katika hospitalini hapo.
Baadhi ya magodoro yaliyopokelewa hospitalini hapo.
……………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-maelezo
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. John
Kijazi ameutaka uongozi wa hospitali ya Mwananyamala kuhakikisha kuwa
dawati la malalamiko kwa wagonjwa linafanya kazi masaa 24 ili kuboresha
huduma katika hospitali hiyo.
Akizungumza katika hafla ya
kupokea msaada wa magodoro Dkt. Kijazi amesema kuwa wagonjwa wanatakiwa
kuhudumiwa kwa wakati na kusikilizwa malalamiko yao muda wote
wanapopatwa na changamoto hospitalini hapo ili kuweza kuboresha huduma
kwa watanzania.
“Nimepata malalamiko kutoka kwa
wananchi ambao walipata matatizo usiku wa kuamkia leo na hakukuwa na mtu
wa kuwasikiliza kwa wakati na kushindwa kupata huduma bora walipokuwa
na shida hivyo naagiza uongozi kuhakikisha dawati la malalamiko kufanya
kazi masaa 24 ili kuondoa kero za Wagonjwa wote”.alisema Dkt Kijazi.
Aidha Dkt. Kijazi ameushukuru
uongozi wa Umoja wa Makanisa ya Pentekoste kwa kutoa msaada wa magodoro
50 yenye thamani ya shilingi milioni 1.631 ili kuendeleza huduma bora
kwa wagonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Akipokea msaada huo Dkt. Kijazi
alisema kuwa anawaomba viongozi wa Umoja huo na taasisi zingineziendelee
na moyo wa kuchangia kwenye shughuli za kijamii kadriwanavyoweza ili
kuifikisha Tanzania salama katika kilele cha mafanikio.
“Nawaomba Umoja wenu, taasisi na
wadhamini mbalimbali kuweza kusaidia kuinua na kukuza huduma bora za
kijamii ikiwemo mahospitalini ili kusaidia serikali kupiga hatua katika
kupambana na changamoto ya vifaa zinazoikabili hospitali ya
Mwananyamala” aliongeza Dkt. Kijazi.
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya
Kinondoni Bw. Ally Hapi amesema kuwa ana Imani na Serikali ya awamu ya
tano katika kutatua kero za wananchi hususani katika Wilaya yake kwani
ameshaona mfano wa kupokea msaada huo na kuungwa mkono na Katibu Mkuu
Dkt. John Kijazi kwa kushirikiana vizuri kwenye shughuli hiyo.
“Nafurahi kukutana na
kushirikiana kwa pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi katika shughuli za
kijamii hususani katika hili la kuendeleza huduma bora zitolewazo na
hospitali ya Mwananyamala ili kuifikisha mbali Tanzania mpya” alisema
Bw. Hapi.
TIGO YAMDHAMINI MWANAMUZIKI BEN POL KUBURUDISHA TAMASHA LA NYAMA CHOMA
Mkuu
wa Kitengo cha Burudani na Digitali wa Tigo, Paulina Shao (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
kuhusu tamasha la nyama choma litakalofanyika Viwanja
vya Leaders kesho kutwa Jumamosi Mei 28, 2016 jijini Dar es Salaam,
ambapo mwanamuziki Ben Pol atatoa burudani kwa udhamini wa kampuni ya
Tigo. Kulia ni Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Carol Ndosi na katikati ni
mwanamuziki Ben Pol.
Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Carol Ndosi (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mwanamuziki, Ben Pol (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Mtaalamu wa Kidigitali, Samira Baamar (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
Kampuni
inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imekubali
kumdhamini mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo za muziki, Bernard
Michael Paul Mnyang’anga, maarufu kama ‘Ben Pol’ kuburudisha katika
tamasha la mwaka huu la Nyama Choma.
Tamasha
hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa tano sasa ni moja ya tamasha
maarufu linalovutia watu wengi kutoka maeneo yote ya Dar es Salaam
litafanyika kwenye viwanja vya Leaders Jumamosi Mei 28, 2016.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Tigo wa masuala ya
Dijitali Paulina Shao alisema kuwa kumuunga mkono Ben Pol kunaonesha
kuendelea kujikita kwa Tigo katika kuwekeza katika kusaidia sekta ya
muziki ya ndani kwa kuhakikisha wasanii wanawezeshwa kufikia viwango
vya juu katika kazi zao.
“Kama
kampuni ya maisha ya kidijitali, Tigo inatambua mchango muhimu wa
wasanii wa Tanzania wanaoutoa katika sekta ya burudani.
Hii
ndio maana tumewekeza kwa kiwango kikubwa kuwasaidia wasanii hususani
wanamuziki wa ndani katika kuhakikisha wanafahamika katika masoko
ndani ya nchi, kikanda na kimataifa kwa kutumia majukwaa ya kidijitali
yanayokuwepo na kushiriki matukio mbalimbali na hivyo kuongeza mauzo
ya muziki wao pamoja na nembo zao,” alisema Shao.
Aidha
akiishukuru Tigo kwa uungwaji mkono huo, Ben Pol aliisifu Tigo kwa
juhudi inazofanya bila kuchoka katika kukuza ukuaji wa sekta ya
muziki wa ndani kupitia Jukwaa la Muziki la Tigo.
“Ninaishukuru
sana Tigo kwa uungwaji mkono ambao ni muendelezo wa mtiririko wa
programu ambazo imezianzisha ili kuinua maisha ya wasanii wachanga wa
Tanzania,” alisema Ben Pol na kutoa changamoto kwa wasanii wanaoibukia
kuwa wasione aibu kuomba msaada kutoka kwa mashirika kama Tigo.
Nguli huyo wa muziki wa Bongo Flava kwa hivi sasa anatamba na kibao ‘MoyoMashine’ ambayo aliitoka hivi karibuni.
Ben Pol
ni miongoni mwa wasanii wanaonufaika na jukwaa la Muziki la Tigo
ambalo lilianzishwa mwaka 2015 likiwa na lengo la kuiunga mkono sekta
ya muziki Tanzania kwa kuwasaidia wasanii wa ndani kupata kipato zaidi
kutokana na mauzo ya kazi zao na kuwawezesha kufahamika katika masoko
ya kimataifa kupitia majukwaa hayo ya kidijitali kama vile Music
portal na Deezer, ambayo ni majukwaa ya kimataifa yaliyo kwenye mtandao
yakiwa na nyimbo kutoka sehemu mbalimbali duniani zaidi ya milioni
36.
SERIKALI YAANDAA MPANGO KABAMBE WA MIPANGO MIJI (MASTER PLANS) ILI KUONDOA MIGOGORO YA ARDHI
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaandaa Mpango Kabambe wa Mipango Miji
(Master Plan) utakaoainisha matumizi bora ya ardhi na kuondoa migogoro
ya ardhi nchini.
Kauli hiyo ilitolewa jana Bungeni
Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. Angelina Mabula wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu mpango wa
Serikali kumaliza migogoro ya ardhi kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Mhe. Mabula alieleza kuwa Wizara
yake inashirikiana na Halmashauri za Wilaya na Miji 18 kwenye program
ya Urban Local Government Supporting Programme (ULGSP) katika kuandaa
Mipango Miji hiyo.
Pia Mhe. Mabula alibainisha kuwa
Wizara inaandaa na kukamilisha programu ya kupanga, kupima na
kumilikisha kila kipande cha ardhi Tanzania itakayotekelezwa kwa kipindi
cha miaka kumi kuanzia 2015 hadi 2025.
“Serikali imekuwa ikiziagiza
Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya upimaji kwa
kuwa inatambua umuhimu wa kupima viwanja na mashamba ili kuwa na
matumizi bora ya ardhi yetu” alisema Mabula.
Aidha, Mabula aliongeza kuwa
Serikali kupitia Mradi wa Benki ya Dunia ipo katika mchakato wa kununua
vifaa vya upimaji ambavyo vitasambazwa katika kanda 8 za Wizara ya Ardhi
ili Halmashauri zote zilizopo ndani ya kanda hizo ziweze kunufaika.
Alieleza kuwa makadirio ya awali
ya gharama za mradi huo ni Dola za Kimarekani Milioni 4 ambapo Dola
Milioni 2 zitatumika kwenye upimaji na Dola Milioni 2 zitatumika kwa
ajili ya ununuzi wa Vifaa.
Katika kupunguza na kutatua
migogoro ya ardhi iliyopo sasa, Mabula alisema kuwa Wizara ya Ardhi
imeandaa kitabu cha orodha ya migogoro nchi nzima kinachoainisha vyanzo
vya migogoro hiyo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Hali kadhalika, Mabula alisema
kuwa Wizara imesambaza Sera na Sheria za Ardhi hasa kwenye maeneo yenye
migogoro, wameimairisha mfumo wa kielektroniki katika kutunza
kumbukumbu, na kuboresha ofisi za Kanda ili kusogeza huduma za ardhi
karibu na wananchi.
44 WAMEBAKI KWENYE MCHUJO
Akizungumza na mbeyacityfc.com, mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya leo (Clinic day 5) kwenye uwanja wa Sokoine kocha msaidizi wa City, Mohamed Kijuso amesema kuwa Vijana 44 wamefanikiwa kuvuka kwenye mchujo wa kwanza hivyo wataingia kwenye wamu ya pili inayotaraji kuanza hapo kesho kwenye uwanja wa Sokoine.
“Tulikuwa na kundi kubwa la wachezaji zaidi ya 106, baada ya mchujo leo, tumefanikiwa kupata 44 ambao wataingia kwenye awamu ya pili hapo kesho, lengo letu ni kuona tunapata Cream nzuri kwa ajili ya timu yetu ya vijana na pia wachezaji saba ambao watakuwa tayari kucheza kwenye timu kubwa msimu ujao”, alisema.
Kuhusu lini itakuwa siku ya mwisho, kocha huyo kijana alitanabaisha kuwa, mchakato huu wa kuska vipaji ulikuwa ufikie tamati hapo kesho lakini uongozi wa City umeamua kusogeza mbele mpaka siku ya jumamosi ambapo wachezaji watakaopatikana kwenye mchujo wa kesho watapata nafasi ya kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na timu ya Ilemi Fc.
“Ilikuwa tuhitimishe kesho lakini tumesogeza mpaka jumamosi ambapo vijana wetu wapya watakaopatikana watacheza mchezo wa kirafiki , na baada ya hapo zoezi litafungwa tayari wa kusubiri maandalizi ya msimu mapema mwezi ujao” alimaliza.
TTCL YAZINDUA NEMBO MPYA NA HUDUMA YA 4G LTE
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza
na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na wadau wa Sekta ya
Mawasiliano (hawapo pichani), wakati uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni
hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Edwina Lupembe
akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa, katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo
na huduma ya 4G LTE
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha
Kazaura akielezea mafanikio ya TTCL kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika hafla ya
uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizindua
nembo mpya ya Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL), jijini Dar es Salam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akijadiliana
jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt.
Kamugisha Kazaura, wakati wa halfla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni
hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wakifatilia sherehe
za uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar
es Salaam.
…………………………………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Kampuni ya
Simu ya (TTCL), kuwa wabunifu ili kuhimili ushindani wa soko katika
sekta ya mawasiliano na hivyo kuiwezesha kampuni hiyo kupata faida.
Akizungumza wakati akizindua
nembo mpya ya kampuni ya TTCL na huduma ya 4G LTE inayowezesha huduma ya
mawasiliano ya sauti na data kwa haraka Prof. Mbarawa amesema huu ni
wakati wa kubadili mtazamo na kufanya kazi kisasa ili kuvutia wananchi
kutumia huduma za TTCL.
“TTCL lazima mubadilike ili
muweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia na hivyo
kumudu ushindani uliopo sasa katika sekta ya mawasiliano”, amesema
Waziri Prof. Mbarawa.
Amewataka TTCL kuhakikisha kituo mahiri cha kutunzia taarifa (Data Centre), kinaanza mapema mwezi Juni ili kuwezesha wadau wengi kunufaika na kituo hicho.
Prof. Mbarawa amesema Serikali
inaunga mkono TTCL na imetenga masafa ya 800 MHZ ambayo yataiwezesha
TTCL kushindana na makampuni mengine ya watoa huduma ya mawasiliano na
kuwaunganisha wateja wengi kutumia huduma za mawasiliano na data.
“Uzinduzi wa nembo mpya ya TTCL
na huduma ya masafa ya 4G LTE uendane na ubunifu kwa wafanyakazi ili
muwavutie watumiaji wengi wa simu na hivyo kupata soko kubwa na kuifanya
TTCL kuchangia kikamilifu pato la taifa”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema mawasiliano
ni kiungo muhimu cha kufanikisha ukuaji wa sekta za kilimo, taasisi za
fedha, uwekezaji, ujasiliamali na utendaji kazi wa Serikali na sekta
binafsi hivyo ubunifu katika utendaji utaiwezesha TTCL mpya kufikia
malengo yaliyokusudiwa.
Katika hatua nyingine Prof.
Mbarawa amewataka wananchi kuzingatia maelekezo wanayopatiwa na Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhusu namna ya kuzitambua simu na vifaa
feki na hatua za kufuata ili ifikapo Juni 16 zoezi la kuzifunga simu
feki litakapotekelezwa wasiathirike.
Kwa upande wake Mwakilishi wa
Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Bi. Edwina Lupembe amesisitiza kwamba TTCL
imejipanga kuboresha huduma za fedha ili kuwezesha watumiaji wengi wa
kampuni hiyo kunufaika na huduma ya kutuma na kupokea fedha.
“Tumekamilisha mradi mkubwa wa
kusimika mitambo ya GSM, UMTS na LTE ambayo itakuwa na uwezo wa kutoa
huduma ya mawasiliano 2G, 3G na 4G”, amesema Bi. Lupembe
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL
Dkt. Kamugisha Kazaura amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa mabadiliko ya
muonekano wa TTCL yataendana na mtazamo mpya wa wafanyakazi wenye lengo
la kuiwezesha kampuni hiyo kuwa ya kisasa hapa nchini.
Amesema TTCL imejipanga kuboresha
simu za mezani, mkononi, na huduma za intaneti ya haraka ili iweze
kupata wateja wengi na hivyo kuongeza mapato yake.
“Teknolojia ya 2G GSM, 3G UMTS na
LTE imeongeza nguvu kwa kampuni yetu kuleta ushindani katika soko la
mawasiliano na zitaendelea kuongeza ufanisi na ubunifu wa huduma zetu
kwa bei nafuu”, amesisitiza Dkt. Kazaura.
Tayari huduma ya 4G LTE inapatikana katika maeneo mengi ya Ilala, Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam.
RaisDk. John Pombe Magufuli akemea vitendo vya Rushwa kwa wakandarasi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia Wakandarasi, Wahandisi na wadau mbalimbali wa sekta ya
Ujenzi kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa Siku mbili wa Mashauriano wa
Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipewa
maelezo kuhusu katapila linalotumika katika kazi mbalimbali za ujenzi
mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya
Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
wakati akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho
ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati
akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa
hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano
wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini
Dar es Salaam.
Wadau
mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi wakiwemo Wahandisi na Wakandarasi
wakipiga makofi wakati wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano huo wa
Mashauriano wa CRB jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakandarasi nchini
kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kulisaidia Taifa kupiga hatua ya
kimaendeleo.
Mhe. Rais Magufuli ameyasema hayo
leo wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa
Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
“Mnaweka viwango vikubwa vya
fedha kwenye miradi ili muweze kupata fedha ya kutoa rushwa, kwa nini
mnafanya hivyo?”amewauliza Mhe. Rais Magufuli na kuwambia kuwa kama wapo
watumishi wa serikali wanaowaomba rushwa ili wapate kazi waitaarifu
Takukuru mara moja ili wachukuliwe hatua.
Mhe. Rais amewataka wakandarasi
wazawa wajipange kufanya kazi na kuwaonya wasiwe wanaweka viwango
vikubwa ambavyo vinachangia kuwakosesha zabuni.
Akitoa mfano, Mhe. Magufuli
alisema katika ujenzi wa mahakama za mwanzo hapa nchini, jengo moja
lilikadiriwa kukamilika kwa milioni 200 lakini wakandarasi wa Tanzania
walioomba zabuni hiyo walitoa kiwango cha kati ya shilimgi milioni 670
na bilioni 1.4. Amesema kwa jinsi hii hata mtu awe na huruma ya namna
gani hawezi kuwapa kazi.
Amesema serikali yake itawajali
kwanza wakandarasi wa hapa nchini lakini akawataka wajipange na pengine
waungane ili kufanya kazi kwa pamoja.
Aidha, Mhe. Rais amesema ujenzi
wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanzania unakaribia kuanza
lakini akauliza wakandarasi wa hapa nchini wamejipangaje katika
kushiriki ujenzi huo.
Kuhusu ulipaji wa madeni ya
wakandarasi, Mhe Rais amesema, serikali yake imekuwa ikilipa madeni hayo
na itaendelea kufanya hivyo hadi deni litakapoisha. Amesema kwa kuanza
serikali imelipa bilioni 650 na baadaye ikatumia bilioni 462 kutoka
Mfuko wa Barabara kuwalipa wakandarasi.
Amesema wakandarasi ni watu wa
muhimu sana katika maendeleo ya Taifa na ni injini ya maendeleo kwani
wako kila sekta ya maendelo. Amesema kwa mfano wako katika ujenzi wa
mioundombinu, kwenye zana za kilimo,kwenye uvuvi, na pia usafirishaji
wakandarasi hawakosekani.
MATUKIO YA BUNGE LEO MJINI DODOMA 26/5/2016.
Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiendelea leo mjini Dodoma.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson
akifuatilia kwa makini michango ya wabunge wakati wa kipindi cha Maswali
na Majibu ndani ya Bunge mjini Dodoma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angela
Kairuki akifuatilia jambo ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
Waziri
wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce
Ndalichako akijadiliana jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde bungeni mjini Dodoma.
Waziri
wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce
Ndalichako akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya
Elimu, Sayansi , Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 20016/2017
mjini Dodoma. Wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2016/2017 imeomba
kupitishiwa shilingi Bilioni 1.39 . Picha/Aron Msigwa-MAELEZO.
Serikali yawapa miezi miwili waishio kijjiji cha michezo Changamani kuhama.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akitoa agizo la kuhama kwa wananchi wa
eneo la changamani Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam(Hawapo Pichani)
kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha Michezo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisistiza jambo mbele ya wajumbe wa kikao
kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke
jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao
kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha
Michezo.
Kaimu
Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya akichangia hoja katika kikao
kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya Temeke
jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi hao
kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha
Michezo.
Mwakilishi
wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw.Mafuku Rajabu akifafanua jambo katika
kikao kati ya Serikali na wananchi wa eneo la changamani Wilaya ya
Temeke jijini Dar es Salaam katika kikao cha kujadilina kuhusu wananchi
hao kuhama eneo hilo kupisha uendelezaji wa eneo hilo kuwa kijiji cha
Michezo.
Eneo
la Changamani kijiji cha Michezo ambalo wananchi wake wanatakiwa kuhama
ndani ya miezi miwili kupisha uendelezwaji wa eneo hilo kwa ajili ya
michezo mbalimbali.
Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM
………………………………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi WHSUM.
Serikali imewapa miezi miwili
wananchi waishio katika kijiji cha michezo cha Changamani kilichopo
Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam kuhama katika eneo hilo kupisha
uendelezwaji wa kijiji cha mchezo.
Agizo hilo limetolewa na Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipokutana na wananchi hao katika kikao cha
kujadili na kukubaliana muda wa kuhama katika eneo hilo leo Jijini Dar
es Salaam.
“Ndugu zangu tumejadiliana wote
na kukubaliana kuwa baada ya miezi miwili mtakuwa mmeshaama katika eneo
hilo kupisha uendelezwaji wa kijiji cha michezo kwa ajili ya shughuli za
mbalimbali za michezo” alisisitiza Bw. Nkenyenge.
Naye Kaimu Meneja wa Uwanja wa
Taifa Bw.Julius Mgaya amesema kuwa mpango wa kuwahamisha wananchi hao
unalenga kutekeleza mradi wa kijiji cha michezo kitakachojengwa kwa
ajili ya kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali.
Kwa upande wake mmoja ya
wawakilishi wa wananchi hao Bw.Atillio Mballa amesema wamekubaliana na
muda huo waliopewa na watafikisha ujumbe huo kwa wenzao na kabla ya muda
hujafika watakuwa wameshatekeleza agizo hilo.
Katika mpango wa kukuza na
kuendeleza michezo nchini Serikali imejipanga kukuza sekta ya michezo
nchini na kuifanya kuwa moja ya rasilimali itakayochangia katika pato la
taifa.
TAARIFA KUTOKA TFF
CAF YAMTEUA MICHAEL WAMBUR
Shirikisho la Soka Barani Afrika
(CAF), limemteua Michael Richard Wambura kuwa Kamishna wa mchezo wa
kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na
Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016.
Wambura ambaye amewahi kuwa
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri
katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. Msumbiji
iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.
TAIFA STARS KWENDA KENYA KESHO
Kikosi cha timu ya soka ya
Tanzania – Taifa Stars, chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na
Hemed Morocco kinatarajiwa kuondoka kesho saa 12.00 alfajiri kwenda
Nairobi, Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa
kimataifa
Mchezo huo ni maandalizi ya
kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia
itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.
TANZANIA KUTOANDAA CECAFA CUP
Shirikisho
a Soka Tanzana (TFF), limetangaza kutoandaa michuano ya kuwania Kombe
la timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na
Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama
ilivyopendekezwa.
Sababu za TFF ya kutoandaa fainali hizo ni kwa kubanwa na ratiba ya michuano ya kitaifa na kimataifa
Awali mkutano mkuu wa CECAFA, uliamua Zanzibar iwe mwenyeji wa michuano ya Kagam
Baadaye kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa ilionekana Zanzibar hawataweza kufanya
Baada ya hapo TFF ilianza kuangalia uwezekano wa mashindano haya kwa kumshirikisha mabingwa wa 2015/16 ambao ni Yanga
Kutokana na ratiba ya Kombe la
Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) iliyotolewa na Shirikisho la Soka la
Afrika (CAF), kipindi ch Juni hadi Agosti, 2016 Yanga watakuwa na kwenye
michuano ya CAF hatua ya makundi hivyo ushiriki wao CECAFA utakuwa
mgumu ilihali michuano ya CECAFA imepangwa kufanyika Juni na Julai,
mwaka huu.
MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI ATEMBELEA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akielezea
majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa
nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake) alipotembelea leo, Makao Makuu ya
Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akielezea
majukumu ya ofisi hiyo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa
nchini Bi. Bella Bird (kulia kwake), Menejimenti ya NBS na wageni
walioambatana na Mkurugenzi Mkazi huyo alipotembelea leo, Makao Makuu ya
Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni Jijini Dar es Salaam. ( PICHA
NA EMMANUEL GHULA)Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Abina Chuwa akimkaribisha
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird (kushoto)
alipotembelea leo Makao Makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Barabara ya Kivukoni
Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Veronica Kazimoto
26 Mei, 2016.
BENKI ya Dunia imeahidi
kuendelea kuisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kifedha ili iweze
kutekeleza majukumu yake ya utoaji wa Takwimu Rasmi nchini.
Akizungumza leo alipotembelea
Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa
nchini Ms. Bella Bird amesema kutokana na umuhimu wa takwimu katika
kupanga na kupima matokeo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
kimaendeleo, Benki ya Dunia itaendelea kuisaidia NBS ili iendelee
kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kutoa takwimu kwa wakati.
“Ili Ofisi ya Taifa ya Takwimu
iweze kutoa takwimu kwa wakati, inahitaji kuwekeza katika matumizi ya
technolojia ya kisasa ya ukusanyaji wa takwimu, hivyo Benki ya Dunia
itaendelea kutoa msaada wa kiufundi na kifedha ili kufikia malengo
yaliyoainishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya utoaji wa takwimu rasmi
nchini”, amesema Ms. Bella Bird.
Mkurugenzi huyo Mkazi
amefafanua kuwa Benki ya Dunia inatambua umuhimu wa takwimu katika
maendeleo ya nchi zote duniani ikiwemo Tanzania katika kupanga sera na
kutekeleza miradi mbalimbali ya nchi husika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa ameishukuru Benki ya
Dunia kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikiisaidia Ofisi ya Taifa ya
Takwimu ambayo imeongeza tija katika ukusanyaji na utoaji wa takwimu
rasmi nchini.
“Napenda kuchukua fursa hii
kuishukuru Benki ya Dunia kupitia ujio wako kuitembelea Ofisi ya Taifa
ya Takwimu na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi hii
ikiwa ni pamoja na ukusanyaji na utoaji wa takwimu rasmi hapa nchini,”
amesema Dkt. Chuwa.
Dkt. Chuwa amesema Ofisi ya
Taifa ya Takwimu imeendelea kupanua wigo wa uzalishaji wa takwimu nchini
ikilinganishwa na karne zilizopita.
Benki ya Dunia inaisaidia Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kutoa
ushauri wa kitalaam pamoja na fedha kupitia Mpango Kabambe wa Kitaifa
wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini ambapo awamu ya kwanza
itakamilika mwezi Juni, 2018.
TAKUKURU yawahamasisha wananchi kushishiriki kampeni ya LONGA NASI
Kaimu
Mkuu wa Sehemu ya Uratibu na utoaji Habari,Idara ya Elimu kwa Umma toka
Taasisi ya Kuzuia na Kupmbana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Matai Kirumbi
akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaa kuhusu faida
za kampeni ya LONGA NASI iliyozinduliwa na Taasisi hiyo hivi karibuni
ikilenga kuhamasisha wananchi kushiriki vita dhidi ya rushwa kwa
kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo. Kushoto ni Afisa
Uhusiano nwa Taasisi hiyo Bi Angela Mulanduzi.
…………………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi – MAELEZO
TAKUKURU yawahamasisha wananchi kushishiriki kampeni ya LONGA NASI ili kukomesha vitendo vya rushwa hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uratibu na utoaji Habari,Idara
ya Elimu kwa Umma toka Taasisi ya Kuzuia na Kupmbana na rushwa
(TAKUKURU) Bw. Matai Kirumbi wakati wa mkutano na vyombo vya Habari.
Akizungumzia Kampeni hiyo,
Kirumbi amesema inalenga kuwajengea uelewa wananchi kuhusu mapambano
dhidi ya rushwa ili kuzuia vitendo vya rushwa .
Katika Kampeni hiyo wananchi
wanatakiwa kutoa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya rushwa au viashiria
vyake kwa kupiga namba 113 au *113# kupitia simu ya kiganjani .
Huduma hiyo inapatikana kupitia mitandao ya AIRTEL,TIGO,HALOTEL,VODACOM na ZANTEL ambapo wananchi hawatatozwa gharama yoyote.
“Taarifa 8000 zimeshapokelewa na
Taasisi yetu tangu kuzinduliwa kwa Kampeni hii na nyingi ni za wananchi
kuombwa hongo na tayari tunazifanyia kazi “alisisitiza Kirumbi.
Akifafanua kuhusu taarifa hizo
Kirumbi amesema kuwa zinaonyesha wananchi wamepokea vizuri kamapeni hiyo
iliyozinduliwa tarehe 24/5/2016 na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu
Hassan.
Katika kampeni hiyo wananchi
watajengewa ujasiri zaidi ili kuongeza ushiriki wao katika mapambano
dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa na kutoa mrejesho wa kero
zilizotatuliwa.
Matarajio ni kuongezeka kwa ubora
wa huduma za jamii kwa kuwa fedha za umma zitatumika kama ilivyopangwa
katika huduma kama vile kununua dawa.
Akizindua kampeni ya LONGA NASI
jumanne tarehe 24,Mei 2016 katika viwanja vya Mwembeyanga Wilayani
Temeke Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan
alisisitiza suala la ushiriki wa kila mmoja katika mapambano dhidi ya
rushwa nchini alisema”Tunahitaji nguvu za pamoja ili kumaliza tatizo la
rushwa nchini”.
ESRF yafanya warsha kujadili Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDG)
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Katika
kusaidia kukamilika kwa Mpango wa Maendeleo Endelevu ambao unataraji
kumalizika 2030, Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) imefanya
warsha ambayo imekutanisha wadau mbalimbali ili kuona ni jinsi gani
wanaweza kubadilishana mawazo ili kufanikisha mpango huo nchini.
Mgeni
rasmi katika warsha hiyo alikuwa ni Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na
Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha ambaye wakati
akifungua warsha hiyo alisema kuwa mpango huo ni muhiu wa nchi yetu kwa
sababu unakwenda kubadili maisha ya kila Mtanzania ili kuondokana na
umaskini na kuwa katika maisha bora kama jinsi malengo 17 ya mpango huo
yanavyojieleza.
Mo
Dewji Blog ilipata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo na kukuandalia
habaroi picha jinsi warsha hivyo ilivyofanyika katika ukumbi wa ESRF.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akitoa neno la ufunguzi katika warsa iliyoandaliwa na ESRF ili
kuzungumzia Mpango wa Mendeleo Endelevu (SDG). (Picha zote na Rabi Hume,
Modewjiblog)
Baadhi
ya washiriki waliohudhuria warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii, Dkt.
Tausi Kida wakati akifungua warsha hiyo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo
akitoa neno kwa niaba ya UNDP ambao ndiyo wasimamizi wa mpango huo.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii
(ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua
Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha
Mgeni
rasmi katika warsha hiyo, Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua
Uchumi kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha akifungua warsha hiyo
iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF).
Washiriki wakiendelea kufatilia kinachoendelea katika warsha hiyo.
Stephen Chacha kutoka Shirika la Beyond 2015 for Africa akizungumza jinsi Mpango wa SDG unaweza kufanyika nchini.
Mmoja wa washiriki, Dkt. Kitila Mkumbo akichangia mada zilizokuwa zikijadiliwa.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
MPANGO MPYA WA UGAWAJI VYANDARUA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO WAZINDULIWA MKOANI MTWARA
Mganga
mkuu wa mkoa wa Mtwara Dr Wedson Sichalwe akionesha moja ya vyandarau
vitakavyokuwa vikigawiwa katika vituo vya afya kwa wakina mama
wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara
katika mpango wachandarua kliniki, mpango unaotarajiwa kuzinduliwa
jumamosi hii na mkuu wa mkoa huo bi halima dendegu. wanao shuhudia
kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi
theresia shirima, mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya
john hopkins university david dadi na kulia kwake ni mratibu wa afya ya
mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
mkuu wa mkoa wa Mtwara Dr Wedson Sichalwe akionesha moja ya vyandarau
vitakavyokuwa vikigawiwa katika vituo vya afya kwa wakina mama
wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara
katika mpango wachandarua kliniki, mpango unaotarajiwa kuzinduliwa
jumamosi hii na mkuu wa mkoa huo bi halima dendegu. wanao shuhudia
kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi
theresia shirima, mkurugenzi wa program ya malaria kutoka taasisi ya
john hopkins university david dadi na kulia kwake ni mratibu wa afya ya
mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
mganga
mkuu wa mkoa wa mtwara dr wedson sichalwe akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya
ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya
umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango wa chandarua
kliniki.pamoja nae walioketi kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya
afya na ustawi wa jamii bi theresia shirima, mkurugenzi wa program ya
malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi na kulia
kwake ni mratibu wa afya ya mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
mkuu wa mkoa wa mtwara dr wedson sichalwe akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya
ugawaji vyandarua kwa wakina mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya
umri wa miezi tisa mkoani mtwara katika mpango wa chandarua
kliniki.pamoja nae walioketi kushoto kwake ni meneja wa kinga wizara ya
afya na ustawi wa jamii bi theresia shirima, mkurugenzi wa program ya
malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david dadi na kulia
kwake ni mratibu wa afya ya mama na mtoto- rch bi albertina mlowola.
Mkurugenzi
wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david
dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo
pichani kuhusiana na zinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina
mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani
mtwara katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa
kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima
dendego.
wa program ya malaria kutoka taasisi ya john hopkins university david
dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo
pichani kuhusiana na zinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina
mama wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani
mtwara katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa
kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima
dendego.
Meneja
wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi Theresia Shirima,
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo pichani
kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama
wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara
katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa
kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima
dendego.
wa kinga wizara ya afya na ustawi wa jamii bi Theresia Shirima,
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wa mkoani mtwara hawapo pichani
kuhusiana na uzinduzi wa mpango mpya ugawaji vyandarua kwa wakina mama
wajawazito na wenye watoto wa chini ya umri wa miezi tisa mkoani mtwara
katika mpango ujulikanao kama chandarua kliniki, unaotarajiwa
kuzinduliwa jumamosi wiki hii na mkuu wa mkoa wa mtwara bi halima
dendego.
JITIHADA
za kutokomeza malaria nchi zimeanza kuonyesha matunda baada ya takwimu
za ugonjwa huo mkoani Mtwara kuonyesha zimeshuka kutoka asilimia 33
mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012 kitaifa
zikifikia asilimia 9 toka asilimia 33.
za kutokomeza malaria nchi zimeanza kuonyesha matunda baada ya takwimu
za ugonjwa huo mkoani Mtwara kuonyesha zimeshuka kutoka asilimia 33
mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka 2011/2012 kitaifa
zikifikia asilimia 9 toka asilimia 33.
Takwimu
hizo zimeshuka ikiwa ni jitihada zinazofanywa na serikali kwa
kushirikiana na USAID pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha jamii
zinatumia vyandarua vyenye kinga kujikinga na ugonjwa huo ili kuupunguza
au kutokomezwa kabisa.
hizo zimeshuka ikiwa ni jitihada zinazofanywa na serikali kwa
kushirikiana na USAID pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha jamii
zinatumia vyandarua vyenye kinga kujikinga na ugonjwa huo ili kuupunguza
au kutokomezwa kabisa.
Takwimu
hizo zimetolewa na Mganga mkuu wa mkoa, Dk Wedson Sichalwe alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa chandarua Kliniki
utakaozinduliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na mkuu wa mkoa Halima Dendego
kwa lengo la kufikisha vyandarua kwa jamii ambao utahusisha wajawazito
na watoto wa miezi tisa watakaohudhuria vituo vya afya.
hizo zimetolewa na Mganga mkuu wa mkoa, Dk Wedson Sichalwe alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpango wa chandarua Kliniki
utakaozinduliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na mkuu wa mkoa Halima Dendego
kwa lengo la kufikisha vyandarua kwa jamii ambao utahusisha wajawazito
na watoto wa miezi tisa watakaohudhuria vituo vya afya.
“Tunataraji
kuzindua mpango wa usambazaji wa vyandarua vyenye viatilifu vya muda
mrefu kupitia kliniki a wajawazito na watoto katika vituo vya kutolea
huduma za afya ikiwa ni mojawapo ya juhudi zinazofanywa na serikali
kupambana na ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
katika kuhakikisha malaria inapungua na madhara yake kwa
wananchi,”alisema Sichalwe
kuzindua mpango wa usambazaji wa vyandarua vyenye viatilifu vya muda
mrefu kupitia kliniki a wajawazito na watoto katika vituo vya kutolea
huduma za afya ikiwa ni mojawapo ya juhudi zinazofanywa na serikali
kupambana na ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
katika kuhakikisha malaria inapungua na madhara yake kwa
wananchi,”alisema Sichalwe
Aidha
Dk Sichwale alisema katika mwaka 2015 jumla ya mahudhurio ya wagonjwa
yaliyotokana na malaria kwa mkoa huo ni 208,473 ikiwa ni wagonjwa wa nje
yani OPD sawa na asilimia 17.5.
Dk Sichwale alisema katika mwaka 2015 jumla ya mahudhurio ya wagonjwa
yaliyotokana na malaria kwa mkoa huo ni 208,473 ikiwa ni wagonjwa wa nje
yani OPD sawa na asilimia 17.5.
Naye
Afisa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria wizara ya afya,maendeleo ya
jamii,jinsia ,wazee na watoto, Theresia Shirima alisema ipo mikakati
mbalimbali ya kuhakikisha vyandarua vinafikishwa kwa jamii ikiwa ni
pamoja na kupitia shuleni kila mwaka na kwa kaya kila baada ya miaka
kadhaa ambayo iliwezesha kufikia jamii kwa asilimia 85 ambayo
wanaiendeleza ili kufikia asilimia 100.
Afisa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria wizara ya afya,maendeleo ya
jamii,jinsia ,wazee na watoto, Theresia Shirima alisema ipo mikakati
mbalimbali ya kuhakikisha vyandarua vinafikishwa kwa jamii ikiwa ni
pamoja na kupitia shuleni kila mwaka na kwa kaya kila baada ya miaka
kadhaa ambayo iliwezesha kufikia jamii kwa asilimia 85 ambayo
wanaiendeleza ili kufikia asilimia 100.
“Hatutumia
wajawazito na watoto pekee,zipo njia mbalimbali za kufikisha vyandarua
kwa jamii, na kwa mkoa wa Mtwara lipo zoezi linaloendelea la kugawa
vyandarua shuleni ikiwa ni njia ya kufikia ambayo ni awamu ya nne kwa
mwaka wa nne na kwenye kaya tunatoa mara moja baada ya miaka kadhaa
ambayo iituwezesha kufikia asilimia 85,”alisema Shirima
wajawazito na watoto pekee,zipo njia mbalimbali za kufikisha vyandarua
kwa jamii, na kwa mkoa wa Mtwara lipo zoezi linaloendelea la kugawa
vyandarua shuleni ikiwa ni njia ya kufikia ambayo ni awamu ya nne kwa
mwaka wa nne na kwenye kaya tunatoa mara moja baada ya miaka kadhaa
ambayo iituwezesha kufikia asilimia 85,”alisema Shirima
Akizungumza
mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Albertina Mlolowa aliwataka
wanajawazito kuhudhuria kliniki na kupatiwa huduma pasipo kubaguliwa na
kusema hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki
wakihofia kuulizwa weza wao na kusema suala la afya ya uzazi ni kwa
manufaa ya baba na mama.
mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Albertina Mlolowa aliwataka
wanajawazito kuhudhuria kliniki na kupatiwa huduma pasipo kubaguliwa na
kusema hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki
wakihofia kuulizwa weza wao na kusema suala la afya ya uzazi ni kwa
manufaa ya baba na mama.
“Nawaomba
kina mama wajawazito wasiogope kuhudhuria kliniki na weza wao kwa faida
yao,hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki
wakihofia kuulizwa weza wao.lakini watambue suala la afya ya uzazi ni la
mama na baba hivyo wanapohudhuria wote kunasaidia kuondoa hatari amabyo
inaweza kujitokeza hapo baadae kama maambukizi mapya na wakati mwingine
kumsababishia mama kukosa huduma kwa wakati,”alisema Mlolowa
kina mama wajawazito wasiogope kuhudhuria kliniki na weza wao kwa faida
yao,hii inatokana na baadhi ya wajawazito kutokuhudhuria kliniki
wakihofia kuulizwa weza wao.lakini watambue suala la afya ya uzazi ni la
mama na baba hivyo wanapohudhuria wote kunasaidia kuondoa hatari amabyo
inaweza kujitokeza hapo baadae kama maambukizi mapya na wakati mwingine
kumsababishia mama kukosa huduma kwa wakati,”alisema Mlolowa
Mpango
wa chandarua kliniki unatekelezwa na mradi wa Vectorworks ambao ni
mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji
na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu
wa chandarua kliniki unatekelezwa na mradi wa Vectorworks ambao ni
mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji
na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu
Tigo yamdhamini Ben Pol kuburudisha ‘Tamasha la Nyama Choma’
Kampuni
inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imekubali
kumdhamini mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo za muziki, Bernard
Michael Paul Mnyang’anga, maarufu kama ‘Ben Pol’ kuburudisha katika
tamasha la mwaka huu la Nyama Choma.
Tamasha hilo ambalo
linafanyika kwa mwaka wa tano sasa ni moja ya tamasha maarufu
linalovutia watu wengi kutoka maeneo yote ya Dar es Salaam litafanyika
kwenye viwanja vya Leaders Jumamosi Mei 28, 2016.
Akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari, Mkuu wa Tigo wa masuala ya Dijitali Paulina Shao
alisema kuwa kumuunga mkono Ben Pol kunaonesha kuendelea kujikita kwa
Tigo katika kuwekeza katika kusaidia sekta ya muziki ya ndani kwa
kuhakikisha wasanii wanawezeshwa kufikia viwango vya juu katika kazi
zao.
“Kama kampuni ya maisha ya
kidijitali, Tigo inatambua mchango muhimu wa wasanii wa Tanzania
wanaoutoa katika sekta ya burudani. Hii ndio maana tumewekeza kwa
kiwango kikubwa kuwasaidia wasanii hususani wanamuziki wa ndani
katika kuhakikisha wanafahamika katika masoko ndani ya nchi, kikanda na
kimataifa kwa kutumia majukwaa ya kidijitali yanayokuwepo na kushiriki
matukio mbalimbali na hivyo kuongeza mauzo ya muziki wao pamoja na
nembo zao,” alisema Shao.
Aidha akiishukuru Tigo kwa
uungwaji mkono huo, Ben Pol aliisifu Tigo kwa juhudi inazofanya bila
kuchoka katika kukuza ukuaji wa sekta ya muziki wa ndani kupitia
Jukwaa la Muziki la Tigo.
“Ninaishukuru sana Tigo kwa
uungwaji mkono ambao ni muendelezo wa mtiririko wa programu ambazo
imezianzisha ili kuinua maisha ya wasanii wachanga wa Tanzania,”
alisema Ben Pol na kutoa changamoto kwa wasanii wanaoibukia kuwa wasione
aibu kuomba msaada kutoka kwa mashirika kama Tigo.
Nguli huyo wa muziki wa Bongo Flava kwa hivi sasa anatamba na kibao ‘MoyoMashine’ ambayo aliitoka hivi karibuni.
Ben Pol ni miongoni mwa
wasanii wanaonufaika na jukwaa la Muziki la Tigo ambalo lilianzishwa
mwaka 2015 likiwa na lengo la kuiunga mkono sekta ya muziki Tanzania
kwa kuwasaidia wasanii wa ndani kupata kipato zaidi kutokana na mauzo
ya kazi zao na kuwawezesha kufahamika katika masoko ya kimataifa
kupitia majukwaa hayo ya kidijitali kama vile Music portal na Deezer,
ambayo ni majukwaa ya kimataifa yaliyo kwenye mtandao yakiwa na nyimbo
kutoka sehemu mbalimbali duniani zaidi ya milioni 36.
RAIS DKT. MAGUFULI AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUWA WAZALENDO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na
wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa
mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwataka
makandarasi wazawa kuwa wazalendo na nchi yao ikiwemo kuepuka vitendo
vya rushwa katika maeneo ya Kazi.
Baadhi ya Makandarasi nchini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakandarasi nchini
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili
ya Makandarasi (CRB).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na baadhi ya wageni na watendaji wa serikali wakati
akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano wa
Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
Kaimu
Msajili kutoka Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Rhoben Nkori
akiongea wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano
wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB)na kuahidi kuendelea kuwapa
kipaumbele makandarasi wazawa na kukabiliana na changamoto
zinazowakabil.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolata Ngimbwa
akiongea na wakandarasi(hawapo pichani) ambapo aliwataka makandarasi
wazawa kufanya kazi kwa weledi na kusisitiza kuwachukulia hatua kali za
kisheria kwa makandarasi wenye nia ya kuwakwamisha.
Waziri
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
akiongea na wakandarasi nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka
wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB) ambapo aliwaahidi
makandarasi nchini kuwasimamia kikamilifu na kuwapa fursa na kazi
mbalimbali za ujenzi nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea
baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano
wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea
baadhi ya mabanda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa mashauriano
wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi ya Wakandarasi na viongozi
wa mkoa wa Wizara ya Ujenzi wa mkoa wa Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo
kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali waliowezesha kufanyika kwa
mkutano wa mwaka wa mashauriano wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB).
BAJETI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPITISHWA, USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI NJE YA TANZANIA WAPIGWA MARUFUKU KWA MIAKA 3.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne akijibu hoja na michango
mbalimbali ya wabunge zilizoelekezwa kwenye wizara hiyo wakati wa
Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka
2016/2017
ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
ambayo imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
Baadhi
ya wabunge wakimpongeza wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe
mara baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kupitishwa Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo
imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
imetengewa kiasi cha shilingi bilioni 135.7.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akimweleza jambo Mbunge
wa Bunda mjini Mhe. Esther Matiku (CHADEMA) nje ya ukumbi wa Bunge mara
baada ya kupitishwa kwa Makadirio ya Mapato na Matumizi
ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017.
ya Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni
mjini Dodoma.
……………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dodoma.
Serikali imesimamisha utoaji wa
vibali na uuzaji wa wanyama hai kutoka katika hifadhi za Taifa kwenda
nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 3 mpaka hapo itakapotangazwa tena.
Waziri wa Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe ametoa agizo hilo bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu hoja na michango mbalimbali ya wabunge iliyoelekezwa kwenye
wizara hiyo wakati wa Majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
Wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 ambayo imetengewa kiasi cha shilingi
bilioni 135.7.
Prof. Maghembe ameiagiza Idara ya
Wanyamapori ipange na kuweka utaratibu mpya utakaotumika kusimamia
biashara hiyo pindi itakaporejeshwa tena baada ya kumalizika kwa muda wa
zuio la Serikali la miaka 3 ikizingatia mazingira ya uhifadhi wa
wanyama hao.
USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI NJE YA NCHI.
Amesema kumekuwa na taarifa za
baadhi ya watanzania wasio waaminifu ambao wamekua wakijihusisha na
vitendo vya kusafirisha wanyama hai waliokatazwa kinyume cha utaratibu
jambo ambalo limeisababishia Serikali ipoteze mapato kutokana na wanyama
hao.
Kuhusu wanyama wanaoruhusiwa
kusafirishwa kama nyani, Kenge,ndege, kobe, wadudu na tumbili amesema
kuwa wamekuwa wakisafirishwa kinyume na utaratibu na baadhi ya
wafanyabiashara wasio waaminifu kwa ajili ya kutumiwa na makampuni ya
kimataifa kwenye shughuli za utafiti wa kisayansi wa tiba na chanjo.
Amesema makampuni hayo yamekuwa
yakinufaika binafsi kwa kupata fedha nyingi pindi yanapofanikiwa kupata
chanjo au tiba husika huku maeneo waliokotoka yakipata fedha kidogo
jambo ambalo serikali ya awamu ya tano imeamua kulifanyia kazi.
Maliasili na Tamisemi wasaini mkataba wa makubaliano uendelezaji misitu
Baadhi ya wajumbe wakiwa katika mkutano huo
Wizara
ya maliasili na utalii kupitia wakala wa huduma za misitu leo wamesaini
mkataba wa makubaliano kuhusu ushirikiano wa uendelezaji misitu na
wizara ya TAMISEMI.
Maeneo ya kuzingatia
katika mkataba huo yametajwa kuwa ni kuimarisha ushirikiano katika
Misitu na utawala bora, uperembaji miradi inayofadhiliwa na mfuko wa
misitu Tanzania pamoja na kuboresha ukusanyaji, ugawaji, utumiaji na
ufuatiliaji wa matumizi ya asilimia 5 ya tuzo za upandaji miti.
Awali kabla ya kusaini
mkataba wa makubaliano katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja
Jenerali Gaudence Milanzi alisema wizara yake inalenga kuimarisha
utendaji wake hivyo aliwaagiza watendaji kusimamia misingi ya mkataba
huo wa makubaliano katika utekelezaji wa majukumu ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu TAMISEMI Injinia Musa Iyombe ambaye amewakilishwa na Bw. Mohamed
Pagawa aliwataka Maafisa Misitu kufanya kazi kwa ushirikiano kama
Mkataba Unavyotaka lakini pia kuzingatia sheria, kanuni na Utaratibu
katika uendelezaji wa Rasilimali Misitu
Mkurugenzi wa Mipango
na Matumizi ya Rasilimali Misitu Bw. Mohamed Kilongo akitoa ufafanuzi
kuhusu makubaliano hayo amesema tathmini ya Rasilimali Misitu
inakabiliwa na changamoto kuu mbili na amezitaja kuwa ni uharibifu
Mkubwa wa Misitu unaofikia kiasi cha hekta 372,000 kwa mwaka na mahitaji
ya mazao ya misitu kwa mwaka yanazidi uwezo wa Misitu kwa zaidi ya Meta
za ujazo Milioni 19.5.
Amesema ili kukabiliana
na changamoto hizo kunahitajika jitihada za pamoja kuboresha usimamizi
wa rasilimali za misitu na kupunguza uharibifu katika hifadhi zetu. Kazi
kubwa iliyopo mbele yetu ni kupanda miti hekta 185,000/= kwa mwaka kwa
ajili ya kukidhi mahitaji ya Mazao ya Misitu.
TAMISEMI yaziagiza Halmashauri zote kukamilisha agizo la Rais ifikapo Mwezi Juni.
Na Daudi Manongi
MAELEZO Dar es Salaam
HALMASHAURI za Miji na Wilaya
nchini Miji zimekumbushwa kukamilisha zoezi la upatikanaji wa madawati
kwa shule za msingi na sekondari ifikapo juni 30 mwaka huu ili
kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu wakati wa mahojiano
na mwandishi wa habari hizi kuhusu uchakavu wa madarasa na ukosefu wa
madawati unaozikabili shule za kinesi A na B zilizopo wilaya ya Rorya
mkoani Mara.
“Suala la upungufu wa madawati na
uchakavu wa madarasa ni changamoto ya kitaifa na kwamba lilishatolewa
agizo na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu halmashauri zote
nchini kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu kila mwanafunzi anaketi
kwenye Dawati” Alisema Kwandu.
Kwa mujibu wa Gwandu alisema
Serikali ya awamu imepania kuinua kiwango na ubora wa elimu nchini
kupitia mikakati na sera ya elimu bure nchini kote.
Aliongeza kuwa hatua hiyo imeibua
changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi kujitokeza kwa asilimia kubwa na
hivyo ni wajibu wa halmshauri hizo kukidhi mahitaji ya madawati ili
wasome katika mazingira mazuri.
“Mpaka sasa Serikali imeendelea
kutoka pesa kwa ajili ya elimu bure nchini kote na kumekuwepo kwa
changamoto mbalimbali kama upungufu wa walimu,madawati na madarasa
ambapo serikali inafanya jitihada za kila namna ili kutatua changamoto
hiyo”
Akifafanua zaidi Gwandu alisema
Serikali inaandaa harambee mbalimbali na kuongeza wigo wa utoaji wa
vibali vya kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ili kutoa nafasi kwa
wadau mbalimbali wenye nia ya kufanya.
BIMA YA AFYA KUANZA HUDUMA YA MAMA NA MWANA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw Bernard Konga, akitoa
salamu za Mfuko kwa wajumbe wa baraza hilo lilikofanyika katika ukumbi
wa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro
salamu za Mfuko kwa wajumbe wa baraza hilo lilikofanyika katika ukumbi
wa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Bw Bernard Konga,(katikati)
akizungumza na baadhi ya wajumbe ndugu Gudluck Kirambe, kulia na
meneja wa mkoa wa Kilimanjaro ndugu Fidelis Stephen.
akizungumza na baadhi ya wajumbe ndugu Gudluck Kirambe, kulia na
meneja wa mkoa wa Kilimanjaro ndugu Fidelis Stephen.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
ya Afya (NHIF) wanaohudhuria kika
……………………………………………………………………………………………………………………..
Kilimanjaro
MFUKO wa taifa wa bima ya afya (NHIF) utaanzisha huduma mpya ya
itakayojulikana kama mama na mwana afya kadi ili kuboresha huduma za
bima ya afya kwa kundi hilo ambalo lipo katika uhitaji maalum.
MFUKO wa taifa wa bima ya afya (NHIF) utaanzisha huduma mpya ya
itakayojulikana kama mama na mwana afya kadi ili kuboresha huduma za
bima ya afya kwa kundi hilo ambalo lipo katika uhitaji maalum.
Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na kaimu mkurugenzi mkuu wa mfuko huo,
bw Bernard Konga alipokuwa akitoa salamu za Mfuko huo kwa wajumbe wa
baraza hili linaloanza kikao chake mjini hapa.
bw Bernard Konga alipokuwa akitoa salamu za Mfuko huo kwa wajumbe wa
baraza hili linaloanza kikao chake mjini hapa.
Bw konga amesema lengo la huduma hiyo mpya ni kuwawezesha kina Mama
Wajawazito na Watoto kupata huduma za matibabu za uhakika zitolewazo
na mfuko wa taifa wa Bima ya afya.
Wajawazito na Watoto kupata huduma za matibabu za uhakika zitolewazo
na mfuko wa taifa wa Bima ya afya.
Chimbuko la hatua hiyo linafuatia matokeo mazuri na mafanikio makubwa
ya mradi unaoendeshwa kwa pamoja kati ya NHIF na benki ya maendeleo ya
ujerumani ya KfW katika mikoa ya Tanga na Mbeya. hatua iliyofikiwa kwa
sasa ni kupata maoni ya wananchi kabla ya kuanza utekelezaji wake
katika mwaka wa fedha wa 2016/17.
ya mradi unaoendeshwa kwa pamoja kati ya NHIF na benki ya maendeleo ya
ujerumani ya KfW katika mikoa ya Tanga na Mbeya. hatua iliyofikiwa kwa
sasa ni kupata maoni ya wananchi kabla ya kuanza utekelezaji wake
katika mwaka wa fedha wa 2016/17.
Awali, akifungua kikao cha baraza hilo, mkuu wa wilaya ya Siha Dr
Charles Mlingwa, aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa huo Meck Sadiki,
aliushukuru mfuko huo kwa kuwa wabunifu katika utoaji wa huduma kwa
makundi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wao wa kulipa. Ameutaka mfuko
huo kutafsiri hotuba za mheshimiwa Rais kuhusu dhana ya afya bora kwa
wote kwa kuweka mikakati katika eneo hilo.
Charles Mlingwa, aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa huo Meck Sadiki,
aliushukuru mfuko huo kwa kuwa wabunifu katika utoaji wa huduma kwa
makundi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wao wa kulipa. Ameutaka mfuko
huo kutafsiri hotuba za mheshimiwa Rais kuhusu dhana ya afya bora kwa
wote kwa kuweka mikakati katika eneo hilo.
Dr Mlingwa pia amesema wilaya ya Siha ni moja ya wilaya zilizofanikiwa
sana kuboresha huduma za matibabu ambapo kwa miaka miwili mfululizo
imeweza kupunguza sana vifo wa watoto wachanga na kufikia mtoto mmoja
kwa kila watoto laki moja.
sana kuboresha huduma za matibabu ambapo kwa miaka miwili mfululizo
imeweza kupunguza sana vifo wa watoto wachanga na kufikia mtoto mmoja
kwa kila watoto laki moja.
MAJALIWA:VITA DHIDI YA RUSHWA SI NGUVU YA SODA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vita inayoendeshwa na Serikali ya
awamu ya tano dhidi ya wala rushwa na wale wanaofanya ufisadi siyo nguvu
ya soda kama wengi wanavyofikiri.
“Serikali ya awamu ya
tano imedhamiria kupambana na wala rushwa na mafisadi. Wala hatutanii.
Hawa tutacheza nao na wala wasidhani vita hii ni nguvu ya soda.
Tutaendelea kuwasaka hadi tufike mwisho,” alisema Waziri Mkuu wakati
akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika
kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia juzi jioni (Jumanne,
Mei 24, 2016).
“Hatutaki tabia
iliyokuwepo ya mwananchi anakuja ofisini kutaka huduma lakini
hasikilizwi hadi atoe chochote, sisi hiyo tabia hatutaki kuisikia
kabisa. Tumedhamiria kurudisha heshima kwenye utumishi wa umma na
nimeanza kupata faraja kwani sasa hivi (nimeambiwa) katika baadhi ya
taasisi unasikia mtu akiulizwa una shida gani, nenda pale, jambo ambalo
zamani halikuwepo,” alisema.
Alisema Serikali
imeamua kupigia debe dhana ya utumishi wenye uadilifu kwa sababu huo ni
utamaduni mpya. “Ni kipindi kigumu kidogo cha mabadiliko lakini
tumesimamia mabadiliko haya na ndiyo maana watumishi wote
tumewasisitizia kuwa suala la uaminifu, uadilifu na uwajibikaji ni
muhimu,” alisema na kuongeza:
“Hatutamvumilia
mtumishi yeyote ambaye hatakuwa tayari kuwatumikia Watanzania au
atakayeendekeza uzembe lakini pia hatutamuonea mtu yeyote. Hapa
tunasisitiza usawa na hatutaki kutengeneza gap kati ya mwananchi
mtumishi na wa mwananchi wa kawaida, tunataka kila mwananchi aione
Tanzania ni nchi yake na kila kinachozalishwa ni sehemu yake. Tukifika
hapo, tunaamini kila mmoja ataweza kuisemea nchi yake.”
Akizungumzia kuhusu
ubadhirifu wa fedha za umma, Waziri Mkuu alionya kwamba Serikali imelipa
kipaumbele suala la uaminifu na uadilifu kwenye fedha za Serikali na
kwamba haitakuwa tayari kuona fedha hizo zikifujwa.
“Hivi sasa Serikali
imetenga fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha hizo
zitaenda vijijini. Tunataka zikafanye kazi iliyokusudiwa, na wale
wadokozi wajue kuwa wamekalia kaa la moto,” alisema huku akishangiliwa.
Alisema watumishi wa
umma wana wajibu wa kusimamia kazi zilizopangwa na kuhakikisha miradi
iliyolengwa inakamilika. “Kama fedha zimeletwa kujenga zahanati simamia
zahanati ijengwe na ni lazima zahanati hiyo ionekane,” alisema.
Alisema bajeti ya mwaka
huu imeongezeka kutoka sh. trilioni 21 hadi trilioni 29 lengo kuu
likiwa ni kuleta maendeleo kwa wananchi. “Ndiyo maana tumepandisha
bajeti ya maendeleo kutoka asilimia 27 hadi asilimia 40. Ole wake
atakayepokea fedha hizi halafu zisifanye kazi yake, ukiipoteza wewe
utafute njia ya kwenda,” alisema huku akishangiliwa.
Akifafanua zaidi,
Waziri Mkuu alisema vita inayoendeshwa imelenga kuifanya Tanzania
ibadilike na itoke kwenye uchumi wa chini na kuingia uchumi wa kati.
“Swali la msingi ni je tunafikaje hapo? Jibu ni kupitia uzalishaji wa
bidhaa viwandani,” alisema.
“Nyote ni mashahidi wa
jinsi ambavyo shilingi yetu imekuwa ikishuka thamani kulinganisha na
dola ya Marekani. Tulitoka sh. 1,600/-, tukapanda hadi sh. 1,900/- na
sasa tumefikia sh. 2,180/-. Hii ni kwa sababu tunaagiza zaidi bidhaa
kutoka nje ya nchi badala ya kuzalisha, hatuwezi kuendelea hivi na ndiyo
maana tumeamua kuwa nchi ya viwanda. Leteni mitaji nyumbani muwekeze,”
alisisitiza.
Akijibu swali kuhusu
Serikali kutafuta njia ya kutoa mikopo kwa Watanzania waishio nje ya
nchi, Waziri Mkuu alisema mkopo ni mkataba kati ya taasisi ya kifedha na
mkopaji kwa hiyo Serikali haiwezi kubeba dhamana hiyo. “Benki wanataka
ijue taarifa zako mkopaji, wanataka wajua dhamana zako ni zipi,
wajiridhishe na shughuli unazofanya. Je panakopesheka hapo?,” alihoji.
Hata hivyo, aliwaeleza
kwamba wakitaka kuwekeza nyumbani wanaweza kupata mikopo kutoka benki ya
maendeleo ya kilimo (TADB), Benki ya Rasilmali (TIB Corporate na TIB
Development). “Hizi benki ni za wakulima na wajasiriamali, na zina
masharti yake, kwa hiyo ni lazima wakakague eneo lako au mahali
unapofanyia biashara au wakague leseni yako na ukweli wa maombi
uliyopelekea. Sasa ukiwa Zambia watawezaje kukukopesha? Kwa hiyo ukitaka
fedha uwe nyumbani,” alisema.
Akijibu swali ni vipi
Serikali itawasaidia wanadiaspora kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu
wakiwa nje ya nchi, Waziri Mkuu alisema Serikali haijawahi kujaribu
jambo hilo licha ya kuwa ilikwishapokea mapendekezo kadhaa kutoka nchi
mbalimbali lakini kwa vile wameliuliza, yeye analibeba na kwenda
kulifanyia kazi.
Tigo yatoa kompyuta 20 zilizounganishwa na intaneti kwa sekondari 3 Mtwara
Wanafunzi wakishuhudia makabidhiano hayo |
Kampuni
inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania leo imetoa
kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi milioni 33 zikiwa na huduma ya
bure ya intaneti iliyogharimu 22m/- kwa shule tatu za sekondari mkoani
Mtwara. Msaada huo uko katika mkondo wa malengo ya kampuni ya kuleta mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya elimu nchini.
Mtwara. Msaada huo uko katika mkondo wa malengo ya kampuni ya kuleta mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya elimu nchini.
Akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano yaliyofanyika Shule ya Sekondari Sino
mkoani Mtwara Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Goodluck Charles
alisema, “Msaada huu kwa shule hizi tatu ni sehemu ya
mkakati wa kampuni wa kuleta mageuzi katika mtindo wa maisha ya kidijitali. Msaada huu wa leo umekuja baada ya kukabidhi kompyuta 10 kwa Shule ya Msingi Chuda mkoani Tanga na kompyuta 25 zilizounganishwa na intaneti kwa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure mkoani Mwanza mwaka jana.
mkakati wa kampuni wa kuleta mageuzi katika mtindo wa maisha ya kidijitali. Msaada huu wa leo umekuja baada ya kukabidhi kompyuta 10 kwa Shule ya Msingi Chuda mkoani Tanga na kompyuta 25 zilizounganishwa na intaneti kwa Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure mkoani Mwanza mwaka jana.
“Msaada
kwa shule ya Sekondari ya Masasi, Tandahimba na Sino ni kielelezo cha
kweli cha uwekezaji wa Tigo katika miradi tofauti yenye mchango kijamii
kupitia mkakati wetu wa kuwekeza kijamii unaowezesha jamii kupokea zana
za kisasa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katikanyanja zote za
kijamii ikiwemo sekta ya elimu,” alisema Charles.
Tukio
hilo ambalo lilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego
ambaye alizitaka sekta binafsi kuisaidia serikali katika mikakati yake
katika kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zilizopo nchini.
Dendego
alisema, “Naipongeza Tigo kwa ukarimu wao wa kuzisaidia shule hizi
natoa wito kwa watu binafsi kampuni za biashara na wadau wengine
kujitokeza katika kuunga mkono juhudi za kuboresha
sekta ya elimu.”
sekta ya elimu.”
Akipokea
msaada huo kwa niaba ya wakuu wenzake wa shule za sekondari, Mkuu wa
Shule ya Sekondari Sino Riyadh Kadhi alisema kwamba kompyuta hizo
zitawawezesha wanafunzi kuwa na uelewa wa kiteknolojia na kuwawezesha
kuipata teknolojia ya habari mapema katika elimu yao. “Tunafurahi kwa
hatua hii ya Tigo; tuna
matumaini kwamba kompyuta hizi zitawaweka wanafunzi wetu katika ngazi moja na wenzao katika mashule mengine yaliyo maeneo ya mjini na duniani kwa ujumla,” alisema Kadhi.
matumaini kwamba kompyuta hizi zitawaweka wanafunzi wetu katika ngazi moja na wenzao katika mashule mengine yaliyo maeneo ya mjini na duniani kwa ujumla,” alisema Kadhi.
No comments:
Post a Comment