Pages

Sunday, January 3, 2016

Usikurupuke kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii



Hakuna kosa wanalofanya wafanyakazi wengi nchini kama kukurupuka  kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii. 

Japo linawezekana likawa jambo linalochukua muda, lakini ukweli ni kuwa huna budi kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kutoa uamuzi sahihi wa kujiunga na mfuko fulani wa hifadhi ya jamii.

Mchangiaji wa michango au Mwekezaji makini anatakiwa aweke mkazo katika kufanya makosa makubwa kwa sababu uchunguzi au utafiti au upembuzi wa mifuko hii ya pensheni inatakiwa ufanyike kisanyansi kwa kuzingatia uchambuzi wa takwimu na uchambuzi nyinginezo ingawa vigezo hivi vya takwimu vinaweza kuwa muhimu lakini mara nyingi huwa havijitesholezi hata kidogo. 

Hivyo shughuli kubwa katika mambo ya kujiunga au kujisajiri na mifuko hii inatakiwa kufanya utafiti, ingawa unagharimu muda mwingi kabla ya maamuzi sahihi. 

Uamuzi wa kuwa mwanachama wa mfuko unatakiwa utokana na takwimu na taarifa nyinginezo makini zinazotakiwa zifanywe na mfanyakazi mwenyewe na siyo kufuata mkumbo wa watu wengi wanasemaje. 

Kwa kufanya hivyo tumeona mara nyingi wafanyakazi wengi hukosea kwa sababu alifuata mazungumzo ya watu wengi juu ya mfuko fulani wa pensheni hivyo anatakiwa kufanya utafiti na uamuzi wake ufuate utafiti na takwimu siyo uzushi au habari motomoto ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wowote. 

Unahitaji wewe kama mfanyakazi kuhakikisha ya kuwa unafanya utafiti au uchunguzi wa kina na kuchambua ripoti za kila mwaka za mifuko huku ukizingatia yale yanayotendeka katika sekta tofauti nchini na kwingineko katika nyanja za mifuko ya hifadhi ya jamii.  

Unahitaji kujua usalama wa michango yako unayochangia kila mwezi. Lazima ujue hiyo michango yako huwekezwa mahali ambapo uwezekano wa kupata hasara ni mdogo sana, na kuchunguza kama huwekezwa sehemu ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kupata faida. 

Hii ijulikane na itambulike ya kuwa kiupambele katika ufuatiliaji wake kwenye michango yako au fedha yako unayochangia kwanza inatakiwa kuwa na usalama wake na siyo faida. Kipa umbele hapa kwanza ni inatakiwa kuwa michango yako na siyo faida unayotakiwa kutarajia. Faida inatakiwa kushika nafasi ya tatu na siyo nafasi ya kwanza au ya pili. 

Unatakiwa kulikumbuka hili jambo sana ukitaki ufanikiwe kutokana na mifuko hii hakikisha unafanya utafiti au uchunguzi kuhakikisha ya kuwa mfuko unafuata utaratibu wa kisayansi wa uwekezaji wa michango yako kwa kufuata kanuni za kulinda usalama wa fedha zako unazotegemea kuchangia na uwekezajji uwe ule wa kuleta faida na kuwa na uwezo wa kitega uchumi kubadili kuwa fedha taslim na siyo vinginevyo.

Unatakiwa mfuko ambao unajitoa kuchangia masuala ya kijamii inayoizunguka na kuwa na uwezo mkubwa wa kutawanya uwekezezaji wa michango yako bila kufuata misukumo ya wanasiasa badala ya kufuata kanuni za kulinda usalama wa michango yako ya pensheni.  

Hata hivyo, ili mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii iweze kutoa huduma bora kwa wakati kama ulivyokusudiwa katika mapatano hayo, lazima wategemee kupata muuitikio na ushirikiano kutoka kwa wateja ili kutimiza makubaliano yaliyowekwa katika mkataba. 

Na mifuko ya pensheni ikumbuke ya kuwa wateja ndiyo viungo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa malengo ya kila siku ya mifuko, kwa kuwa taarifa zinazotoka ndizo zinazowezesha mifuko kutoa huduma stahiki. 

Utahitaji kujifunza zaidi utendaji wa mifuko ya pensheni kutoka kwa wataalamu na mamlaka inayohusika kama vile mdhibiti na msimamizi wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii yaani SSRA na hata kwenye makala za kijamii kama vile makala za HakiPensheni

Sawa umepewa uhuru huo wa kuchagua kujiunga na mifuko hii ya pensheni, hivyo ningependa kukuuliza wewe mfanyakazi uliyeajiriwa leo je unajua mfuko unaotoa mafao bora zaidi ya kulingana na kiwango cha shirika la kazi duniani ILO? yaani kwa idadi ya mafao, ubora wa mafao, na kulipwa pensheni kulingana na ukali wa maisha ya kila siku.


No comments:

Post a Comment