Pages

Thursday, January 28, 2016

Unilever yatoa zawadi kwa wanafunzi shule ya msingi Tumaini

 Balozi wa Blue Band Ayubu Athumani akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa darasa la sita Joseph Deogratius wa shule ya msingi Tumaini iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka mshindi katika shindano la Band ‘Kula Tano’, jana. Wapili kulia ni mwalimu wa michezo Naelijwa Shaidi.

SATZ yakabidhi jengo la mafunzo na madawati Kilombero

 Mwakilishi wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi  jengo ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa  5.5, Jenga Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana. Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. 
 Mweka hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero
Mke wa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Louise Bainbridge akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilombero, Muungano, Kantui, Ujirani, Lyahira na Mapinduzi (hapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi madawati  jana, Kilombero. Katiakti ni Meneja Mkuu wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mark Roe-Scott na kulia ni meneja utawala wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Allawi Mdee.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

KANDA WA MBEYA 
MTU MMOJA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.
 MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI MKOANI MBEYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA CHILANGA WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA AITWAYE EMANUEL NZUNDA [55] ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KICHWANI NA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MTU AITWAYE MENGO MKISI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHILANGA, KATA YA IHANDA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI, BAADA YA MAREHEMU KUMTUHUMU MTUHUMIWA KUWA NA MAHUSIANO NA MKE WAKE AITWAYE TELEZIA AZIMIO [31] MKAZI WA CHILANGA, AMBAYE AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO.
INADAIWA KUWA, MAREHEMU BWANA EMANUEL NZUNDA [55] ALIPORUDI NYUMBANI TOKA KAZINI HAKUMKUTA MKE WAKE NA HIVYO KUAMUA KWENDA NYUMBANI KWA MTUHUMIWA NA KUMKUTA MKE WAKE AKIWA NA MTUHUMIWA NA NDIPO UGOMVI UKATOKEA. MAREHEMU ALIFARIKI KUTOKANA NA KIPIGO NA KUTOKWA NA DAMU NYINGI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI KWA UCHUGUZI ZAIDI WA KITABIBU. MTUHUMIWA ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWENDESHA PIKIPIKI MKAZI WA MBIMBA WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NELSON MSHEMWA [54] ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 998 DDL AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA KENEDY MJELWA [35] MKAZI WA MLOWO.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 27.01.2016 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KIJIJI CHA MBIMBA, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.
CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI WA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 998 DDL AINA YA MITSUBISHI FUSO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. DEREVA WA GARI ALIKIMBIA BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA NA KUHESHIMU SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA WA GARI AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Serikali yasema haijafuta vipindi vya Bunge TBC

NDE4
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii,na Michezo  Nape Nnauye akitoa  kauli Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016.
……………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kwa umma kuwa imefuta vipindi vya shughuli za Bunge kuoneshwa katika televisheni ya Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) kama zisemazo taarifa zilizozagaa mitaani.
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mose Nnauye wakati akiongea na wananchi moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini kutolea ufafanuzi taarifa za upotoshaji juu ya TBC kufuta vipindi vya matangazo ya vikao vya Bunge.
Mhe.Nape Moses Nnauye amesema Serikali haijafuta vipindi vya Bunge bali ilichofanya ni kubadilisha muda wa kurusha vipindi hivyo kutoka muda wa mchana na kuviweka usiku kwa lengo la kupunguza gharama za kurusha moja kwa moja matangazo hayo ya Bunge na pia  kuwapa fursa wananchi zaidi kuangalia na kufatilia yanayoendelea Bungeni kwa kuwa muda wa usiku watu wengi wanakuwa wamesharejea kutoka katika shughuli zao za ujenzi wa taifa.
Ameongeza kuwa Serikali imechukua uamuzi wa busara katika hili kwani TBC imekuwa ikitumia Sh Billion 4.2 kwa mwaka kama gharama za urushaji wa moja kwa moja wa matangazo hayo , hivyo itasaidia katika kubana matumizi ya shirika hilo kwani fedha hizo hazipo katika bajeti ipewayo shirika bali ni fedha za ndani zinazokusanywa na shirika hilo
Aidha amesema kuwa sio kitu kigeni kwa Bunge kutotangazwa moja kwa moja kwani kuna baadhi ya mabunge katika nchi nyingine urekodiwa na kurushwa baadae kama kipindi maalum cha Bunge,amezitaja baadhi ya nchi hizo kuwa ni New Zealand, India, Malawi, Lesotho, Uingereza na Singapore.
Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) lilianza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 ila baada ya Serikali  kukaa na kujadili kwa kina kuhusu gharama za urushaji wa matangazo hayo moja kwa moja ikaamua kubadili mtindo wa urushaji wa matangazo hayo kutoka matangazo ya moja kwa moja kwa siku nzima kwenda kwenye mfumo wa kuyarekodi na kuyarusha katika kipindi cha LEO KATIKA BUNGE.

No comments:

Post a Comment