Pages

Sunday, January 3, 2016

BALOZI OMBENI SEFUE AFUNGUA SEMINA ELEKEZI KWA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU WAO, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Januari 2, 2015 (Picha na Ikulu).

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 2, 2016. Semina hiyo ya kwanza katika utawala wa serikaliya awamu ya tano kwa viongozi wakuu wa serikali, imefanyika sikumoja tu baada ya makatibuna manaibu wao kuapishwa na rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam, Ijumaa Januari 1, 2016. (Picha na Ikulu)

Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam

SAFARI ZA TRNENI YA KWENDA MIKOA YA KIGOMANA MWANZA ZAFUTWA BAADA YA MAFURIKO

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL umetangaza kusitisha kwa muda kuanzia jana Januari 01, 2016, kutoa  huduma zake za usafiri baada ya eneo la reli kati ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma tuta la reli kukumbwa na Mafuriko.
Taarifa fupi iliyotolwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana leo Jumamosi Januari 2, 2015 imesema, taarifa za kifundi eneo lililoathiriwa na mafuriko ni kubwa hivyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako eneo la mafuriko kutathmini ukubwa wa kazi yenyewe.

Kutokana na uamuzi huo treni ya abiria kutoka bara ilibidi safari yake ikatizwe ilipofika Dodoma na tayari utaratibu unaandaliwa wa kupata mabasi 17 kuwasafirisaha hadi Dar es Salaam abiria 1,119 . wa treni hiyo.

Hali kadhalika kwa vile tarahe ya kuanza tena huduma bado haijaujulikana, safari zote kuanzia jana Januari 01, 2016, kwenda bara zimefutwa na abiria husika wametakiwa kufika katika vituo vya reli walikokata tiketi ili warejeshewe fedha zao na kupata fursa ya kutafuta usafiri mbadala.

Aidha imesisitizwa kuwa Uongozi kwa wakati muafaka itatoa taarifa kamili kuhusu lini huduma za TRL kwenda bara zitaanza tena.

Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.

No comments:

Post a Comment