Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi |
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Jeshi
la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Lukas Wambura (38) Mkazi wa
Banana – Dar es salaam mwenye shahada ya dharura ya kusafiria
ab-10044029 akiwa na
vipande vinne vya meno yadhaniwayo kuwa ya tembo vyenye uzito wa kilo
8.4 yenye
thamani ya dola za kimarekani 30,000, sawa na tshs 64,140,000/=.
Tukio hilo limetokea Novemba 30 -2015 majira ya saa12 jioni katika eneo la custom – mpakani tunduma, ,
wilaya ya momba Mbeya ..
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya
Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo alikuwa
anavuka mpaka akitokea nchi jirani ya Zambia kuingia nchini na mzigo huo
alikuwa ameuficha ndani ya begi lake la nguo.
Wakati huo jeshi hilo la polisi linawashikilia watu wanne kwa
kukutwa na silaha mbili pamoja na nyara za serikali.
Kamanda Msangi amewataja watuhumiwa
hao kuwani M ohamed Ndilava [55], Mkazi
wa Mkwajuni , Nassora Omary [65] Mkazi
wa Tabora na Mwanza Mtokambali [39] Mkazi
wa Njelenje pamoja na Frank Jonas [32], Mkazi wa Bitimanyanga.
Msangi amesema watuhumiwa hao
sita walikamatwa Novemba 30 mwaka huu majira ya saa 3 usiku katika kijiji cha
Kapalala Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .
Amesema watuhumiwa walikutwa na silaha moja aina ya
riffle 416 yenye nambari c.6539833 na gobole moja lisilokuwa na namba, pia
walikutwa na nyara za serikali kichwa
kimoja cha paa, nyama ya paa na nyama ya sungura vyote vikiwa na thamani ya
tshs 1,176,000/=.
Kufuatia matukio hayo Kamanda Msangi anatoa
wito kwa yeyote mwenye taarifa
juu ya wahalifu wakiwemo majangili
kuzitoa katika mamlaka husika ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe mara
moja.
Mwisho.
(JAMIIMOJABLOGMBEYA )
Washiriki wa Mbio za Kilimanjaro Health Run KM 10 wakianza mbio hizo katika eneo la nje ya uwanja wa Majengo mjini Moshi. |
Washiriki wa Mbio za Km 5 zilizowashirikisha zaidi watoto wanao lelewa katka ituo mbalimbali mjin Moshi. |
Mkurugenzi wa Zara Tanzania na Zara Charity,Zainab Ansel akishiriki mbio hizo pamoja na mdogo wake Rahma wakikimbia mbio za Km 5. |
Mshindi wa mbio za KM 10 kwa wanaume ,Lameck Msiwa akimaliza mbio katika uwanja wa Majengo mjini Moshi. |
Baadhi ya washiriki wa mbio hizo kutoka nje ya nchi wakimalizia mbio katika uwanja wa Majengo mjini Moshi. |
Usalama kwa wakimbiaji uliimalishwa zaidi. |
Mwanariadha Banuelia Bryton akihitimisha mbio akiwa nafasi ya kwanza katika mbio za KM 10 kwa upande wa wanawake. |
Mkurugenzi wa Zara Tanzania,Zainab Ansel akimalizia mbio za KM 5. |
Askari Polisi wa Kikosi cha usalama barabarani ,Salatory Mtanange akiwasindikiza washiriki wa mbio hizo waliokuwa mwishoni kabisa huku akikimbia nao kwa karibu. |
Baadhi ya washiriki wa mbio za KM 3 katika mbio za Kilimanjaro Health Run 2015. |
Kampuni ya Vinywaji baraidi ya Bonite ya mjini Moshi ilidhamini zawadi kwa washindi wa mbio hizo. |
Zoezi la utoaji wa zawadi kwa washindi wa mbio hizo z likianza rasmi. |
Baadhi ya wakurugenzi wa mashirika mbalimbali waliofika kwa ajili ya mbio za Kilimanjaro Health Run ambazo hufanyika kila mwaka. |
Katibu wa Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro ( KAA ),Amini Kimaro akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi. |
Mkurugenzi wa Zara Tanzania ,Zainab Ansel akizungumza katika sherehe za kilele cha mbio hizo. |
Viongozi wa mashirika mbalimbali wakiwa tayari kukabidhi zawadi kwa washindi. |
Mshind wa kwanza wa Mbio za Km 10 ,Lameck Msiwa akikabidhiwa zawadi zake mara baada ya kuibuka mshindi katika mbio hizo. |
Mshindi wa kwanza kwa wanawake katika mbio za KM ,10 Banuelia Bryton akikabidhiwa zawadi zake. |
Mshindi wa pili kwa wanawake Mbio za KM 10 Adelina Aclati akikabidhiwa zawadi. |
Mshind kwa upande wa walemavu pia alijipatia zawadi zake. |
Diwani wa kata ya Longuo ,Ray Mboya akizungumza katika sherehe mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. |
RAY MBOYA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA NAFASI YA MEYA MANISPAA YA MOSHI
Msimamizi wa Uchaguzi wa nafasi ya Meya ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Makabayo akizungumza jambo wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi huo. |
Baadhi ya Madiwani walioshiriki zoezi la kumpata Meya wa manispaa ya Moshi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). |
Meya wa Manispaa ya Moshi aliyemaliza muda wake na Mbunge wa sasa wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Hotel ya Umoja. |
Madiwani wakimsikiliza Mbunge Michael kwa makini . |
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Basil Lema akizungumza katika kikao hicho. |
Madiwani wakimpongeza Ray Mboya baada ya kutangazwa mshindi. |
aliyekuwa akiogombea nafasi ya Meya ,Francis Shio akizungumza mara baada ya kushindwa na Ray Mboya huku akiwataka madiwani kuungana kufanya kazi ya ahadi walizotoa kwa wananchi. |
Mshindi wa nafasi ya Naibu Meya ,Peter Minja akishukuru mbele ya madiwani waliompigia kura na kufanikiwa kushika nafasi hiyo. |
aliyekuwa akigombea nafasi ya Naibu Meya ,Jomba Koi na kushindwa na Peter Minja akizungumza katika kikao hicho akitoa ahadi ya kushirikiana na Meya aliyechaguliwa. |
Mwenyekiti wa baraza la wazee wa chadema manispaa yaMoshi,Ally Mwamba akizungumza jambo katika kikao hicho. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. |
No comments:
Post a Comment