Pages

Saturday, January 30, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA KUSHIRIKI IBADA YA ASKOFU MKUU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHELI TANZANIA (KKKT) MJINI MOSHI.

IMG_4361 (1024x683) 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizungumza na wanahabari ofisini kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani Kilimanjaro.
IMG_4355 (1024x683)
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amosi Makala ali-pozung4umza nao ofisini kwake.
……………………………………………………..
5

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MRADI WA UMWAGILIAJI GEREZA LA KILIMO IDETE, MKOANI MOROGORO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mhe. Balozi Simba Yahya akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili gerezani hapo kwa ziara ya kikazi Januari 29, 2016 kujionea ujenzi wa mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete lililopo Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro(anayefuatia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
6
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(wa pili kulia) akiwa ameongozana na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kushoto) kuelekea katika Ukumbi wa Gereza hilo kwa ajili ya kupata taarifa kamili ya utekelezaji wa mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kutoka kwa Wakandarasi wa mradi na Mshauri Mwelekezi mradi(kulia) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero, Bw. Yahya Sinaniya.
7
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya akiangalia sehemu ya banio la kutunzia maji ya mradi wa Gereza la Kilimo Idete akiwa pamoja na msafara wa Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Manyama Mapesi(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
8
Muonekano wa mfereji wa maji yatakayokuwa yakitumika katika mradi wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete, Mkoani Morogoro kama inavyoonekana katika picha.
9
Mshauri wa Mradi, Mhandisi Nzobonaliba Imani akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(katikati) alipotembelea mradi wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete lililopo Mkoani Morogoro(kulia) ni Mkuu wa Gereza hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja wakiaangalia ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Gereza hilo
10
Wakandarasi wa Kampuni ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Gereza Kilimo Idete, lililopo Mkoani Morogoro wakiendelea na ujenzi wa mifereji ya maji kama inavyoonekana katika picha.
11
Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakipata maelezo ya Kitaalam kutoka kwa Mshauri Mwelekezi walipotembelea mradi huo kujionea hatua mbalimbali za ujenzi. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kilombero.
……………………………………………………………………….
Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Morogoro
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya “Tanzania Building Works ya Jijini, Dar es Salaam” inayojenga mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kuukamilisha mradi huo katika muda walioongezewa ili kuwezesha kuanza kwa shughuli za uzalishaji gerezani hapo.
Akizungumza na Wakandarasi wa Kampuni hiyo alipofanya ziara ya kikazi Gereza Idete, Balozi Yahya amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni mkombozi kwa Jeshi la Magereza kwani utawezesha uzalijashi wa chakula cha kutosha cha wafungwa waliopo magerezani pamoja na kuzalisha ziada itakayouzwa kwa Wananchi ili kuongeza Mapato Serikalini.
“Ni matarajio yangu kuwa Mkandarasi wa Mradi huu kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi na Wadau wa Jeshi la Magereza atakamilisha mradi huu kwa wakati kama alivyotuahidi hivyo kuanza mara moja shughuli za uzalishaji”. Alisisitiza Balozi Yahya.
Naye Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Lodia Mallion alisema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo tayari uchimbaji na ujenzi wa mifereji itakayokuwa ikipitisha maji kwenda mashambani imekwisha kukamilika.
“Mito inayotumika kama vyanzo vya maji ni mto Kilombero pamoja na mto Kiwiliwili ambapo banio linalotunza maji kwa shughuli za umwagiliaji tayari limekamilika”. Alisikika Mhandisi Mallion.
Awali Mkuu wa Gereza Idete, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja akiwasilisha taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Yahya amesema kuwa kazi ya kuandaa mradi huu ilianza rasmi mwaka 2013 ambapo mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka huu 2016 ambapo gharama za mradi huo zinakadiriwa kufikia kiasi cha Tsh. 2.5 Bilioni.
Aidha amesema kuwa chakula kitakachopatikana katika mradi huo wa Gereza Idete kitatumika kulisha wafungwa waliopo magerezani na ziada itakayopatikana itauzwa kwa Wananchi hivyo kuongeza pato la Taifa.
Gereza la Kilimo Idete lipo Wilayani Kilombero, Mkoani Morogoro linajishughulisha na Kilimo cha mpunga wa chakula na pia mpunga kwa ajili ya mbegu bora za Kilimo hapa nchimi. Gereza hilo lilianzishwa rasmi mwaka 1983 kwa ajili ya Kilimo cha mazao mbalimbali hususani Kilimo cha mpunga.

MWONEKANO WA KUUDHI KATIKA LANGO KUU LA KUINGILIA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA.

Mwonekano katika lango Kuu la Kuingilia katika Uwanja wa mpira wa CCM Kirumba Jijini Mwanza pindi mvua inaponyesha. Ni zaidi ya Usumbufu, kero na adha kwa wanaoingia na kutoka Uwanjani hapo pindi mvua inaponyesha.
Ni zaidi ya Usumbufumbu kwa mashabiki wa mpira pindi mvua inaponyesha wanapokuwa wakiingia amba kutoka Uwanjani, katika Uwanja wa CM Kirumba Jijini Mwanza kutokana na maji kutuama katika barabara inayoingia na kutoka katika lango Kuu la kuingilia Uwanjani hapo.
Wahusika mlione hili kama changamoto inayopaswa kutafutiwa utatuzi.
Picha na George Binagi-GB Pazzo Wa BMG.

BONDIA OMARI KIMWERI KUPANDA TENA ULINGONI FEB. 26 MWAKA HUU AUSTRALIA


BONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatarajia kucheza mpambano wake mwingine  feb 26 akizipiga na  Michael Camellion kutoka Philippines  mpambano wa raundi kumi wa ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title .
…………………………………………………………………………………………………. 
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
 
Kimweri mpaka sasa amepanda ulingoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
 
Bondia huyo mtanzania anayefanya shughuli zake Australia  amewaomba watanzania kumuombea dua kwa ajili ya mchezo wake  huo ili afanye vizuri na kushinda mchezo huo  ambapo baada ya hapo atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA.
 Kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana 
 akishinda mchezo huo itabadilisha maisha ya mchezaji huyo  wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na mkanda wa WBA ambao ameahidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii ya Feb. 26
 
Kimweri alitoa shukrani kwa wadau wanaomsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa kwake katika mchezo wa masumbwi, makocha hao ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila ‘Super D’ 
 
Kocha wa Tanzania Prison Remmy Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga 
 
Ambao wamekuwa chachu kwake katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na hata kama anaishi nje ya Tanzania amesema hawezi  kusahau asili yake kwa kuwa kitovu Tanzania ndipo kitovu chake kilipozikiwa.
AVIANA MATATA AKABIDHI MSAADA WA CHOO S/M MSINUNE, BAGAMOYO
015
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation (kushoto) na Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi wakionekana wenye nyuso za furaha baada ya kufunua kitambaa kwenye jiwe la msingi.
019
Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi akikata utepe kuzindua rasmi choo cha kisasa katika shule ya Msingi Msinune kilichojengwa na Mo Dewji Foundation. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Msami Mgoto pamoja na wanafunzi wa shule hiyo wakishuhudia tukio hilo.
026
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.
 Taasisi ya Flaviana Matata, imekabidhi choo katika Shule ya Msingi Msinune ya Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani kitakachosaidia wanafunzi wa shule hiyo.
Tukio la kukabidhi choo hicho limefanyika katika shule hiyo mapema leo na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Bi. Flaviana Matata ambapo ameelezea kuwa, wamekua wakiwapatia wanafunzi wa Msinune vifaa vya shuleni tangu mwaka 2014 na mwanzoni mwa mwaka jana aliombwa kuwa mlezi wa Shule na  kuweza kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemo suala hilo la vyoo vya waalimu na wanafunzi, madarasa pamoja na nyumba za walimu.
Flaviana amesema baada ya kuguswa aliweza kumshirikisha Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji, alikubali kutoa msaada huo kupitia taasisi yake hiyo ya Mo Dewji Foundation na kuweza kujenga choo hicho chenye matundu nane.
 Kwa upande wake, Mkuu wa Shule hiyo ya Msinune, Bw. Msami Mgoto ameshukuru taasisi ya Mo Dewji kwa msaada wa kufadhili ujenzi wa choo hicho huku akielezea kuwa  itasaidia wanafunzi zaidi ya 300 wanaosoma hapo licha ya kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya majengo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Msinune, Ramadhani Mtokeni aliishukuru Taasisi ya Mo Dewji kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Msinune huku akiomba iendelea kuwasaidia pindi wanapokuwa na matatizo.
Kwa upande wa mwakilishi kutoka Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi amepongeza juhudi za Flaviana Matata  za kusaidia jamii ikiwemo kukua kwa elimu hapa nchini hivyo wataendelea kushirikiana naye bega kwa bega.
Francesca ameongeza kuwa, Mo Dewji kupitia msaada huo, wanafunzi watakuwa katika mazingira mazuri na safi kwa afya zao ikiwemo kusoma bila kuwa na tatizo la awali la choo, kwa sasa na miaka ijayo choo hicho kitakuwa mkombozi na msaada mkubwa.

WADAU WAHAMASISHWA KUWEKEZA TASNIA YA UONGEZAJI THAMANI MADINI

MAD1
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe akiangalia madini mbalimbali kupitia kifaa kinachotumika kukuza mawe ya madini ili yaweze kuonekana vizuri ikiwemo kubaini kasoro . Kabla ya kutunuku vyeti Wahitimu 14 wa Mafunzo ya kunga’risha na kukata madini ya Vito, Prof. Msofe amepata fursa ya kuangalia bidhaa mbalimbali za mapambo zilizotengenezwa na wahitimu hao ikiwemo vifaa vinavyotumika wakati wa mafunzo. Anayemwonesha kushoto ni Mtumishi katika  cha Jimolojia Tanzania, Salome Tilumanywa (kushoto). Wengine wa kwanza kulia ni Kaimu Mratibu wa Kituo hicho John Mushi, anayefuata ni Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia masuala ya Uchumi na Biashara ya Madini, Salim Salim.
MAD2
Mmoja wa Walimu katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Ramadhan Haizer (kushoto) akimwonesha mfano wa mapambo ya vito ambayo Wahitimu wamepata mafunzo ya kutengeneza katika mikato mbalimbali katika fani za Unga’rishaji na uchongaji madini ya vito Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James (wa pili kushoto). Katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Ally Samaje.
MAD3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James  akiangalia  madini ya vito yaliyokatwa katika maumbo mbalimbali kutoka kwa Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Unga’rishaji na Ukataji wa Madini ya Vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).
MAD4
Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito wakitumia mashine mbalimbali za Kuchonga katika maumbo mbalimbali na kungarisha madini ya  Vito.
MAD5
Baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo ya Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito wakitumia mashine mbalimbali za Kuchonga katika maumbo mbalimbali na kungarisha madini ya  Vito.
MAD6 MAD7
Wahitimu wa Mafunzo ya Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito wakiwa wameshika mchoro wa umbo la Ramani ya Tanzania ambalo lililowekwa  Madini ya aina katika maumbo mbalimbali kulingana aina za  madini hayo yanavyopatikana katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo wamemkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe ikiwa ni njia ya kuonesha ubunifu wao  baada ya kuhitimu mafunzo.
MAD9
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kutoka Makao Makuu na walio katika ofisi za Madini za ARusha na Moshi na Kituo cha Jemolojia Tanzania, wakati wa Mahafali ya Pili ya  Mafunzo ya Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito.
……………………………………………………………………………………………………….
Na Asteria Muhozya, Arusha
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje katika  Sekta ya Madini kuwekeza katika kuanzisha  Vituo vya Uongezaji Thamani Madini ili kuendeleza fani hiyo kwa manufaa ya uchumi wa taifa.
Wito huo umetolewa leo jijini Arusha na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Sekta ya Madini, Profesa James Mdoe wakati  wa Mahafali ya Pili katika fani za Ukataji na Unga’rishaji Madini ya Vito katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGDC).
Profesa Mdoe amesema kuwa, uongezaji thamani madini unalenga kuongeza fursa za ajira, kwa Watanzania watakaofanya kazi katika vituo hivyo, ikiwemo pia kutoa fursa za wataalamu wa sekta hiyo kujiajiri na hivyo kuongeza mapato kwa Serikali jambo ambalo pia litasaidia kuongeza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa.
Ameongeza kuwa, Kituo hicho kina historia ya  ya pekee katika historia ya sekta ya Madini  kwa kuwa kimekuwa kituo cha kwanza na pekee kuanzishwa hapa nchini,  na kuongeza kuwa, uwepo wake ni kielelezo sahihi cha kazi za ubunifu na uongezaji thamani madini ya vito.
Pia amesema kuwa, kuanzishwa kwa kituo hicho ni moja ya hatua za Serikali za kutimiza malengo yaliyomo katika Sera ya Madini ya Mwaka 2009 yenye lengo la kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la taifa na ajira kwa watanzania kupitia uongezaji thamani madini, ikiwa pamoja na mafunzo ua Jemomojia, ukataji na unga’rishaji wa madini ya vito , utengenezaji wa bidhaa za mapambo na uchongaji wa vinyago vya mawe.
Aidha, Profesa Msofe ametoa wito kwa Kampuni zinazofanya biashara ya madini ya vito na wadau wengine kuchangia maendeleo ya Kituo hicho ili kiwe kitovu cha kutoa Wataalamu wanaokidhi mahitaji ya tasnia ya madini ya vito nchini.
Akizungumzia zuio la mwaka 2010 la kusafirisha Tanzanite ghafi inayozidi gramu moja nje ya nchi, amesema lengo la zuio hilo ilikuwa ni kuhamasiaha ujenzi wa vituo , vyuo, taasisi na viwanda vya kuongeza thamani ya madini hayo nchini  na kuongeza kuwa, jambo hilo pia ndilo lililopelekea Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kuanzisha kituo hicho.
Awali, akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo, Monica Laiton, amesema kuwa, mafunzo hayo  yamewapa  ujuzi wa kukata madini ya aina tofauti ikiwemo Tanzanite katika mikato mbalimbali na kuongeza kuwa, ujuzi  huo utawawezesha kuajiliwa au kujiajiri na  kuongeza kuwa, mafunzo hayo yamedhihirisha wazi kuwa, wanawake wanaweza kufanya kazi katika sekta hiyo tofauti na dhana iliyokuwepo awali kwamba shughuli za sekta hiyo zinafanywa na wanawake pekee.
Jumla ya Wahitimu 14 wamehitimu mafunzo hayo kwa muda wa miezi sita, ambapo walipata ufadhili   kupitia Kamati inayoandaa Maonesho ya Vito ya Arusha  (Arusha Gem Fair)  chini ya Mfuko wa kuendeleza Wanawake katika tasnia ya madini.  Maonesho ya Arusha huandaliwa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) kwa ushirikiano na Wizara ya Nashati na Madini. Mwaka huu maonesho hayo yatafanyika jijini Arusha katika Hotel ya Mount Meru kuanzia tarehe 19- 21, Aprili, 2016.

MBWANA SAMATA ASAINI MKATABA WA MIAKA MINNE KUCHEZEA TIMU YA GENK YA LIGI KUU UBELGIJI

SAM
Mbwana Samata amewasili nchini Ubelgiji na kusaini mkataba wa miaka minne na Club  mpya ya FC Genk ili kucheza katika ligi kuu ya nchi hiyo, Ubelgiji  imekuwa moja ya nchi zinazotoa wachezaji wakubwa  ulaya na kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo ni moja kati ya timu kali duniani.
Mbwana amesema katika ukurasa wake wa Instagram kuwa anamshukuru Mungu kwa fursa hii na ataitumia vyema ili kujiletea mafanikio na kuleta mafanikio kwa taifa lake pia.
Meneja wa mshambuliaji huyo, Jamal Kisongo, alisema amewasiliana na Samatta na kumweleza kwamba amefika salama na ameanza kufuata taratibu zote ili aweze kufanya kazi nchini humo.

Samatta ambaye alitwaa tuzo ya kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, alikubali kujiunga na timu ya KRC Genk na kugomea ofa zilizotolewa na klabu za Nantes na Olympique Marseille za Ufaransa
SAM2

No comments:

Post a Comment