Pages

Sunday, January 31, 2016

JENERALI MWAMUNYANGE ABAKISHWA JESHINI HADI 2017, AMIRI JESHI MKUU RAIS MAGUFULI AMUONGEZEA MUDA




Jenerali Mwamunyange, (kulia), akiwa na Amiri Jeshi Mkuu, Rais John Pombe Magufuli, wakati wa kufunga maonyesho ya medani jirani na kambi ya mafunzo ya kijeshi Monduli hivi majuzi
MKUU wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, amesema Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, amembakiza Jeshini kwa mwaka mmoja hadi Januari 30, 2017.
Jenerali Mwamunyange aliwaambia waandishi wa habari makao makuu ya jshi, Ngome, Upanga jijini Dar es Salaam kuwa. “Sisi wanajeshi huwa tunabakishwa, Mh. Rais akiona anakuhitaji kumsadia, basi muda wako wa kustaafu ukifika, wewe unabakishwa na anaweza kukuongezea cheo, lakini mimi siwezi tena kuongezewa cheo maana hapa ndio mwisho.” Alisema Jenerali Mwamunyange.
Tayari Mnadhimu Mkuu mpya wa JWTZ, Luteni Jenerali Venance Salvatori Mabeyo, ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Usalama na Utambuzi ya JWTZ, ameapishwa kushika wadhifa huo mpya baada ya mtangulizi wake, Luteni Jenerali Samwel Ndomba, kustaafu.
Majenerali kadhaa wametaafu na tayari wengine wameteuliwa kushika nafasi zao.
 
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya akina mama waliojifungua kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Rufaa Mawenzi, mkoani Kilimanjaro. Waziri Mkuu yuko mkoani humo kwa ziara ya kikazi ambapo leo Januari 31, 2016 anatarajiwa kuhudhuria hafla ya kuwekwa kazini kwa askofu wa KKKT, Kanisa Kuu la Moshi
Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisalimiana na Waziri mkuu  Majaliwa.
Waziri Mkuu  akislimiana na Mstahiki meya wa  Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya .
Waziri mkuu akiwasili katika hosiptali  ya rufaa ya Mawenzi alipofanya ziara  ya  kushtukiza.
Waziri mkuu akitizama chumba cha kupigia  pcha za mionzi (X Ray) katika hosspitali  ya rufaa  ya Mawenzi.

Waziri mkuu akiwa wodi ya watoto alipotembelea kujionea namna ambavyo  wagonjwa wanahudumiwa.
Waziri mkuu Majaliwa akizungumza jambo na mganga  mkuu wa mkoa  wa Kilimanjaro,Dkt Mtumwa  mwako.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri  mkuu  Kassim Majaliwa.
Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia walipokutana Ikulu ndogo mjini Moshi.
Baadhi ya Viongozi walifika Ikulu ndogo mjini Moshi kwa ajili ya kumsikiliza ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

 Helikopta hiyo ikiwa chini baada ya kuanguka

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
RUBANI wa helikopta ya Doria ya Mamlaka ya Wanyamapori Nchini, (TANAPA), Roger Gower raia wa Uingereza ameuawa baada ya kupigwa risasi akiwa angani na watu wanaosadikiwa kuwa majangili kwenye pori la akiba maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu majira ya jioni Januari 30, 2016.
Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Simiyu, Jonathan Shana ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio, amesema, askari mmoja wa wanyamapori aliyekuwemo ndani ya helikopta hiyo amejeruhiwa.
“Helikopta hiyo haikudunguliwa, bali risasi ilimpata Rubani na hivyo akauawa na helikopta kupoteza mwelekeo na kuanguka.” Alifafanua Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Simiyu, Jonathan
“Tutawasaka pori kwa pori, pango kwa pango, kijiji kwa kijiji hadi tuwatie mbaroni wahalifu hao. Tumeleta FFU wenye silaha za nkutosha, ili kutekeleza amri ya kamanda IGP, Kamanda DCI na RPC, ndio maana tuko hapa na silaha nzito.” Alisema Mkuu huyo wa upelelezi wa Mkoa wa Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, walifika eneo la tukio na kushngazwa na tukio hilo ambapo waziri alisema, sasa wahalifu hawa wamefikia kiwango cha juu cha uhalifu hadi kuhujumu teknolojia ya kuhifadhi mazingira, kwa kuwashambulia watendaji wetu, Waziri alisema kwa huzuni na kuongeza
Serikali haitavumilia uhalifu huo na kuahidi kuwasaka popote walipo.
Hili ni tukio la kwanza kwa majangili kutungua kushambulia helikiopta ikiwa angani na kusababisha kifo.

 Waziri Profesa Maghembe, akizungumza baada ya kufika kwenye eneo la tukio. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi
 Waziri akionyeshwa sehemu risasi ilipopenya kwenye helikopta hiyo
Askari na maafisa wa serikali wakionyeshana sehemu helikopta hiyo ilipopigwa risasi na kuanguka baada ya rubani kuuawa

No comments:

Post a Comment