Mkuu
wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akishuhudia
mabati yaliyotolewa ma Mfuko wa Pensheni LAPF kwa ajili ya ujenzi wa
madarasa wilayani Geita ikiwa jitihada za Mfuko wa LAPF kuunga mkono
jitihada za Serikali kutoa elimu bure. Jumla ya mabati 300 yenye thamani
ya Shs. 7,000,000/= yalikabidhiwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akikagua mabati
yaliyokabidhiwa kama msaada na mfuko wa Pensheni wa LAPF wilayani Geita,
kulia ni Meneja Masoko wa Mfuko wa LAPF Bw. James Mlowe wengine ni
maofisa kutoka wilaya ya Geita.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita akitoa neno la shukrani kwa Mfuko wa Pensheni LAPF kwa
msaada wa mabati 300 yanayotosheleza kuezeka vyumba sita (6) vya
madarasa yanayoweza kuchukua wanafunzi 45 kwa kila chumba na hivyo
kupunguza tatizo la ukosefu wa mazingira bora ya kufundishia.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akiteta jambo na
Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni LAPF pamoja na mbalimbali wa Wilaya
ya Geita mara baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati kwa ajili ya
ujenzi wa vyumba vya madarasa.
PICHA NA MPIGA PICHA WETU
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Ndugu Amon
Mpanju wakati Naibu Mpanjo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu
Dar es salaam leo March 31, 2016.(Picha na OMR)
SERIKALI KUPITIA UPYA MIKATABA YA TRL
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati)
akimsikiliza mmoja wa abiria anayetumia usafiri wa reli ya kati mkoani
Kigoma. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe na Kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Saveli Maketta.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza
na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kapteni wa Meli ya MV Liemba ya
namna inavyoendeshwa, mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu
kulia), akipata ufafanuzi wa namna ya injini za Meli ya MV Liemba
zinavyofanya kazi wakati alipotembelea Meli hiyo mkoani Kigoma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mwenye
kizibao cha njano), akimsikiliza Kapteni Winton Mwassa (wa kwanza
kulia), kutoka Kampuni ya huduma za meli mkoani Kigoma mara baada ya
kutembelea na kuona hali ya MV Liemba.
……………………………………………………………………
Serikali imeliagiza Shirika la
Reli Tanzania (TRL), kupitia upya mikataba ya ununuzi wa vichwa vya
treni na mabehewa ili kubaini kasoro zilizojitokeza na kuchukua hatua
stahiki kabla ya maboresho ya reli ya Tanga-Moshi-Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma
wakati akikagua miundombinu ya reli na kusissitiza nia ya serikali
kufufua reli ya kanda ya kaskazini ili kuimarisha huduma ya uchukuzi
katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
“Kama Serikali tumewekeza vya
kutosha katika TRL, hivyo tunawataka mfanye biashara itakayolipa nasi
tutahakikisha popote reli ilipo inatoa huduma iliyokusudiwa na kuchangia
kukuza uchumi wa nchi”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amewataka
wafanyakazi wa TRL kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kupata bidhaa
na abiria wengi wa kuwasafirisha nchini kote.
Amesema Serikali imedhamiria
kuliongezea nguvu TRL ambapo baadhi ya mitambo kutoka Kampuni Hodhi ya
Rasilimali za Reli (RAHCO) itakabidhiwa kwa shirika hilo hivyo kulitaka
kuwa na mpango madhubuti wa kufanya biashara na kurudisha hadhi ya
usafiri wa reli hapa nchini.
“Fanyeni bidii ili mpate mzigo wa
kusafirisha kutoka Tanga kwenda Moshi na Arusha ili kufikia lengo la
kubeba mzigo wa tani milioni moja kwa mwaka”, amesisitiza Waziri Prof.
Mbarawa.
Amezungumzia umuhimu wa TRL
kuafanya kazi kwa karibu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini
(TPA), ili kuongeza kasi ya huduma za uchukuzi nchini, kuongeza fursa za
ajira na kukuza pato la shirika na taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
TRL, Bw. Masanja Kadogosa amesema TRL imejipanga kutafuta masoko ndani
na nje ya nchi ili kuboresha huduma za uchukuzi na kukuza pato lake.
Katika hatua nyingine Prof.
Mbarawa amekagua Meli ya MV Liemba na kuitaka Mamlaka ya Usimamizi wa
usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kuhakikisha meli za MV Liemba
na MV Mwongozo zinakaguliwa na kufanya kazi inavyostahili katika Ziwa la
Tanganyika.
“Tumieni fursa ya kuwa karibu na
nchi za maziwa makuu kufanya biashara ili meli zetu zipate mzigo wa
kutosha na kuongeza mapato kwa taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa ambaye yupo katika
ziara mkoani Kigoma amewataka viongozi na wafanyakazi wa taasisi zilizo
chini ya wizara yake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuibua fursa za
kiuchumi katika ukanda wa magharibi na hivyo kufufua miundombinu
itakayochochea uchumi wa mikoa ya magharibi mwa Tanzania yenye fursa
nyingi za kibiashara.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
TCRA waikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) imeikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi inayokuja
kuwekeza katika huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao
‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali’ (Digital Payment
Services). Leseni hiyo imekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba kwa kampuni ya Agano Safi huku
akiikumbusha kufanya shughuli zake kwa kuzingatia vigezo na masharti ya
leseni.
Akipokea leseni hiyo, Mkurugenzi
wa Kampuni ya Agano Safi Iyaloo Ya Nangolo alisema anaishukuru TCRA kwa
kuwaamini na kuwakambidhi leseni ya kufanya biashara ya mfumo wa malipo
kwa njia ya mtandao, hivyo kampuni hiyo itahakikisha inafanya kazi kwa
ufanisi na kushirikiana na vyombo husika ikiwemo BoT ili kuhakikisha
jamii na taifa linanufaika na shughuli hizo.
Alisema kampuni hiyo inayoundwa
na Wanamibia kwa ushirikiano na baadhi ya Watanzania imejipanga kuja na
teknolojia ya kisasa katika mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao kwa
kushirikiana na kampuni ya malipo ya MobiPay iliyojijengea heshima ya
huduma zake katika nchi za Kusini mwa Afrika huku ikiwa na makao yake
nchini Namibia.
Hafla hiyo ya makabidhiano
imehudhuriwa pia na Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia
Samaria ambaye amepongeza Agano Safi kufanikiwa kufanya biashara hiyo
nchini Tanzania jambo ambalo linaongeza ushirikiano baina ya nchi hizo
huku zikibadilishana teknolojia kwa masuala mbalimbali na ubunifu
kibiashara.
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akizungumza katika hafla ya TCRA kuikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi leo jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya maofisa wa TCRA wakiwa katika hafla hiyo. |
Baadhi ya maofisa wa kampuni ya Agano Safi (kulia) wakiwa na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo. |
Balozi wa Namibia nchini Tanzania, Bi. Theresia Samaria akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa TCRA, Fortunata Mdachi mara baada ya zoezi la kukabidhiana leseni kukamilika. |
No comments:
Post a Comment