Pages

Wednesday, February 3, 2016

KATIBU MKUU NISHATI NA MADINI, JUSTUS NTALIKWA, AFANYA ZIARA HUKO SONGOSONGO


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PanAfrican Energy David K. Roberts (kulia) akimuelezea jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa wakati wa ziara yake huko Songosongo katika visima vya gesi asilia.
Ni katika ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa katika visiwa vya Songosongo.
PanAfrican Energy Operational SH Engineer, Onestus Mujemula akielezea jambo kwa wana habari katika ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini huko Songosongo kwenye visima vya gesi, kutoka kushoto ni PanAfrican Energy Country Chairman Patrick Rutabanzibwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa na CSR Manager Andrew Kashangaki (wakwanza kulia)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akipata maelezo ya mradi kutoka PanAfrican Energy Operational SH Engineer Onestus Mujemula kuhusu mradi wa uchimbaji gesi asilia katika visima vinne uliomalizika kwa kutumia mtambo wa kisasa wa “RIG”
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa akiongea na wana habari wakati wa ziara yake ya kikazi katika visiwa vya Songosongo.

MO DEWJI BLOG YAWANASA LIVE WAFANYAKAZI WA TAMBAZA WAKIOMBA RUSHWA (PICHA&SAUTI)

Agizo la serikali kuzuia usafiri wa bodaboda mjini umegeuka kuwa kitega uchumi kwa baadhi ya vijana walioajiriwa kuhakikisha agizo inatekelezwa.
Hii imethibitika baada ya mwandishi wa Mo Dewji Blog kufumania tukio la vijana wa jiji wakidai rushwa wazi wazi bila woga kwa mwendesha pikipiki wa magurudumu watatu maarufu kama bajaji.
Kachero wetu (jina limehifadhiwa) alifanikiwa kupata picha za wala rushwa pamoja na kunasa sauti za tukio lote.
IMG-20160203-WA0009
Baadhi ya wafanyakazi wa Tambaza wakiwa pembezoni ya barabara katika daraja la Salenda.
IMG-20160203-WA0010
Mmoja wa mfanyakazi wa Tambaza akisimamisha bajaji.
IMG-20160203-WA0014 IMG-20160203-WA0015
Wafanyakazi wa Tambaza wakizungumza na dereva wa bajaji na kumuomba rushwa ya shilingi 10,000
IMG-20160203-WA0012

Katibu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Februari 3,2016. wakati akitoa taarifa ya kupinga kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.Sheikh hiyo machachari "amemzodoa" sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Alhad Musa Salim, ambaye alinukuliwa akisema, kiongozi wa Uamsho ambaye yuko korokoroni akikabiliwa na mashtaka ya kusababisha hofu Kyle Zanzibar, Sheikh Farid, kuwa ameridhia uchaguzi wa Zanzibar kurudiwa. "Mimi nimemtembelea Leo, (Jana Feb 2, 2016), sheikh Farid na baada ya kumuuliza KUHUSU taarifa ya sheikh Alhadi, alipinga vikali nakukanusha maneno hayo." Sheikh Ponds aliwaambia waandishi wa habari.

Msemaji wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam Tanzania, Sheikh Rajab Katimba akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi huo Zanzibar.
Sheikh Ponda akisalimiana na mwanahabari Said Powa wa gazeti la Tanzania Daima baada ya kumaliza kuzungumza na wanahabari.
Sheikh Ponda akiondoka baada ya kuzungumza na wanahabari.
 Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Februari  3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Manyovu, Albert Obama Ntabaliba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari3, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Abuu Jumaa (katikati) na Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson  Rweikiza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 3, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

:Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana kwa furaha na wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao, Leo February 3, 2016.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
Kigamboni, jijini Dar es salaam
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitembelea chumba cha kujifungulia cha zahanati ya  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema akimkaribisha Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kuhutubia wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
Kigambo ni, jijini Dar es salaam 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mchele, unga na maharage Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mchele, unga na maharage Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, 
Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu
Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar. 
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano  TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali  unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06#  na utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15  mfano   IMEI 12456789067654  Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY  C5555 - Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mikononi Tigo,
Diego Gutierrez, akizungumzia uzinduzi huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam usiku wa Februari 2, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
KAMPUNI ya simu za mikononi Tigo, imezindua huduma ya bure ya WhatsApp kwa wateja wake kuanzia Usiku wa Februari 2, 2016, wateja watakuwa wanachat bure. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,  Diego Gutierrez amewaambia wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel jijini Dar es Salaam
“Ushirikiano huu ni wakwanza nawaina yake katika sekta ya mawasiliano hapanchini.” Aliandika Diego kwenye WhatsApp yale iliyorushwa moja kwa moja kupitia screen kubwa iliyokuwa ukumbini.
“Ushirikiano huu wa kihistoria una maa kuwa, wateja wa Tigo sasa ni sehemu ya familia kubwa ya kimataifa ya watumiaji Milioni 900 na huduma ya WhatsApp Duniani.” Alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Tigo.
“Na hii ni namna yetu ya kutoa shukrani za dhati kwa wateja wetu kwa kuwapa huduma bora na za viwango vya juu zaidi kwa lengo la kuwafurahisha wateja wetu wa tigo.” Alimaliza ujumbe wake Mkurugenzi huyo wa tigo.
Tigo ambayo kwa sasa ina jumla ya wateja Milioni 10 waliosajiliwa na kutoa ajira 300,000 kote nchini ilianzishwa mnamo mwaka 1994.

 Ujumbe wa Mkurugenzi Mtendajiwa Tigo
 Ilikuwa ni furaha na usiku wa mask

 wakichukua Selfie tayari kWhatsaap jamaa na marafiki bureeee




 Wageni waalikwa wakifuatilia
  Diego Gutierrez, akiandika ujumbe wa uzinduzi wa Whatsaap ya bure
 Diego Gutierrez, akizungumza jambo na msanii maarufu wa vichekesho hapa nchini, JOTI, (katikati) na meneja wake Betty Nelson
 Diego akiwashukuru washereheshaji

JI MKUU WA KENYA AFURAHIA UTENDAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA.

index
Jaji Mkuu wa Kenya Mhe. Dkt. Willy Mutunga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji wake wa kusikiliza  na kuamua mashauri mengi yanayopelekwa mahakamani. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman na Kulia ni Jaji Kiongozi Mhe. Shaan Lila.
index1
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumzia ujio wa Jaji Mkuu wa Kenya.
…………………………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
Jaji Mkuu wa Kenya Mhe. Dkt. Willy Mutunga ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji wake wa kusikiliza  na kuamua mashauri mengi yaliyopelekwa mahakamani kwa mwaka wa sheria uliopita wa 2015 na kutoa wito kwa watendaji wa Mahakama ya Tanzania kuendelea kufanya vizuri licha ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Jaji Mkuu wa Kenya ametoa pongezi hizo mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kukutana na kuongea na Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani Tanzania kufuatia mwaliko alioupata wa kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yatakayofanyika Februari 4 mwaka huu.
Mhe. Dkt. Mutunga amesema kuwa  nchi ya Kenya mpaka sasa ina mashauri yapatayo 300,000 ambayo bado hayajaamuliwa na kuongeza kuwa asilimia 5 ya wananchi wa Kenya ndio hupeleka mashauri yao Mahakamani huku asilimia 95 iliyobaki wakitafuta ufumbuzi wa kesi zao nje ya Mahakama.
“Ni kweli Tanzania mnafanya vizuri katika katika kusikiliza mashauri kwa haraka, asilimia 95 ya Wakenya hutafuta ufumbuzi wa kesi zao kwa viongozi wa kidini na Kimila kutokana na baadhi yao kukosa fedha za kutosha za kufuatilia na kugharamia kesi zao” Amesema.
Ameongeza kuwa Mahakama ya Kenya kwa mwaka huu 2016 imejipangia malengo ya kuhakikisha kuwa inasuluhisha mashauri yote ndani ya mwaka mmoja ili kuongeza ufanisi na imani kwa wananchi.
Ameeleza kuwa Tanzania ina jambo la kujifunza kutoka Kenya kufuatia mageuzi ya Katiba iliyoyafanya mwaka 2010 hususan kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo na nafasi ya Mahakama kwenye Katiba Mpya ambayo Tanzania inaendelea na mchakato wake.
Akizungumzia mageuzi hayo ambayo tayari Kenya imeyafanya kufuatia kuwepo kwa Katiba mpya Mhe. Mutunga amesema kuwa ni pamoja kupungua kwa madaraka ya Rais katika kuteua Majaji, na nafasi za Majaji kutangazwa na watu kupeleka maombi na sifa zao kujadiliwa ambapo wananchi huruhusiwa kutoa maoni kwa Tume ya Mahakama ya Kenya kuhusu majaji hao kabla ya kuapishwa.
Aidha, ameeleza kuwa Watanzania wana kila sababu ya kujivunia umoja na mshikamano uliopo ambao umesababishwa na waasisi wa taifa hilo huku akibainisha kuwa majadiliano na upatikanaji wa Katiba Mpya utafanywa na Watanzania wenyewe kwa kuwa Watanzania ni walimu na mfano wa kuigwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akizungumzia ujio wa Jaji Mkuu wa Kenya amesema kuwa Mahakama ya Tanzania imenufaika na ujio wake kwa kuwa iko kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo huwakutanisha wadau mbalimbali wa sharia kujadili changamoto na mafanikio ya Sekta ya Sheria nchini.
Amesema kuwa kufuatia ziara ya Jaji Mkuu wa Kenya Mahakama ya Tanzania imejifunza masuala mbalimbali ambayo ni muhimu katika ufanisi wa shughuli zake ikiwemo Maslahi ya Watumishi wa Mahakama, Jukumu la Mahakama kutafsiri Katiba kwa kuangalia historian a uchumi pia kuazima baadhi ya hukumu zilizotolewa nchini Kenya kama ushauri.
Aidha, amebainisha kuwa Mahakama ya Tanzania inao wajibu wa kuendelea kuongeza uwazi katika upatikanaji wa watendaji wake wenye nia ya kuwatumikia wananchi na kuboresha njia za kuwapata majaji.

SHEIKH ISSA PONDA APINGA MARUDIO YA UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR

 Katibu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam Tanzania, Sheikh Issa Ponda (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kupinga kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
 Msemaji wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam Tanzania, Sheikh Rajab Katimba akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi huo Zanzibar.
 Sheikh Ponda akisalimiana na mwanahabari Said Powa wa gazeti la Tanzania Daima baada ya kumaliza kuzungumza na wanahabari.
Sheikh Ponda akiondoka baada ya kuzungumza na wanahabari.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UONGOZI WA BENKI YA CRDB NA BENKI YA POSTA TANZANIA

4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki hiyo Dkt. Charles Kimei wakati Uongozi huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 03,2016 kwa lengo la kumuelezea kuhusu Banki hiyo itakavyoweza kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo.
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati  akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki hiyo Dkt. Charles Kimei wakati Uongozi huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 03,2016 kwa lengo la kumuelezea kuhusu Banki hiyo itakavyoweza kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo.
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa Benki ya Posta Tanzania wakati Uongozi huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 03,2016 kwa lengo la kumuelezea kuhusu Banki hiyo itakavyoweza kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati  akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya Posta Tanzania wakati Uongozi huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 03,2016 kwa lengo la kumuelezea kuhusu Banki hiyo itakavyoweza kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo.
(Picha na OMR)

HAKUNA MGOMO WA MADAKTARI MASWA-DED

madaktari 
Na Benedict John-MAELEZO-Dar es salaam.
………………………………………………..
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simiyu Trasias Kagenzi amekanusha madai yaliyoandikwa na baadhi ya vyombo vya Habari kuhusiana na taarifa za kufanyika kwa mgomo unaotarajiwa kufanywa na baadhi ya Madaktari na Wauguzi katika Hospitali mkoani Simiyu na kusema habari hizo sio za kweli.
Kauli hiyo ameitoa leo katika mahoajiano na Mwandishi wa Habari hii juu ya kuwepo kwa mgomo huo  ambapo alifafanua kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote kwani siku ya tarehe 02 Februari mwaka huu, alikuwa na kikao na watumishi wote wa Hospitali hiyo ambapo kati ya mambo walioyajadili ni stahili na hali ya kazi hospitalini hapo.
”Hapa wilayani kwetu kuna baadhi ya waandishi ambao hawazingatii maadili ya kazi zao hasa kwa kuandika habari zisizo na ukweli, nimeshangaa kusikia taarifa hii kwasababu ukweli ni kwamba mimi nilikaa na watumishi wote jana wakiwemo madaktari, wauguzi na madereva na moja ya mambo tuliyojadili ni pamoja na mishahara yao na posho zao, na tulimaliza kikao chetu kwa amani kabisa, sasa waandishi kama hawa tunawaita makanjanja maana haina ukweli wowote”, alisema Kagenzi.
Aliongeza kuwa, kitendo walichokifanya baadhi ya waandishi hao kuandika habari hiyo sio jambo la busara kwani linaleta mkanganyiko na chuki baina ya watumishi na viongozi wao na hata kwa serikali yao na amelaani jinsi waandishi hao wanavyotumia kalamu zao vibaya kwa kupotosha umma wa watanzania
”Inasikitisha kwa kweli mtu anakurupuka bila kuwasiliana na Utendaji Mkuu wa Hospitali na kuanza kuanza kukutana na madaktari anaowajua na kuanza kuandika taarifa kama hizi na kuzirusha katika vyombo vya habari”, alisisitiza Kagenzi.
Mkurugenzi huyo amewataka waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi zao ili waweze kuandika habari ambazo zinatoa picha halisi badala ya kuwaogopesha wananchi na hivyo kushindwa kwenda kupata huduma.
Kwa upande wake Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bi.  Stella  Kalinga alieleza kuwa baada ya kufuatailia taarifa aligundua kuwa siyo za kweli kwani hakuna dalili yoyote ya mgomo kwa watumishi hao wa afya na wako kazini wakiendelea na majukumu yao kama kawaida.

MATUKIO KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA

1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 3, 2016.
2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Manyovu, Albert Obama Ntabaliba kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari3, 2016.
4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Abuu Jumaa kwenye viwanja vya Bunge mJini Dodoma, Februari 3, 2016
5
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Abuu Jumaa (katikati) na Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson  Rweikiza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 3, 2016.
3
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Februari  3, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CFAO MOTORS YAFANYA ONYESHO LA BIASHARA YA MAGARI AINA YA SUZUKI KATIKA JENGO LA PSPF GOLDEN JUBILEE TOWERS

DSC_2617Moja ya Suzuki Grand Vitara magari ya CFAO yaliyopo kwenye maonyesho ya bidhaa mpya walizonazo katika jengo la PSPF Golden Jubilee Tower lililopo Posta jijini Dar es Salaam.
DSC_2588
Gari hilo la Suzuki Vitara linavyoonekana kwa nyuma.
DSC_2592
Gari hilo aina ya Suzuki Grand Vitara linavyoonekana ubavuni.
DSC_2580
Moja ya Suzuki magari ya CFAO yaliyopo kwenye maonyesho ya bidhaa mpya walizonazo katika jengo la PSPF Golden Jubilee Tower lililopo Posta jijini Dar es Salaam.
DSC_2584Gari hilo la aina ya Suzuki linavyoonekana ubavuni..
DSC_2561
Suzuki hiyo inavyookena upande wa nyuma.
DSC_2575
Gari ndogo Suzuki OMNI inavyookena kwa mbele.
DSC_2600
upande wa ndani unaogawa gari hilo la Suzuki ambao unaonesha upande wa dereva na upande ambao mtu anaweza kutumia kwa kuweka mizigo na mambo mengine.
DSC_2597
upande wa nyuma wa ndaniu wa gari hilo aina Suzuki OMNI.
DSC_2602Magari hayo yanavyoonekana katika showroom hiyo ndani ya jengo la PSPF Golden Jubilee Towers.
…………………………………………………………………………
Kampuni ya uuzaji magari ya CFAO imefanya onyesho la kuonyesha bidhaa mpya walizonazo katika jengo la PSPF Golden Jubilee Tower lililopo Posta jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Modewji Blog, Meneja Masoko wa CFAO Motors, Sheikha Said amesema sababu ya kampuni hiyo kufanya onyesho katika jengo hilo ni kuwaonyesha wateja wa kampuni hiyo bidhaa mpya walizonazo katika sehemu zao wanazouzia magari (showroom).
Amebainisha kuwa, mbali na kuwaonyesha wateja lakini pia kuwaonyesha wafanyakazi na wananchi mbalimbali ambao walikuwa hawajui bidhaa zinazopatikana CFAO Motors au kwa wengine kuwa na shughuli nyingi hivyo kushindwa kufika katika ‘showroom’ zao na kupitia onyesho hilo wataweza kupata magari katika maeneo yao ya kazi.
“Tupo hapa kwa hili kuwasogezea huduma watu wa aina mbalimbali na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali waone bidhaa tulizonazo,” alisema Bi. Said.
Nae Afisa Mauzo wa Suzuki, David Kritsos alisema kupitia onyesho hilo wananchi na wafanyakazi wa ofisi mbalimbali wanaweza kununua magari wanayopendelea na wanaweza kusaidiwa na CFAO Motors kupata mkopo benki ili waweze kupata fedha za kununua magari hayo na kulipa mkopo taratibu.
Alisema CFAO ndiyo kampuni pekee nchini yenye nafasi ya kusambaza bidhaa za Suzuki na magari yote wanayoyauza bado ni mapya yakiwa bado hayajatumika kabisa.
Showroom hiyo itaendelea hadi hapo 4 Februari.

DK. SALIM KUZINDUA KITUO CHA UTAFITI NA MAFUNZO YA UYOGA CHA CHUO KIKUU CHA KAIRUKI

 Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert Kairuki yatakayofanyika kuanzia Februari 4. Kushoto ni Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni.
 Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la Kairuki (KHEN), Dk. Muganyizi Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert
Kairuki yatakayofanyika Februari 4. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu
ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni na Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni. 
…………………………………………………………………………………..
Katika  kuadhimisha miaka 17 ya kumbukuzi ya mwaasisi wa chuo kikuu  cha  kumbukumbu ya Hubert kairuki kuanzia tarehe  4 hadi  6 Feb ambayo  itakuwa ni siku  ya kilele.Mh Dr Salmin
Ahmed Salim  ambaye  pia ndio mkuu wa chuo hicho atazindua jengo la
utafiti  na  mafunzo ya Uyoga  lililopo huko  Boko katika eneo la chuo hicho.

Sambamba na uzinduzi huo  pia shughuli  nyingine katika  kumbukizo hizo  itakuwa ni pamoja na muhadhara kuhusu Uyoga utakaotolewa na
Profesa  Keto  Mshigeni  ambaye ndiye  makamu mkuu  wa chuo hicho  na mwanasayansi aliyebobea katika  tafiti  za uyoga.

Pia  hospital  ya Kairuki it ataendesha zoezi maalum la upimaji na matibabu ya
macho  bila  ya malipo kwa siku  mbili  mfululizo.

Pia patakuwepo matembezi ya hiara kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo  ya
saratani ya kizazi.

Aidha  wanafunzi wa zamani wa chuo  hicho waliopo  Mwanza  na mikoa ya kanda ya ziwa wataadhimisha
kumbukizo hizo  kwa  kufanya  zoezi la kupima afya
bure  kwa wakazi  wa huko.

Wananchi wahimizwa kujitokeza kupima Saratani.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulusubisya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani
leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa saratani duniani .
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulusubisya akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa saratani duniani.
 
Picha na Ally Daud
…………………………………………………………..
 
Na Nyakongo Manyama
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wanatarajia
kutoa  elimu, huduma na vipimo vya  bure vya magonjwa ya saratani ili kuiwezesha jamii
kujikinga na ugonjwa huo nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumatano) Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa  Wizara hiyo, Dkt. Ulisubisya Mpoki huduma hizo za matibabu na vipimo vitaenda sambamba na maadhimisho ya siku ya saratani
duniani inayoathimishwa ulimwenguni kote tarehe 4. Februari ya kila mwaka.
Aidha Dkt. Mpoki aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma ya kupima ugonjwa wa saratani katika
katika Hospitali ya Ocean Road ili kujihadhari na maambukizi ya ugonjwa huo.
“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road tunapenda
kuwaambia wananchi wote wajitokeze kupima ugonjwa huo ikiwemo saratani ya tezi
dume kwa wanaume na saratani ya matiti kwa wanawake bila ya malipo” aliongeza
Dkt. Mpoki.
Dkt. Mpoki amewataka watu wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata vipimo na matibabu ya
saratani ya ngozi na kuwataka wajilinde ili wasipate miale ya jua inayoathiri
ngozi zao na kupelekea maambukizi ya ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa Dkt. Mpoki alisema ugonjwa wa saratani huchangiwa zaidi na ulaji usiozingatia kanuni za afya,matumizi
ya vilevi, uvutaji wa sigara na matumizi ya makubwa ya sukari.
Kaulimbiu ya Maadhimisho yaSiku ya Saratani Duniani mwaka huu ni ‘TUNAWEZA, NINAWEZA. KWA PAMOJA TUWAJIBIKE KUPUNGUZA
JANGA LA SARATANI DUNIANI.”

MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA KAMBI YA WAZEE WASIOJIWEZA NA WALEMAVU YA NUNGE, KIGAMBONI, DAR ES SALAAM LEO

1
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
2 3
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
4
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
5
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akioneshwa maeneo mbalimbali  na Bw. Ojuku Mgedzi, Mkuu wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
6
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wagonjwa waliofika kupata huduma katika zahanati ya  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,  Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
8
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitembelea chumba cha kujifungulia cha zahanati ya  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
9
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana kwa furaha na wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
10
Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema akimkaribisha Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kuhutubia wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
11
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
13
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mchele, unga na maharage Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti wa wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
14
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea shukurani kutoka kwa Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti  wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
15
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru  Mzee Anthony Kingongoti Mwenyekiti  wakaazi wa  Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
PICHA NA IKULU

TAARIFA KUHUSU WATUMISHI WA UMMA KUUZIWA FOMU ZA OPRAS

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
NEMBO YA TAIFA
FOMU YA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI (OPRAS) HAIUZWI
Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inawaelekeza waajiri wote nchini kuhakikisha watumishi katika sehemu zao za kazi wanapata Fomu ya Wazi ya Mapitio na Upimaji Utendaji Kazi (OPRAS) kwa utekelezaji bila usumbufu.
Fomu za OPRAS zinapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma yenye anuani, www.utumishi.go.tz. Waajiri wote wanaelekezwa kutembelea tovuti hii na kutoa nakala za kutosha kwa idadi ya watumishi katika maeneo yao ya kazi. Kwa watumishi wanaoweza kutoa fomu hizi wenyewe wanaruhusiwa kufanya hivyo.
Imebainika kuwa katika baadhi ya Taasisi za Umma watumishi wanaelekezwa kununua fomu za OPRAS kutoka kwa watu binafsi. Kitendo hiki ni kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo na pia ni usumbufu kwa watumishi. Fomu za OPRAS haziuzwi na watumishi hawatatakiwa kuzinunua. Endapo Mtumishi atashawishiwa au kulazimishwa kununua fomu za OPRAS atoe taarifa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora ili hatua stahiki zichukuliwe. Waajiri wote wanakumbushwa kuwa ni wajibu wao kuwapatia watumishi walio chini yao fomu hizi na kuzihifadhi baada ya utekekelezaji na si vinginevyo.
Serikali ilianzisha matumizi ya Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) Mwezi Julai 2004, kupitia Waraka wa Utumishi Na. 2 wa mwaka 2004. Hivyo kutoka wakati huo, OPRAS ilifuta mfumo wa zamani wa kupima utendaji kazi wa mtumishi kwa njia ya siri.
Mabadiliko ya kutathmini utendaji kazi wa Watumishi wa Umma kwa uwazi yanakwenda sambamba na Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1998 kama ilivyorekebishwa mwaka 2008 ambazo zote zinasisitiza uwekaji wa mifumo ya menejimenti ya utendaji bora wa kazi inayojali matokeo.
Utekelezaji wa OPRAS katika taasisi za Umma ni hatua muhimu kwa Serikali katika kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma kwa Umma. Hivyo ni wajibu wa kila mwajiri kusimamia na kuhakikisha kuwa watumishi wote walio chini yao wanajaza fomu hizo na kuwasilisha taarifa za utekelezaji katika Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora bila kukosa.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI Kny: KATIBU MKUU OFISI YA RAIS-UTUMISHI

MKOA MPYA SONGWE NA WILAYA MPYA ZAANZISHWA

indexWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simachawene akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kuhusu kuanzishwa kwa Mkoa mpya waSongwe na Wilaya sita mpya .
…………………………………………………………………………………….
(Na Raymond Mushumbusi-maelezo)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini.
Akitoa tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.
Mhe George Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.
Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.
“ Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema Mhe Simbachawene.

MATUKIO YA PICHA KATIKA KIKAO CHA BUNGE MJINI DODOMA

1
Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Andrew Chenge pamoja na  Waziri wa Nchi Ofisi Utumishi na utawala Bora Mhe.Angellina Kairuki wakiwasili katika viwanja vua Bunge kwa ajili ya kushiriki kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
2
Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Andrew Chenge akiwasili katika ukumbi wa Bunge tayari kwa kuongoza kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
4
Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Andrew Chenge akiongoza sala kwa ajili ya Bunge na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
5
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge Kazi, Vijana na Ajira Mhe Anthony Mavunde akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
6
Waziri wa Nchi Ofisi Utumishi na utawala Bora Mhe.Angellina Kairuki akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
7
Wairi wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Mhe dkt Hussein Mwinyi akiteta jambo na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
8
Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mhe.prof Makame Mbalawa akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
9
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.George Masaju  akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

KANDA WA MBEYA MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU KUGONGANA JIJINI MBEYA.
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WAWILI WA NCHINI ETHIOPIA KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 08 KWA MAKOSA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA [DEREVA] WA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 321 CSV AINA YA TOYOTA COASTER AITWAYE LWIMIKO MWANSASU [36] MKAZI WA UYOLE ALIFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 877 CWE AINA YA SCANIA BASI MALI YA KAMPUNI YA SUPERSHEM LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL JOHN [42] MKAZI WA MWANZA KUGONGANA NA GARI HILO NA KISHA KULIGONGA GARI JINGINE LENYE NAMBA ZA T. 321 CSV AINA YA TOYOTA HIACE LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAKISYE MBOMA [45] MKAZI WA AIRPORT.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI HUKO ENEO LA SOWETO, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA BASI HILO LILILOKUWA LINATOKA MBEYA KUELEKEA MWANZA. DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UPELELEZI UNAENDELEA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI ETHIOPIA 1. AYNO ASATA [21] NA 2. CHARU SUMESO [18] KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO ENEO LA MAJENGO, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAENDELEA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO 1. HAIDAN RODRICK [35] 2. JULIUS BUTEMELE [53] 3. VISENT MAPILE [29] 4. DOTO MWASHITETE [25] NA 5. JOSEPH BUTEMELE [40] WOTE WAKAZI WA ISANGAWANA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA WAKIWA WANAKUNYWA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [5].
WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO KIJIJI NA KATA YA ISANGAWANA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
MTU MMOJA MKAZI WA IYULA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMANNE HAONGA [32] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA KUMI [10].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 11:20 ASUBUHI HUKO KIJIJI, KATA NA TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
MTU MMOJA MKAZI WA ILOLO WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DANIEL NZUNDA [30] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA POMBE MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [5].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.02.2016 MAJIRA YA SAA 13:40 MCHANA HUKO KIJIJI NA KATA YA ILOLO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA ZA KUINGIA NCHINI ILI KUJIEPUSHA NA MATATIZO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WANANCHI WAASWA KUTOKUVAMIA MAENEO YA VIWANJA KIHOLELA KWANI WANACHANGIA MIGOGORO YA ARDHI

images modified
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
…………………………………………………
JAMII hapa nchini imetakiwa kuachana na vitendo vya kuvamia  mashamba na viwanja vya waatu kiholela  bila ya kuzingatia na taratibu na  zilizizowekwa  kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa  kuchochea vurugu na na uvunjifu wa amani kutokana na kuwepo kwa migogoro ya ardhi.
Hayo yamesemwa na  Afisa mtendaji wa Tarafa ya Sungwi iliyopo Wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani  Thomas Mollel wakati alipokuwa akijibu malalamiko kwa waandishi wa habari yaliyoyotolewa na  baadhi ya wananchi wa kiluvya ‘B’ kuhusina na suala la uvamizi wa maeneo yao ya viwanja  kinyume na taratibu.
Mollel alisema kwamba anashangazwa kuona baadhi ya wananchi wamekuwa wakijichukulia sheria wenyewe kwa kuvamia maeneo ya watu na kuanza kufanya ujenzi kitu ambacho kimesababisha kuwepo kwa hali ya uvunjifu wa amani, ambapo ameongeza hawezi kuifumbia macho na atalivaia njuga suala hio hili haki iweze kutendeka kwa kila mtu  mwenye eneo lake kihalali.
“Kwa kweli mimi sipendi kuoana  wanannchi wanavunja sheria ambazo zimewekwa kwa kuamua kuvamia maeneo ya watu na kuanz akufanya ujenzi hii sio sahihi kwani kufanya hivyo mwisho wa siku kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani kutokaja na kuibuka kwa migogoro hiyo ya ardhi kwa ahiyo naomba waachane na tabia hiyo,” aisema Mollel.
Aidha Afisa Mtendaji huyo alibainisha kwamba wananchi wanapswa kubadiika na kuzingatia sheria za nchi ziizowewekwa ii kuepekuna na hali ya kugombania maeneo ya viwanja na mashamba  kitu amabcho amedai ni kitendo cha kujichukulia sheria mikononi.
Kwa upande wake mmoja wa wananchi ambao wameingia katika mgogoro mkubwa kutokana na eneo lake kuvamia anayejulikana kwa jina la Januaris Maganga alimwomba Waziri mwenye dhamana kuliingilia kati sakata hilo kwani kwa sasa limedumu kwa muda mrefu bila ya kutafutia ufumbuzi jambo ambalo linamweka katika hali ya kuishi kwa mashaka kutokana na vitisho anavyovipata kwa sasa.
“Mimi nina eneo langu kama hekai mbili na nusu lakini nashangaa kuna mzee mmoja ameamua  kulivamia kinyume cha sheria kabisa wakati mimi eneo hii ni langu kihaai na nina hati ambayo ninayo lakini bado analeta ukorofi kwa hiyo mimi hai kama hii inabadi waziri mwenye dhamana atusaidie ili tuweze kutatua mgogoro huu na mimi niweze kupata haki yangu,”alisema Maganga.
Naye mmoja wa wazee wa siku nyingi katika kijiji hicho cha kiluvya ‘B; Rashid Kilusungu akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake kuhusina na tabia ya wananchi kuvamia maeneo kiholela alisema sio jambo zuri kwani linaweza kuchochea kutokea kwa vurugu hivyo ni vema busara zikatumika ili hali ya amani na upendo iwepo.
MIGOGORO ya viwanja na mashamba katika maeneo ya Wilaya ya Kisarawe bado inaonekana kuwa ni sugu kutokana na mamlaka ambazo zinahusika zinachangia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuchelewesha kutoa hati za wamiliki halali wa maeneo hayo, hali ambayo inasababisha wananchi kuamua kuvamia na kujenga bila ya kuwa na kibali halali.

POLISI KUDHIBITI UPORAJI WA FEDHA KWENYE MABENKI

2Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yussuf Massauni akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika kikao cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………………………………………..
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi imejipanga kudhibiti uhalifu unaofanywa na na baadhi watu kwa kupora fedha za wafanyabiashara au watu binafsi kwa kutumia usafiri wa Pikipiki maarufu kama bodaboda.
Akijibu swali la Mhe. Oscar Rwegasira Mukasa Mbunge wa Biharamulo Magharibi (CCM) lililouliza ni zipi takwimu sahihi za matukio ya ujambazi yanayohusiana na uporajiwa fedha,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yussuf Massauni amesema matukio ya ujambazi yanayohusisha uporaji wa fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 kama takwimu zinavyosema , kwa mwaka 2013 matukio 1.266, mwaka 2104 matukio 1,127 na mwaka 2015 yalikuwa 931.
” Jeshi la polisi limechukua hatua kwa kufanya kazi karibu na mabenki nchini ili kubaini kama kuna wafanyakazi wa mabenki wanashirikia na majambazi kufanya uporaji huo na watakaobainika tutawachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani watakaokamatwa”
“ Napenda kuwaomba wananchi kutupa ushirikiano na hasa kwa wafanyabiashara wanaochukua fedha nyingi ili tuweze kuwapatia ulinzi ili kupunguza, ama kuondoa kabisa vitendo hivi vya uporaji wa fedha vilivyokothiri nchini kwa sasa” Alisema Mhe Massauni.
Aidha amewaomba waheshimiwa Wabunge kutoa elimu kwa wananchi wao kuhusu maswala ya ulinzi na usalama ili kupunguza vitendo vya uhalifu hasa uporaji wa fedha kwa wafanyabiashara kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wakiona tukio lolote linalopangwa kwa ajili ya kupora fedha.
Serikali kupitia Jeshi la Polisi linafanya ukaguzi wa pikipiki zote nchini ili kubaini uhalali wake na uhalali wa wamiliki wake ili kuweza kubaini pikipiki na wamiliki wanaohusika na vitendo vya uporaji wa fedha vinavyoshamiri siku hadi siku

Millioni 300 kujenga Barabara Rukwa

indexNaibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika cha 7 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
……………………………………………………………………………………
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO )
Serikali katika mwaka wa fedha 2015/2016 ilitenga Shillingi million 300 kwa ajili matengenezo na ujenzi wa Barabara ya Kitosi- Wampembe katika Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ili kufanya Barabara hiyo iweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
Akijibu swali la Mhe.Desdelius John Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini (CCM) liliouliza ni lini Serikali itaitikia kilio hiki cha wananchi wanaopata shida kwa Barabara hizo kutopitika katika kipindi chote cha mwaka,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani amesema Serikali kupitia Wizara yake imesikia kilio cha wananchi wa Wilaya ya Nkasi na inaendelea kutoa fedha za matengenezo ya Barabara ya Kitosi-wampembe.
“ Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ilitoa jumla ya Shillimgi Millioni 500 ili kufanya matengenezo ya Barabara ya Kitosi-Wampembe ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka” Alisema Mhe Ngonyani.
Aidha ,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ilitenga jumla ya Shillingi Millioni 45 na Shillingi Millioni 60 zimetengwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 kwa ajili ya matengenezo ya aina mbalimbali ya barabara ya Nkana-Kala kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ili kuhakikisha inapitika kwa kipindi chote cha mwaka.
Ukarabati wa barabara ya Kitosi-Wampembe yenye urefu wa kilomita 67 na Barabara ya Nkana –kala yenye urefu wa kilometa 68 uko chini ya Mfuko wa Barabara ikisimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) na Barabara zote hizi ziko chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambayo inawajibika kuwezesha Barabara zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka.

SIDA WARIDHISHWA NA MIRADI YA REA

 2
Mtambuzi wa miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijini, Mhandisi Elneema Mkumbo akitoa maelezo juu ya utekelezaji wa miradi ya REA, kwa Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlokom ( aliyeweka mikono kifuania) ambao ni miongoni mwa wafadhili wa miradi hiyo akiwa na ujumbe wake pamoja na wadau wengine wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ujerumani( GIZ) wakati wakikagua utekelezaji wa miradi ya REA katika mikoa ya kanda ya kaskazini.
1
3 4 5
Muonekano wa nyumba zilizounganishwa na huduma ya umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati vijijini REA katika kijiji cha Kwedizinga mkoani Tanga.
……………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Shirika la Kimataifa la maendeleo la Sweden( SIDA), limeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Umeme inayofahiliwa na Shirika hilo hususan usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini REA kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini( Tanesco), katika maeneo mbalimbali nchini.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la maendeleo la Sweden( SIDA) Maria Van Berlekom amesema hayo mara baada ya kuona maendeleo ya wananchi wa vijijini wakati wa ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa miradi hiyo katika mikoa ya kanda ya kaskazini .


Diaego akitoa hotuba

No comments:

Post a Comment