Rais Dkt John Pombe Joseph
Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Msshariki Mhe Joshua Nassari
aliyekuwa mmoja wa viongozi na wananchi waliojitokeza kwa wingi
kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki utofanyika jijini Arusha.
Picha na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa
Balozi Agustine Mahiga mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi
mbalimbali vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa
Arusha na Kilimanjaro waliofika Uwanja wa ndege wa KIA kumpokea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni
mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimatifa wa Kilimanjaro
(KIA). PICHA NA IKULU
IBRAHIM AJIB AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA
Katika
kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya
Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa
Septemba 2015.
SHULE 18 DAR KUNUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KUTOKA KWA CFAO MOTORS GROUP NA ALLIANCE AUTOS
Meneja
wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama
barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika
Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin,
(katikati) na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya
Go4school, Henning Nathow.
kampuni ya CFAO Motors Group imekuwa ikihusika
kufanikisha mbio hizo.
Mwanzilishi
wa mashindano ya mbio za magari ya go4school, Henning Nathow (wa pili
kushoto) akielezea dhumuni lengo lao la kusaidia upatikanaji wa elimu
bora kupitia mradi wa go4school.
“Mbio
hizi zimeanzishwa na Wajerumani ili kusaidia elimu ya Rwanda na hii sio
mara ya kwanza tayari yamefanyika mara mbili barani Afrika na sisi
kama CFAO tumekubali kuungana na taasisi ya Opportunity International
Germany ili kusaidia upatikanaji wa elimu,”
Afisa
Elimu wa Ilala, Helen Peter akitoa neno la shukrani kwa kampuni ya CFAO
Motors Group kwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani kwa shule
18 zilipo ndani ya Manispaa ya Ilala.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin (wa pili kushoto) akimkabidhi
Afisa Elimu ya Ufundi wa Manispaa ya Ilala, Bi. Helen Peter (wa kwanza
kushoto) msaada wa vifaa vya usalama barabarani kusaidia wanafunzi
wavukapo barabarani pamoja na vifaa vya michezo, Wanaoshuhudia tukio
hilo ni Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed na (kulia) na
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Group nchini, Bi. Attu Mynah akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
MAJALIWA APOKEA MISAADA WILAYANI RUANGWA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa
ambao unafanywa kwa ufadhili wa kampuni ya HUAWEI ya China , kijijini
hapo, Februari 28, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Jordan
Lugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea hundi ya shilingi milioni tisa kutoka kwa Mtalaam wa Ufundi wa
Kampuni ya simu ya Halotel wa mkoa wa Lindi, Tran The Hoang ili ziweze
kugharimia malipo ya kadi za bima ya Afya kwa baadhi ya wakazi wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwa. Alikuwa katika ziara ya siku moja
wilayani humo Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa ma Mwanaidi Mussa na Mkussa Lukoloma (kushoto) wote wa kijiji
cha Nandagala wilayani Ruangwabaada ya kuwakabidhi kadi zao za bima ya
Afya ambazo zimegharimiwa na Kampuni ya Simu ya Halotel iliyochangia
shilingi milioni tisa kuwawezesha wakazi wa kijiji hicho kufaidi huduma
za Bima ya Afya, Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti
watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji
cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo
kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akipokea msaada wa vyakula na nguo kutoka kwa Eric Shigongo Mwenyekiti
watu waliojitotelea kusaidia waliopatwa na maafa ya mvua katika kijiji
cha Mtondo wilayani Ruangwa wakati Waziri Mkuu alipokwenda kijijini hapo
kuwapa pole wananchi Februari 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa
Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa
Ruangwa baada ya kuwasili mjini hapo kwa ziara ya siku moja Februari 28,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MKOANI TANGA KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI MKOANI HUMO LEO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantum Mahiza alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga
kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku Mbili Mkoani humo leo
Februari 28, 2016
Chipukizi wa Umoija wa Vijana wa
CCM Mkoa Tanga akimvisha Skafu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga
kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani hum oleo
Februari 28,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Vijana
wa Chipkizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga alipowasili uwanja wa
ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani
humo leo Februari 28,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa
Mkoa wa Tanga baada ya kupokea Taarifa ya Mkoa huo kutoka kwa Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa Rais
yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa
Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.(Picha
na OMR)
WAZIRI NAPE AZINDUA NA KUSHIRIKI KILIMANJARO MARATHON 2016
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na
wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza kwa wingi kushiriki mbio za
Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo mwaka huu zaidi ya watu elfu 8
walishiriki kutoka nchi mbali mbali ambapo kati ya hao 200 walitoka
nchini Kenya.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikimbia kwenye
riadha ya Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo alikimbia kilomita 5 pamoja
na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Anthony Mtaka, mashindano hayo ya riadha yameshirikisha zaidi ya nchi 40.
Mshindi
wa kwanza wa kilometa 42.2 Kiprotich Kirui akiinua mikono juu kama
ishara ya kushangilia ushindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisoma risala
mara baada ya kuhitimisha mbio za Kilimanjaro Marathon ambapo
aliwapongeza wahiriki wote, wadhamini na kuwataka Watanzania kutumia
mbio hizo kama fursa ya kuutangaza utalii uliopo nchini.
DK.KIGWANGALLA AHIMIZA JAMII KUWA NA UTAMADUNI WA KUPIMA AFYA ZAO MARA MWA MARA
Naibu Waziri wa Afya, Dk.
Kigwangalla akitoa hutuba fupi wakati wa tukio hilo la kambi maalum ya
matibabu ya bure kwa wananchi wote iliyoandaliwa na Care Foundation kwa
kushirikiana na wadau wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Ilala, Mh.
Mussa Hazan Zungu.
………………………………………………………………………………………………………………………………….
Tukio likiendelea
Naibu
Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwa katika meza ya kupima afya ya
mwili ikiwemo magonjwa yasio ambukiza kama vile Magonjwa ya moyo,
sukari, shinikizo la damu na mengine mengi katika zoezi linaliendelea
katika viwanja vya Bustani ya jiji iliyopo mkabara na Ukumbi wa
Karimjee.
Naibu Waziri wa Afya. Dk.Kigwangalla akiwa katika vipumo hivyo..
Mbunge wa Ilala, Mh. Mussa Hazani Zungu, akipima afya katika zoezi hilo..
Dk.
Efrahim Mika Zaky wa Msimbazi Eyes Vision Center, (kushoto) akimpima
macho mmoja wa wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo linaloendelea
leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Bustani ya jiji, mkabara na
Ukumbi wa Karimjee.
Uchunguzi wa macho ukiendelea..
Dk. Efrahim Mika Zaky wa masuala ya macho, akimpima macho Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla wakati wa zoezi hilo..
Naibu
Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akiwa katika kupima macho kwenye kambi
maalum ya kutoa huduma za matibabu ya bure yaliyoandaliwa na Care
Foundation na wadau wengine katika viwanja vya Bustani ya Jiji, Posta
Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Dk.Kigwangalla akiwa katika moja ya sehemu ya kutolea dawa na
miwani kwa watu watakaobainika kuwa na matatizo katika macho..
Naibu
Waziri akipokea ua maalum kama ishara ya kukaribishwa katika ufunguzi
huo wa kambi maalum ya matibabu ya bure yaliyoandaliwa na CARE
Foundation na wadau wengine akiwemo Mbunge wa jimbo la Ilala, Mussa
Hazzan Zungu.(Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog/Mo tv).
MH PAUL MAKONDA AFANIKISHA MPANGO WA KUWASAFIRISHA WALIMU BURE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.
Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Lamada
Posta jijini Dar es salaam leo wakati alipozungumzia mpango wa
kuwasafirishwa walimu bure jijini Dar es salaam wakati wa kwenda na
kurudi kazini huku akiwa ameongozana na viongozi wa vyama vya
usafirishaji wa abiria jijini Dar es salaam pamoja na viongozi wa
Madereva wa Daladala jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti waUmoja wa Madereva, Shabani Mdemu na katikati ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam, (Uwadar), William Masanja
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.
Paul Makonda wa pili kutoka kushoto akimsikiliza Said Mabrouk
Mwenyekiti wa Chama Chama Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es salaam
wakati akizungumzia mwitikio wa wamiliki hao kuhusu
kuwasafirisha walimu ili kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Wilaya ya
Konondoni Mh. Paul makonda na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kutoa
elimu bure hapa nchini.…
FULL MKANDA PAMBANO LA CHEKA NA MSERBIA LEADERS JANA, CHEKA ASHINDA KWA …’.POINTI’
Bondia
Mtanzania Francis Cheka (kulia) akichapana na mpinzani wake bondia
kutoka nchini Serbia, Geard Ajetovic, wakati wa pambano lao la raundi 12
la ubingwa wa Mabara , uzito wa Super Midle wa WBF lililofanyika usiku
wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Cheka akijitahidi kupangua konde la mpinzani wake….
Cheka,
alichanika katika raundi ya nane baada ya mpinzani wake kumbananisha
kwenye kona iliyokuwa na utelezi ambapo aliteleza na kupoteza mwelekeo
na kushambuliwa mfululizo. Na Mafoto Blog.
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE Continue reading →
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE Continue reading →
WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI BANDARI YA MTWARA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amekagua bandari ya Mtwara na kunusa harufu ya ufisadi katika utoaji wa
zabuni ya ujenzi wa gati mpya tatu.
‘SERIKALI YATENGA SH. BILIONI 1.6/- VYUO VYA UALIMU”
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni
1.65/- kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwenye vyuo vya walimu hapa
nchini.
Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), wakati akizungumza na walimu na watumishi wa sekta ya elimu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mtwara uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara
Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), wakati akizungumza na walimu na watumishi wa sekta ya elimu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mtwara uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara
Waziri Nape avitaka vyombo vya Habari vya Serikali kuwa vinara wa ufichuaji wa maovu.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Bw.Nape Nnauye akiwa anakazia jambo kwa wafanyakazi wa
kampuni ya magazeti ya serikali ya TSN kuhusu kuboresha kazi zao na
kuandika habari zinazofichua maovu katika jamii na kusimamia haki bila
kumuonea mtu.
Mhariri wa magazeti ya Daily News
Bw.Charles Masele akimweleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Bw.Nape Nnauye(hayupo pichani) mapungufu mbalimbali ya kampuni
ya TSN na kumwomba waziri uyo awasaidie kuiboresha kampuni hiyo.
Mwenyekiti wa RAAWU tawi la
Tanzania Standard Newspaper(TSN) Bw.Oscar Mbuza akimweleza waziri
Nape(kulia) changamoto mbalimbali ya wafanyakazi.
Sehemu ya wafanyakazi wa kampuni
ya magazeti ya serikali(TSN) wakimskiliza Mhe. Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye(hayupo pichani).
Waziri Nape nnauye akipiga “Selfie” na mfanyakazi wa magazeti ya kampuni ya serikali ya TSN baada ya mkutano na wafanyakazi hao katika ofisi za kampuni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni
ya magazeti ya Serikali(TSN) wakifurahia picha ya pamoja na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape Nnauye.
Picha na Daudi Manongi.
RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AZINDUA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU – JUNIOR NATIONAL BASKET ASSOCIATION (JR.NBA)
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumzana na wadau mbilimbali wa mpira wa kikapu (NBA) juu ya Timu
bora nane kutoka kila kundi zitakazofuzu kushiriki kweye ngazi ya
mitoano Oktoba 2016. Timu bora mbili kutoka kila kundi zitakutana
kwenye michezo kuwania ubingwa ili kumpata Bingwa wa kwanza wa ligi ya
mpira wa kikapu kwa vijana, katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu
ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akizinduwa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana (Junior NBA),leo jijini Dar
es Salaam.
Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, leo jijini Dar es
Salaam.
Rais Mstaafu DKT. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mchezaji Mwandamizi wa (WNBA) Allison Feaster, leo jijini Dar es Salaam
Sehemu
ya mashabiki wa Mpira wa kikapu walio fika katika uzinduzi wa Ligi
ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
No comments:
Post a Comment