Mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii
nchini inatakiwa kujiwekea malengo na mikakati mbalimbali ili kuleta ufanisi na
tija katika shughuli za ulipaji wa mafao.
Huu
ni muda wa muafaka kwa mifuko kuanzisha utaratibu wa kuwa na mapatano ya utoaji
wa huduma baina taasisi hizo na wateja wao kwa kuanzisha mikataba ya huduma kwa
wateja kwa kutekelezwa kwa vitendo.
Ambapo
mikataba hiyo inakuwa ni hatua muhimu sana katika utoaji wa huduma bora katika
misingi ya uwazi na uwajibikaji.
Kwa
kufanya hivyo kwa mifuko wateja wao ambao ni wanachama, wastaafu na familia
zao, na wageni wanaofanya kazi kwa mikataba watapata uhuru na uelewa wa
kufahamu matarajio yao katika huduma zinazotolewa na mifuko
Wateja
watafahamu hata viwango vya muda ambavyo vitawawezesha kupanga mambo yao vyema
kabisa bila kusumbuka, badala ya kusubiri huduma bila ya kufahamu upatikaji
wake wa huduma hizo na kwa viwango fulani vilivyoanishwa wazi kwa wateja wa
ndani na wa nje.
Mifuko
kwa kufanya hivyo itawezesha kuwa na mapatano yatakayowawezesha wateja wao
kufahamu huduma zinatolewa na mifuko, vikiwemo na hata viwango vya huduma na
hatua ambazo mteja anaweza kuzichukua iwapo viwango vya huduma vitakuwa kinyume
na matarajio ya mkataba.
Jambo
la kuangalia kuhusu mifuko ni kujua bidhaa au huduma zake. Je huduma au bidhaa hiyo
inahitajika na watu wote, chukua mfano wa fao la matibabu.
Hivyo
jaribu kujiunga na mfuko ambao huduma zake zinahitajika na wengi au wafanyakazi
wengi na familia zao, pamoja na wazee, vijana, watoto, walemavu, wajane, pamoja
na watoto yatima kwa kukidhi mahitaji yao wanapopatwa na majangwa ya aina
mbalimbali.
Lazima
ujiulize kama huduma zinazotolewa na mfuko zina mbadala au hazina mbadala. Na
hiyo huduma ina uhakika mkubwa wa soko. Ina nguvu kubwa ya ukiritimba ikiwa na
maana ya kuwa na uwezo wa huduma kuwa na soko kubwa lenye uwezo wa kudai bei
kubwa bila kupunguza uhitaji na matumizi. Hivyo jiunge na mfuko wenye huduma
zenye sifa nzuri.
Unahitaji
kufanya uchunguzi wa kutosha au kina kuhusu utendaji wa mifuko hii hasa kwa
kufanya utafiti wa kutambua thamani, soko, kutatua udhaifu, kutoa majibu ya
maswali tata, kupata taarifa zaidi na za uhakika.
Kujiunga
na mfuko wowote wa hifadhi ya jamii ni kutafuta sehemu yenye usalama ya kuweza
kuwekeza michango yako ya kila mwezi kwa ajili ya aina mbalimbali ya majanga
yanayoweza kusababishwa na ugonjwa, kuumia ukiwa kazini, kifo, kupata ulemavu,
na kadhalika.
Hivyo
unahitaji kufanya utafiti wa makini sana kwa kuchunguza taarifa mbalimbali juu
ya mfuko huo unaotaka kujiunga nao ili taarifa hizo ziweze kukusaidia kutoa
maamuzi wa busara wa kukuwezesha kuzingatia kanuni misingi na vigezo maalumu
ambazo vitakusaidia kujibu maswali mengi.
Baadhi
ya maswali muhimu yanaweza kuwa kama vile utawezekeza wapi? Na mfuko upi, na
watakata kiasi cha asilimia ngapi kutoka katika mshahara wangu, na mwajiri
wangu yeye atatoa kiasi cha asilimia ngapi kama umeajiriwa.
Hivyo
ni juu ya mtu au mfanyakazi mwenyewe kama mwekezaji kufanya utatafiti wa kina
ili kujua ubora wa mfuko huo unaotegemea kujiunga nao kabla ya kujisajiri.
Unatakiwa usiwe mwepesi wa kufanya maamuzi bila kwanza kuwekeza kwenye utafiti
hasa kama vile kuwaona wataalamu wanaoweza kukusaidia kukupa ushauri mahiri.
Ni
muhimu kuangalia mifuko hii ya pensheni kwa kuangalia uongozi, yaani
menejimenti, hali ya kifedha, thamani ya mfuko wa pensheni kwa sasa, taarifa
mbalimbali, matarajio ya mfuko wa pensheni
kwa kipindi kijacho kama pamoja na thamani ya mfuko wa pensheni kwa
miaka ijayo.
Uchambuzi
unahitajika uwe unaolenga zaidi katika kuchambua thamani ya mfuko wa pensheni
kutokana na taarifa halisi zilizopo na siyo taarifa za matarajio ya baadaye.
No comments:
Post a Comment