Meneja Masoko na Mawasiliano wa
LAPF, James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wao
uliofanyika Milenium Tower jijini Dar es salaam wakati alipoelezea
kuhusiana na mkutano wa mwaka wa wadau wa LAPF unaotarajiwa kufanyika
kwenye ukumbi wa AICC mwezi huu kwa sikU mbili jijini Arusha. Pichani
kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama Bw. Valerian Mablangeti.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia taarifa iliyotolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa
LAPF, James Mlowe wakati akizungumza nao katika ofisi za Shirika hilo
zilizopo Mkumbusho jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama
Bw. Valerian Mablangeti akiwafafanulia jambo waandishi wa habari wakati
wa mkutano huo kulia ni Bw. James Mlowe Meneja Masoko na Mawasiliano wa
LAPF.
………………………………………………………………………………..
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.
Hayo
yalibainishwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF James Mlowe
wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
leo asubuhi kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa
kufanyika Machi 10 na 11 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC
jijini Arusha.
Alisema LAPF imeendelea kupiga hatua kila mwaka ukilinganisha na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii hapa nchini.
”
LAPF imeweza kutoa mikopo ya masomo kwa watu 800 katika maeneo
mbalimbali nchini yenye thamani ya sh.bilioni 1.2 jambo ambalo
tunajivunia” alisema Mlowe.
Akizungumzia
kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian
Mablangeti alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika kwa wadau wa
mfuko huo kupatiwa barua za mualiko.
Alisema
mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene na kuwa
mawaziri wengine wakaoshiriki kwenye mkutano huo ni Waziri wa Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na Naibu Waziri
Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Jafo Selemani .
Alisema
katika mkutano huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atatoa
taarifa ya hesabu za mfuko huo na pia kutakuwa na mada inayohusu afya
kutoka kwa Daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
GAPCO YAWAPA NEEMA WALEMAVU KATIKA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON 2016
Mshindi wa mbio za Kilometa 10 za
Kilimanjaro Marathon 2016, Vosta Peter (30) akishangilia mara baada ya
kumaliza. Mbio hizo za Kilometa 10 zilidhaminiwa na kampuni ya GAPCO na
kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mshindi wa kwanza kwa mbio za
walemavu kilomita 10, Vosta Peter (30) akipokea cheki ya Shilingi
Milioni Moja kutoka kwa kampuni ya GAPCO, wanaomkabidhi ni Meya wa
Manispaa ya Moshi Raymond Mboya (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Gapco Afrika Mashariki, Macharia Irungu (anayepiga makofi toka kushoto)
na Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania, Vijay Nair. Picha na Cathbert
Kajuna wa Kajunason Blog.
OLDUVAI GORGE IS IN TANZANIA
Tanzania Tourist Board (TTB) has
been following up the ongoing discussions on social media following a
video clip being posted on YouTube (https://www.youtube.com/watch?v=iveX49WE7fw)
which has been circulating through various media channels showing a
person claiming that Oldupai Gorge, a site in Tanzania that holds
evidence of the earliest existence of mankind is in Kenya.
This video clip has triggered a
lot of discussions on the different social media among Tanzanians and
other people who have good wishes for Tanzania tourism who know very
well that Oldupai Gorge is in Tanzania and NOT in Kenya.
As a public institution,
responsible for marketing and promotion of Tanzania tourist attractions,
Tanzania Tourist Board is also dismayed by this misleading information
which intends to distort the good work the Board has been doing in
promoting Tanzania tourist attractions including the Oldupai Gorge.
The Board would like to take this
opportunity to strongly refute this statement delivered by the said
person from a neighboring country while addressing one of the sessions
of the International Young Leaders Assembly (IYLA) in USA, August 2015.
We would like to inform the world
that as it is the case for Mt. Kilimanjaro, Serengeti National Park,
Zanzibar to mention just a few, Olduvai Gorge which is referred to as
the Cradle of Mankind, where Dr. Louis and Mary Leakey discovered
important hominid remains of the nutcracker ‘Australopithecus bosel’,
who lived nearly two million years ago, is also in Tanzania and not
elsewhere in the world. It is located in the eastern Serengeti Plains in the Arusha Region and about 45 km, from Laetoli, another important archaeological site of early human occupation. The paleoanthropologist-archeologist team Mary and Louis Leakey
established and developed the excavation and research programs at
Olduvai Gorge which achieved great advances of human knowledge and
world-renown status. Olduvai Gorge is one of the key tourist attractions
for Tanzania.
We call upon Tanzanians and those
with good wishes for Tanzania wherever they are to continue supporting
the effort’s undertaken by TTB in marketing Tanzania and her all tourism
attractions. We believe that it is the role of every single Tanzanian
to promote Tanzania as Africa’s best destination and ask them to join
and support Tanzania Tourist Board in its efforts to promote destination
Tanzania.
We would like to applaud the
reaction made by Tanzanians and non-Tanzanian within and out of
Tanzania, who through this incident were able to stand up as ‘one voice’
and tell the world that OLDUPAI GORGE is INDEED IN TANZANIA!
Issued by:
Public Relations Office
TANZANIA TOURIST BOARD
March 01, 2016
WATANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU KWA HIYARI KUOKOA MAISHA
Makamu wa
Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa
vipimo na mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed
(kulia) wakati wa zoezi la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali
hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia
damu kwa hiyari lilifanyika eneo la Karume jijini Dar es Salaam kwa siku
mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa wiki.
Makamu wa
Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto), akifanyiwa
vipimo na mfanyakazi wa Maabara ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed
(kulia) wakati wa zoezi la kuchangia damu lilioratibiwa na Hospitali
hiyo Kitengo cha Dharura. Zoezi hilo la kuhamasisha wananchi kuchangia
damu kwa hiyari lilifanyika eneo la Karume jijini Dar es Salaam kwa siku
mbili (Alhamisi na Ijumaa) mwishoni mwa wiki.
Mfanyakazi wa
Maabara ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Kibuna Mohammed
(kushoto) akimfanyia vipimo mmoja ya wakazi wa Dar es Salaam
waliojitokeza kwa hiyari wakati wa zoezi la kuchangia damu
lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura
hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Makamu wa
Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na
Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo
baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la
kuchangia damu kwa
hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akizungumza na Afisa Uhisiano wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Muhimbili, Bi. Neema Mwangomo baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya zoezi la kuchangia damu kwa hiari lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura hospitalini hapo katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakifanyiwa
vipimo katika zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha
Dharura cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala
mwishoni mwa wiki.
Mmoja
wa mkazi wa Dar es Salaam akipimwa presha kabla ya kushiriki zoezi la
kujitolea damu kwa hiari wakati wa zoezi la kuchangia damu
lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura cha Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala mwishoni mwa wiki.
Mmoja
wa mkazi wa Dar es Salaam akishiriki zoezi la kujitolea damu kwa hiari
wakati wa zoezi la kuchangia damu lililoendeshwa na Kitengo cha Dharura
cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika eneo la Karume, Ilala
mwishoni mwa wiki.
Shida ya maji jiji la Dar es salaam kuwa historia
Mafundi wakikarabati bomba kuu la kusambaza maji toka Ruvu juu katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani. |
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO AKABIDHI MICHANGO YA TWIGA STARS
Naibu Waziri wa Habari ,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi Mhasibu
wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau
wa michezo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia
timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Fedha hizo zimewekwa
katika Benki ya NMB Bank House akaunti namba “20110001677
inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”.
Naibu Waziri wa Habari ,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimsikiliza Mhasibu
wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya kumkabidhi shilingi milioni
tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka jina lake litajwe
kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars.
Ijumaa ya wiki hii timu hiyo itacheza na Zimbabwe mashindano ya
awali ya kufuzu kombe la Afrika kwa wanawake.
Naibu Waziri wa Habari ,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimweleza jambo
Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya kumkabidhi
shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka
jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa
miguu ya Twiga Stars. Mhasibu Osmund alizipeleka fedha hizo katika
Benki ya NMB Bank House akaunti namba “20110001677 inayojulikana kwa
jina la Twiga Stars Special Fund”.
Picha na Anna Nkinda
Serikali yalitaka Dira ya Mtanzania kukanusha tuhuma dhidi ya Balozi Ombeni Sefue
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Bw.Assah Mwambene (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa za
upotoshaji zilizotolewa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la tarehe
29/02/2016 kuhusu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo Habari, Bw.Jamal Zuberi na
Mkurugenzi Msaidizi Habari Bw.Vicent Tiganya wote kutoka Idara ya Habari
(MAELEZO).
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya
Habari, Bw.Assah Mwambane (ambaye hayupo katika picha) iliyokuwa
ikiutaka uongozi wa Gazeti ya Dira Mtanzania kukanusha habari waliyoitoa
hivi karibuni iliyokuwa na kichwa cha habari “Uchafu wa Ombeni Sefue
Ikulu”.
Na Anitha Jonas – MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………………………
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Bw.Assah Mwambene ameutaka uongozi wa Gazeti la Dira ya
Mtanzania kukanusha haraka na kuiomba radhi Serikali na Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kutokana na taarifa waliyoitoa katika
toleo namba 404 la tarehe 29/02/2016 lenye kichwa cha habari “Uchafu
wa Ombeni Sefue Ikulu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi huyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
kuhusu taarifa kuwa hazikuwa na ukweli wowote kwani Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue hakuhusika katika uteuzi wa Mkurugenzi wa MSD wala
kuhusika na kampuni ya CRJE katika utoaji wa tenda ya kujenga Chuo Kikuu
cha Dodoma Oktoba 2007 kwani katika kipindi hicho alikuwa Balozi wa
Tanzania nchini Marekani.
“Serikali inautaka uongozi wa
Gazeti la Dira ya Mtanzania ukanunushe taarifa hiyo kwa uzito ule
uliyotumika kuchapisha habari hiyo na kama wanapinga wakidai wana
ushahidi basi waupeleke mara moja kwenye vyombo vinavyohusika ikiwemo
Sekretarieti ya Maadili na TAKUKURU”,alisema Bw.Mwambene.
Aidha, Bw.Mwambene amesema
gazeti hilo liliandika kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
alipigia chapuo Kampuni ya “UGG” iliyowahi kuonyesha nia ya kujenga
reli ya Kati nchini. Taaarifa hii pia siyo ya kweli na hakuna kampuni
yenye jina la “UGG” ilishawahi kuonyesha nia ya kujenga reli hiyo.
Mkurugenzi aliendelea kusema kuwa
gazeti hilo lilimtuhumu pia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
kuhusika na kumsafisha Bwana Eliakim Maswi wakati alichokifanya Balozi
Sefue ilikuwa ni kusoma matokeo ya uchunguzi ambao hakuufanya yeye.
Waliomsafisha ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma na Kamati ya Uchunguzi iliyoongozwa na Jaji
wa Mahakama Kuu kwani ndio waliiyofanya uchunguzi huo.
Hata hivyo serikali imewashauri
wamiliki wa vyombo vya habari,wachapishaji,wahariri, na waandishi wa
habari wajikite kwenye weledi na ukweli pia wafanye utafiti wa kina na
kuandika mambo waliyo na uhakika nayo
Wataalamu TPRI wapelekwa Kilombero kufanya uchunguzi
Na Jacquiline Mrisho
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
imewapeleka wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viuwatilifu ya
Kitropiki (TPRI) wilayani Kilombero kufanya uchunguzi wa zao la mpunga
linalosadikiwa kuharibiwa na dawa zilizomwagwa na Kampuni ya Kilombero
Plantation (KPL) inayomiliki mashamba yanayopakana na mashamba ya
wananchi.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa
Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mali Mkoa wa Morogoro Bw. Ernest Mkongo
kuhusu uchunguzi unaoendelea kufanyika katika mashamba ya wananchi ili
kutathmini athari zinazotokana na dawa hizo.
Serikali yawapa motisha wachezaji wa Twiga Stars
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya
Taifa ya mpira wa miguu wanawake “Twiga Stars” wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es
Salaam.Twiga Stars inatarajiwa kucheza mechi na Timu ya Taifa wanawake
ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa tarehe 4 katika uwanjja wa Taifa.
Picha na WHUSM
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza na
wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars”
alipowatembelea kambini kwa leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge na Mjumbe wa Baraza
la Michezo la Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia).
Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Selestine Mwesiga akitoa shukura kwa
Serikali kutokana na jitihada zake za kuitafutia wadhamini Timu ya Taifa
ya Mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakati Naibu Waziri wa Habari,
Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura(wapili kutoka
kushoto) alipo watembelea wachezaji wa Timu hiyo leo jijini Dar es
Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi.
Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia). Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo
Makoye Nkenyenge.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akisalimiana
na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars”
(Nasra Juma) alipowatembelea kambini kwao leo jijini Dar es Salaam.
Katikati ni mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Jeniffer
Mmasi Shang’a.
Mjumbe wa Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a. akisalimiana na Kocha wa Timu ya
Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga Stars” Bibi. Nasra Juma
wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) kambini kwao leo jijini
Dar es Salaam.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKAMILISHA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI TANGA
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan aliangalia vijana wa kikundi cha sanaa cha Tanga kwanza
alipowasili Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuzungumza na
Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016. Makamu wa Rais amekamilisha
ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi
Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan alipokua akizungumza nao katika Ofisi ya CCM Mkoa Tanga. Makamu
wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo
March 01.2016.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akiagana na vijana wa kikundi cha wasanii cha Tanga kwanza
alipokua akiondoka katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa Tanga
baada ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016.
(Picha na OMR)
Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa
CCM Mkoa Tanga Mwanakombo Mwakuru akimvisha Skafu Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kwa
ajili ya kuzungumza na Wanachama wa Chama hicho leo March 01, 2016.
Makamu wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga.
Kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe.Henri Shikifu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akizungumza na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani
Tanga katika Ofisi ya CCM Nkoa Tanga. Makamu wa Rais amekamilisha ziara
ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo March 01,2016.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi
Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan alipokua akizungumza nao katika Ofisi ya CCM Mkoa Tanga. Makamu
wa Rais amekamilisha ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga leo
March 01.2016.
Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi kwa Rais Mstaafu Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha Kaka yake Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kilichotokea leo asubuhi nchini India.
Mzee Selemani Mrisho Kikwete alikuwa nchini India kwa matibabu.
Katika salamu zake Rais Magufuli
amesema amepokea kwa mshituko taarifa za kifo cha Mzee Selemani Mrisho
Kikwete na amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete
kuombeleza kifo cha mtu muhimu kwa familia hiyo.
“Napenda kukupa pole nyingi
wewe Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, familia yenu
yote, ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mtu muhimu katika
familia, natambua uchungu mkubwa mlionao lakini nawaomba muwe uvumilivu
na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu” Alisema Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli amemuombea Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete apumzishwe mahali pema peponi, Amina.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Arusha
01 Machi, 2016
KUZIONA TWIGA, ZIMBABWE ELFU 2000/=
Kiingilio cha chini cha mchezo wa
kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake kati ya timu
ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake ‘Taifa Stars’ dhidi ya timu ya taifa ya
wanawake Zimbambwe kitakua shilingi elfu mbili tu.
Mchezo huo namba 3, unatarajiwa
kuchezwa siku ya Ijumaa saa 10 kamili jioni katika uwanja wa Azam
Complex uliopo Chamazi, huku kiingilio cha juu kikiwa shilingi elfu tatu
kwa jukwaa kuuu.
Waamuzi wa mchezo huo ni Lidya
Tafesse, akisaidiwa na Yehuzewdubizua Yehuw, Tsige Sisay,
Woinshetkassaye Abera kutoka nchini Ethiopia, huku Kamisaa wa mchezo huo
Geneviev Kanjika akitoka Congo DR wote wanatarajiwa kuwasili siku ya
Alhamisi mchana kwa shirika la ndege la Kenya (KQ).
Wakati huo huo kikosi cha Twiga
Stars kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo wa siku ya Ijumaa,
huku kocha mkuu wa timu hiyo Nasra Juma akisema vijana wake wote wapo
katika hali nzuri na tayari kuwakabili Wazimbambwe.
Aidha Kocha Nasra amewaomba wadau
wa mpira wa miguu nchini na watanzania wote kwa ujumla, kujitokeza
uwanjani siku ya Ijumaa kuja kuwapa sapoti katika mchezo huo, ambapo
watakua wakiwakilisha na kupeperusha bendera ya Tanzania.
JAFO AMUAGIZA MKURUGENZI WA KISARAWE KUMTAFUTIA KAZI NYINGINE MENJEJA WA MAMLAKA YA BODI YA MAJI
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE PWANI
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais
Tamisemi Utumishi na Utawala bora, Seleman Jafo amemuagiza Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kumtafutia kazi nyingine meneja wa
Mamlaka ya Bodi ya Maji Kisarawe Listern Materu kutokana na kushindwa
kutatua kero ya maji kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment