Pages

Wednesday, February 3, 2016

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA OFISI NDOGO YA CCM LUMUMBA

MAK1
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam leo Februari 02, 2016 wakati Makamu wa Rais alipotembelea katika Ofisi hiyo (Picha na OMR)
SIDA WARIDHISHWA NA MIRADI YA REA
 2
Mtambuzi wa miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijini, Mhandisi Elneema Mkumbo akitoa maelezo juu ya utekelezaji wa miradi ya REA, kwa Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlokom ( aliyeweka mikono kifuania) ambao ni miongoni mwa wafadhili wa miradi hiyo akiwa na ujumbe wake pamoja na wadau wengine wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ujerumani( GIZ) wakati wakikagua utekelezaji wa miradi ya REA katika mikoa ya kanda ya kaskazini.
1
3 4 5
Muonekano wa nyumba zilizounganishwa na huduma ya umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati vijijini REA katika kijiji cha Kwedizinga mkoani Tanga.
……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Shirika la Kimataifa la maendeleo la Sweden( SIDA), limeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Umeme inayofahiliwa na Shirika hilo hususan usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini REA kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini( Tanesco), katika maeneo mbalimbali nchini.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlekom amesema hayo mara baada ya kuona maendeleo ya wananchi wa vijijini wakati wa ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa miradi hiyo katika mikoa ya kanda ya kaskazini .

VIONGOZI WA NGAZI YA VIJIJI WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA KUTOKOMEZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU HADI KUFIKIA MACHI 30 MWAKA HUU

1Waziri wa afya,maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto,ummy mwalimu akiongea na kikosi kazi cha udhibiti wa ugonjwa wa kipindupindu,kulia nina kaimu mganga mkuu wa mkoa wa dodoma,dkt.nassoro mzee.
2Kaimu mganga mkuu mkoa wa dodoma dkt.nassoro mzee akisoma taarifa ya hali ya kipindupindu ya mkoa
3
4Baadhi ya kikosi hicho toka idara na wadau mbalimbali wakimsikiliza waziri huyo.
5Kaimu mganga mkuu wilaya ya bahi dkt. Gerald Maro akielezea jambo ,kikosi kazi toka wizara ya afya na wale wa mkoa(hawapo pichani) mara baada ya kufika kwenye kambi ya kipindupindu iliyopo kwenye zahanati ya isangha iliyopo wilayani bahi, Kulia ni bwana afya wilaya ya bahi selemani yondu
6Mtaalamu toka wizarani dkt. Vida Makundi(wakwanza kushoto)akifafanua jambo kwenye kambi hiyo
7Mwenyekiti wa kijiji cha Isangha,Andrea Lusinde(katikati) akielezea jinsi kijiji hicho kilivyoweza kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na kipindupindu pamoja na ujenzi wa vyoo na kuvitumia,jumla ya vyoo zaidi ya 300 vimejengwa katika kaya,kulia ni diwani wa kata ya chibelela mh.chalula Gerald.
………………………………………………………………………
Na.Catherine Sungura_Dodoma
Viongozi wote kuanzia ngazi ya vijiji wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu hadi kufikia tarehe 30 machi mwaka huu
Wito huo umetolewa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Ummy Mwalimu wakati alipokutana na kikosi kazi cha cha udhibiti wa kipindupindu Mkoa wa Dodoma
“Kipindupindu siyo suala ya afya peke yake,bali ni suala mtambuka hivyo sekta zote zinapaswa kujumuika katika kupambana na kutokomezwa ugonjwa Huu
Ummy alisema kipindupindu bado ni changamoto na nina janga hivyo kila mikoa inatakiwa kuliwekea kipaumbele kwakuwa ugonjwa huo unaua kwa haraka hivyo viongozi wote washiriki kikamilifu na si kuwaachia waganga.wakuu wa mikoa au wilaya
Aidha alisema licha ya kuwa na sheria ndogo Za kila halmashauri za kusimamia usafi na mazingira lakini katika kudhibiti kuenea kwa kipindupindu lazima liatakuja suala la kufungia biashara hususan za mbogamboga,matunda pamoja na chakula”suala la kukusanya mapato lipo na litaendelea kuwepo lakini suala la kipindupindu linapoteza maisha,maisha hayatafutwi lakini pesa zinatafutwa lakini ukikosea utapoteza maisha ya watu wengi”
Ummy alisema tangu kipindupindu kiingie nchini agosti mwaka jana,halmashauri zimetumia pesa nyingi katika kutokomeza ugonjwa huo,lakini wangeweza kuzuia mapema,pesa hizo.zingeenda kutatua tatizo la madawati katika shule za msingi nchini
“Mnapoona hamjaridhika na uendeshaji wa migahawa,msisite kuzifungia mara moja,mapato mtakusanya haraka kwa kuwa na nguvu za pamoja baada ya kutokomeza ugonjwa na kuweza kuingiza mapato mengi na kwa haraka tofauti na kuwa na hilo tatizo
Hatahivyo alizitaka vikosi vyote vya mikoa nchi,kuwashirikisha wadau wote wakiwemo viongozi wa dini zote kuweza kuelimisha kuweza kutoa elimu ya jinsi gani ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu kwa waumini wao
Mkoa wa dodoma umetumia takribani shilingi milioni 124 za kitanzania toka kipindupindu,hadi leo kuna wagonjwa wanne katika kambi ya kipindupindu wilaya ya bahi,jumla ya wagonjwa 450 waliugua na vifo12,wilaya zilizoathirika ni bahi,dodoma mjini na chamwino

Unilever yaendelea kuwazawadia wanafunzi shule mbambali

Mwanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi Maarifa, Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam  Ester Lawrence akipokea fulana kutoka kwa Balozi wa Blue Band Neema Upendo shuleni hapo jana akiwa ni mmoja wa washindi wa shindano la Blue Band ‘Kula Tano’ linalowamasisha wanafunzi kutambua umuhimu wa kula vyakula vyenye virutubisho. Kushoto ni mwalimu wa michezo Edith Katundu.

Mkutano wa kuhifadhi urithi wa utamaduni na ubunifu viwanda katika sekta ya utamaduni wafungwa jijini Dar es Salaam

H1
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi(aliyesimama) akifunga mkutano wa urithi wa utamaduni na ubunifu viwanda katika sekta ya utamaduni uliokuwa na dhumuni la kuwajengea uwezo wasanii wa sanaa mbalimbali ili waweze kuhamasisha jamii katika kuwaletea maendeleo chanya.
H2
Washiriki wa mkutano wa urithi wa Utamaduni na ubunifu Viwanda katika sekta ya utamaduni wakimskiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi(hayupo Pichani) wakati alipokuwa akifunga mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
H3
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi akipokea moja ya zawadi ya mfuko kutoka umoja wa nchi za ulaya (EU) kutoka kwa Afisa Miradi sehemu ya Uchumi na utawala kutoka umoja huo Bi Alexa DU PLESSIS wakati wa mkutano wa urithi wa utamaduni na ubunifu viwanda katika sekta ya utamaduni leo jijini Dar es Salaam.
H4
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Leah kihimbi akiongea jambo na mkuu wa Idara ya uchumi na utawala kutoka umoja wa nchi za ulaya(EU).Bw.Olivier Coupleux wakati wa mkutano wa urithi wa utamaduni na ubunifu viwanda katika sekta ya utamaduni uliokuwa na dhumuni la kuwajengea uwezo wasanii wa sanaa mbalimbali ili waweze kuhamasisha jamii katika kuwaletea maendeleo chanya.
H5

MANISPAA YA ILEMELA YAWEKA MSIMAMO WAKE DHIDI YA WAFANYABIASHARA WA HOTEL NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni.
Wafanyabiashara wa Hotel na
Nyumba za Kulala Wageni katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wametakiwa kufanya
biashara zao kwa mjibu wa kanuni na sheria za biashara zao ikiwemo kulipa
ushuru na kodi mbalimbali kama ilivyoidhinishwa na Serikali.
Kauli
hiyo imetolewa hii leo na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga, katika Kikao
cha Viongozi wa Manispaa ya Ilemela na Wafanyabiashara hao, juu ya Ufafanuzi wa
Sheria ya Kodi ya Malazi, ambayo imeanza kukusanywa kwenye Hotel pamoja na
nyumba zote za kulala wageni.
 
“Kama
una wajibu wa kulipa kodi Majengo, leseni ya biashara, mabango, ushuru wa
malazi, ushuru wa huduma na kodi nyingine zote zilizo kisheria, ni vyema
ukalipa bila kushurutishwa. Kutokufanya hivyo utatufanya twende kwenye ule
mkono mwingine ambao tusingependa sana kuutumia ambao ni kushurutishana”.
Amesema Wanga.
 
Hata
hivyo licha ya agizo hilo, Wafanyabiashara katika Manispaa hiyo wameiomba
Serikali kuwapunguzia mzigo wa Kodi walionao kwa kuwa hivi sasa wanakabiriwa na
mzigo mkubwa wa kodi pamoja na Ushuru jambo ambalo wamesema ni tofauti na ahadi
ya kuondoa kero ya kodi mbalimbali aliyoitoa Mhe.Rais John Pombe Magufuli wakati
wa Kampeni zake.
 
“Kodi
zimekuwa nyingi sana kwa sisi wafanyabiashara wa Hotel na Guest Houses (nyumba
za kulala wageni), kwa mfano kodi ya majengo, leseni ya biashara, ardhi,
mabango na nyinginezo. Yaani nyumba moja inakuwa na kodi zaidi ya 11 sasa
itafika sehemu tutashindwa kufanya biashara. Sisi tuko tayari kulipa kodi ya majengo,
ardhi na leseni hivyo serikali iangalie namna ya kutusaidia”. Alisema Nuru
Ramadhan ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa
ya Ilemela na kuungwa mkono na wenzake.
 
Hawa
Waziri ambae ni Mwanasheria wa Manispaa ya Ilemela, amewasihi Wafanyabiashara
hao kuwa tayari kulipa kodi zilizopo kisheria, ikiwemo Kodi ya Malazi huku
wakiendelea kujenga hoja Serikalini ili Sheria hizo zifanyiwe marekebisho
bungeni na hatimae kupunguzwa.
 
Awali
Wafanyabiashara wa Hotel na Nyumba za Kulala Wageni, walikuwa wakilipa Kodi ya
Malazi ambayo ni asilimia 20 ya mapato yanayotokana na malipo ya kila mteja,
kabla ya kodi hiyo kusitishwa na Serikali ambapo hata hivyo imerejeshwa tena na
Wafanyabiashara hao wanatakiwa kulipa kodi ya asilimia 10 ya mapato
yanayotokana na mteja badala ya 20 kama ilivyokuwa awali.
Kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni kikielendelea
Afisa biashara Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Hawa Waziri ambae ni Mwanasheria wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi kwa wanahabari juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Cyprian Oyier ambae ni mmoja wa wafanyabiashara wa hotel Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Lemmy Muganyizi Mboyelwa ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Nuru Ramadhani ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Melikior Fundi Minsa ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela wakiwa katika kikao cha ufafanuzi juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi
Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela wakiwa katika kikao cha ufafanuzi juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi
Kushoto ni Stella Lwakatare ambae ni Afisa Biashara Mkuu katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akifafanua jambo kwenye kikao cha Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi.
Katikani ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Paul Wanga na Kulia ni Peter Revelian ambae ni Mwekahazina wa Manispaa ya Ilemela.
Watumishi wa idara mbalimbali katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE AUGUSTINE MAHIGA ALA KIAPO CHA UBUNGE LEO

MAHIGA 2Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Kikanda, Augustono Mahiga akiapa  Bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAHIGA1
Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson akimwapisha  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki na Kikanda, Augustono Mahiga , Bungeni mjini Dodoma Februari 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UTEUZI – TRL

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemteua Bwana Masanja Kungu Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), ambako anakwenda kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias Mshana ambaye anastaafu hivi karibuni.
Kabla ya Uteuzi huo Bwana Masanja Kadogosa alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mikopo Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB). Uteuzi huo unaanza mara moja.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
02 Februari, 2016

MALINZI AMPONGEZA KIKWETE

jakayaRais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznaia (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa kukubali uteuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) na GAVI utakaomfanya kuwa bingwa wa chanjo na balozi wa mradi wa Africa United Duniani.
“Familia ya mpira wa miguu inajua umuhimu wa chanjo na hasa katika maendeleo ya vipaji na wanamichezo kwa ujumla na jinisi chanjo inavyoweza kuwapa watoto siyo tu fursa ya maendeleo bali pia haki ya kuishi” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Katika barua hiyo, Malinzi ameelezea furaha ya TFF kuona kiongozi wa Tanzania akiongoza mapambano ya kuokoa afya na uhai wa kizazi cha sasa na kijacho katika Afrika na dunia kwa ujumla.
“TFF itaunga mkono juhudi zako ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na ushirika wa chanjo” ilimalizia barua hiyo ambayo nakala yake imetumwa kwa Rais wa Caf, Issa Hayatou.

WANANCHI WA JIMBO LA BUMBULI WAMPONGEZA WAZIRI MAKAMBA

11
NA RAISA SAIDI, BUMBULI.
SERIKALI ya Tanzania imevunja rasmi mkataba na mwekezaji
wakiwanda cha kuzalisha Chai cha Mponde kilichopo wilayani Bumbuli
Mkoani Tanga na kuamuru kitwaliwe na kianze kazi mara moja.
Akizungumza katika mkutano uliowajumuisha wadau wazao la
chai,Msajili wa Hazina Laurence Mafuru amesema kuwa kwa mamlaka
aliyopewa amevunja rasmi mkataba huo kwasababu Mwekezaji
aliyekuwepo kashindwa kutekeleza makubaliano yaliyoweka .
Mafuru alisema kuwa wamefikia uwamuzi huo kutokana na
kujiridhisha pamoja na kupitia mikataba walioingia na mwekezaji
huyo ndipo serikali imeamua ikirudishe kiwanda hicho mikononi
mwa Wizara ya Viwanda na Biashara ili utaratibu mpya wa
uendeshwaji wa kiwanda uanze huku Bodi ya Chai Tanzania
ukiendelea kukisimamia mpaka hapo serikali itakapotafuta mwekezaji
mwingine.
Mei mwaka 2013, wakulima wa chai waliitisha mkutano na kumwalika
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Januari Makamba na kueleza kutokuwa na
imani na mwekezaji na Chama cha Wakulima wa Chai cha Usambara (UTEGA)
na kuamua kukifunga kiwanda licha ya Mbunge kuwasihi wasichukue uamuzi
huo wa hasira.
Tangu wakati huo jitihada nyingi zimefanyika zikiongozwa na Mheshimiwa
Makamba kuhakikisha kwamba kiwanda kinafunguliwa na wakulima wanauza
chai yao.
‘’ Tuliteseka kwa muda mrefu na leo Serikali imefanya uamuzi
wa kukirudisha kiwanda mikononi mwetu, Tunaishukuru Serikali kwa
kutusaidia sisi wananchi tulioteseka kwa muda mrefu ,” Alisema
Challes Ngovi ambaye ni mkulima wa chai Mponde.
Hata hivyo Mafuru alibainisha kuwa ucheleweshaji wa kukifungua
kiwanda hicho ulitokana na utaratibu uliokuwa ukifanywa na Serikali
na baada ya kujiridhisha ndipo ikaamua kumuandikia rasmi
barua Mwenyekiti wa Utega inayoonyesha kuvunjwa kwa mkataba huo
na kuamuru kiwanda kirudi Serikalini.
index
Kwa upande wake, Mbunge wa Bumbuli January Makamba alisema kwamba
kazi waliyomtuma wananchi ya kukirudisha kiwanda mikononi mwao
imekamilika ingawa imechukua muda mrefu.
Makamba ambaye pia ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
anayeshughuliokia Mazingira na Muungano alitumia nafasi hiyo
kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Magufuli kwa
kuingilia kati mgogoro huo ambao umedumu kwa zaidi miaka mitatu
na hatimae kuumaliza.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Umoja wa Wakulima wa Chai Usambara UTEGA
William Shelukindo aliilaumu serikali kutoka na uamuzi wake wa
kukitaifisha kiwanda hicho bila ya kutoa nafasi kwa mwekezaji kuweza
kujitetea kwani ni ameshindwa kuzalisha.
“Serikali katika hili imeshindwa kutupa nafasi ya kujitetea ili kuweza
kujua sababu za kushindwa kuzalisha ,lakini kwa sasa hatuna cha
kufanya zaidi ya kutekeleza matakwa yao”alisema Shelukindo.
Ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alisema kuwa siku 90 za
kupeleka malalamiko na utetezi kwa seriklai zilishatangazwaa na
kumalizika kilichobaki ni utekelezaji wa kanuni na taratibu za
serikali kukichukuwa kiwanda na kuanza uzalishaji .
“Niwaombe wananchi hakikisheni mnazalisha zao hilo kwa wingi ili
kiwanda kiweze kufanyakazi na kuboresha uchumi wa kila mmoja
wenu,wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla kwani Bumbuli mnategemea zao la
chai kwa kiasi kikubwa.
Wakati huo huo,Wananchi waishio maeneo mbalimbali katika Jimbo la
Bumbuli wilayani Lushoto mkoani Tanga wamempongeza Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira kwa
hatua ya kuwasaidia kuishawishi serikali kukipatia ufumbuzi mgogoro wa
kiwanda cha chai cha Mponde.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi, mmoja ya
wakulima hao,Swahiba Mbili alisema kuwa kufunguliwa utawasaidia
wananchi ambao walikuwa na changamoto ya mazao yao kuharibika shambani
kupata soko la uhakika ambalo linaweza kuwainua kimaisha.
Swahiba alisema kuwa wao kama wakulima pamoja na kuishukuru serikali
kutwaa kiwanda lakini wanamshukuru Januari Makamba kwa sababu hakuweza
kuwa mbali nao kwenye kipindi chote wakati kiwanda hicho kimefungwa na
kuaidi kumpa ushirikiano katika kipindi cha kuwatumikia wananchi hao.

fastjet yaongeza ndege ya tano 

 
Dar es Salaam, Januari
28, 2016
-Fastjet
Tanzania imeongeza ndege nyingine aina ya Airbus A319 kwenye  idadi ya ndege zake nne  na hivyo kuliweka shirika hilo la ndege la
gharama nafuu kuendelea na mipango yake ya kupanuka.
 
“Ndege
za fastjet kwa hivi sasa ni nne na zote zinatumika  na ongezeko la ndege ya tano  ni jibu kwenye mikakati yetu ya  kupanuka pamoja na hitaji la kuongeza uwezo
wa kubeba kwenye safari zetu za ndani na za kimataifa”, alisema  Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania, John Corse.
 
Ndege hiyo ya nyongeza  inafanya jumla ya
nafasi inayokuwepo kwa siku kwenye safari kwa ajili ya wateja kufikia 1,000.
 
Fastjet ilianza safari zake nchini mwaka 2012na hivi sasa inajiendesha kwa kutumia
ndege tano  aina ya A319 kwenye mtandao
wake wa safari ambao unahusisha Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro na
Zanzibar na kuifanya ijikite kuufanya usafiri wa anga ndani ya Tanzania watu
wote waumudu.
 
Hali kadhalika ilianzisha safari za kimataifa
kwenda Entebbe nchini Uganda, Nairobi Kenya,  Harare Zimbabwe, Johannesburg Afrika Kusini
na Lusaka nchini Zambia katika kipindi cha miaka mitatu ya kuendesha shughuli
zake.
 
“Tangu tuanze safari zetu  tumeshabeba abiria
zaidi ya 1,800,000 ambapo utafiti wetu unaonesha kuwa  zaidi ya theluthi moja  ya abiria wetu walikuwa ndio mara yao ya kwanza
kumudu  kusafiri kwa ndege”, anasema
Corse.
 
Aliendelea kusema, “kuongeza ndege  nyingine  kwenye safari zetu  kunatupa fursa muhimu ya kuongeza masafa kwa  njia zetu zilizopo  ili kukidhi
mahitaji ya wateja, na na inasaidia kwenye lengo letu la kuongeza njia
moja ya kimataifa kwenye mtandao wetu kwa mwaka huu 2016”.
 
Hali kadhalika, Corse anabainisha kuwa  ndege
hiyo mpya  inamanisha kuwa fastjet ni sawia
na ni kubwa katika kutosheleza kupanuka kwa shughuli za fastjet.
 
Ndege hiyo A319  ambayo ni Airbus  ni ya injini mbili  ambazo zinatoa kiwango cha juu cha ufanisi
pamoja na kiwango cha chini kabisa cha madhara kwenye mazingira, ikiwa ni
nyongeza kwenye  viwango vya juu vya hali
ya kuliwaza ndani ya ndege hiyo ya kisiasa.
 
Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba  abiria  156 ambaop wanamudu viwango vya chini vya
kuendesha mtindo wa maisha wa gharama nafuu ambao unaendeshwa na Fastjet
Tanzania.
 
Baadhi ya  njia muhimu ambazo ndege hiyo mpya
itakuwa inahudumia  ni njia mpya iliyoanzisjhwa hivi karibuni kati ya Dar es Salaam na Nairobi, Kilimanjaro na Nairobi  na Dar es Salaam kwenda Zanzibar ambazo zote zilianza kwa mara ya kwanza Januari 11, 2016. njia hizi mpya  zote ni kielelezo muhimu muda mrefu kwenye
upanuzi wa  njia za fastjet kitaifa na
kimataifa.
 
Fastjet inatarajia kuongeza ndege zaidi kwenye njia yake ya Kenya  kutokana na mahitaji ya wateja kuongezeka kunakosababisha na kumudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati, na hali
kadhalika  imeshajionesha kuwa  kuna matarajio ya  kuzindua
safari kati ya Zanzibar na Nairobi
na hali kadhalika kati ya Dar es Salaam na Mombasa baadaye mwaka 2016.
 
“Usafiri wa anga unaoumudu ni muhimu kwenye  kukuza uchumi wa Tanzanoa, hususani kwenye   kukuza sekta za biashara na utalii”, alisema
Corse.
 
Hali  kadhalika Corse alibainisha  kuwa ndege hiyo mpya inamaanisha kwamba ndege za
Fastjet zitatosheleza kiasi cha kutosha  kusaidia kwenye changamoto za usimamizi na uendeshaji  iwapo
ndege moja miongoni mwake  itakuwa haifanyi kazi au kama ipo kwenye matengenezo au ukarabati wa lazima.

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA

1
Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson akiingia Bungeni tayari kuongoza Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
2
Mhe. Balozi Dkt Augustine Maiga akuungia Bungeni tayari kwa kuapishwa.
3
Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson akimwapisha Mhe. Balozi Dkt Augustine Maiga.
4
Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson akiongoza Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
5
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa,majaliwa akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.George Masaju wakati kuongoza Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
9
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akifatilia Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
6
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika  Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
7
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika  Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
8
Baadhi ya wageni wakifatilia Kikao cha 6 cha Mkutano wa pili wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

KANDA WA MBEYA 
WAZEE WAWILI WAMEUAWA KIKATILI WILAYANI KYELA MKOANI MBEYA KUTOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA.
 MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAPAMBANO JIJINI MBEYA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
 MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WAZEE WAWILI WAKAZI WA KITONGOJI CHA BULINDA WILAYA YA KYELA MKOANI MBEYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. GENELI KAPWELA [65] NA 2. RAHABU BUNGULU [70] WALIUAWA KWA KUKATWA NA VITU VYENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA KISHA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.
MIILI YA MAREHEMU ILIKUTWA KATIKA NYUMBA WALIMOKUWA WAKIISHI MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KITONGOJI CHA BULINDA, KIJIJI/KATA YA MATEMA, TARAFA YA NTEMBELA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.
KATIKA TUKIO HILO, GENELI KAPWELA ALIUAWA KWA KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI NA KUKATWA MKONO WA KUSHOTO NA VIUNGO HIVYO HADI SASA HAVIJULIKANI VILIPO NA RAHABU BUNGULU ALIUAWA KWA KUCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.
INADAIWA KUWA, WANANCHI HAO WALIVAMIA NYUMBA WALIYOKUWA WAKIISHI MAREHEMU KISHA KUWAKATA NA VITU VYENYE NCHA KALI NA BAADA YA KUTEKELEZA MAUAJI HAYO, WATU HAO WALIANGUSHA NYUMBA WALIYOKUWA WAKIISHA AMBAYO ILIKUWA IMEJENGWA KWA MIANZI NA KISHA KUICHOMA MOTO.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI MAREHEMU WALIKUWA WANATUHUMIWA KULETA UGONJWA WA KIPINDUPINDU KIJIJI HAPO KWA NJIA ZA KISHIRIKINA. WATU WAWILI WAMEKAMATWA KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. ALIKO MWAMTOBE [47] MKAZI WA MATEMA NA 2. ALISOLOMON MWAMTOBE [49] MKAZI WA KITONGOJI CHA BULINDA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAPAMBANO ILIYOPO JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FELISTA MWANSASU [12] AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.949 CVS AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA NSAJIGWA ALISALA [39] MKAZI WA MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 07:50 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MAFIATI, KATA YA MUUNGNANO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA, UPELELEZI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWENDESHA PIKIPIKI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ASIFIWE MWANTOBE [25] MKAZI WA TUNDUMA MKOANI MBEYA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 975 CPS AINA YA TATA BUS LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA EMANNUEL ADAM [36] MKAZI WA MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO MAPOROMOKO KATIKA BARABARA YA TUNDUMA/MBEYA, WILAYA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MARA BAADA YA AJALI HIYO PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA MAREHEMU ILITOROSHWA NA WATU WASIOJULIKANA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA WA BASI AMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA NA KUHESHIMU SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUWA MAKINI KATIKA MATUMIZI YA BARABARA HASA KWA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

DC KINONDONI, PAUL MAKONDA APOKEA SARUJI MIFUKO 1640 KUTOKA KWA WADAU WA MAENDELEO KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARY

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Duma, Areeq Amran Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mfuko mmoja wa saruji kati ya 640 aliyoitoa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule za Sekondari za wilaya hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Katika makabidhiano hayo Makonda alipokea mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Alex Malasusa aliyetoa mifuko 500. 
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo (kulia), akimkabidhi saruji hiyo DC Makonda.
 Lori lilibeba saruji hiyo likiwa eneo la tukio.
 DC Makonda na wageni wake wakiwa eneo la tukio kabla ya makabidhiano ya saruji hiyo.
 Mhe. Bulembo akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo.
Wanahabari wakizungumza na watoa msaada huo.

Serikali kuimarisha miundombinu kuboresha Utalii nchini.

indexNaibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu maswali toka kwa wabunge katika kikao cha 6 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO
………………………………………………….
Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imejipanga kuimarisha miundombinu inayoelekea kwenye mbuga za wanyama na vituo vingine vya utalii nchini ili kuboresha utalii wa ndani na wa nje ya nchi kwa kujenga barabara ili kuwezesha watalii kufika kwa urahisi katika sehemu za vivutio vya kiutalii.
Akijibu swali la Mhe.Risala Said Kabongo Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) lililoulizwa serikali ina mikakati gani kuboresha miundombinu ya barabara, malazi na viwanja vya ndege katika hifadhi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani amesema jitihada zimefanya na zinaendelea kufanywa ili kuboresha na kuimarisha barabara mbalimbali zinazoelekea katika hifadhi mbalimbali nchini kwa kiwango cha lami ili kuongeza wigo wa watalii kutembelea maeneo hayo kwa urahisi.
Amezitaja barabara ambazo zilizoko kwenye mpango wa kuziboreshwa ili kurahisisha watalii kuyafikia maeneo hayo kuwa ni barabara ya Sumbawanga-kasanga, barabara ya Kigoma kuelekea kusini hadi Kalya na Mwese.
“Sio tutaboresha barabara tu ila tunaviangalia pia viwanja vya ndege vinavyotumika kwa kuviimarisha na kuviboresha viwanja vya ndege vya Songwe,Kigoma na Mpanda ambavyo vitasaidia kufikika kwa urahisi maeneo ya vivutiio”
“ Tunaendelea kuvutia wawekezaji binafsi kutoa huduma mbalimbali za watalii kama malazi na mpka sasa tumetoa vibali 11 kwa wawekezaji kuwekeza katika malazi yaani Hoteli za kitalii katika Hifadhi za Ruaha,Mikumi,katavi na Mahale na uwekezaji huo uko katika hatua za utekelezaji” Alisema Mhe. Ramo Makani.
Wizara kwa kushirikiana an Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Shirika la USAID inaandaa mikakati ya kuendeleza na kuutangaza utalii kwenye maeneo mbalimbali na kuboresha miundombimu ili kuwezesha watalii kufikia vivutio kiurahisi.

MSANII WA FILAMU ROSE NDAUKA NA MENEJA WAKE WAZINDUA JARIDA LITAKALOKUWA LIKITOKA KWA WIKI MARA MOJA

 Msanii wa Filamu nchini, Rose Ndauka (kushoto) na Meneja wake Ramaehan Mwanana wakionesha Jarida jipya litakalojulikana kama  Rozzie Magazine wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
 Meneja wa Ndauka Ramaehan Mwanana (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Rose Ndauka, akizungumza katika uzinduzi huo.
…………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
MSANII wa filamu Tanzania, Rose Ndauka  amezindua jarida  jipya liitwayo Rozzie litakalotoka  mara moja kwa kila mwezi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, wakati wa uzinduzi huo, Rose alisema dhumuni kubwa la jarida hilo ni kuelimisha, kuiburudisha, kuikosoa na kuichochea jamii katika kufikia malengo yao ya kimaisha  kwa ujumla  na kujenga taifa bora lenye maendeleo.
“Pia katika kurasa za ndani  za jarida hilo  zipo kurasa zilizobeba mambo ya fasheni, maisha pamoja na mambo mbalimbali yanayoikosoa jamii pale inapokosea,” alisema.
 
Alisema kuwa lengo la kutoa jarida hilo ni kuwafikia watanzania wote na nakala yake itapatikana  kwenye mtandao ya kijamii mara moja kwa kila wiki.
Alisema magazine hiyo anaitoa bure  kiwa watanzania wote  na litakuwa likitoa taarifa  taarifa mbalimbali  kwenye mitandao yote ya kijamii ambayo ni Facebook, Instagram, Twitter na You Tube.
 
Meneja  wa jarida la Rozzie, Ramadhani Mwanana, alisema wameanza kwa kuchapisha kopi 5,000 na jinsi wanavyoendelea waziongeza  nyingi zaidi.
Alisema jarida  hilo ltasambazwa katika mikoa yote hapa nchini  kwa kutumia magari makubwa ya mikoani, maduka mbalimbali pamoja na nyingine zitakazowezesha watanzania kupata magazine hiyo.

Mpango wa TASAF Awamu ya Tatu kuboreshwa

ang1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Angella Kairuk akijibu maswali toka kwa  wabunge katika kikao cha 6 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na raymond Mushumbusi MAELEZO
…………………………………………………………………………………
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
Serikali imejipanga kuborsha zaidi mpango wa kunusuru Kaya masikini nchi ujulikanao kama TASAF kwa awamu ya tatu kwa kutengeneza miundombinu mizuri ya kutambua Kaya zinazolengwa na kuondoa malalamiko ya wananchi kuwa mpango huu umekuwa ni wa Kaya chache na fedha hizo utolewa kwa upendeleo.
Akijibu swali la Mhe.Magdalena Hamisi Sakaya Mbunge wa Kaliua (CUF) lililouliza ni vigezo gani vinatumika kuondoa Kaya zilizopendekezwa kwenye mradi na kubakiza Kaya chache, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema mpango wa kunusuru Kaya maskini hutambulishwa kijijini na wataalam kutoka Halmashauri husika kwa kusimamiwa na uongozi wa kijiji kisha kuweka vigezo vya Kaya maskini.
“  Wakusanya taarifa huchaguliwa kutoka miongoni mwa vijana wanaoishi kijijini hapo na kupitia nyumba kwa nyumba kuorodhesha Kaya ambazo zinakidhi vigezo vilivyoanishwa na mkutano wa Kijiji ila bado kuna malalamiko yanayotolewa kuwa Kaya maskini zinaachwa na kupewa Kaya nyingine ambazo sio maskini  kwa kuliona tatizo hilo suala hili tunalifanyia uchunguzi na tunaomba watu watoe taarifa ikiwa wataona ukiukwaji wa uorodheshaji wa Kaya zitakazohusika na mpango huu ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya yoyote atakaye bainika kufanya hivyo”
“ Mpaka sasa kutokana malalamiko yaliyojitokeza katika kuorodhesha Kaya maskini zinazotakiwa kuwezeshwa na mpango huu tumewaajibisha watendaji toka Wilaya za Karagwe, Kagera na Kibondo, Kigoma na tuomba kupewa taarifa kwa sehemu yoyote ambapo kutatokea tatizo kama hili na tutachukua hatua mara moja kuokoa fedha zilizotakiwa kwenda kusaidia watu husika” Alisema Mhe Angella Kairuki.
Aidha Mhe. Angella Kairuki ameongeza kuwa kuna taarifa zinazoenezwa kuwa fedha za mpango wa TASAF Awamu ya Tatu ni fedha za freemasons, taarifa hizo sio za kweli kwani fedha hizi zizantolewa na Serikali ili kusaidia Kaya maskini ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kupata Elimu Malazi na chakula bora.
TASAF ni mpango wa kunusuru Kaya maskini na imekuwa katika awamu tatu mpaka hadi sasa kwa ajili ya kuwezesha Kaya maskini kujikwamua kiuchumi.

Serikali itaendelea kuwafungia mageti watumishi

KIP1
Na.Catherine Sungura-Nzega
Serikali haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa umma wachache wakinufaika na kufaidi pesa za walipa kodi hususan wa kipatao cha chini na wale maskinini
Hayo yamesema wilayani hapa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangwalla alipokuwa akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo
Dkt.Kigwangwalla alisema serikali ya awamu ya tano inawataka watumishi wote nchini kufanya kazi  za kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu hii haiwezi kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.
“Serikali haitowav umilia watumishi wazembe,hivyo tutaendelea kuwafungia mageti na kuwashughulikia wale wazembe,tunataka watumishi wa umma wafanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi,mtumishi akizembea tutamtumbua majipu,akichelewa tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na kumpeleka jela,hii ndiyo serikali ya hapa kazi tu”
Aidha alisema serikali ya awamu ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe kazi na kutekeleza ahadi zote za  ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.
“hatutomuonea mtu,lakini tutafanyia kazi pale penye matatizo,tunataka Tanzania mpya ya mwaka 2015 inakua,hatutaki hadithi wala ahadi”
Hatahivyo aliwataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa kwenda shule kuwapeleka watoto wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na hakuna michango yoyote.
“natoa wito kwa walimu wote wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi wanaowapeleka kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za kuendeshea shule hizo.
Dkt. Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa umma kujipanga na kama watagundulika ni majipu bali hawatosita kuwatumbua hadi kina kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma

Waziri Suleiman Jafo:Serikali kuongeza ajira

jafo1
Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe  Suleiman Jafo akijibu maswali toka kwa  wabunge katika kikao cha 6 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
………………………………………………………………………………………………….
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 imepanga kuongeza ajira kwa vijana ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania kwa kuongeza ajira na kuwezesha wengine kujiajiri kupitia mifuko ya uwezeshaji toka Halmashauri za Wilaya nchini.
Akijibu swali la Mhe.Mgumba Tebweta Omary Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM) lenye sehemu a na b lililouliza Serikali itaanza lini kuwawezesha vijana wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki  kifedha ili waweze kujiajiri na kuondokana na tatizo la ajira na umaskini ,Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe  Suleiman Jafo amesema vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kusini Mashariki wamekuwa wakiwezeshwa kiuchumi kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambapo kila Halmashauri hupaswa kutenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kila mwaka kwa ajili ya vijana.
Mhe  Suleiman Jafo ameongeza kuwa katika Bajeti ya mwaka 2014/2015,Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilifanikiwa kutoa Shillingi Millioni 10.3 kwa vikundi vya vijana 19 kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi na katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016 vikundi vya vijana vilitengewa Shilllingi Millioni 87.5 ili kuviwezesha kiuchumi kwa kujiajiri.
“ Katika kutatua changamoto zilizopo kwa vijana tunawawezesha  kifedha ili kujiajiri ili kumekuwa na tatizo la fedha kuchelewa kufika kwa walengwa ila Serikali kupitia Wizara yangu tunalifanyia kazi ili fedha zifike kwa wakati na tumetenga Shillingi Millioni 50 kwa kila kijijikwa ajili ya kuwezesha vijana walioko katika vikundi mbalimbali mfano SACCOS ili waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi kwa kujiondoa katika hali ya umaskini”
“ Napenda kuwaomba wabunge tusaidiane sababu wao  wanahusika katika kamati za fedha za Halmashauri za Wilaya, waende wakasimamie hizo fedha kwa ajili ya kuwezesha vijana  zitoke na ziwasaidie walengwa” Alisema Mhe Jafo.
Aidha Mhe  Suleiman Jafo amesema kuwa Serikali imetenga Shillingi Billioni 233 kwa ajiri ya kuajiri vijana wapya takribani 71,408 kati ya hao watumishi wapya wa Afya wanatarajiwa kuwa takribani 10,871 na Waalimu 40,000 kwa nchi nzima ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza vyuo mbalimbali nchini.
Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya imejipanga katika kuwawezesha vijana katika maeneo yao kujikwamua kiuchumi kwa kujiajiri na kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali itaboresha zaidi mifuko ya kuwezesha vijana katika Halmashauri za Wilaya kwa kununua vifaa zaidi vya kujifunza stadi mbalimbali za kazi zitakazowezesha vijana wengi zaidi kuwa na ujuzi utakaowasaidia kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi.

MTUMISHI WA WIZARA YA HABARI AFARIKI KWA AJALI YA GARI.

kif1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel ameitumia salamu za Rambirambi familia ya Mzee Dellan Tarmo kufuatia kifo cha  kijana wao mpendwa Jovitha Dellan kilichotokea kwa ajali ya gari mkoani Arusha juzi tarehe 31.1.2016.
“Pokea rambirambi zangu za dhati, sote kwa pamoja tumepoteza kijana  mchapakazi, hodari na aliyepen
da kushirikiana na wenzake katika kazi zake, hakika tutamkumbuka siku zote”
Katibu Mkuu amesema.
Katibu Mkuu, Pia amemtumia salamu za pole kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu(KBF) na Wafanyakazi wote wa Bodi ya  Filamu Tanzania.
“Nimepokea taarifa za kifo cha Jovitha Dellan kwa huzuni kubwa, najua machungu na maumivu mliyonayo kwa kuondokewa na kiungo muhimu katika utendaji wenu, poleni sana,  niko nanyi katika msiba huu mzito kwenu”, amesema Katibu Mkuu huyo.
Katibu Mkuu amesema pamoja na kwamba kifo hakiepukiki, bado ni kitu ambacho kinashtua, kuhuzunisha na kuleta unyonge mkubwa kwa wafiwa katika jamii.
 “Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu kumuombea kijana wetu Jovitha Dellan ili mwenyezi Mungu ampe mapumziko mema ya Milele” Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape uvumilivu na subira katika kipindi hiki”.
“Niko nanyi katika kipindi hiki kigumu kwa hali na mali, nawaomba msijisikie wapweke” Katibu Mkuu amesema na kuwatakia utulivu na amani katika kipindi hiki cha msiba mkubwa kwa familia.
Marehemu Jovitha Dellan  amefariki juzi tarehe 31 Januari, 2016 mkoani Arusha ambapo alikuwa njiani kurejea kazini jijini Dar es salaam.
                                               Marehemu Jovitha Dellan anatarajiwa kuzikwa wiki hii mkoani Manyara .
                                               Jovitha Dellan alikuwa ni Afisa Utamaduni aliyekuwa akifanya kazi katika Bodi ya Filamu Tanzania iliyopo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Jovitha Dellan mahali Pema Peponi, Amina.

WASANII WATAKIWA KUEPUKA RUSHWA KWENYE KAZI ZA SANAA

kw1Msanii mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star Mayunga Malini (Kulia) akiongea na wadau wa Sanaa (hawako pichani) mapema wiki hii kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Wengine katika picha ni Afisa Habari wa BASATA, Aristides Kwizela (Katikati) na Afisa Sanaa wa Baraza hilo Augustino Makame.
kw2Msanii mkongwe wa Sanaa za Maonesho Nkwama Ballanga akimpongeza Msanii Mayunga kwa juhudi zake na kujituma katika kazi anazofanya. Wadau wengi wa Sanaa waliohudhuria kwenye programu ya Jukwaa wiki hii walifurahishwa na juhudi binafsi za Msanii Mayunga.
kw3Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria programu ya Jukwaa la Sanaa wakimfuatilia kwa makini Msanii Mayunga.
…………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
Wasanii nchini wametakiwa kujituma na kutengeneza kazi za Sanaa zenye ubora na kuachana na dhana ya kutegemea rushwa na hongo katika kuyafikia mafanikio yao kisanaa.
Wito huo umetolewa mapema wiki hii na wadau wa Sanaa kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa ambayo huandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kufanyika kwa mwezi mara mbili siku ya Jumatatu kwenye ukumbi wa Baraza hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau hao walisema kwamba kumekuwa na wimbi la wasanii na mameneja wa wasanii kutegemea rushwa za fedha na wengine kufikia hatua kutoa rushwa za ngono ili kufanikiwa kisanaa hasa katika kuvishawishi vituo vya radio na televisheni kucheza nyimbo zao.
“Ukweli ni kuwa rushwa na hongo zinaendekezwa na wasanii walioshindwa. Msanii anayejitambua hawezi kutoa rushwa ili wimbo wake uchezwe. Lazima wasanii waachane na dhana hii potofu, waelewe kwamba kazi ya Sanaa iliyo bora itapendwa tu na kukubalika na jamii” alisema Nkwama Bhallanga ambaye ni Msanii wa Sanaa za Maonesho.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha wachezesha disko (TDMA) Asanterrabi Mtaki alisema kuwa dhana kwamba wasanii lazima wahonge watangazaji au ma DJs ili nyimbo zao zichezwe ni potofu na ni chanzo cha kutangaza muziki au kazi za Sanaa zisizo bora na kuziacha zile zenye ubora.
“Kama wimbo wako ni mzuri kwa nini uhonge au utoe rushwa ili uchezwe? Hapa ndipo tatizo la kuendekeza kazi mbovu za Sanaa linapoanzia. Muziki wa wenye fedha na wanaohonga ndiyo unasikika, ule mzuri unaondaliwa na wasanii wasiyo na uwezo haupati nafasi” alisema Mtaki.
Alitoa wito kwa wasanii kufikiria njia mbadala za kutangaza nyimbo zao hasa kumbi za disko badala ya kutegemea vituo vya radio pekee.
Awali akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa, Msanii na mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star Mayunga Malini alisema kuwa wasanii hawana budi kujituma, kutafuta fursa na kuzitumia ipasavyo hasa kwa kutumia muda mwingi kubuni kazi zenye ubora.
Aliongeza kuwa, wasanii hawana budi kuachana na dhana ya utegemezi na kutegemea fedha na hongo katika kupata mafanikio kwani kazi za Sanaa zikitengenezwa kwa ubora na kwa kuzingatia vigezo vyote zitapendwa na kutuzwa tu.

Mwamuzi wa kwanza mtanzania wa mchezo wa Baseball.

kij
Kijana Innocent Kennedy ni mtanzania mwenye umri wa miaka 19 tu na kwasasa amekuwa ni gumzo kwa vyama vya kulipwa vya mchezo huu wa baseball barani Asia hususani nchini Japan.
Innocent ameonyesha umahiri mkubwa wa kuamua na kwa mara ya kwanza alishiriki katika kuamua mashindano ya Africa ya kutafuta uwakilishi wa kombe la Dunia la mchezo huu, mashindano yaliyofanyika nchini Kenya katika jiji la Meru hapo Disemba, 2014.
Kwasasa kijana Innocent anaendelea na masomo yake ya ICT jijini Dar es Salaam na ametenga muda wake wa kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 13 :30 hadi saa 18:30 jioni kufika viwanjani Azania Sekondari kushiriki mazoezi ya timu ya Taifa ya baseball.
Katibu mkuu wa mchezo wa Baseball bwana Alpherio Nchimbi alipoulizwa juu ya ndoto ya kumuendeleza kijana huyo, bwana Nchimbi alisema kwa kifupi kuwa lengo kuu ni kuzalisha akina Innocent wengi lakini kwa Innocent anafanyiwa mipango mahususi ya kumpeleka nchini Japan kwa mafunzo zaidi.

WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA SILAHA KUHAKIKI SILAHA ZAO KWA WAKATI

 
Kamanda Liberatus Sabas, alipokuwa akifunga Kampeni za ABIRIA PAZA SAUTI, Jijini Arusha,
………………………………………………………………………….
Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limewataka watu wote wanaomiliki silaha kwa njia halali wafike kwenye kituo cha polisi kuhakiki silaha zao na kuzilipia kama inavyostahili na kwa kufuata utaratibu kama sheria inavyoagiza. 
 Hayo ya mesemwa Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, kwamba kila mwaka huwa kila mwenye silaha anafika polisi na silaha yake na vitabu vyake kwaajili ya kuihahiki na kuilipia kama inavyostahili ,na kama zipo tuhuma zozote kutokana na matumizi ya silaha, itasimamishwa kwaajili ya taratibu zingine na kunyang’anywa hadi hapo jeshi litakapojiridhisha kuwa silaha hiyo matumizi yake ni sahihi ama siyo sahihi
Kamanda amesema utaratibu huu huwa unaratibiwa na makao makuu ya jeshi la polisi kwaajili ya kuhakiki silaha ,ikiwa ni pamoja na kulipia mapato ya serikali ,amewataka watu wanaomiliki silaha wafuate masharti yake kama inavyotakiwa, nawakumbuke sheria inambana kila mtu mara anapotenda kosa ,na kama mtu akiitumia ndivyosivyo atanyang’anywa silaha kwa kutumia sheria iliyowekwa. 
Ameongeza kuwa wapo watu ambao wamewatishia silaha wenzao,na wengine kesi zao zipo tayari na zingine zimefutiwa umiliki kwa mujibu wa sheria, amesema kimsingi kabla mtu hajakabidhiwa silaha ili amiliki, yapo masharti yakufuata na yapo kwenye kitabu kile cha leseni anachopewa wakati wa umiliki, amesema kuwa ukitoka nje ya hayo masharti huna sifa ya kumiliki silaha. 
 Kamanda Sabas ametoa anagalizo kwa wamiliki wa silaha na kusema kuwu silaha ya moto siyo kama panga,silaha hiyo ukiifanyia kosa mara moja yaweza kuua mtu au watu hivyo amewataka kuwa makini sana katika ufuatiliaji wa umiliki, pamoja na namna zinavyotunzwa,amesema jeshi la polisi lipo makini kufuatilia kwa ukaribu wakithibitisha silaha haitunzwi kama inavyostahili utanyang’anywa.aidha amesema kwa wazee amabao umri wao umeenda nab ado wanamiliki silaha huwa wanaichukua na kuihifadhi . 
Amehitimisha kwa kusema kuwa kila , mtu amnayetaka kumiliki silaha, kamati za ulinzi na usalama kuanzia kwenye kata ,Wilaya, Mkoa wakamuidhinisha kuwa na silaha afuate masharti na kuitunza silaha isije ikaangukia kwenye mikono ya wahalifu wakaitumia isivyo halali sheria itafuata mkondo wake, Silaha huwa zinatakiwa kulipiwa kila mwaka kuanzia mwezi julai hadi septemba ukichelewa kulipia unapigwa penati kwa mujibu wa sheria.

MADEREVA DALADALA JIJINI MWANZA WATISHIA KUGOMA IKIWA MAJIPU YA TAX BUBU HAYATATUMBULIWA.

Ridhione Senga (wa pili kushoto) ambae ni Mwenyekiti wa Madereva wa Daladala wanaofanya shughuli zao katika barabara ya Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza, jana akilalamikia suala la uwepo wa tax bubu linalowasumbua katika shughuli zao.
 
Alisema licha ya madereva wa tax bubu wanaobeba abiria kama daladala katika eneo wanalofanyia kazi hususani kubeba abiria wanaoenda na kutoka katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kuzuiliwa, bado madereva hao wa tax bubu wameendelea na biashara hiyo kama kawaida.
 
Senga alibainisha kwamba hatua hiyo inawaweka katika wakati mgumu katika kutimiza majukumu yao kutokana na kupata hasara kila kukicha ambapo amesema ikiwa itaendelea wataitisha mgomo ili kushinikiza kilio chao kufanyiwa kazi.
 
“Sisi tunalipa mapato, lakini jambo la ajabu hawa madereva wa tax bubu ambao hawana leseni ya kubeba abiria wamekuwa ndio wanafanya kazi ya daladala licha ya kupigwa marufuku katika kikao tulichokaa ijumaa iliyopita baina ya Sumatra, halmashauri ya Jiji, Polisi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na wawakilishi wengine bila kuwasahau viongozi wa daladala na tax. Kama hali hii itaendelea tutafanya mgomo hapa na hakuna huduma yoyote ya kubeba abiria itakayotolewa”.Alisema Senga.
 
Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko Jijini Mwanza aliunga mkono hoja ya mwenyekiti huyo na kusema kuwa ikiwa mamlaka husika zitashindwa kutatua suala la tax bubu katika eneo hilo, wao watachukua hatua ya kusitisha huduma ya usafirishaji katika barabara hiyo ya Bugarika-Buzuruga.
 
“Hizi tax bubu tunasikia ni za wakubwa na ndiyo maana hawa madereva wanaoziendesha wana jeuri mno. Sisi tunasema haya ni majipu na tunawaomba viongozi wengine wakubwa akiwemo Mhe.Magufuli, waangalie huku Jijini Mwanza maana kuna majipu makubwa ya kutumbua”.Alisema Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.
 
Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza, ameshauri suala hilo kutatuliwa na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuwa ndilo lenye jukumu la kukamata vyombo vya usafiri vinavyofanya kazi kwa kukiuka sheria na taratibu zilizoweka na mamlaka husika ikiwemo halmashauri ya Jiji Mwanza ambayo ndiyo inasimamia taratibu la utendaji kazi wa tax.
 
Juhudi za kuwatafuta madereva wa tax hizo zinazodaiwa kufanya kazi kinyume cha sheria (tax bubu) bado zinaendelea ili kujua kuzungumzia malalamiko yanayowakabiri.
Ramadhan Idd ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Madereva wa daladala za Bugarika-Muzunguko akitoa malalamiko yake.
Athuman Bin Malick ambae ni mmoja wa madereva wa daladala za Bugarika-Mzunguko Jijini Mwanza.
Kulia ni Kaptaini Michael Rogers ambae ni Afisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi wake.

MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI WANUFAISHA KAYA MILIONI 1.1 NCHINI

Mpango wa Kijamii wa Uzalishaji Salama ili kusaidia kaya masikini kupambana na umasikini (PSSN) umefanikiwa kuwa na matokeo mazuri kwa kusaidia kaya Milioni 1.1 nchini na kusaidia juhudi za serikali kupambana na umasikini.
Hayo yamefahamika wakati washirika wa maendeleo ambao ni Umoja wa Mataifa, Benki Kuu ya Dunia, Serikali ya Uingereza kupitia kitengo cha Maendeleo ya Kimataifa, Irish Aid, USAID, Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Sweden (SIDA) walipotembelea miradi ya maendeleo katika wilaya za Unguja, Chamwino, Babati, Sumbawanga (Manispaa na Wilaya), Singida na Hanang kwa kipindi cha siku tatu kuanzia Januari, 19 hadi 22.
unnamed
Bi. Kazijya Kila ambaye ni mmoja wa wanufaikaji wa fedha akitoa ushuhuda kuhusu mradi wake wa chakula ulivyowezeshwa na TASAF ambapo hadi hivi sasa anatengeneza faida ya Shilingi 7000 kwa siku na kabla ya kuwezeshwa alikuwa akikaa nyumbani na mama yake bila kuingiza kipato chochote.
Katika Mpango huo ambao utekelezwaji wake unasimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unafanyika Tanzania Bara na Tanzania visiwani ukiwa na lengo la kuzisaidia kaya masikini pesa za matumizi ili kukidhi mahitaji ya kupata chakula pamoja na kuwawezesha kusaidia watoto wao kupata elimu jambo ambalo linaonekana kuzaa matunda kwa maeneo mengi ikiwepo Tanzania visiwani.
Serikali ya Tanzania imekuwa ikisaidia na washirika wa maendeleo ili kupunguza umaskini uliokithiri kwa wananchi wake na mwaka 2013 iliweka mpango wa kusaidia kaya masikini 275,000 kwa kipindi cha miaka mitano na tangu ianzishe mpango huo ilifanikiwa kusaidia kaya 275,000 kwa mwaka 2013 pekee katika wilaya nane nchini.
unnamed (1)
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed (kushoto) na Msimamizi wa mpango wa PSSN, Bw. Ramadhani Madari wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu kwa wanufaikaji wa fedha hizo.
Na mpaka kufikia sasa mpango huo umeshatoa malipo mara 12 na jumla ya kaya masikini milioni 1.1 zimeshafaidika na mpango huo ikiwa ni kwa wilaya 161 na vijiji 9789 nchini.
Malengo ya serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa ni kuhakikisha kufikia mwaka 2030 kunakuwa hakuna masikini hivyo ni wajibu wa kila nchi kuhakikisha inawasaidia wananchi wake ili wajijengee uwezo wa kujitegemea na kuondoka katika janga la umasikini.
unnamed (2)
Asilimia kubwa ya wanufaikaji wa mpango huo ni wanawake, kama wanavyoonekana pichani.
unnamed (3)
Mkurugenzi wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus Kamagenge akizungumza na wanufaikaji wa mpango wa TASAF (hawapo pichani).
unnamed (4)
Mkurugenzi wa Huduma za jamii kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Amadeus Kamagenge (kushoto) akifurahi jambo na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed.
unnamed (5)
Timu ya TASAF na wadau wa maendeleo wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo.
unnamed (6)
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Jamii kutoka Benki ya Dunia, Bw. Muderis Abdulahi Mohamed na Aine Mushi wa UN/NRA.
unnamed (8)
Bi Jabo Omari Othman akiwa kwenye shamba lake alilonunua kutokana na fedha za TASAF visiwani Unguja.

No comments:

Post a Comment