Pages

Sunday, May 29, 2016

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA NIDA, ATOA HABARI NJEMA KWA WATUMISHI 597 WALIOSITISHWA MIKATABA YAO

1 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) akimsalimia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba, wakati alipokuwa anawasili katika ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi.
2 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo katika Jengo la BMTL, jijini Dar es Salaam, jana. Katika hotuba yake, Rwegasira aliwataka watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao waondoe hofu kwani hivi karibuni Serikali itaanza kuwalipa fedha zao baada ya taratibu chache za kiutendaji kukamilika.
3 
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ansigar Chilemba akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
4 
Afisa Usajili Kitengo cha Ubora wa Kadi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jemima Mulokozi (kushoto) akimuonyesha vitambulisho vilivyokamilika vikiwa na ubora unaohitajika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba. Rwegasira alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam jana.
5 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tano kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya Katibu Mkuu kumaliza ziara ya kikazi katika ofisi za Mamlaka hiyo, jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………………………..
Na Felix Mwagara, MOHA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema fedha za kuwalipa watumishi 597 waliositishiwa mikataba yao katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) zipo na watalipwa hivi karibuni.
Rwegasira alisema kiasi cha shilingi bilioni 2.3 zimetengwa kwa ajili ya malipo ya Watumishi hao waliachishwa kazi Machi 7, 2016 ambapo wanaidai Mamlaka mishahara ya miezi mitatu nyuma, malimbikizo ya fedha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na makato ya fedha za Bima ya Afya.
Akuzungumza na watumishi wa Makao Makuu ya NIDA pamoja na Maafisa Wasajili wa Vitambulisho vya Taifa, jijini Dar es Salaam jana, Rwegasira aliwataka watumishi hao waliositishiwa mikataba yao, wasipotoshwe na mtu yeyote kuhusu kutokulipwa haki zao kwani wapo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha taratibu ndogo ndogo  kabla ya kuanza kuwalipa.
“Naomba muwaambie waondoe wasiwasi wowote, waache maneno, watulie kwani Serikali ipo makini na fedha tunazo na tutaanza kuwalipa mara tumalizapo taratibu ndogo ndogo zilizobaki.” Alisema Rwegasira.
Aidha, Rwegasira aliwataka watumishi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha ifikapo Desemba 31 mwaka huu Watanzania Milioni 23 wanatakiwa watambuliwe na kupata namba kabla ya kuanza kupewa Vitambulisho vya Taifa.
Hata hivyo, watumishi hao walimuakikishia Katibu Mkuu huyo, kuwa kazi hiyo ya utambuzi  itakamilika kama ilivyopangwa na itafanyika kwa umakini mkubwa kama inavyotarajiwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modestus Kipilimba alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kuwatembelea na kuwatia hamasa katika kukamilisha kazi pamoja na kufikisha lengo lao la kukamilisha utambuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
“Tunakuahidi Katibu Mkuu kuwa tutatimiza lengo letu na tunakuakikishia tutafanya kazi kadiri ya uwezo wetu tukiongozwa na kauli mbiu ya ‘hapa kazi tu’, alisema Dk. Kipilimba
Katibu Mkuu Rwegasira alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji.

NAPE AENDELEA KUKUTANA NA WANANCHI WA VIJIJI VILIVYOPO NDANI YA JIMBO LAKE AAHIDI KUMALIZA AHADI ZAKE MAPEMA

Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kilimanjaro kilichopo kata ya Mtumbya ikiwa muendelezo wa mikutano yake ya kila kijiji katika jimbo lake ambapo alizungumzia utekelezaji wa ahadi alizoahidi na kuwahakikishia wananchi hao kuwa ahadi zake zitakamilika mapema mno.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiongozana na wakazi wa kijiji cha Kilimanjaro kilichopo kata ya Mtumbya kwenda kujionea maendeleo ya ujenzi wa zahanati.
  Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya wanakijiji cha Kilimanjaro kilichopo jimbo la Mtama , wilaya ya Lindi Vijijini.
  Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwasomea wakazi wa kijiji cha Mtumbya vijiji vitakavyopata umeme wa mradi wa umeme vijijini ( REA) awamu ya tatu katika jimbo la Mtama.
Mkazi wa kijiji cha Mtumbya Bw. Subiri Hashimu Saidia akiuliza swali wakati wa mkutano wa  Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na wananchi hao.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na wakazi wakijiji cha Mpenda, Mtama
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Mpenda ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa barabara ya kutoka Mtama, kupitia Mpenda , Mtumbya kwenda Kilimanjaro mkandarasi ameshapatikana na ataanza kazi hiyo mara moja na kuwahakikishia kuwa pamoja na kuwepo miradi mikubwa ya maji lakini Mpenda na Kilimanjaro watapata visima mapema.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFANYA ZIARA YA KICHAMA PEMBA

sh1 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Fidel Castro Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusnini Pemba leo alipofika kuwashukuru wanachama cha Mapinduzi CCM kwa ushindi waliompatia katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.] 29/05/2016.
sh3Wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya chakechake Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza nao leo, wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza   kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh4 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza   kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh5 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza   kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh6 
Kiembe Ramadhan Khamis kutoka Tawi la Mkoroshoni  akitoa mchango wake wakati  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh7 
Balozi Mohamed Kombo Juma (Wawi) akitoa mchango wake wakati  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza wanachama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Chakechake Pemba kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh8Mwenyekiti wa Wilaya ya Chakechake Pemba akitoa taarifa wakati  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza WanaCCM kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,(kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia),[Picha na Ikulu.]29/05/2016.
sh9Wanachama cha Mapinduzi CCM wialayanya Chakechake akinyanyua mkono juu kuunga mkono maelezo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein wakati alipofika katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro leo kuwapongeza kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa Marudio uliofanyika mwezi Machi mwaka huu,[Picha na Ikulu.]29/05/2016.

JK AWAFUNDA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU JIJINI DAR ES SALAAM LEO JIONI

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete akihutubia katika mahafali ya 2016 ya Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wa CCM yaliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam leo jioni.
 Vijana vyuo vikuu Dar es Salaam wakiserebuka katika mahafali yao.
 Vijana hao wakiendelea kuserebuka.
 Hapa ni furaha kwa kwenda mbele.
Ni kama wanasema’  Hapa ni ushindi tu 2020 kwani vijana tumejipanga.
Vijana wakiwa kwenye mahafali hayo.

taifa STARS NA HARAMBEE stars zatoana sare 1-1.

1 
Kikosi cha kwanza cha timu ya Soka ya Tanzania -Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Harambee Stars ya Kenya Jumapili.
2Mshambuliaji wa Taifa Stars, Elias Maguli (Kulia) akichuana na David Odhiambo wakati wa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika Uwanja wa Moi Kasarani, Nairobi Kenya. timu hizo ziliamua kutoka sara ya 1-1.
3 
Winga wa Taifa Stars, Shiza Ramadhani akichuana na beki Joakins Atudo wa Harambee Stars katika mchezo huo.  

Ben Pol Akonga Nyoyo za maelfu wa mashabiki katika Tamasha la Nyama Choma Jijini Dar es salaam

 Mwanamuziki mahiri  wa Rnb hapa nchini  , Bernard Michael Paul, maarufu kama ‘Ben Pol’ akitoa burudani  kwa maelfu ya wakazi wa Dar es salaam waliohudhuria maadhimisho ya miaka mitano ya  Tamasha la Nyama choma 2016,ambapo Tigo ilimdhamini kutumbuiza katika tamasha hilo , mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam .
 
BEN POL akicheza na mashabiki zake jukwaani wakati wa tamasha la nyama choma katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam 
Mashabikiwa muziki wa bongo fleva wakishangilia wakati Benpol anatumbuiza kibao chake cha MOYO MASHINE 
 
Benpol akihojiwa na mtangazaji wa Clouds fm Askofu Tza baada ya kutumbuiza katika tamasha la Nyama choma mapema jana katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Baadhi ya mawakala wa tigo waliokuwepo katika viwanja  vya Leaders kutoa msaada na huduma mbali mbali toka tigo ikiwemo huduma za intaneti ya kasi ya Tigo 4G LTE
Wakala wa tigo akisajili laini ya mteja katika tamasha la Nyama choma mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.
 
 
Mtangazaji wa Choice fm na mshindi wa Bigbrother 2014 Idris sultan akifurahi jambo na Mcheza kikapu wa kimataifa Hasheem Thabit wakati wa Tamasha la Nyama Choma lililofanyika mapema jana usiku katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaam.
 
Msanii mahiri wa Bongo fleva Vanessa Mdee akiongea jambo na mmoja wa shabiki zake katika viwanja  vya Leaders Jijini Dar es salaam
Mabanda ya tigo yaliyokuwepo uwanjani katika kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wa tigo  waliofika katika tamasha la Nyama Choma 
 
Mmoja wa wapishi wa nyama akichoma nyama wakati wa tamasha la Nyama Choma mapema jana katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.
 
Wadau wakiendelea kufurahia muziki na kula nyama choma katika tamasha liliofanyika mapema jana
 
Mmoja wa wakala wa Tigo akimsaidia mteja  kufungua intaneti ya tigo katika simu yake katika tamasha la Nyama Choma .liliofanyika mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam,
Maelfu ya wakazi waliofika katika tamasha wakifurahia muziki toka kwa wasanii mbali mbali waliotumbuiza jukwaani

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA ZIARA YA KIKAZI GEREZA MSALATO – DODOMA ATEMBELEA MRADI WA KUPONDA KOKOTO

mau1 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea saluti kutoka kwa Mkuu wa Gereza Msalato, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Stevin Mwihambi alipowasili Gerezani hapo kwa ziara ya kikazi.
mau2 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(Mb) akitoka katika lango Kuu la Gereza Msalato alipofanya ziara ya kikazi katika Gereza hilo leo Mei 29, 2016 Mkoani Dodoma(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Casmir Minja.
mau3 
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja(wa pili kulia) akiwa ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(wa pili kushoto) walipofanya ziara ya kikazi katika Gereza Msalato lililopo Mkoani Dodoma(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Antonino Kilumbi.
mau4 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akisaini Kitabu cha Wageni kabla ya kupokea taarifa fupi ya hali ya Ulinzi na Usalama wa Gereza Msalato alipofanya ziara ya kikazi leo Mei 29, 2016.
mau5 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto) akiongea na Wafungwa wa Gereza Msalato(hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo(katikati) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP John Casmir Minja kwa pamoja wakisikiliza kero mbalimbali za Wafungwa
mau6Muonekano wa eneo la Gereza Msalato ambalo linajishughulisha na mradi wa upondaji wa kokoto kama inavyoonekana katika picha.
mau7 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano maalum na Waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea eneo la mradi wa kuponda kokoto katika Gereza Msalato lililopo Mkoani Dodoma(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

MH. WAZIRI :JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA WAFUGAJI

ar1 
Waziri wanchi,Ofisi ya Makamo wa Rais, Muungano na Mazingira Mh.January Makamba alitembelea Jamii ya wafugaji wa kimasai wanaoishi Mkoani Mrogoro,walayani Kilosa kata na kijiji cha Parakuyo. Waziri huyo aliwatembelea wafugaji hao kwa lengo la kuzungumza nao na kuwahamasisha wafugaji hao kuwasomesha watoto wao wa kike ili wapate elimu na kukomboa familia zao kielimu mara watakapoelimika.
Aliwapa mfano wa viongozi wanawake mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ambao wamekuwa wakifanya kazi zao kwa uwezo mkubwa hivyo akawaambia wafugaji hao kuwa iwapo  watasomesha watoto wao wa kike watakuwa wameelimisha jamii ya wafugaji pia,  kama anavyoonekana kwenye picha January Makamba akizungumza na wanafunzi katika shule ya sekondari ya Parakuyo ambayo watoto wengi wanaosoma hapo wanatoka katika jamii ya  wafugaji(PICHA NA IMANI SAMILA)
ar2
Hapa waziri January Makamba akizungumza na watoto wa kike kutoka familia za wafugaji katika kijiji cha Parakuyo.
ar4
Baadhi ya akina mama kutoka familia za wafugaji wakimsikiliza waziri January Makamba wakati alipokuwa akizungumza nao kijini Hapo.
ar5
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza
AR6
Waziri January Makamba akivishwa vazi la asili na wananchi wa kijiji cha Parakuyo kutoka jamii ya wafugaji.
AR7
Waziri January Makamba akiwashukuru mara baada ya kumvisha vazi hilo.
AR8
Waziri January Makamba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Parakuyo kutoka jamii ya wafugaji wakati alipowatembelea kijijini hapo leo.
AR9 
Waziri January Makamba akisalimiana na watoto mbalimbali kutoka jamii ya wafugaji wakati alipotembelea katika kijiji cha Parakuyo.

WADAU WACHANGAMKIA WINDHOEK TAMASHA LA NYAMA CHOMA VIWANJA VYA LEARDERS JIJINI DAR ES SALAAM

 Mtaalamu wa kuchoma nyama kutoka mkoani Arusha, Jackson Isaya akionesha ufundi wa kuchoma nyama katika Tamasha la Nyama choma lililofanyika ,viwanja vya Learders Dar es Salaam jana.
 Wadau wa Windhoek wakipata kinywaji hicho katika tamasha hilo.
 Timu nzima ya kutoa huduma ya Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd wakati wa tamasha hilo.
Wadau wa Windhoek wakionesha kinywaji hicho wakati wakinywa. Kulia ni Meneja wa Kampuni hiyo, Mr Ruta, Kushoto ni mdau wa Windhoek kutoka Kilimanjaro, Nurudin Sagafu na wa pili kulia ni  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Mabibo, Jerome Rugemalira.

WILAYA YA MPWAPWA KUFANYA HARAMBEE YA KUPATA MADAWATI JIJINI DAR ES SALAAM JUNI 4, 2016

 Mkuu wa Wilaya  ya Mpwawa iliyopo mkoani Dodoma, Mohamed Utaly (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu harambee ya kupata fedha za kununulia madawati itakayofanyika Juni 4 mwaka huu Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi,Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Samuel Albertus Coy.
 Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Utaly.
………………………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpwapwa Dodoma Juni 4 mwaka huu inatarajia kufanya harambe ya kupata fedha za kununulia madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari wilayani humo ambayo itafanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkuu wa Wilaya hiyo Mohamed Utaly alisema wamefikia hatua hiyo ili kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule hizo ambapo pamekuwa na changamoto kubwa.
Alisema awali halmashauri hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 16,000 lakini baada ya kuwashirikisha wananchi na kufanya harambee mbalimbali walifanikiwa kupata madawati 6000 na kubaki kiasi cha madawati 10,000 ambayo yanahitaji.
Utaly alisema halmshauri hiyo katika bajeti yake ya mwaka 2015-2016 ilitenga sh. milioni 180 kwa ajili ya madawati ambapo kunamafanikio makubwa ya kupata madawati hayo yaliyosalia hivyo akatumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali wa ndani wa wilaya hiyo na nje kujitokeza katika harambee hiyo ili waweze kufanikisha jambo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mohamed Maje alisema changamoto kubwa waliyoibaini ni kutokuwa na kitengo cha kufanya ukarabati wa madawati yaliyo haribika ambacho hivi sasa kimeanzishwa.
“Kwa muda mrefu hatukuwa na kitengo cha kukarabati madawati yaliyoharibika lakini sasa tumekianzisha na kitasaidia kupunguza changamoto hiyo kwa kitengo hicho kitakuwa kikisaidia na wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya watu 20 ambavyo vipo sita kwa ajili ya kufanya kazi hiyo” alisema Maje.

Mh January Makamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira azungumzia siku ya mazingira

JA1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh January Y. Makamba, akionyesha Tamko Rasmi kwa Waandishi wa Habari  (hawapo pichani) kuhusu siku ya Mazingira Duniani.
JA3 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,BwanaMbarak  M. Abdulwakil ( wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais( wa pili kushoto )Injinia Ngosi Mwihava wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh.Makamba wakati akitoa Tamko la Siku ya Mazingira Duniani.
JA4 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Y. Makamba,akiongea na waandishi wa Habari  kuhusu Tamko la Siku ya Mazingira Duniani.
…………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
Serikali imeandaa mkakati mpya wa kitaifa wa kupanda na kutunza miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hatua ambayo itarudisha hali ya mazingira kama yalivyokuwa awali miaka ya nyuma.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
 “Mkakati huu mpya umezingatia kurekebisha changamoto zilizojitokeza katika kampeni za upandaji miti zilizofanyika katika vipindi mbalimbali tangu uhuru wan chi yetu” alisema Waziri Makamba.
Ili kukabiliana na changamoto hizo, Waziri Makamba amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake imetenga kiasi cha Sh. bilioni 2 ikiwa kianzio kwa lengo la kusimamia mkakati huo katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Katika kuhakikisha suala la mazingira limepewa kipaumbele, Mfuko wa Taifa wa Mazingira ambao ni mdau mkuu wa mazingira utatengewa vyanzo vya mapato yanayokadiriwa kufikia Sh. bilioni 100 ikiwa ni juhudi za kugharimia mpango huo na mipango mingine ya hifadhi ya mazingira.
Mkakati huo ni wa miaka mitano ambao unaanza kutekelezwa 2016 hadi 2021 na unakadiriwa kugharimu kiasi cha Sh. bilioni 105.2.
Aidha, Waziri Makamba amebainisha kuwa masuala ambayo yatazingatiwa katika kutekeleza mpango huo ni pamoja na uhamasishaji na utoaji motisha kwa watumiaji wa nishati mbadala ili kuondoa matumizi ya kuni na mkaa.
Ili kuhakikisha mazingira yameboreshwa na yawe rafiki kwa kila kiumbe, utekelezaji na usimamiaji wa mkakati huo, utaanza kutekelezwa kuanzia ngazi ya chini hadi juu ambapo kila kijiji, kitongoji, mtaa, kaya na kila taasisi itapewa lengo la pandaji miti kama msingi wa zoezi hilo.
“Tutashindanisha shule na vijiji katika upandaji na ukuzaji wa miti na tutatoa zawadi nono na maeneo ya wazi ya Serikali yatapandwa miti” alisema Waziri Makamba.
Katika kuhakikisha miti iliyopandwa inalindwa na kukua,  Ofisi ya Makamu wa Rais itashirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mkioa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha halmashauri zinatunga sheria ndogo ndogo za kuhimiza upandaji na utunzaji miti nchini.
Maadhimisho ya mwaka huu Kimataifa yanafanyika nchini Angola ambayo yanalenga kupambana na biashara ya meno ya tembo na pembe za faru yakiongozwa na kaulimbiu “Tunza wanyama porini kwa maisha”
Siku ya mazingira Duniani imeanza kuadhimishwa  mwaka 1972 ambapo Baraza la Umoja wa Mataifa lilifanya wa mkutano wake wa kwanza unaohusu mazingira uliofanyika Stockholm nchini Sweden na kuundwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira diniani (UNEP).

JAJI MKUU AZITAKA MAHAKAMA MKOANI GEITA KUMALIZA KESI KWA WAKATI

chief-justice2 
Na Lydia Churi – Geita.
 
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amezitaka Mahakama za mkoa wa Geita kuhakikisha zinamaliza kesi kwa wakati ili kutekeleza lengo lililowekwa na Mahakama ya Tanzania.
 
Akizungumza na watumishi wa Mahakama jana mkoani Geita, Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania ilijiwekea malengo ya kumaliza kesi katika mahakama zake kwa wakati kulingana na aina ya mahakama.
 
Alisema kwa mahakama za Hakimu Mkazi, mahakama za Wilaya pamoja na Mahakama za   Mwanzo lengo lilikuwa ni kumaliza kesi zote ndani ya mwaka mmoja ili kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na imani na mahakama zao kwa kuwa ni zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wanahudumiwa na mahakama hizo.
 
Jaji Mkuu alisema kwa mahakama za Mwanzo ambazo ziko 970 nchini kote lengo lilikuwa ni kuhakikisha hazikai na kesi kwa zaidi ya miezi sita kwa kuwa ndizo mahakama zinazohudumia wananchi wengi zaidi.
 
Alisema ili kuziwezesha Mahakama kutekeleza lengo walilojiwekea, tayari Mahakama ya Tanzania imeajiri Mahakimu wapya 107 ambao watasambazwa kwenye Mahakama zote za Mwanzo nchini kwa ajili yakwendakutoa huduma ya msingi ya mahakama ya kutenda haki kwa wananchi wa Tanzania.
 
Akizungumzia suala la utoaji wa nakala za hukumu, Jaji Mkuu amezitaka Mahakama za mkoa wa Geita kutoa nakala hizo mapema iwezekanavyo ili kutoa haki ya kukata rufaa kwa wananchi ambao hawakuridhishwa na hukumu walizopewa katika kesi zao.
 
Alisema Mahakama ya Tanzania itaongeza idadi ya Makatibu Mahususi na kuongeza vifaa katika Mahakama zake ili kuongeza kasi ya uchapaji wa nakala za hukumu. Alisema asilimia 80 ya bajeti inayotolewa kwa muhimili huo imetengwa kwa ajili ya kuendesha kesi katika mahakama za Mwanzo, Wilaya na zile za Hakimu Mkazi.
 
Jaji Mkuu anaendelea na zaira yake katika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza ambapo anatembelea mikoa Mwanza, Geita na Mara ili kukagua shughuli za kimahakama katika kanda hiyo.

UPIMAJI AFYA NA UCHANGIAJI DAMU KWA HIARI MWANZA

v1Mkurugenzi wa Shirika la Rich And Support All (RASA) Shughutta Abdulla akimpima shinikizo la damu mwandishi wa gazeti la Jambo Leo  Baltazar Mashaka, wakati wa zoezi la kupima afya lililoandaliwa na Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi al Tanzania. Zaidi ya wananchi 200 walijitokeza kupima afya zao na kupewa ushauri ambapo kati ya hao asilimia tano walibainika kuwa na kisukari, asilimia 37 waligundulika kuwa na shinikizo la kawaida  na asilimia 50 walipatikana na shikizo la juu ( Pre-Highpantation Heart Desease).Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mbugani jijini Mwanza.
v2 
Mwandishi wa gazeti la Jambo Leo Baltazar Mashaka akipimwa shinikizo la damu katika zoezi lililofanyika juzi kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mbuangani Jijini Mwanza ambapo zaidi ya watu 200 walijitokeza kupima afya zao kwa ufadhili wa Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania
v4 
Mary Mathias akitolewa damu na mhudumu wa shirika la RASA kwa ajili ya kupima kisukari katika zoezi hilo lililofadhiliwa an Taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania lilikuwa mahususi kupima uzito, shinikioz la damu na kisukari pamoja na kuchangia damu kwa hiari ambapo watu zaidi ya 200 walijitokeza kupima na kupewa ushauri na watalamu kutoka shirika la RASA na kituo cha Damu Salama Kanda ya Ziwa.
v5Mkurugenzi msaidizi wa Shirika la Rich And Support All (RSAS) Shughutta Abdulla akimpima shinikizo la damu mmoja wa wakazi wa Jiji la Mwanza kwenye zoezi la upiamji afya lililofadhiliwa na taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania. Watu zaidi ya 200 walijitokeza kupima ambapo asilimia tano waligundulika kuwa na kisukari, asilimia 37 walipatikana na shinikizo la kawaida ambapo 50 asilimia walibainika kuwa na shinikizo la ju (Pre- Highpantation heart deases) na wanastahili kuhudhuria hospitali kwa matibabu.
v6 
Musa Zuberi (kushoto ) na Michael Leonard (kulia) wakitolewa damu na wauguzi katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililofadhiliwa na taasisi ya The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania. Zoezi hilo lilisimamiwa na wataalamu wa Kituo cha Damu Salama Kanda ya Ziwa wakishirikiana na wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana -Butimba.         
v7 
Musa zuberi akichangia damu wakati wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari na upimaji afya bure chini ya ufadhili wa Taasisi ya The Desk  & Chair Foundation Tawi la Tanzania .Katika zoezi hilo zaidi ya watu 200 walijitokeza kupima afya na baadhi kujitolea kuchangia damu kwa hiari.
Picha zote na Baltazar Mashaka
……………………………………………………………………………………………………….
Na Baltazar Mashaka,Mwanza
 
MWENYEKITI wa Taasisi ya The Desk & Chair foundation Tawi la Tanzania, Alhaji Sibatain Meghjee amelalamikia bei ghali ya vifaa tiba vya ugonjwa wa kisukari kuwa inachangia wananchi wasio na uwezo kushindwa kupima afya zao ili kubaini kama wanaugua ugonjwa huo tishio.
 
Kutokana vifaa vya kupimia kuuzwa bei ghali kulingana na aina ya mashine ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi na ushuru kwenye vifaa hivyo ili watu wengi wahamasike kupima na kujua afya zao.
 
Alhaji Sibtain alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani jijini wakati wa zoezi la wananchi kupima afya bure na uchangiaji damu kwa hiari lililofadhiliwa na taasisi yake.
 
“ Mgonjwa wa kisukari anahitaji kupima mara nne kwa siku ili kufahamu sukari imepanda au kushuka kwa kiwango gani.Hiyo inawasaidia wasipate madhara ya kukatwa viungo vyao kutokana na kuathiriwa na ugonjwa huo.Sasa njiti za kupimia  ugonjwa huo zinauzwa kwa shilingi 36,000 hadi shilingi 50,000 kulingana na aina ya mashine,hiyo ni bei ghali sana,”
 
“Serikali ijitahidi na kuhakikisha bei ya njiti hizo pamoja na mashine vinapungua bei kwa sababu inakwamisha watu wengi kupima afya zao na kusababisha wapate matatizo ya figo.” Alisema alhaji Sibtain.
 
Mwenyekiti huyo wa The Desk & Chair aliongeza kuwa serikali iongeze       madaktari bingwa wa magonjwa hayo na wataalamu wa kutoa elimu ya kukabiliana na ugonjwa wa kisukari ili wananchi wajue njia ya kujikinga kwa kufuata masharti hasa ya lishe na  elimu itolewe kwa jamii kwa kutumia magazeti, vipeperushi, redio na luninga.
 
Aidha, Imani Kamugisha ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Rich and Support All (RASA) linalotoa huduma ya upimaji na ushauri alisema kwa siku tatu watu zaidi ya 200 walijitokeza kwenye zoezi kupima afya hasa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu na wengi wao walionekana kuwa na matatizo ya magonjwa hayo.
 
Alisema kuwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu yanaweza kuchukua miaka 10 bila mtu kujitambua kuwa anaugua magonjwa hayo na kuwataka watanzania kujenga tabia ya kupima na kujua afya zao wasisubiri hadi dalili zianze kuonekana.
 
“Tatizo la magonjwa haya yanachukua muda wa miaka hata 10 kujijenga na ukigundulika kuwa nayo huwezi kuyatibu kama malaria.Dalili zikianza kuonekana tiba ni hadi mwisho wa maisha yako yote na watu wanaotumia vyakula vya mafuta na pombe wako katika hatari kubwa msaada pekee ni tiba,”alisema Kamugisha.
Alieleza kuwa wamekuwa wakipima na kutoa ushauri na tangu wameanza zoezi hilo asilimia 37 ya wananchi waliopima wako katia hatua ya kwanza na ya pili ya shinikizo la damu,asilimia 50 wako katia hatua ya juu na hao wanashauriwa kwenda hospitali kwa matibabu.
 

Jukumu la kuwainua watoto wa kike ni la kila mmoja.Emma Oriyo

T1 
Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiongea na baadhi ya  wazazi wa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali waliofika kwenye  viwanja vya TTCL Kijitonyama  jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya siku ya hedhi  Salama  mwishoni mwa wiki.
T2

Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo,akiwagawia kinywaji cha Grand Malt  baadhi ya  wazazi wa watoto wanaosoma katika shule mbalimbali waliofika kwenye  viwanja vya TTCL Kijitonyama  jijini Dar es Salaam, wakati wa madhimisho ya siku ya hedhi  Salama  mwishoni mwa wiki.
T3 
Baadhi ya wanafunzi wa kike wakimsikiliza  Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa TBL Group,Emma Oriyo wakati wa maadhimisho hayo.
……………………………………………………………………………………………
Na Mwandish wetu
Meneja Uhusiano wa nje wa kampuni ya TBL Group,Emma Oriyo, amesema kuwa jukumu la kuwainua watoto wa kike nchini sio la serikali bali linamhusu kila mtanzania ikiwemo makampuni,taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi duniani iliyoadhimishwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ,alisema kuwa siku hiyo ni muhimu kuadhimishwa kwa kuwa inatukumbusha watanzania kutofumbia matatizo yaliyopo kwenye jamii yetu na kuangalia  namna ya kuyashughulikia.
“Hapa Tanzania Changamoto za hedhi kwa watoto wa kike ni kubwa wengi wakiwa wanakosa vifaa vya kuwaweka salama pia shule nyingi hazina miuondombinu rafiki kwa wasichana kujiweka salama wanapokuwa kwenye hedhi,matokeo yake wengi wanakuwa hawahudhuri masomo na kujikuta wamebaki nyuma ya wenzao wa kiume”.Alisema.
Amesema TBL Group katika miradi yake ya afya ya kusaidia jamii imeanza kuliangalia suala hili kwa undani ili kuweza kushirikiana na wadau wengine kukabiliana nalo “Leo kampuni yetu ni moja ya wadhamini wa tukio hili la siku ya hedhi ambalo lengo lake kubwa ni kuelimisha jamii umuhimu wa kuungana kuondoa changamoto na hedhi na tutaendelea na jitihada hizi na kutekeleza  miradi mingine ya kusaidia kuboresha afya  nchini”.Alisema.
Alisema  watanzania wakiungana na serikali katika  kukabiliana na changamoto hizi  hali itakuwa nzuri na watoto wa kike kusoma katika mazingira mazuri na itapelekea wafanye vizuri kwenye masomo yao sambamba na wenzao wa kiume.
Emma alisema kuwa hali ya kukosa vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi na miundombinu isiyo rafiki mashuleni mbali na utoro mashuleni pia inawasabishia watoto  wa kike kutojiamini na wakikua bila kujiamini wanakuwa hawawezi kutoa maamuzi sahihi.
“Wadau wote tukiungana katika suala hili tutaweza kutekeleza dira ya maendeleo ya taifa ambayo kwa upande wa elimu ina kauli mbiu isemayo Elimu Bora bila ubaguzi inawezekana.Timiza wajibu wako”

REAL MADRID MABINGWA WAPYA WA UEFA CHAMPION LEAGUE, WAITANDIKA ATLETICO MADRID PENATI 5-4

 
 
ZINWachezaji wa timu ya Real Madrid wakishangilia mara baada ya kuwafunga wapizani wao Atletico Madrid katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa ya Ulaya UEFA Champions League uliofanyika kwenye uwanja wa San Siro  Milan, Italy uliomalizika usiku huu.

imaDk 15, Ramos anaiandikia Madrid bao la kwanza kwa kuunganisha mpira wa kupara wa kichwa wa Bale
  Ni dakika ya 12, Madrid wamefanikiwa kufanya angalau mashambulizi matatu lakini bado hakuna bao.
Inaonekana Madrid wana kasi zaidi wanapoingia upande wa Atletico.
Kila upande umeanza mechi kwa kasi na kunaonekana kuna presha kubwa.
Sasa ni Mapumziko timu zote zimeingia vyumbani kwa ajili ya mapumziko ngoja tuone Kocha Zinedine wa Real Madrid na Kocha Diego Simeone wa Atletico Madrid wataleta mabadiliko gani katika kipindi cha pili kinachotarajiwa kuanza mara baada ya dakika 15 za mapumziko.
zine
Kocha Zinedine Zidane wa Real Madrid akihamasisha wachezaji wake kucheza kwa kujituma katika mchezo wa fainali dhidi ya mahasimu wao  timu ya Atletico Madrid katika mchezo wao unaofanyika nchini Italia hivi sasa Atletico Madrid wanakosa penati ambayo imepigwa na mchezaji Antoine Griezmann baada ya mchezaji wa timu Real Madrid  Fernado Torres kuanguswa katika eneo la hatari.
Lakini kwa sasa huenda Real Madrid wakaongeza tena mashabulizi ili angalau kutoka na ushindi katika mchezo huo na kuchukua uchampioni wa ligi ya klabu bingwa ulaya,  Hata hivyo si kazi rahisi ngoja tuone mwelekea wa mchezo unavyoenda katika dakika 90 za mchezo huo.Lakini kwa sasa huenda Real Madrid wakaongeza tena mashabulizi ili angalau kutoka na ushindi katika mchezo huo na kuchukua uchampioni wa ligi ya klabu bingwa ulaya,  Hata hivyo si kazi rahisi ngoja tuone mwelekea wa mchezo unavyoenda katika dakika 90 za mchezo huo.
carvasoMchezaji wa Atletico Madrid Yannick Ferreira Carrasco akishangilia mara baada ya kufunga goli la kusawazisha katika dakika ya 89 ya mchezi kipindi cha pili.
Mchezaji wa Carrasco wa Atletico Madrid anaisawazishia goli timu yake katika dakika ya 89 ya mchezo  na matokeo kuwa Real Madrid 1-Atletico madrid -1,  mpira umekwisha na  zinaongezwa dakika  30 , baada ya hapo kama hatapatikana mshindi timu zitaingia katika uamuzi wa kupiga penati tano kila timu ili kupata mshindi katika mchezo huo
PENATI ZINAPIGWA SASA
 Sasa dakika 30 za nyongeza zimekwisha timu zinaingia tena uwanjani kwa ajili ya kupiga penati 5 kila moja ukumbuke kwamba upigaji wa penati unategemea sana uwezo wa magolikipa kuzuia penati langoni lakini poia upigaji mzuri wa penati kwa wachezaji wa uwanjani  hebu tungoje na tuone ni timu gani inao uwezo katika penati lakini pia ni golikipa gani ana uwezo mzuri wa kuzuia penati  katika ya Keylor Navas wa Real Madrid na Jan Oblak wa Atletico Madrid.
Christiano Ronaldo anapiga penati ya tano na ya ushindi na kuitangazia dunia kuwa klabu ya Real Madrid inachukua ubingwa wa klabu bingwa za vilabu ulaya kwa kuwafunga wapinzani wao wakubwa nchini Hispania Real Atletico kwa penati 5-4 mara baada ya mchezaji wa timu ya Atletico Madrid  Juanfran kukosa penati ya nne katika mchezo huo hivyo Real Madrid wanachukua ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya UEFA Champions League Hongereni Real Madrid Hongera Kocha Zinedine Zidane

BWANA EDWIN MASHAYO NA BI. MARY MOLLEL WAUAGA UKAPELA

Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT – Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam leo May 28, 2016. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog -(Kajunason Studio).
Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT – Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam. Pembeni ni wasimamizi wao.
Waumini waliohudhuria.
Mchungaji wa Kanisa la KKKT – Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam akifungisha ndoa ya Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel.
Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakila kiapo.
Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakila kiapo.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akitoa sadaka.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akisaini katika cheti kama shaidi wa ndoa hiyo mara baada ya Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel kufunga ndoa.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa akiwapongeza maharusi.
Mchungaji wa kanisa la KKKT – Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam akiweka saidi katika cheti.
Maharusi wakipongezana kwa kupeana cheti.
Maharusi wakitoka kanisani.
Picha ya pamoja.
Pongezi.
Salamu za hapa na pale.
Wazazi wakiwapongeza watoto wao.

MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA AWATAKA VIJANA KUWA MFANO KATIKA NCHI ZAO

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez akizungumza katika mkutano wa Baraza Kivuli la Umoja wa Mataifa kuhusu  Vijana kutoka nchi nane Afrika uliofungwa jana kwenye makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha .
Mratibu wa Kongamano hilo Marx Chocha akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
Vijana wakisikiliza kwa makini mada mijadala iliyokua inatolewa.
Ushiriki wa vijana wa kike ulipewa umuhimu wa kipekee katika mkutano huo na walionesha uwezo wao katika kujadili masuala mbalimbali yakiwemo ajira ,usalama na amani na mabadiliko ya tabia nchi.
Mshiriki kutoka Zanzibar,Asma Omar  akifatilia kwa makini.
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UN)Hoyce Temu
Mshiriki kutoka Zanzibar,Asma Omar  akipokea zawadi yake baada ya kuibuka mshindi katika kusambaza habari za mkutano kwa njia ya mitandao
Mshiriki kutoka jijini Dar es Salaam,Lilian Kimani akipokea cheti chake baada ya kutambuliwa kufanya vizuri kama mkuu wa Itifaki kwenye mkutano huo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez akimkabidhi mmoja wa vijana cheti cha kutambua mchango wake .
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez akimkabidhi mmoja wa vijana cheti cha kutambua mchango wake .
Vijana wakiwa wamechangamka kwenye mkutano wa Baraza Kivuli la Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez(katikati)akiwa na washindi  waliofanya vizuri katika matumizi ya mitandao.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka nje ya nchi waliohudhuria mkutano huo.
Spika wa Bunge la Muungano mstaafu,Mzee Pius Msekwa na mke wake,Mama Anna Abdallah .

Angalia Kipindi Chote Cha ‘ Football Family’ Kilichorushwa TBC1

Waziri Mwijage kufungua maenesho ya Tanga Trad Fair

indexNa Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Mhe.Charles. Mwijage anatarajia kufungua maonesho ya kibiashara ya Tanga (Tanga Trade Fair) kesho katika viwanja vya Chalinze vilivyoko Kijiji cha Mwahako, Mkoa wa Tanga.
Hayo yamesemwa leo  na Mwanakamati wa Maonesho hayo, Aisha Salim alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii  ambapo amesema kuwa maonesho hayo ya kibiashara ni fursa kwa wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali kuonyesha na kuuza  bidhaa zao  pamoja na kupata elimu.
“Maonesho haya ni ya kibiashara yanayojumuisha wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka ndani na nje ya nchi kwahiyo, ni fursa kubwa kwao kuonyesha na kuuza bidhaa zao pamoja na kupata elimu kutoka kwa wenzao wa nchi zingine zitakazoshiriki kama  Syria, Kenya na Uganda”,alisema Aisha.
Aisha  aliongeza kuwa sio tu wafanyabiashara na wajasiariamali peke yao bali kuna baadhi ya Wizara, Mamlaka, Taasisi pamoja na Mifuko ya Kijamii ambazo wanashiriki katika maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wafanyanyabiashara hao, baadhi ya washiriki hao ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za Fedha, Mamlaka ya Bandari pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Alitoa rai kwa wakazi wa mkoani Tanga kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili kuwaunga mkono wafanyabiashara hao kwani wana vitu ambavyo ni imara na vizuri pia wataweza kujifunza vitu mbalimbali ambavyo hawavijui au hawajawahi kuviona.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Luhende Singu amesema kuwa wamefurahi kuwa miongoni mwa washiriki katika maonesho hayo ambayo yatawasaidia wao kutoa elimu kwa wanachama wao pia watatoa bure baadhi ya huduma za vipimo kwa wakazi wa Tanga.
“Tutatoa elimu kwa umma kuhusu huduma za NHIF, elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na kupima shinikizo la damu, kiwango cha sukari kwenye damu na uwiano wa uzito na urefu, pamoja na kutoa ushauri wa kidaktari,huduma hizi zinatolewa bure zikiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuepukana na maradhi yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vingi”,alisema Singu.
Kwa upande wake Afisa Uanachama wa Mfuko huo, Miraji Kisile  ameeleza kuwa muitikio wa watu huenda ukawa mdogo kwa kuwa  maonesho hayo yanafanyika pembezoni mwa mji ambapo ni mbali na mjini kwahiyo ni changamoto kwa wakazi wa Mkoa huo kuja kwa wingi kwenye maonesho hayo,hivyo amewashauri waandaji wa maonesho hayo kuyasogeza karibu na watu wengi ili mwitikio uwe mkubwa.
Maonesho hayo yalianza mwaka 2013 na yanafanyika kila mwaka mkoani humo,yatafanyika kwa siku kumi kuanzia Mei 28 hadi Juni 6 mwaka huu yakijumuisha wafanyabiashara mbalimbali wakiwa na biashara za vipodozi,vifaa vya ujenzi,vitu vya asili,vyakula, samani za nyumba na maofisi  pamoja na maonesho ya wanyama.

Serikali yawatoa hofu Watanzania kuhusu upatikanaji mafuta ya ndege.

muh1 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
muh2 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
muh3 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaamWaziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam
muh4 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam eneo yalipo matanki ya mafuta ya kampuni ya GAPCO ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
muh6Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni wa Kampuni ya Oryx Energies Godifrey Fernandes akimuonesha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo baadhi ya maeneo yanapohifadhiwa mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam.
muh7 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (wa pili mtasari wa kwanza kulia) akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta eneo la “Deport” ya PUMA wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta katika leo jijini Dar es salaam.
muh8 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya madereva wanaosafirisha mafuta ndani na nje ya nchi leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Serikali imewatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania na abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini kwamba mafuta ya ndege yapo ya kutosheleza matumizi kwa muda wa siku 14 wakati shehena nyingine za mafuta hayo zinaendelea kuingia nchini.
Hayo yamesememwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alipofanya ziara leo jijini Dar es salaam kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege nchini baada ya kugundua baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
“Mafuta ya ndege yapo na ndege zitaendelea kufanya safari kama ratiba zao zilivyopangwa na Watanzania msiwe na wasiwasi, tumejiridhisha, mafuta yanatosheleza kwa muda wa siku 14 wakati hatua ya shehena nyingine kuingia nchini zinaendelea” alisema Prof. Muhongo.
Ziara hiyo ya Waziri Prof. Muhongo inafuatia kugundulika kwa mafuta ya ndege yaliyoingizwa nchini mapema mwezi Mei mwaka huu, ambayo hayafai kwa matumizi yaliyokusudiwa kutokana na kuchanganywa na mafuta ya petroli.
Aidha, Prof. Muhongo ameitaka kampuni ya Sahara Energy Resources yenye makao yake makuu nchini Nigeria ambayo ndio ilioingiza mafuta hayo nchini, kusimamisha shughuli zake mara moja hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Imeonekana si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuingiza mafuta machafu nchini, hatua iliyomfanya Waziri huyo kuchukua msimamo huo wa Serikali hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Akizungumzia hatua hiyo na hali ya mafuta nchini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uingizaji Mafuta kwa Pamoja nchini, Michael Mjinja amesema kuwa mafuta ya ndege yapo na yanatosheleza kwa wiki mbili kuanzia sasa.
Mjinja aliongeza kuwa wanakuhakikisha uhaba wa mafuta hayo hautokei tena nchini ambapo wanaendelea kushirikiana na kampuni ya Total na SP Rwanda ambazo hadi sasa ndio zenye mafuta safi yanayokubalika kwa matumizi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIPER iliyoko eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam, Stephane Gay amesema kuwa kampuni yake ina nafasi ya kutosha ya kuyahifadhi mafuta yote ambayo hayastahili kutumika ili matanki na mitambo ya kampuni zote zilizopata mafuta hayo yafanyiwe usafi upya tayari kwa kuweka mafuta safi yanayoingia nchini.
Ziara ya Waziri Prof. Muhongo imehusisha kutembelea matanki ya kampuni tano za mafuta ikiwemo Puma, GAPCO, Oil Com, TIPER pamoja na Kampuni ya Oryx Energies.

SERIKALI YATANGAZA KUISAFISHA SEKTA YA ELIMU NA WATUMISHI WA UMMA WENYE VYETI BANDIA.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
 ………………………………………………………………………………………..
Na.Aron Msigwa – DODOMA.
 
Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa kampeni ya
kuwashughulikia na kuwaondoa katika utumishi wa umma watumishi wote
walioajiriwa katika  sekta hiyo  wakitumia vyeti bandia .
Aidha, imewataka watumishi hao waanze kujitathmini na kuanza kujiondoa wenyewe kabla ya kufikiwa na  mabadiliko makubwa ya kusafisha sekta ya elimu na utumishi wa umma
yanayokuja nchini. 
 
Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa
Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako wakati wa majumuisho
ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kufanya
mabadiliko makubwa katika Sekta ya Elimu nchini ili kuhakikisha kuwa Elimu
inayotolewa katika shule, vyuo na taasisi mbalimbali inazalisha wahitimu wenye
sifa na ubora kwa maslahi ya Taifa .
Amesema katika kulitimiza hilo Serikali itawachukulia hatua
kali za kinidhamu na kisheria watendaji wote walioshiriki na wale wanaoendelea
kushiriki kwa namna moja au nyingine kukwamisha maendeleo ya elimu nchini ikiwa
ni pamoja na wale waliohusika katika udahili wa wanafunzi wasio na sifa katika
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Songea.
“Serikali ya awamu ya tano imedhamilia kwa

SERIKALI YAAHIDI KUVIPATIA MAJI VIJIJI VINAVYOZUNGUKA BOMBA KUU LA MAJI LA ZIWA VICTORIA NA MAENEO YA PEMBEZONI MWA TANZANIA.

1 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
……………………………………………………………………………………………
Na.Aron Msigwa- MAELEZO.
 Serikali imesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 itatekeleza mradi wa maji katika vijiji 100 vilivyo pembezoni mwa bomba kuu la maji linalotoka ziwa Victoria hadi Kahama na Shinyanga ili kuwawezesha wanachi wanaoishi katika vijiji hivyo kupata huduma ya maji safi na salama.
Akizungumza Bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa mradi wa kuvipatia maji vijiji hivyo utakwenda sambamba na uboreshaji wa huduma ya maji kwenye vijiji 40 vilivyotambulika katika Halmashauri za Misungwi, Kwimba, Shinyanga na Msalala.
Amesema kazi ya kupima na kufanya usanifu wa miradi katika katika vijiji hivyo vya Halmashauri ya Msalala na Shinyanga imeanza na gharama yake imekadiriwa kufikia shilingi bilioni 2.59 huku akiongeza kuwa hadi machi, 2016 ujenzi wa miradi ya maji umekamilika katika vijiji 11 vya Halmashauri hiyo.
Mhe.Lwenge amesema katika mwaka wa bajeti 2016/2017 Wizara yake itakamilisha ujenzi a miradi ya maji katika Halmashauri za wilaya za msalala na Shinyanga na kuanza Usanifu wa miradi hiyo kwenye Halmashauri za Kwimba na Misungwi  ambapo kiasi cha shilingi milioni 760.67 kimetengwa kwa kazi hiyo.
Amevitaja baadhi ya vijiji ambavyo sasa wananchi wake wanapata maji safi na salama kufuatia kukamilika kwa miradi hiyo kuwa ni Nyashimbi, Magobeko, Kakulu, Butegwa, Ngihomango, Jimodoli, Kadoto,Lyabusalu ,Mwajiji Ichongo na Bukamna.
Katika hatua nyingine Mhe.Lwenge amesema Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kushirikiana na Serikali ya Ubelgiji itatekeleza mradi mkubwa wa maji utakakaowawezesha wananchi Laki mbili (200,000) wa Halmashauri zote za mkoa wa Kigoma kupata maji safi na salama.
Amesema mradi huo unatarajia kugharamia kiasi cha Euro milioni 8.8 ambapo kati ya fedha hizo Euro milioni 8 zitatolewa na Serikali ya Ubelgiji na fedha iliyobaki itatolewa na Serikali ya Tanzania.
Ameongeza kuwa vijiji 26 vya kipaumbele vya mkoa wa Kigoma vimeainishwa kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi  na kuongeza kuwa wizara yake tayari imeshatenga kiasi cha shilingi bilioni 5.28 zote zikiwa ni fedha za nje  kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Pia amesema Serikali katika mwaka wa 2016/2017 wa fedha imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1 kufanyia ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya maji ili kuzipatia maji kata saba za wilaya ya Masasi zenye idadi ya watu  84,082.
Aidha, amesema katika mwaka huo wa fedha serikali itatekeleza mradi wa kutoa maji mto Ruvuma kuyapeleka Mtwara –Mikindani pamoja na vijiji 26 vitakavyopatikana kilometa 12 kutoka eneo la bomba kuu.
Mradi huo utatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya China kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 189.9 ambapo kazi ya ujenzi wa chanzo kutoka mto Ruvuma , Chujio la kutibu maji , nyumba ya kusukuma maji , matanki 26, tanki kuu la ujazo wa lita milioni 30 litakalojengwa eneo la maghamba.
Aidha, vituo vya kuchotea maji 234 na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali kilometa 63 yatajengwa ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 9 hadi lita milioni 120 kwa siku ili kutosheleza mahitaji ya watu na viwanda mbalimbali vinavyojengwa vikiwemo vya Saruji na Gesi.

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA AITEMBELEA TIMU YA TAIFA MAZ

di1Kipa wa timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, Deogratius Munishi maarufu kwa jina la Dida, akifanya mazoezi ya kuzuia penalti kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi.  Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).
di2 
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, kikikifanya dua kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).
di3Mshambuliaji Elius Maguri na Kiungo Hassan Kabunda wakipumzika katika mazoezi hayo.
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, kikikifanya dua kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars  ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. (Picha na Alfred Lucas wa TFF).
di5 
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Haule akipiga picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya soka ya Tanzania baada ya kuzungumza nao na kuwatoa hofu ya maisha na usalama wakiwa Nairobi, Kenya. Taifa Stars ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)

CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA BUNGE CHAPATA MWENYEKITI MPYA

BN1Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dodoma Bw. Mchenya John akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge (hawapo pichani) kabla ya Uchaguzi wa Viongozi wa TUGHE tawi la Bunge uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi hiyo Bibi. Emma Lyimo.
BN2Mwenyekiti  aliyemaliza muda wake kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge Bw. Abdallah Hancha (wa kwanza kulia) akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wenzie wa Ofisi ya Bunge kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa TUGHE uliofanyika mapema wiki hii Mkoani Dodoma. Walioambatana naye ni wajumbe wa Kamati Kuu ya TUGHE tawi la Bunge.
BN3 
Wasaidizi wa kamati ya Uchaguzi wakihesabu kura wakati wa Uchaguzi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge uliofanyika mapema wiki hii kwenye Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma.
BN4Mwenyekiti mpya wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Bunge Bw. Chacha Nyakega akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi  wa uchaguzi wa TUGHE uliofanyika mapema wiki hii kwenye Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma.
PICHA ZOTE NA FATMA SALUM-MAELEZO

Vijana wahinizwa kudumisha uzalendo

index 
Na Lorietha Laurence
Vijana wamehimizwa kuendeleza upendo na uzalendo katika kutambulisha Taifa la Tanzania  ikiwemo kutangaza utamaduni wake kwa mataifa mengine  Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.  
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utamaduni  wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi, Lilian Beleko jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za kuzindua klabu za  Vijana  ya Mwalimu Nyerere  chini ya usimamizi wa Taasisi ya Ariseamka Afrika ikiwa na lengo la kuwapatia vijana elimu ya msingi kuhusu historia ya ukombozi wa bara la Afrika  na masuala mbalimbali ya kijamii.
“Klabu ni jambo jema na zuri kwa vijana wa sasa ukizingatia wengi wao hawakuwepo wakati ukombozi wa bara la Afrika hivyo kupitia klabu hizi mtajifunza mengi” alisema Bi.Beleko.
Aidha aliongeza kuwa viongozi wa Afrika walijitolea kwa moyo mmoja kuonyesha uzalendo kwa kuwaunganisha waafrika  katika kupigania uhuru wa bara la hilo ili kuwakomboa kutoka mikononi mwa wakoloni na kuweza kujitegemee kwa kuwa na viongozi wake.
Naye Mwanzilishi wa Taasisi ya Ariseamka Afrika Bi Kulthum Maabad ameleza kuwa ili vijana waweze kujikomboa kutoka katika umaskini ni muhimu kwanza kujikomboa kifikra  kwa kupata elimu muhimu ikiwemo ya uzalendo wa kuitumikia nchi zao kwa uaminifu.
Kwa upande wake  Msaidizi Maalum wa mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere nchini ameeleza kuwa kuna umuhimu wa kujifunza na kuujua mchango mkubwa uliofanywa na Mwalimu Nyerere katika ukombozi wa bara la Afrika kwa kusoma vitabu vyake na kupitia nukuu zake
Uzinduzi wa klabu za Vijana ya Mwalimu Nyerere umeenda sanjari na kilele cha maadhimisho ya wiki ya ukombozi wa afrika ambapo hukumbukwa kwa kuwaenzi waasisi wa upigania uhuru kwa kuwepo kwa maonyesho mbalimbali ya Sanaa,Lugha na Utamaduni.

TANCDA YAPIMA AFYA ZA WABUNGE DODOMA

 Mbunge wa Viti Maalum, Bupe Mwakang’ata (CCM) Mkoa wa Rukwa, akipimwa mapigo ya moyo wakati wa programu maalumu ya wabunge kupimwa afya zao. Programu hiyo ilifanywa bure na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza katika Zahanati ya Bunge, Dodoma leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Leonidas Gama akipimwa afya na Muuguzi Asha Shao bungeni Dodoma
 Mbunge wa Viti Maalum, Joyce Sokombi akipimwa afaya na Muuguzi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Asha Shao. Katikati ni muuguzi mwingine Christina Chamwela
 Mhudumu wa Afya wa Hospitali ya Dodoma akimpima kimo Mbunge
 Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Costantine Kanyasu akipimwa mapigo ya moyo
 Mbunge Kanyasu akipimwa kimo
 Mbunge wa Jimbo la Nachingwe, Hassan Masala akipimwa kimo
 Mbunge wa Jimbo la Makambaku, Deo Sanga akipimwa afya
Baadhi ya wabunge wakipata ushauri nasaha

SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA LAMSHUKURU RAIS WA TFF,JAMAL MALINZI KWA MCHANGO WA TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA OLYIMPIC.


LUHAGA MPINA ASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA UDOM

luh1 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira,Luhaga  Mpina akishirika kufanya usafi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udom wakati usfi wa mazingira kitaifa iliyofanyika, Dodoma jana
luh2 
Luaga Mpina akiongozana  na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM wakati wa siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa iliyofanyika eneo la Chuo hicho jana
luh3 
Luaga Mpina akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDOM wakati siku ya usafi wa Mazingira Kitaifa iliyofanyika eneo la Chuo hicho jana

TAWLA yawataka wanawake kushiriki shughuli za kiuchumi ili kundoa utegemezi

1Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Ms. Aisha Zumo Bade akisoma hotuba yake waakati wa wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama hicho unaofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam leo.   6
Mtoa Mada Agustus  Emmanuel Fungo akiwasilisha mada ya masuala ya kiuchumi kwa wanasheria wa Chama cha wanasheria wanawake TAWLA wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika Hyyat Regency jijini Dar es salaam leo.
7
Mtoa Mada Dr. Elie Waminian Akizungumza wakati akitoa mada wanawake kujiamini katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kutokuwa wavivu.
8
Baadhi ya wanasheria wanawake walioshiriki katika mkutano huo wakifurahia mada zilizokuwa zikitolewa.
9Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Wanasheria wanawake Tike Mwambipile akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano hu.
2
Baadhi ya majaji na wanasheria wakishiriki katika mkutano huo.
3 4 
Baadhi ya wanasheria wa kutoka TAWLA wakiwa katika mkutano huo.
5……………………………………………………………………………………………………………………..
Na Jonas Kamaleki- MAELEZO
Wanawake wametakiwa kushiriki shughuli za kiuchumi ili kujikomboa na kukandamizwa na mifumo ya kijamii iliyopo sasa nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA), Bi Tike Mwambipile leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa chama hicho.
Bi Mwambipile amesema kuwa wanawake wa Kitanzania wananyanyasisika sana kwani hawana vipato vya kutosha, hivyo inabidi waongeze juhudi katika kuibua na kubuni miradi endelevu ya ujasiriamali ili kukuza vipato vyao.
“Wanawake mnapaswa kujiunga na VICOBA na Saccos ili muweze kupata mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kufanyia biashara,”alisema Bi Mwambipile akiongeza kuwa kipato kinachopatikana inabidi wanawake wawe na maamuzi ya kukitumia bila kusubiria maelekezo ya waume zao.
Naye Mwenyekiti wa TAWLA, Bi Asia Bade amesema kuwa wakati umefika kwa wanawake kujitambua kuwa ni sehemu muhimu katika jamii hivyo kutumia uwezo wao kujikwamua kiuchumi pasipo kutegemea wanaume.
Bi Bade ameongeza kuwa suala la ushirikishwaji wa wanawake katika shughuli za kiuchumi litawakomboa na utumwa wa kipato ambao umewatesa kwa kipindi kirefu.
Kwa upande wake mjumbe wa Mkutano huo, Dkt. Pindi Chana ameishauri Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuweka sharti la mkakati wa kuwainua wanawake na vijana kwenye mabenki yanayoomba usajili. Ameongeza kuwa bila kuonyesha makakati huo, BOT isitoe kibali kwa benki yoyote.
Dkt. Chana ameonyesha kukerwa na riba za mikopo kuwa juu sana kwa wakopaji na kusema, “Watanzania tunayafanyia mabenki kazi kutokana na riba kubwa wanazotuwekea kwenye mikopo, hii haitunufaishi bali inatutesa katika kurejesha.”
Akionyesha kukerwa na utegemezi wa wanawake, Mjumbe wa Mkutano huo, wakili Mary Kessy amesema ni wakati wa wanawake kuacha kubweteka wakisubiri kupokea kutoka kwa waume zao bali wachangamkie fursa zilizopo ili wawe na kipato cha uhakika.
Bi Kessy amesema kwamba kuna fursa nyingi za kuwainua wanawake kiuchumi ambazo ni pamoja na ushiriki katika shughuli za madini, kilimo, mifugo na uvuvi pia kutumia mabenki ya wanawake.
“Huu sio wakati wa kuchagua kazi, wanawake tujitume, fursa ziko nyingi sana hapaTanzania, kama ni kwenye migodi tuwemo, biashara za kimataifa tufanye na kwenye nafasi za uongozi tujitokeze badala ya kulalamika” amesisitiza Bi Kessy.
Huu ni Mkutano wa 25 ambao unawajumuisha wanawake wanasheria nchini kuweza kubainisha namna ya ushiriki katika shughuli za kiuchumi na kuweka mikakati ya kutoa elimu endelevu ya uzalishaji mali.

REKODI YA SERENGETI YAIVUTIA KENYA

Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyorejea nchini kutoka ziara ya India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016), imerudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Serengeti Boys imecheza mfululizo michezo 7 ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Kore, Malaysia, na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Mratibu wa timu ta Tanzania kutoka Shirikisho la Soka la Kenya, Anthony Achia, amesema walikuwa wanafuatilia michuano hiyo na mafanikio ya Serengeti. “Timu imefanya vema, ikitunza hii inaweza kuitoa Afrika Mashariki kimasomaso. Unajua sisi sote ni wa East Africa (wa Afrika Mashariki). Sasa ukiona mwezako anafanya vema, lazima useme. Endeleeni. Itakuja kuirithi hii”
Katika mashindano ya AIFF, timu hiyo pekee kutoka Afrika na ambayo ilikua kipenzi cha mashabiki katika jiji la Goha ilicheza na timu ambazo ziko juu katika hatua za juu katika mtoano wa kuwania kushiriki Kombe la Dunia kupitia mabara yao yaani CONCACAF (USA) na AFC (India, Korea na Malaysia). Haishangazi nchi nyingi za Ulaya, Asia na Marekani zimeulizia uwezekano wa timu hii kutembelea nchi zao kwa michezo ya kirafiki.
Awali timu ya Serengeti Boys ilipewa nafasi ndogo ya kufanya vizuri kwa sababu ya rekodi zilizokuwa zinaiweka Tanzania katika viwango vya chini katika umri huo kwa nchi za Afrika Magharibi na Kaskazini zilikuwa juu zaidi na vilevile ukweli wa kwamba timu kama USA, Korea, Malasyia na India zilikuwa na bajeti kubwa iliyogharamiwa na Serikali zao na walikuwa na vifaa vya kila namna kiasi cha kuomba magari kwa ajili ya vifaa vya mazoezi na mechi.
Kikosi cha Serengeti kinavunja kambi kabla ya kurejea siku si nyingi ili kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Afrika chini ya miaka 17 (Madagascar 2017) dhidi ya Ushelisheli hapa tarehe 25 Juni katika uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Benchi la ufundi limeahidi kuendelea kukiimarisha kikosi hiki na vilevile kutengeneza mpango endelevu wa kuwa na wachezaji bora zaidi kila mwaka.
Serengeti Boys ilimaliza Mashindano ya AIFF katika nafasi ya tatu kwa kuifunga Malaysia mabao 3-0.
Serengeti Boys na Bingwa Korea hawakupoteza mchezo hata mmoja na awali walipokutana walitoka sare ya 2-2.

No comments:

Post a Comment