Na Waandishi wa NEC, Mbeya
Serikali imeombwa kuzifadhili
Asasi za kiraia zinazotoa Elimu ya Mpiga kura ili ziweze kuwaelimisha
wananchi kwa wakati umuhimu wa kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa Rais,
Wabunge na Madiwani.
Katika Uchaguzi Mkuu uliopita
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa vibali vya kutoa Elimu ya Mpiga kura
kwa Asasi za kiraia 447 kutoka maeneo mbalimbali nchini lakini ni asasi
chache zilizofanikiwa kupata fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya
kutoa elimu hiyo.
Wakizungumza kwenye Mkutano wa
tathmini ya Elimu ya Mpiga Kura kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na
Asasi za Kiraia uliofanyika leo jijini Mbeya, wawakilishi wa Asasi hizo
walisema Elimu ya Mpiga Kura inapaswa kutolewa mapema kwani katika
Uchaguzi Mkuu uliopita asasi zilipata fedha kipindi kifupi kabla ya
kufanyika Uchaguzi Mkuu.
Walisema kutokana na Asasi nyingi
kutokupata fedha kutoka kwa wafadhili, Elimu ya Mpiga Kura haikuweza
kuwafikia wananchi wengi zaidi na hivyo kusababisha baadhi ya wananchi
wengi kutojitokeza kupiga kura na kura nyingi kuharibika.
Aidha, wajumbe hao pia wameitaka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia na kuratibu Elimu ya Mpiga Kura ili
iwe endelevu badala ya kusubiri kutoa Elimu hiyo katika kipindi cha
Uchaguzi Mkuu pekee.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi wa
jiji la Mbeya Dkt. Samwel Lazaro amezitaka Asasi za kiraia kuhakikisha
zinatoa elimu hiyo mpaka kwenye maeneo ya vijijini ambapo wananchi
hawapati taarifa za kutosha ukilinganisha na maeneo ya mijini.
Alisema Elimu hiyo ikitolewa kwa
ufasaha itasaidia kupunguza idadi ya kura zinazoharibika na kuongeza
idadi ya wananchi wanaojitokeza kupiga kura wakati wa uchaguzi Mkuu.
Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka
2015, jumla ya wananchi milioni 22,658,247 waliandikishwa kwenye
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo kati ya hao, 15,596,110 sawa na
asilimia 67 waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura. Kura
zilizoharibika au kukataliwa zilikuwa ni 402,248 sawa na asilimia 2.5.
Mkutano wa Tathmini ya Elimu ya
Mpiga Kura kati ya Tume na Asasi za Kiraia ulizishirikisha Asasi za
kiraia zaidi ya 15 kutoka mikoa mitatu ya Mbeya, Rukwa na Katavi
zilizopewa kibali na Tume ili kutoa elimu ya mpiga kura katika uchaguzi
mkuu wa mwaka 2015.
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AWATEMBELEA WAHADZABE NA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA JAMII HIYO
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akipozi kwa picha na Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe
Chifu Edward Mashimba kushoto na Mama Sara Philipo mwenye nyumba hiyo
wakati alipozungumza na chifu huyo leo, Katika ziara hiyo Kinana katika
kijiji cha Kibampa na kukagua miradi mbalimbali ya jamii hiyo ya
Kihadzabe ikiwemo maji, mabweni ya watoto wa jamii hiyo pamoja na
zahanati iliyopo katika kijiji cha Munguli kata ya Mwangeza wilaya ya
Mkalama mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Ndugu
Parseko Kone amewajengea mabweni na kuwawekea mradi wa maji, Umeme na
kuwafundisha kilimo cha mihogo na mazao mengine ili kuweza kujikimu kwa
chakula kwani jamii ya kabila hilo inakula nyama, mizizi ya miti na
asali.
Lakini pia vijana hamsini wa
Kabila hilo wamejiunga na jeshi la wananchi kwa mpango mkuu wa mkoa wa
Singida Ndugu Parseko Kone na serikali kwa kuwaendeleza kielimu na
kimaendeleo, kuna vijana wengine sitini wataingizwa jeshini ikiwa ni
mkakati wa kuielimisha jamii hiyo ili kubadili maisha bila kuharibu mila
yao.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MKALAMA -SINGIDA)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe
Chifu Edward Mashimba wakati alipotembelea na kujadiliana naye mawili
matatu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana na Mama Sara Philipo mwenye nyumba hiyo wakitoka nje
mara baada ya Kinana kuzungumza na Chifu Edward Mashimba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward Mashimba
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi hao wa jamii ya Wahadzabe
huku Mwenyekiti wa Jamii ya Wahadzabe Chifu Edward Mashimba akitafsiri
katika kijiji cha Kibampa kata ya Mwangeza.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika
mkutano huo wakimsikiliza Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati
alipokuwa akiwahutubia.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akishiriki katika kazi ya kupanda mbegu ya muhogo na
vijana wa Kihadzabe katika shamba darasa ililopo kijiji cha Kibampa kata
ya Mwangezi ikiwa ni mafunzo ya kilimo kwa jamii hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya jamii hiyo wakati alipokuwa akiwasili kijiji cha Kibampa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza ngoma ya asili ya jamii ya Kihadzabe.
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana ukikatisha misitu na mabonde wakati ukielekea
kata ya Mwangeza kijiji cha Kibampa ambako jamii hiyo inaishi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akisaklimiana na vijana wa kisukuma aliowakuta
wakipalilia shamba, vijana hao walimweleza Kinana kuwa wanahitaji
serikali iwatengenezee barabara yao jambo ambalo litarahisha hata uuzaji
wa mazao yao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa maji katika kijiji cha Munguli
ambao umejengwa maalum kwa ajili ya jamii hiyo anayetoa maelekezo ni
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akikagua mabweni ya watoto wa jamii ya Kihadzabe
yaliyojengwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone katika kijiji
cha Munguli mabweni hayo yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 60 wa kiume
30 na wakiume 30 yamejengwa maalum kwa ajili ya jamii kulia ni Mkuu wa
wilaya ya Mkalama Ndugu Christopher Ngubiagai.
Baadhi ya wananfunzi wa shule hiyo
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya
Munguli Athman Kinyere akisoma taarifa ya shule hiyo kwa Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Hii ni moja ya nyumba zinazotumiwa na jamii hiyo ya Kihadzabe.
Baadhi ya wananchi wa jamii hiyo wakiwa katika mkutano
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akikagua mtambo wa Sola unaoendesha maji katika
mradi wa maji wa kijiji cha Munguli ambao umejengwa maalum kwa ajili ya
jamii hiyo anayetoa
TFF YAONYA UPANGAJI WA MATOKEO
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limewaonya viongozi wa vilabu,
wachezaji, waamuzi na wasimamizi wa mchezo kutojihusisha na upangaji wa
matokeo (Match fixing) katika michezo inayoendelea sasa katika ligi za
ngazi mbalimbali za nchini.
TFF
imejipanga na inasimamia vizuri michezo ya Ligi Kuu (VPL), Daraja la
Kwanza (FDL), Daraja la Pili (SDL) na Azam Sports Federation Cup (ASFC)
inayoendelea na yoyote atakayebainika kujihusisha na mchezo huo wa
upangaji matokeo, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa.
Katika
michezo yote inayoendelea TFF ina maofisa wake wanaofuatilia kwa
ukaribu michezo hiyo, hivyo endapo kiongozi, mchezaji, msimamizi au
mwamuzi atabainika kujihusisha na upangaji wa matokeo hatua kali
zitachukuliwa .
TFF
inawaomba viongozi, wachezaji, wasimamizi wa michezo na waamuzi
kutojihusisha na mchezo huo wa upangaji wa matokeo kwani kufanya hivyo
ni kukiuka katiba, sheria na kanuni zinaongoza mpira wa miguu nchini.
MAGALA 275 KUJENGWA KUDHIBITI UKOSEFU WA CHAKULA NCHINI
Na Raymond Mushumbusi-Dodoma)
……………………………………..
Serikali katika kuongeza na kuimarisha uhakika na usalama wa chakula hapa nchini, Serikali imepanga kujenga maghala 275 kwa awamu katika sehemu zenye uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi ambapo hadi sasa jumla ya maghala 125 yanaendelea kujengwa na kukarabatiwa katika maeneo hayo.
Akifafanua hilo wakati akiharisha shughuli za Mkutano wa Pili wa Bunge la 11 lilikuwa na vikao 9 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema Serikali imejipanga katika kuondoa tatizo la upungufu wa chakula nchini kwa kujenga magala mengi zaidi ya kuhifadhi chakula katika maeneo mbalimbali yenye changamoto za upungufu wa chakula.
Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema hali ya chakula kwa mwaka 2015/2016 katika maeneo mengi ya nchi imeendelea kuwa ya kuridhisha kufuatia mavuno mazuri yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2014/2015 na takwimu za Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi zinaonesha kuwa albaki kutoka msimu uliopita nchi ilikuwa na ziada ya chakula licha ya kuwepo kwa maeneo machache ambayo hayakuwa na chakula.
“Kutokana na uzalishaji wa mazao ya chakula kwa msimu wa 2014/2015 kuwa Tani milioni 15.5 na mahitaji ya chakula kwa mwaka 2015/2016 kuwa Tani milioni 12.9 hivyo nchi imejitosheleza kwa chakula kwa ziada ya Tani milioni 2.5 sawa na asilimia 120 na napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa Serikali itaendelea kuhudumia maeneo yote yenye uhaba wa chakula”
“Ili kukabiliana na hali ya uhaba wa chakula katika maeneo hayo, Serikali inaendelea kutoa chakula katika maeneo hayo ambapo jumla ya Tani 23,871.6 za chakula zilitengwa kwa ajili hiyo na hadi kufikia tarehe 17 Januari, 2016, jumla ya Tani 11,860.8 zilikuwa zimechukuliwa toka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwenda kwenye Halmashauri za Wilaya zenye upungufu wa chakula kwa ajili ya usambazaji pia natoa wito kwa Halmashauri ambazo hazijachukua mgao wao kufanya hivyo mara moja ili Wananchi katika maeneo hayo wasizidi kuathirika” Alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha, Mhe Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema Serikali kwa kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kujenga maghala ya kimkakati kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya Taifa na Kwa sasa ghala moja lenye uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 limeshajengwa Wilayani Mbozi Mkoani Mbeya na Serikali imepata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya Poland ambao utawezesha kujenga vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa kuhifadhi Tani 160,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 90.
Ameongeza kuwa Pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali, amewataka viongozi wa Mikoa, Wilaya na watendaji katika Halmashauri zote Nchini kuwahamasisha Wananchi kutumia vizuri mvua zinazonyesha nchini kote kwa kulima kwa bidii ili kuweza kuvuna na kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha kwa ajili ya kaya zao wakati wote wa mwaka na wawahamasishe wafanyabiashara na wadau wengine kusaidia Serikali kuchukua chakula kutoka maeneo yenye ziada na kupeleka katika maeneo yenye upungufu na kwa kuzingatia maelekezo haya pamoja na juhudi za Serikali zilizooneshwa, tatizo la uhaba wa chakula nchini litapungua, kama siyo kumalizika kabisa.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa,Majaliwa amehairisha Mkutano wa Pili Bunge amehairisha shughuli za Bunge mpaka tarehe 19 mwezi April 2016 saa 3 Asubuhi likaporejea katika Mkutano wa kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017.

UJUMBE KUTOKA CHUO CHA ULINZI WA TAIFA WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA
Kamishna
wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akisalimiana na
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos
Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es
Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi
wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016(kushoto) ni Kamishna wa
Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisalimiana na
Mkufunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa ambaye ni raia kutoka
China(katikati) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia
Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo
hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiongea na Ujumbe
kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani). Ujumbe huo wa Washiriki
wa Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza
hapa nchini.
Wakufunzi
wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati yao
na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo
pichani). Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia
Jenerali, Jairos Mwaseba.
Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo
mafupi kwa Washiriki wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa
walipotembelea Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kwa ziara yao ya
Mafunzo(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna
Mwandamizi wa Magereza, Augustine Mboje.
Baadhi
ya Washiriki wa Mafunzo kutoka chuo cha Ulinzi wa Taifa wakimwangalia
mmoja wa wafungwa ambaye amepatiwa ujuzi gerezani wa kukata vitambaa vya
nguo tayari kwa kushona nguo za wafungwa wliopo magerezani kama
anavyoonekana katika picha katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Jijini
Dar es Salaam.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWASALIMIA WAKAZI WA MOROGORO PAMOJA NA KUKAGUA BARABARA YA MOROGORO-DODOMA ENEO LA KIBAIGWA.
Msafara
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli ukipita katika eneo la Msamvu mjini Morogoro kuelekea Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wakazi wa Msamvu mjini Morogoro wakati akiwa njiani
kuelekea Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wakazi wa Wami dakawa mkoani Morogoro wakati akiwa njiani
kuelekea Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wakazi wa eneo la Magole mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ukarabati
unaondelea katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa .
sehemu ya barabara hiyo inakarabatiwa chini ya usimamizi wa Wakala wa
Barabara nchini TANROADS.
PICHA NA IKULU
DINAH SAMANYI: MIAKA 39 YA CCM, MAKADA WATULIE NDANI YA CHAMA ILI WASIJUTE BAADAE.
…………………………………………………………………………………….
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Ikiwa hii leo ni Maadhimisho ya Miaka 39 tangu kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi CCM, Wanachama wake wametakiwa kutulia ndani ya Chama hicho badala ya kujitoa katika chama jambo ambalo huwafanya baadae kujutia.
Kauli hiyo imetolewa Mkoani Mwanza na Katibu wa Wazazi wa Chama hicho Ndg.Dinah Somba Samanyi, wakati akizungumza na BMG, kuhusiana na maadhimisho ya miaka 39 ya CCM mwaka huu 2016.
Samanyi ametanabaisha kwamba, mwaka huu ikiwa ni miaka 39 tangu CCM kuasisiwa February 05,1977 ikiwa ni baada ya Muungano wa wa vyama viwili vya ASP kutoka Zanzibar na TANU kutoka Tanganyika, ni vyema wanachama wake wakawa waadilifu na kuepukana na tabia zisizo za kimaadili ambazo ni pamoja na kujitoa ndani ya chama hicho kama ambavyo baadhi yao wameshuhudiwa wakifanya jambo ambalo hata hivyo huwafanya baadae kulijutia.
Kuhusu maadhimisho amesema “Chama kimejipanga vizuri katika kuadhimisha Siku hii na tangu kuzinduliwa Kitaifa kwa sherehe za maadhimisho haya kule Zanzibar, kumekuwa na shughuli mbalimbali zinazolenga kuimarisha uhai wa chama pamoja na kushiriki shughuli tofauti tofauti za kijamii”.
Samanyi amebainisha “Katika Mkoani Mwanza kila Wilaya imepewa fursa ya kuandaa shughuli mbalimbali kwa ajili ya maadhimisho haya. Jumuiya mbalimbali ikiwemo Jumuiya ya Wazazi zimeshiriki shughuli tofauti tofauti kama vile kutembelea mashuleni, kufanya usafi wa mazingira pamoja na kutembelea wagonjwa Mahospitalini”.
Nao baadhi ya makada wa vyama vya siasa Mkoani Mwanza wametoa maoni yao kuhusiana na miaka 39 ya CCM kikiwa ni chama kinachoongoza Serikali, ambapo Kada wa CCM Sarah Ramadhan anasema anasema kuwa miaka 39 ya chama hicho, taifa limepiga hatua kubwa kimaendeleo ikilinganishwa na miaka iliyopita huku Amos Joseph ambae ni Kada ya Chadema akisema kuwa miaka 39 ya uongozi wa CCM taifa limeshindwa kutatua changamoto za kimaendeleo ikizingatiwa kwamba maendeleo yaliyopatikana hayaendani na raslimali za asili zilizopo nchini.
Pengine Maoni ya Makada hao ni fursa nyingine ya kuiwezesha CCM kuzidi kuwatumikia vyema Watanzania ili miaka 40 ijayo mwakani kusiwepo na utofauti wa kimtizamo pindi makada wa vyama vya siasa watakapokuwa wakitoa tena maoni yao.
Kitaifa Sherehe za Miaka 39 ya Kuasisiwa Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka huu, zilizinduliwa Visiwani Zanzibar na Dkt.Ali Mohamed Shein ambae ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na kilele chake kinahitimishwa Mjini Singida katika Uwanja wa Namfua ambapo zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

STATEMENT BY UNFPA EXECUTIVE DIRECTOR, DR. BABATUNDE OSOTIMEHIN, ON THE ZIKA VIRUS
UNFPA
will continue to lead efforts to promote widespread information about
the virus and about voluntary family planning. Given reported cases of
Zika virus transmission through sexual contact, the role of UNFPA as the
world’s leading agency on reproductive and maternal health, and the
biggest public sector supplier of family planning commodities, including
condoms, is ever more pertinent.
Women
and girls should be able to make informed decisions about their
reproductive health and family planning methods, and to protect
themselves and their babies if they decide to be pregnant. UNFPA will
continue to work with countries around the world to scale up access to
information and to a wide range of voluntary family planning commodities
so that women can make informed decisions and protect themselves.
Kambi ya Upinzani yatangaza Mawaziri wake
(Na Raymomd Mushumbusi-Dodoma)
…………………………………………..
Kiongozi
wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe Mbunge wa Hai
(CHADEMA) ametangaza rasmi Baraza la Mawaziri vivuli litakalosaidiana na
Serikali katika kuendesha shughuli za kimaendeleo.
Akitangaza
Mawaziri hao vivuli kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani amesema
anawaomba Mawaziri wa Wizara husika kuwapa ushirikiano wale wote
walioteuliwa kuwa Mawaziri vivuli katika Kambi ya Upinzani ili kupeleka
mbele gurudumu la maendeleo nchini.
Waliotangazwa
Katika Orodha hiyo ni Pamoja na Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi,
Utumishi na Utawala Bora Jaffar Michael, Manaibu wake ni Joseph Nkundi
na Ruth Mollel, Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Ali Saleh Abdalla na Naibu wake ni Pauline Gekul, Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu Esther Bulaya na
Manaibu ni Yusuph Makame na Maftah Abdalla, Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi ina mawaziri wawili ambao ni Magdalena Sakaaya na Emmaculate Swari
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Inj. James Mbatia na Naibu
Waziri Willy Kombucha.
Aidha
ameendelea kuwataja Mawaziri wengine kuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango
Halima Mdee na Naibu Waziri ni David Silinde, Waziri wa Nishati na
Madini
John Mnyika na Naibu Waziri ni John Heche, Waziri wa Katiba na Sheria Tundu Lissu na Naibu Waziri Abdalla Mtolela, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Peter Msigwa na Naibu Waziri Riziki Shaghal, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Juma Omari na Naibu Waziri Mwita Waitara, Waziri ya Mambo ya Ndani Godbless Lema na Naibu Waziri Masoud Abdalla, Waziri ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilfred Lwakatare na
Naibu Waziri Salum Mgoso.
Wengine walioteuliwa katika
Baraza kivuli ni Waziri wa Maliasili na Utalii Esther Matiko na Naibu
Waziri Cecilia Pareso, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Anthony
Komu na Naibu Waziri Cecil Mwambe, Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia
na Ufundi Suzan Lyimo Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph, Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel na
Naibu Waziri Zubeda Sakul, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Joseph Mbilinyi na Naibu Waziri Devotha Minja na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Hamidu Hassan na Naibu Waziri Peter Lijualikali.John Mnyika na Naibu Waziri ni John Heche, Waziri wa Katiba na Sheria Tundu Lissu na Naibu Waziri Abdalla Mtolela, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Peter Msigwa na Naibu Waziri Riziki Shaghal, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Juma Omari na Naibu Waziri Mwita Waitara, Waziri ya Mambo ya Ndani Godbless Lema na Naibu Waziri Masoud Abdalla, Waziri ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wilfred Lwakatare na
Naibu Waziri Salum Mgoso.
LIGI KUU YA VODACOM RAUNDI YA 18 WIKIENDI HII
Jumamosi
ligi ya kuu ya Vodacom itaendelea kwa mchezo mmoja tu, ambapo katika
uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, African Sports watawakaribisha Stand
United kutoka mkoani Shinyanga.
Michezo
saba itachezwa siku ya Jumapili ambapo maafande wa JKT Ruvu watakuwa
wenyeji wa Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, na
Ndanda FC watawakaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Nangwanda
Sijaona mjini Mtwara.
Kagera
Sugar watacheza dhidi ya Simba SC katika uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga, Azam FC watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa Chamazi, Majimaji
dhidi ya Mgambo uwanja wa Majimaji mjini Songea na Toto Africans
watawakaribisha Coastal Union uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula kwenye jengo la Utalwala la Bunge
mjini Dodoma Februari 5, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Longido, Onesmo Ole-
Nangole kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Simanjiro , James Ole
Millya (kulia)kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016.
Katikati ni Mbunge wa longido, Onesmo Ole Nangole.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (katikati) na
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Patrobas katambi
(kulia) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwenye
viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
JAJI MKUU WA ZANZIBAR ATANGAZA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA ZANZIBAR
Jaji
Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akizungumza na waandishi wa habari
Ofisini kwake Vuga, Mjini Zanzibar, kuhusiana na maadhimisho ya wiki
ya Sheria Zanzibar iliyoanza tarehe 5 mwezi huu.
PICHA NA ABDALLA OMAR-HABARI MAELEZO ZANZIBAR
MATUKIO KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA
Waziri
wa fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (Kulia) pamoja na Waziri wa
Elimu,Ufundi,Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Joyce Ndalichako wakiwasili
katika ukumbi wa Bunge kushiriki kikao cha 9 cha Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma.
Askari wa Bunge akiweka Siwa katika ukumbi wa Bunge kuashiria kuanza kwa kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson akiongoza kikao cha 9 cha Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji wakatiakitoa Taarifa ya
Utendaji wa Soko la Bima Nchini kwa kipindi cha Mwaka unaoishia tarehe
31 Desemba,2014 wakati wa kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea
Mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu,Ufundi,Sayansi na
Teknolojia Mhe. Prof Joyce Ndalichako akiwasilisha Taarifa ya mwaka ya
chuo Kikuu Cha Dodoma kwa mwaka wa Fedha 2013/2014 katika kikao cha 9
cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiteta
jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Mhe.Dkt Hussein Ali
Mwinyi wakati wa katika kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini
Dodoma.
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
JESHI LA POLISI LIMEJIPANGA KUIMARISHA ULINZI WAKATI WA UPIGAJI KURA KWENYE UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIMBAR.
Na Maanja Mabula –Pemba
…………………………………………………
Kamishna wa Jeshi la Polisi
Zanzibar Hamdan Omar Makame amesema kwamba Jeshi hilo limejipanga
kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya Unguja na Pemba wakati wa
upigaji kura kwenye uchaguzi wa marudio .
Akizungumza na gazeti hili
Kisiwani Pemba Kamishna Hamdan amewatoa hofu wananchi kuwa hakuna
mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura ambaye hataweza kwenda kupiga kura
tarehe 20 machi mwaka huu wakati wa uchaguzi wa marudio kutokana na
sababu za vitisho .
Amesema kwamba tayari Jeshi la
Polisi limeanza kutengeneza mazingira ambayo yatawaweza wananchi kila
mmoja kuwa huru na kuhakikisha kuwa usalama wa nchi utaendelea
kudumishwa .
Katika
mazungumzo na gazaeti hili katika Makao Makuu wa Jeshi hilo Mkoa wa
Kaskazini Pemba , Kamishna Hamdan amefahamisha hakuna mwananchi ambaye
hatapiga kura kutokana na vitisho , labda aache kwa sababu zake mwenyewe
.
“Hakuna
mwananchi ambaye atapata fursa ya kupiga kura kwa sababu za vitisho ,
labda yeye asiende kwa sababu anazozijua yeye , lakini sio suala la
vitisho ulinzi utaimarishwa maeneo yote ya Unguja na Pemba ”alisisitiza
Hamdan .
Aidha
Kamishna Hamdan amesema pamoja na kazi ya ulinzi wa wananchi na mali
zao kuwa ni Polisi , lakini iko haja kwa wananchi nao kuwapa
ushirikiano askari pindi wanapobaini kuwa viasharia vya vitisho au
uvunjifu wa amani .
Ameeleza
kwamba ni kazi ya Jeshi la Polisi kuona wanannchi wanaishi kwa amani
katika nchi yao na wanafanya mambo kwa mujibu wa sheria , na kuongeza
tayari changamoto zinazojitokeza ikiwemo vitisho wanazifahamu na
wanazifanyia kazi ili zisilete athari wakati wa zoezi la uchaguzi .
“Niwahakikishie
wananchi kwamba changamoto zinazojitokeza ikiwemo vitisho tunazifahamu
, na tunashukuru wanazisema wazi wazi , labda niwahakikishie wananchi
tumejipanga kuzikabili ili zisileta madhara kabla na baada ya uchaguzi
huo ”alifahamisha .
Kamishna
Hamdan pia ameeleza kwamba Jeshi limejipanga pia kubadilisha mfumo wa
kusimamia ili changamoto zilizojitokeza katika uchaguzi uliofanyika 25,
oktoba mwaka jana wazigeuze kuwa fursa .
Akizungumza
ulinzi katika maeneo ya Visiwa Vidogo vidogo , amesema kwamba
watawatumia askari shehia kutoa taarifa ili waweze kuyafikia maeneo yote
huku akisisitiza kwamba namba za simu za makanda wa Polisi Mikoa yote
ziko wazi na zinafahamika na wananchi waliowengi .
“Sisi
tupo wengi na maeneo yote tunayafahamu , kwa hili tutawatumia zaidi
askari wetu wa shehia na kikubwa zaidi ni kwamba makamanda wote wa mikoa
Zanzibar namba zao za simu ziko wazi muda wote wananchi wanatakiwa
kuwapigia na kuwaeleza changamoto zinazowakabili ”alieleza.
Hata
hivyo alisema kwamba Jeshi la Polisi litafanya kazi kwa karibu na
Serikali za Shehia kwa kuwatumia masheha na kamati zao kuhakikisha
taarifa zote za uvunjifu wa amani zinaripotia na zinachukuliwa hatua kwa
mujibu wa sheria .
Geita nayo yachomoza Tamasha la Pasaka
Na Mwandishi Wetu
…………………………………….
KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka imeiteua Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kuwa eneo mojawapo litakalofikiwa na tamasha hilo linalotarajia kufanyika Machi 28 Wilayani humo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2016, Alex Msama Kahama ni eneo la tatu litakalofikiwa na Tamasha la Pasaka mwaka huu.
Msama alisema wamepokea idadi kubwa ya maombi kutoka kwa wakazi wa Wilaya hiyo kama ilivyokuwa mikoa ya Geita na Mwanza.
Msama alisema Tamasha hilo kwenye mikoa ya Geita litafanyika Machi 26 huku Mwanza litafanyika Machi 27 na kumalizia Kahama.
“Kamati yangu imepokea idadi kubwa ya maombi kutoka mikoa hiyo mitatu, hivyo hapana budi kuikubalia kwa sababu tunafanya kazi ya Mungu kupitia muziki wa Injili hasa waimbaji mahiri wa muziki huo,” alisema Msama.
Msama alitumia fursa hiyo kwa wakazi wa mikoa ambayo imefanikiwa kupata baraka ya kufikiwa na tamasha hilo na maeneo ya karibu kujitokeza kwa wingi kwa sababu ya umuhimu wa tamasha hilo kwa jamii hasa katika maeneo ya wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane.
“Hili Tamasha lina umuhimu wake hasa kuzungumza na Mungu sambamba na kufikisha matakwa ya jamii yenye uhitaji maalum ambao hawana pa kukimbilia,” alisema Msama.

Serikali yatoa tamko kuhusu udhalilishaji wa mwanafunzi wa kitanzania India
…………………………………..
Serikali imetoa tamko la kulaani kitendo kilichotokea nchini India kwa mwanafunzi wa kike wa kitanzania kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani ambapo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na kimataifa imetoa tamko la kulaani suala hilo kwa kuitaka Serikali ya india kuchukua hatua.
Akitoa tamko hilo Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt Augustine Mahiga amesema ni kweli kwamba kuna mwanafunzi wa kike wa kitanzania alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji nchini India kwa kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani suala ambalo lilizua mijadala mikubwa nchini kuhusu udhalilishaji huo.
“Wizara yetu imezungumza na Balozi wa India nchini na kumweleza ni kwa jinsi gani watanzania wamefadhaika na kusononeshwa na kitendo alichofanyiwa mtanzania mwenzao huko India na Balozi alituhakikishia kwamba amewasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi yake na kusema Serikali ya India kwa kushirikiana na Jeshi la polisi nchini humo wamefanikisha kuwakamata wote waliohusika na kitendo hicho na kuwafikisha mahakamani kujibu mashataka hayo”
“ Pia Serikali ya India imeahidi kutoa ulinzi kwa wanafunzi wa kitanzania na wenye asilia ya Afrika wanaosoma huko ili kuwalinda na kuwaepusha na vitendo hivyo vinavyofanya na raia ambao hawana nia njema kwa mahusiano mazuri ya kimataifa yaliyopo kati ya India na Tanzania”Alisema Mhe. Mahiga.
Serikali ya Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na Serikali ya India kwa miaka mingi sasa na kutokana na kitendo hiki kilichotokea nchini India,Waziri wa Mambo ya Nje ya India amefatana na Balozi wa Tanzania nchini humo kwenda Mji wa Bangalo ili kuongea na wanafunzi wakitanzania na wale wenye asili ya Afrika wanaosoma huko ili kujenga mahusiano mazuri na wazawa ikiwa ni jitihada za kupunguza vitendo hivyo kutokea mara kwa mara.
Waganga wanaochochea mauaji ya walemavu wa ngozi kushughulikiwa
………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali
kupitia Jeshi la Polisi imekua ikifanya operesheni maalum za mara kwa
mara za kukamata waganga wa jadi wanaopiga ramli chonganishi ambazo ni
kichocheo kikubwa cha ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi nchini.
Akijibu
swali la Mhe.Mgeni Jadi Kadika Mbunge wa Viti Maaalum(CUF) lililouliza
Serikali ina mpango gani wa kuwalinda na kuhakikisha usalama wa maisha
ya watu wenye ulemavu wa ngozi,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mhe.Hamad Yussuf Massauni amesema Serikali imeanzisha vituo vya
kuwahudumia watu wenye ulemavu wa ngozi ambavyo vimesaidia kuimarisha
ulinzi ikiwa ni pamoja na Polisi kuwatumia Polisi Jamii kutoa elimu kwa
umma juu ya madhara ya vitendo vya kikatili vya mauaji na kujeruhi
vinavyofanywa na baadhi ya watu kwa msukumo wa imani potofu za
ushirikina.
“Kwa
takwimu halisi tulizonazo tangu mwaka 2006 mpaka 2015 jumla ya mauaji ya
walemavu wa ngozi 43 yametokea na jumla ya watuhumiwa 133 walikamatwa
kuhusika na vitendo hivyo na watuhumiwa 19 walihukumiwa adhabu ya kifo”
“
Katika kupambana na vitendo hivi Jeshi la Polisi linakumbwa na
changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa askari katika kuhudumia wananchi
ambapo kwa Tanzania askari mmoja anahudumia wananchi 1000 mpka 1500
ikiwa ni nje ya matakwa ya kimataifa ya askari mmoja kuhudumia wananchi
400 mpka 450 na uhaba wa magari kwa ajili ya doria mbalimbali ambapo
takribani magari 387 yamegawanywa katika maeneo mbalimbali nchini ili
bado tunaendelea kupambana na kutatua changamoto hizi kadri ya bajeti
iyakavyoruhusu” Alisema Mhe.Massauni.
Wizara
kupitia Jeshi la Polisi ikishirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama za
Vijiji,Kata,Wilaya, na Mikoa imeanzisha vikosikazi(TASK FORCES)
hususani kwenye Mikoa na Wilaya zilizokithiri matukio ya ukatili dhidi
ya walemavu wa ngozi ambapo Vikosikazi hivyo hukusanya taarifa za
kiintelejensia na kuzifanyia kazi.
Billioni 60 kufufua General Tyres Arusha
Waziri
wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles John Mwijage akijibu hija
mbalimbali toka kwa wabunge katika kikao cha 9 cha Bunge la 11
linaloendelea Mjini Dodoma.
Picha na Raymond Mushumbuai MAELEZO.
………………………………………………………………….
Shillingi
Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General
Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa
Serikali, na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya
kiwanda hicho na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya
utengenezaji wa matairi duniani.
Akijibu swali la Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) lililouliza ni lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa Jijini la Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na wako mbioni kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi nchini.
“ Tumeanzisha viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa watanzania na sio kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa ambazo tunaweza kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia Wizara yangu tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili kianze kufanya kazi mara moja”
“ Sio tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia viwanda vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza viwanda hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta wawekezaji wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe. Mwijage.
Aidha Mhe. Charles John Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri katika uendeshaji wake ukiacha mifano ya makampuni machache yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania Breweries Limited (TBL),Morogoro Polyester 21st Century na Tanzania Cigarette Company Limited (TCC), hivyo Wizara yangu ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya Viwanda ilifanya tathmini iliyoonesha kuwa mashirika mengi yaliyobinafsishwa hawakutekeleza mikataba ya mauziano kikamilifu.
Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya taifa.
Serikali kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali itakayowajengea imani kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli zao za kibiashara na pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya kati unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha Viwanda vya Mkoa vya kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na ufugaji kupitia njia hii ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo la ajira nchini.

MWAKALEBELA AKANUSHA TUHUMA DHIDI YAKE
KUKANUSHA UPOTOSHAJI DHIDI YANGU
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
Kumekuwa
na upotoshwaji wa taarifa zinazosambaa juu ya aliyewahi kuwa Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF, na Mkuuwa Wilaya ya
Wanging’ombe, Fredrick Wilfred Mwakalebela, ambapo baadhi ya vyombo vya
habari kama Magazeti na mitandao ya kijamii vimekuwa viripoti tofauti.
Akizungumza
na mtandao huu, wa Sufianimafoto.com kwa njia ya simu, Mwakalebela
alisema kuwa zimekuwepo taarifa za upotoshwaji dhidi yake baada ya
kuibuka kesi ya mtuhumiwa aliyepandishwa Kizimbani mwenye jina
linalofanana na lake mwenye jina la David John Mwakalebela (56).
Aidha
Mwakalebela alisema kuwa Mtuhumiwa huyo, aliyewahi kuichezea timu ya
Yanga ya jijini Dar es Salaam, na timu ya Taifa, wakati yeye akiwa ni
Katibu Mkuu wa TFF, alipandishwa kizimbani yeye na aliyewahi kuwa Mr.
Tanzania 2015, Muhammad Khalil (32) wakikabiliwa na mashitaka saba
likiwemo la kuishi nchini bila kibali na kumsaidia Mshitakiwa kutoa
taarifa za uongo.
Kutokana
na kufanana kwa majina hayo,kumekuwepo na sintofahamu na usumbufu
mkubwa kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya huyo ya Wanging’ombe huku ndugu, jamaa na
marafiki wakihaha huku na huko na wengine wakimpigia simu kwa mshituko,
jambo ambalo si la kweli.
”Zimeene
taarifa potofu juu yangu zikielekeza tuhuma hizo dhidi yangu kwa
makusudi au kwa kutofahamu jambo ambalo ni Hatari kwa Mimi binafsi,
familia na marafiki kwa ujumla, nawaomba wahusika wawe wakifuatilia
undani wa stori yenyewe ili kupata uhakika kabla ya kuanza kueneza
uzushi na kuzua taflani,
Aidha
napenda kuwapa pole wanafamilia yangu, ndugu, jamaa na marafiki kwa
usumbufu wote uliojitokeza kwao kutokana na sintofahamu hii na
kusababisha kadhia dhidi yako”. alisema Mwakalebela
Mtuhumiwa David Mwakalebela, akiwasili Mahakamani,ambaye amefananishwa na Fredrick Mwakalebela.
Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano katika Kituo mahiri cha Taifa cha Kutunzia kumbukumbu
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora(wa
pili kushoto) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja Mradi bw. Xiong
Hazbin (Kushoto) na kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA Eng. Peter Philip
katika ziara ya kutembelea kituo mahiri cha taifa cha kutunzia
kumbukumbu kilichopo kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora(kushoto)
akimsikiliza maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo
Eng. Peter Philip kuhusu mitambo ya kupozea umeme iliyoko katika kituo
mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kilichopo kijitonyama jijini
Dar es Salaam.
Mitambo ya kupozea umeme iliyopo katika kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora(kulia) akiongozana
na Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo Eng. Peter Philip na baadhi ya
maaafisa wa Wizara wakati wa ziara ya kukagua kituo mahiri cha taifa cha
kutunzia kumbukumbu kilichopo kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin
Kamuzora(kushoto) akipewa maelezo ya namna hali ya usalama
inavyozibitiwa katika kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu
kilichopo kijitonyama jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mkurugenzi wa
TEHAMA Eng. Peter Philip .
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin
Kamuzora(kushoto) akionyeshwa mitungi ya kuzimia moto Salaam kutoka kwa
Mkurugenzi wa TEHAMA Eng. Peter Philip alipofanya ziara yake ya
kutembelea kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu kilichopo
kijitonyama jijini Dar es .
Katibu
Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin
Kamuzora(kushoto) akionyeshwa sehemu ya chumba cha kuhifadhia Jenereta
kilichopo katika kituo mahiri cha taifa cha kutunzia kumbukumbu
kijitonyama jijini Dar es Salaam ,kutoka kwa Mkurugenzi wa TEHAMA Eng.
Peter Philip .
(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)
JUMUIYA YA MARADHI YA SARATANI ZANZIBAR YAAADHIMISHA SIKU YA SARATANI DUNIANI KWA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya maradhi ya saratani Zanzibar Dkt. Msafiri Marijani
akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Jumuiya hiyo Mpendae
ikiwa ni maadhimisho ya siku ya saratani duniani, kushotoni kwake ni
Mkurugenzi wa Utumishi na uendeshaji Wizaraya ya Afya,
PICHA NA MAKAME MSHENGA/MAELEZO ZANZIBAR
……………………………………………………………………………
RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR
Mwenyekiti wa Jumuiya ya maradhi ya Saratani Zanzibar Dkt. Msafiri Marijani ameitanabahisha jamii kwamba maradhi ya saratani yamekuwa janga linalosumbua dunia nzima kwa sasa na kila mmoja anawajibu wa kusaidia katika kukabiliana na maradhi hayo sugu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Jumuiya hiyo Mpendae nje kidogo ya Mjini Zanzibar, ikiwa ni maadhimisho ya siku ya saratani duniani, Dkt. Marijani amesema mtu anaweza kujikinga na maradhi hayo iwapo hatua za mapema zitachukuliwa.
Amezitaja hatua zinazopaswa kuchukuliwa na wananchi katika kukabiliana na saratani kuwa ni kujenga mwamko wa kuchunguza afya mara kwa mara ili kugundua mapema iwapo mtu anazo dalili za maradhi hayo.
Amesema hatua nyengine ni kuacha kutumia bidhaa zinazotokana na tumbaku, ulevi wa kupindukia, kupunguza matumizi ya mafuta kwenye chakula, kutumia zaidi vyakula vya matunda na mbogamboga na kujenga tabia ya kufanya mazoezi kila siku.
Dkt. marijani amewakumbusha wananchi kuwa saratani ni uvimbe mpya kwenye mwili na baada ya muda mfupi huzalisha chembechembe zinazosababisha athari kubwa na kama haikuwahiwa mapema inasababisha donda kubwa na kuwa halitibiki tena.
“Saratani inaweza kuzuilika iwapo itawahiwa mapema, tuongezeni nguvu kukabiliana nayo vyenginevyo inaweza kuathiri wananchi wengi kwani gharama ya matibabu yake ni kubwa na wagonjwa wengi hushindwa na kupoteza maisha,” alisisitiza Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Amesema saratani ya matiti na shingo ya kizazi ndizo zinaongoza kwa wanawake Zanzibar na saratani ya tenzi dume inaongoza kwa upande wa wanaume.
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya maradhi ya Saratani Zanzibar, ambae ni Daktari bingwa wa uchunguzi wa saratani, amewaeleza waandishi wa habari kwamba mpaka hivi sasa hakuna takwimu rasmi za wagonjwa wa maradhi hayo Zanzibar lakini Hospitali ya Ocean Road ya Dar es salaam imekuwa ikipokea wagonjwa 1,000 kila mwaka kutoka Zanzibar mbali na wagonwa wengine wanaopelekwa nje ya nchi na wanaobakia majumbani kupatiwa dawa mbadala.
Amesema kutokana na kadhia hiyo mwaka 2013 ilianzishwa Jumuiya ya kupambana na saratani Zanzibar ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya njia za kujikinga na kuishauri serikali njia zinazofaa kupunguza ongezeko la maradhi hayo.
Ameitaka Serikali kuongeza wataalamu na dawa za kupunguza maumivu katika hospitali kuu ya Mnazimmoja na hospitali nyengine za Zanzibar kwani zimekuwa hazitoshi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Ndugu Omar Mwinyi Kondo amewapongeza wanachama wa Jumuiya hiyo kwa juhudi kubwa wanayochukua kuelimisha jamii kujikinga na saratani.
Amewahakikishia viongozi wa
Jumuiya hiyo kwamba Serikali itaanzisha utaratibu rasmi wa kuwasajili
wagonjwa wa saratani na kuongeza huduma za matibabu Hospitali kuu ya
Mnazimmoja hasa dawa za kupunguza maumivu na wataalamu.Mwenyekiti wa Jumuiya ya maradhi ya Saratani Zanzibar Dkt. Msafiri Marijani ameitanabahisha jamii kwamba maradhi ya saratani yamekuwa janga linalosumbua dunia nzima kwa sasa na kila mmoja anawajibu wa kusaidia katika kukabiliana na maradhi hayo sugu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Jumuiya hiyo Mpendae nje kidogo ya Mjini Zanzibar, ikiwa ni maadhimisho ya siku ya saratani duniani, Dkt. Marijani amesema mtu anaweza kujikinga na maradhi hayo iwapo hatua za mapema zitachukuliwa.
Amezitaja hatua zinazopaswa kuchukuliwa na wananchi katika kukabiliana na saratani kuwa ni kujenga mwamko wa kuchunguza afya mara kwa mara ili kugundua mapema iwapo mtu anazo dalili za maradhi hayo.
Amesema hatua nyengine ni kuacha kutumia bidhaa zinazotokana na tumbaku, ulevi wa kupindukia, kupunguza matumizi ya mafuta kwenye chakula, kutumia zaidi vyakula vya matunda na mbogamboga na kujenga tabia ya kufanya mazoezi kila siku.
Dkt. marijani amewakumbusha wananchi kuwa saratani ni uvimbe mpya kwenye mwili na baada ya muda mfupi huzalisha chembechembe zinazosababisha athari kubwa na kama haikuwahiwa mapema inasababisha donda kubwa na kuwa halitibiki tena.
“Saratani inaweza kuzuilika iwapo itawahiwa mapema, tuongezeni nguvu kukabiliana nayo vyenginevyo inaweza kuathiri wananchi wengi kwani gharama ya matibabu yake ni kubwa na wagonjwa wengi hushindwa na kupoteza maisha,” alisisitiza Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Amesema saratani ya matiti na shingo ya kizazi ndizo zinaongoza kwa wanawake Zanzibar na saratani ya tenzi dume inaongoza kwa upande wa wanaume.
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya maradhi ya Saratani Zanzibar, ambae ni Daktari bingwa wa uchunguzi wa saratani, amewaeleza waandishi wa habari kwamba mpaka hivi sasa hakuna takwimu rasmi za wagonjwa wa maradhi hayo Zanzibar lakini Hospitali ya Ocean Road ya Dar es salaam imekuwa ikipokea wagonjwa 1,000 kila mwaka kutoka Zanzibar mbali na wagonwa wengine wanaopelekwa nje ya nchi na wanaobakia majumbani kupatiwa dawa mbadala.
Amesema kutokana na kadhia hiyo mwaka 2013 ilianzishwa Jumuiya ya kupambana na saratani Zanzibar ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya njia za kujikinga na kuishauri serikali njia zinazofaa kupunguza ongezeko la maradhi hayo.
Ameitaka Serikali kuongeza wataalamu na dawa za kupunguza maumivu katika hospitali kuu ya Mnazimmoja na hospitali nyengine za Zanzibar kwani zimekuwa hazitoshi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji Wizara ya Afya Ndugu Omar Mwinyi Kondo amewapongeza wanachama wa Jumuiya hiyo kwa juhudi kubwa wanayochukua kuelimisha jamii kujikinga na saratani.
ujumbe wa mwaka huu katika siku ya saratani duniani ni mimi na wewe tunaweza kujikinga na saratani.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
MWENYEKITI WA CCM DK. JAKAYA KIKWETE AWASILI MKOANI SINGIDA TAYARI KWA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu
Abdulrahman Kinana wakati alipowasili mkoani Singida tayari kwa
maadhimisho ya Miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM yanayotarajiwa kufanyika
Februari 6 mwaka huu siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Namfua mkoani
humo, Kauli Mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Kufanya Kazi”(PICHA NA
JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-SINGIDA)
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi
mkoani Singida wakati alipowasili mjini Singida.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu
Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kulia baada ya kuwasili mjini
Singida , Kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
CCM na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mkuu wa mkoa wa
Singida Mh. Parseko Kone.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
CCM na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya
Kikwete akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu
Abdulrahman Kinana wakati walipokuwa na mazungumzao katikati ni Mkuu wa
wilaya ya Singida Said Amanzi.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi
na Uenezi CCM na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
akifurahia jambo na Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP. Thobias
Sedoyeka.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi
na Uenezi CCM na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana.
MUDHIHIRI M. MUDHIHIRI AZINDUA KITABU MWELE BIN TAABAN
Kutoka
kulia ni Msanii Mrisho Mpoto, Abdallah Mkumbila (Muhogo Mchungu),
Mudhihir Mudhihir, Majid Mswahili Majidi na Masoud Kipanya wakizindua
kitabu cha Mwele bin Taabani.
Mudhihir Mudhihir ambaye ndio mtunzi wa kitabu hicho akielezea maudhui ya kitabu kwa ufasaha.
Majid
Mswahili, mchambuzi wa maswala ya kiuchumi,siasa na jamii kutoka katika
Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo.
Abdallah
Mkumbila (Muhogo Mchungu) akielezea baadhi ya vipengele vya kitabu huku
akiwasihi watanzania kukisoma kitabu hicho kwani kina mafunzo kwa
wanajamii.
…………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
Mudhihiri Mohamed Mudhihiri ambaye
ni mwanasiasa mkongwe na mtunzi mahiri wa vitabu leo hii jijini Dar Es
Salaam amezindua kitabu chake cha Riwaya ya Mwele Bin Taaban.
Kitabu cha Mwele bin Taabani, tayari ameshakiingiza sokoni, kimebeba uhalisia wa maisha ya Mtanzania wa hali ya chini ambaye anakumbana na madhila, ambayo msingi wake ni utawala na watawala wanaojali zaidi masilahi yao, kuliko ya wapiga kura wao.
‘Mwele bin Taabani’ ni riwaya inayoyaakisi magumu ya Watanzania wengi hasa wa vijijini ambao wanalima sana, lakini wanavuna kidogo huku wakikosa watu wa kuwasemea na kusikiliza matatizo yao pamoja na kuwapo kwa Serikali ambayo imekuwa ikikusanya kodi kila uchwao kwenye mazao yanayozalishwa na mafukara hao.
Ukifanikiwa kukisoma kitabu hicho na kukielewa, hakika utakubaliana na mtunzi wake kuwa amedhamiria kufikisha sononeko la wananchi masikini kwa viongozi Serikalini.
Kwa kulifahamu hilo, Mudhihiri kwa kauli yake amesema kitabu hicho kinafaa sana ndani ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwani ndiyo mkongojo mujarabu kwa masaibu ya Wanakazamoyo (Wananchi).
Mbali na kitabu cha Mwele bin Taabani, vingine vipo kwenye ngazi ya muswaada ambavyo ni Msaliti, Nyungu ya Mawe, Nasaha za Mswahili na Viungo vya Ushairi.
Kwa mujibu wa Mudhihiri, tafsiri ya Mwele ni mgonjwa. Mwele bin Taabani kwa muktadha wa riwaya hii si mwanadamu bali ni kadhia ya ustawi duni wa jamii ya Wanakazamoyo.
Pia kitabu hiki kinafaa mashuleni na vyuoni. EMAC wametaka kitumike kidato cha tano na sita na vyuoni pia na hivi sasa Wahadhiri nchini wameonesha dhamira ya kukitumia kitabu hiki katika fasihi kwa ngazi ya uzamili.
Mikakati inaendelea ili kukifikisha kwenye maeneo mbalimbali ya nchi kwa bei nafuu isiyozidi shilingi 6,500.

MADIWANI WA CHADEMA WALALAMIKA KUBURUZWA NA MSTAHILI MEYA WA JIJI LA MWANZA
Na:George Binagi-GB Pazzo
Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema Jijini Mwanza, wamemlalamikia Mstahiki Meya wa Jiji hilo kwa madai ya kuliongoza kibabe baraza la Madiwani.
Chadema Jijini Mwanza, wamemlalamikia Mstahiki Meya wa Jiji hilo kwa madai ya kuliongoza kibabe baraza la Madiwani.
Wakizungumza
baada ya kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi hii leo, Madiwani hao
wamelalamikia kitendo cha kuzuiliwa kujadili taarifa ya Kamati ya fedha
iliyowasilisha katika kikao hicho
kwa madai kwamba jukumu la baraza hilo ni kupitisha taarifa hiyo na si
kuijadili.
kwa madai kwamba jukumu la baraza hilo ni kupitisha taarifa hiyo na si
kuijadili.
Samwel Range ambae ni diwani wa Kata
ya Pamba pamoja na John Pambalu ambae ni diwani wa Kata ya Butimba (Wote
Chadema), wamesema wamesikitishwa kuona kanuni za vikao zikivunjwa huku
madiwani wakinyimwa fursa ya kujadili taarifa ya kamati ya fedha
iliyowasilishwa.

“Tumeshuhudia utawala wa kibabe
ukianza katika halmashauri yetu huku mhe.Mwenyekiti wa kikao (Meya) pamoja na
Mkurugenzi wake wakiamua kutofuata kanuni na kuamua kufuata matakwa yao
binafsi. Tumeletewa taarifa ya kamati ya fedha, wakati wa kujadili tunaambiwa hakuna
sababu ya kuijadili isipokuwa kuipitia na kuiidhinisha taarifa hiyo, kitu
ambacho madiwani wa Chadema na Upinzani tunakilalamikia”. Alisema Pambalu.

Nae Samwel Range amesema “Kamati ya
fedha haina mamlaka ya kuidhinisha chochote ndani ya halmashauri ya Jiji la
Mwanza. Inapaswa ilete taarifa yake na kuileta katika baraza la Madiwani ambapo
sisi tunauwepo wa kuikubali au kuikataa”.
fedha haina mamlaka ya kuidhinisha chochote ndani ya halmashauri ya Jiji la
Mwanza. Inapaswa ilete taarifa yake na kuileta katika baraza la Madiwani ambapo
sisi tunauwepo wa kuikubali au kuikataa”.
Hata hivyo malalamiko hayo yamepingwa
na James Bwire ambae ndie Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na diwani wa Kata ya
Mahina (CCM), ambapo amefafanua kwamba malalamiko ya madiwani wa Chadema hayana
msingi wowote ikizingatiwa kwamba taarifa iliyowasilishwa na kamati ya fedha
iliishajadiliwa ndani ya kamati hivyo hakukuwa na umuhimu wa kuijadili tena
ndani ya baraza la madiwani bali kuipokea na kuipitisha.

Baraza la Madiwani Jijini Mwanza linaundwa
na Madiwani 24 na linaongozwa na Chama cha Mapinduzi CCM kwa upande wa Mstahiki
Meya pamoja na Naibu Meya ambapo kuna Madiwani 19 kutoka CCM huku Chama cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema kikiwa na Madiwani Watano.

Kutokana na Uwiano huyo, Madiwani wa Chadema
wanalalamika kuburuzwa katika baraza hilo kutokana na uchache wao, madai ambayo
hata hivyo yanapingwa na Madiwani kutoka CCM ambao wanasema suala lolote lenye
maslahi kwa umma linapewa nafasi sawa ndani ya baraza hilo bila kujadi itikadi
za vyama vya siasa.

Kushoto ni Naibu Meya Jiji la Mwanza, Katikati ni Mstahiki Meya na Kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Waheshimiwa Madiwani Jijini Mwanza
Waheshimiwa Madiwani Jijini Mwanza
Watendaji wa Idara mbalimbali Jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Mgeni Rasmi Siku ya Sheria nchini, Asisitiza Ufanisi wa Mahakama na utoaji wa Haki kwa Wakati
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akipokewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman leo jijini
Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Rais,
Dkt. John Magufuli alikua mgeni rasmi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
(katikati) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria
leo jijini Dar es salaam.
Wimbo
wa Taifa ukipigwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Kulia) akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman
Baadhi
ya Viongozi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakiwa
wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa
Kenya Dkt. Willy Mutunga, Jaji Kiongozi wa Tanzania Mhe. Shaaban Lila
(katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Mecki Sadiki.
Baadhi
ya Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini na wadau muhimu wa
Mahakama waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakitoa heshima zao
wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Rais
wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Charles Rwechungura akitoa
salam na ujumbe wa Chama hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria
leo jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akifuatilia hotuba
zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Sheria. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein
Katanga.
Jaji
Mkuu wa Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwahutubia
viongozi, mabalozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi
waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.
Continue reading →RAIS MAGUFULI AZINDUA MWAKA MPYA WA KIMAHAKAMA (SIKU YA SHERIA) JIJINI DAR ES SALAAM
Jaji
Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akisoma hotuba yake kabla ya
kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Mahakama katika
Siku ya Sheria Duniani katika uwanja wa Mahakama mtaa wa Chimala eneo la
Ocean Road jijini Dar es salaam leo Jumatano February 4, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Mahakama katika Siku ya
Sheria Duniani katika uwanja wa Mahakama mtaa wa Chimala eneo la Ocean
Road jijini Dar es salaam leo Jumatano February 4, 2016
PICHA NA IKULU
Bodi ya Filamu yafanya kikao cha mapitio ya Filamu ya “DADA”
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya na Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi.Costancia Gabusa (katikati)
akichangia mada wakati wa kikao cha kupitia Filamu ya “DADA”
kilichofanyika katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es
Salaam. Kikao hicho kimejumuhisha wajumbe kutoka Ofisi ya Uhamiaji
Makao Makuu, Jeshi la Polisi, Wizara ya Afya na Maendeleo ya jinsia,
wazee na watoto na TCRA.Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na kushoto ni Afisa Utamaduni kutoka Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Fredrick Mgaza.
Katibu
Mtendaji waBodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akielezea jambo wakatika
wa kikao kazi kwa ajili ya mapitio ya Filamu ya “DADA” iliyowasilishwa
ofisini kwake kwa ajili ya ukaguzi leo jijini Dar es Salam.Kushoto ni
Mtengenezaji na Mmiliki wa Filamu hiyo Bi. Christina Mroni.
Wajumbe wa kikao cha mapitio ya Filamu ya “DADA” wakifuatilia Filamu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (mwenye gauni la
kitenge) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa kikao cha mapitio ya Filamu ya
“DADA” wakifuatilia Filamu hiyo leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni
Muongozaji wa na Mmiliki wa Filamu hiyo Bi. Christina Mroni.
Picha na Frank Shija,WHUSM

No comments:
Post a Comment