Rais John Magufuli akitia saini kitabu cha wageni wakati
alipomtembelea Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa ofisini kwake
jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015 na kuzungumza nao kwa takribani
saa moja (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais
John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa
wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26,
2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. (picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Rais
John Magufuli akiagana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa
wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26,
2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja. (picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Serikali yajidhatiti kupambana na kemikali zenye madhara maeneo ya bandari
Meneja
wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Mashariki Bw. Daniel Ndiyo
akiwakaribisha wadau wa masuala ya kemikali kutoka Mataifa mbalimbali
kushiriki katika mafunzo ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali
zenye madhara kwa afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini
Dar es salaam.
Mkemia
Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele akifungua mafunzo ya kujiandaa
kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya na mazingira
kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam.
Wadau
wa masuala ya kemikali kutoka Mataifa mbalimbali wakifuatilia mafunzo
ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa afya
na mazingira kwenye maeneo ya bandari leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi
kutoka nchini Ujerumani Bibi. Stefane Deuser akichangia mada kwenye
warsha ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa
afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari.
Mratibu
wa Kanda kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira
(UNEP) Bw.Patrick Mwesigye akizungumza leo jijini Dar es salaam kwenye
warsha ya kujiandaa kukabiliana na dharura ya kemikali zenye madhara kwa
afya na mazingira kwenye maeneo ya bandari.
Picha Zote Na Fatma Salum (MAELEZO)
Picha Zote Na Fatma Salum (MAELEZO)
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha ya muziki wa injili
nchini Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
salaam wakati alipofafanua mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya tamasha
la kushukuru baada ya kufanyika na kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa
Tanzania salama salimini.
Msama amesema maandalizi
yanaendelea vizuri na amemtangaza rasmi mwimbaji Rose Muhando kama mmoja
wa waimbaji wa muziki wa injili watakaoshiriki katika tamasha hilo,
linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Desemba 25 na
kushirikisha waimbaji wa kimataifa kutoka nchi za Afrika na Ulaya,
ambapo ameongeza kwamba mazungumzo bado yanaendelea na waimbaji wengine
kutoka nje ya nchi.
Katika picha katikati ni Mwimbaji
wa muziki wa Injili Rose Muhando akishiriki katika mkutano huo na
kushoto ni William Kapawaga mmoja wa waratibu wa Tamasha hilo kutoka
Kampuni ya Msama Promotion.
Mwimbaji
wa muziki wa Injili Rose Muhando akiwaelezea waandishi wa habari jinsi
alivyojiandaa kutumbuiza katika tamasha hilo la kushukuru, Kulia ni
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama.
baadhi ya waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa kampuni ya Msama
Promotion wakati alipokuwa akizungumza nao jijini Dar es salaam
kuhusiana na Tamasha hilo.
Mbunge wa Chumbuni Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD Akiwashukuru Wapiga Kura Wake Wananchi wa Jimbo la Chumbuni
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni
Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la
Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake
mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi
Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni
Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la
Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wapiga kura wake
mkutano uliofganyika katika Afisi za Jimbo Tawi la CCM Muembemakumbi
Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni
Zanzibar Mhe Ussi Salum Pondeza AMJAD akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la
Chumbuni Zanzibar wakati wa mkutano wake wa kutowa shukrani kwa Wananchi
wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kuwataka kuwa wamoja na
kujiandaa na maendekleo katika jimbo lake.
Na kusema sasa makundi basi
iliobaki ni Kazi Tu kwa maendeleo ya Wananchi wa Jimbo hilo na kusema
yeye ni Mbunge wa Wananchi wa Chumbuni wote
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakimsikiliza Mbunge wao wakati wa hafla ya kuwashukuru
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni
wakimsikiliza Mbunge wao wakati akitowa shukrani kwa wapiga kura wake
katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Jimbo Tawi la
CCM Muembemakumbi Zanzibar.
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni
wakimsikiliza Mbunge wao wakati akitowa shukrani kwa wapiga kura wake
katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Afisi ya Jimbo Tawi la
CCM Muembemakumbi Zanzibar.
MBUNGE WA UBUNGO SAID KUBENEA AWATEMBELEA WANANCHI WAKE KUWASHUKURU KUMCHAGUA NA KUJUA CHANGAMOTO ZAO
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akiongea na wananchi Stendi ya Mabasi
ya Ubungo Dar es Salaam leo, kuwashukuru kwa kumchagua na kujua
changamoto zao mbalimbali. Mbunge huyo jana alitembelea Soko la Ndizi la
Mabibo, Soko la Mabibo, Kituo cha Mabasi cha Mawasiliano na kumpa pole
ya sh. milioni 1.1 Diwani wa Kata ya Manzese, Ramadhani Kwangaya ambaye
ni Mkuu wa Chuo cha Mus’ab kilicho chomwa moto na kuunguza magodoro 30.
Kubenea akizungumza na waandishi wa habari na wananchi katika Soko la Ndizi la Mabibo.
Hapa akiwaunga mkono wananchi kununua mananasi katika soko la ndizi la mabibo
Mbunge Kubenea akisalimiana na wananchi katika soko hilo.
Wafanyabiashara katika soko la ndizi la mabibo wakimsikiliza mbunge wao Said Kubenea.
Vijana wakiserebuka baada ya kuzungumza na mbunge wao Said Kubenea katika Soko la Mabibo.
Mbunge Kubenea akizungumza na viongozi wa soko la Mabibo.
Hapa akiwahutubia wananchi katika soko la Mabibo.
WFP YAFAFANUA MAFANIKIO YAKE HAPA NCHINI
Ofisa
Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa nchini (UN WFP – Tanzania),
Tala Loubieh (kulia), akifafanua jinsi Shirika hilo linavyofanya kazi
hapa nchini tangu mwishoni mwa Juni 2014 lilipobadili utamaduni wake
wa zamani wa kugawa chakula moja kwa moja shuleni na kutumia mtindo
mpya wa kustawisha mazao kwa kushirikiana na Shule, unaojulikana kama
“Home Grown School Meals Programme.” Kwa kushirikiana na wilaya husika
kuratibu mpango huo wa kuwapatia chakula wanafunzi shuleni kwa
kununua chakula hicho kutoka kwa wakulima wadogo wadogo na jinsi
mkakati huu ulivyoweza kuendeleza wakulima vijijini na kuimarisha
uzalishaji wa wakulima wadogo pia kuinua uchumi wao.
Picha na Philemon Solomon-Fullshangweblog
Askofu Mkuu wa Tabora Kuongoza ujumbe wa Tanzania kumuona Papa Francis Uganda.
Na Joseph Ishengoma, MAELEZO
Askofu Mkuu wa jimbo kuu la
Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka kesho (tarehe 27.11.2015) anatarajia
kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa
Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis nchini Uganda.
Baba Mtakatifu Francis
anatarajia kuwasili nchini Uganda kesho kwa ziara ya siku mbili akitokea
Kenya kabla ya kuelekea Afrika ya Kati.
Hii ni ziara ya kwanza kwa
kiongozi huyo Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kutembelea Bara la Afrika
tangu alipoliongoza Kanisa Katoliki mwaka 2013.
Katibu wa Baraza la Maaskofu
(TEC) nchini Padre Raymond Saba amesema Mabaraza ya Maaskofu ya Kenya
na Uganda kwa pamoja yalitoa mwaliko kwa TEC kushiriki katika ziara ya
Baba Mtakatifu katika nchi hizo.
“Tulipata mwaliko kutoka Kenya
na Uganda, lakini tumeangalia nafasi yetu na jinsi ya kushiriki katika
ziara hii. Hatukuweza kutuma mwakilishi Kenya, lakini Askofu Ruzoka
ataiwakilisha TEC Uganda,” amesema.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, jana
mabasi mawili ya waumini wa dini ya Kikristo yaliondoka mjini Mwanza
kuelekea Namugongo, Uganda ambapo Baba Mtakatifu atakapofanyia ibada.
Eneo la Namugongo ndipo Mfalme Kabaka Mwanga II alipowachoma na kuwaua mashahidi 22 wa Uganda waliofia dini katika karne ya 18.
“Natoa wito kwa waumini wa
Kanisa Katoliki nchini, wafuatilie na kusikiliza kwa makini ujumbe wa
Baba Mtakatifu aliouleta katika Barani Afrika kwa sababu unagusa moja
kwa moja amani na ushirikiano miongoni mwa jamii,” amesema.
Kwa mujibu wa Padre Saba, Baba
Mtakatifu hufanya ziara kufuatia mwaliko wa kanisa na serikali ya mahali
husika au tukio la kimataifa linalohusiana na imani Katoliki.
Amesema, “Kanisa pekee yake
haliwezi kufanikisha ziara ya Baba Mtakatifu. Ndio maana alipofika Kenya
alipokelewa na Rais Uhuru Kenyatta na hata alipokuwa Marekani
alipokelewa na Rais Baraka Obama ingawa sio rahisi kwa kiongozi wa
Marekani kumpokea mgeni uwanja wa ndege.”
Ziara ya Baba mtakatifu nchini
Marekani ilipangwa kabla hajawa kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki. Ziara
hiyo ilitokana na kongamano la kimataifa la familia lililofanyika mjini
Filadelphia.
Papa Francis anatarajia kuhudhulia kongamano la vijana ulimwenguni nchini Poland mwaka 2016.
TAMASHA KUBWA LA BURUDANI LA INSTAGRAM PARTY KUFANYIKA JUMAMOSI VIWANJA VYA ESCAPE ONE MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Freconic ideaz, Fred Ngimba.
Mkurugenzi
wa Freconic ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la
burudani la Instagram party litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya
Escape One Mikocheni likiwa na kauli mbiu Bongo Throw Back. Kulia ni
Meneja Mawasiliano, Krantz Mwantepele.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
…………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Freconic Ideaz, imeandaa tamasha la burudani la ‘Instagram party’
litakalofanyika kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini
Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwakumbusha wapenzi wa muziki,
mavazi na misemo ya kizamani.
Akizungumza
Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba
alisema pia tamasha hilo litahusisha watu wenye ushawishi mkubwa katika
mitandao ya kijamii na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu.
Alisema
wadau na marafiki mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii watakutana
siku hiyo kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo huku wakipata
burudani mbalimbali.
“Kiingilio
katika tamasha hili kitakuwa ni sh. 50,000 kwa viti maalumu na vile vya
kawaida ni sh. 10,000, ambapo halitaishia hapa ila litaendelea katika
Mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma na Iringa,” alisema Ngimba.
Alitoa mwito kwa wadau wa muziki wa mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani itakayotolewa siku hiyo.
NHC YAZINDUA MAUZO YA NYUMBA KATIKA MRADI WA KAWE JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.
Nehemia Kyando Mchechu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari
Novemba 26, 2015 Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa mauzo ya nyumba katika mradi mpya wa Seven Eleven (711)
ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam (kulia) Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hamad Abdallah.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.
Nehemia Kyando Mchechu akiwaonesha waandishi wa habari michoro ya
ramani ya mradi wa nyumba ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza kwa umakini, Bw. Nehemia Kyando Mchechu.
Mkutano ukiendelea.
Waandishi wa habari wakitembelea katika eneo la ujenzi huo.
Ujenzi ukiendelea
Ujenzi ukiendelea
Waandshi wa habari pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakati wa uzinduzi huo.
Picha zote na Philemon Solomon-Fullshangweblog.
……………………………………………………………………………………..
Na Philemon Solomon Fullshangweblog
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) lazindua mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe ,ambapo ujenzi huo ulianza Januari 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.
Nehemia Kyando Mchechu alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa
kukamilika ifikapo Desemba 2018 ,ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya
kuanza ujenzi. Mradi huo una ukubwa wa mita za mraba 111,842.90 ambao
unatarajiwa kugarimu kiasi cha zaidi ya Sh 187, 927, 105,500 mpaka
utakapomalizika .
Pia ikumbukwe kuwa mradi huu ni seemu ya mji
mpya wa kisasa (Satellite City) unajengwa hapa ,mradi huu upo katika
eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko mita chache kutoka
fuko za bahari ya Hindi pia karibu na maeneo muhimu kama Mbezi Beach,
Masaki, Oysterbay, Morocco na Mikocheni mradi huu una jumla ya nyumba
422 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo nane tofauti ya ghorofa 18 kila
moja, ukiwa na huduma zote muhimu za kijamii.pia kutakuwepo na seemu ya
maduka makubwa kwa ajili ya wakazi na maeneo ya jirani”Alisema Mchechu.
Serikali imejipanga kukuza na kuendeleza Stadi za Kazi nchini
Mkurugenzi Msaidizi Toka Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Dkt.Jonathan Mbwambo akifafanua kwa
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mpango wa Serikali
wa kuendeleza stadi za kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili
kuongeza tija katika sekta zote nchini,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.
Mkurugenzi
Msaidizi Toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Dkt.Jonathan
Mbwambo akiwaeleza waandishi wa Habari kuhusu faida za kuendeleza stadi
za kazi ikiwemo kuongeza uzalishaji katika sekta zote nchini,kulia
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi. Zamaradi Kawawa.
Baadhi
ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi stadi na vyombo vya habari leo jijini Dar eS Salaam
uliolenga kueleza mpango wa Serikali kuwawezesha wananchi kupitia mpango
wa kuendeleza stadi za kazi unaotarajiwa kuanza mwaka wa fedha
2016/2017.
Picha Zote na Fatma Salum (MAELEZO)
Picha Zote na Fatma Salum (MAELEZO)
Serikali kuendelea kushirikiana na Vijana katika kutatua changamoto zao
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na Vijana kutoka
Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la
Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015
ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki.
Picha na Frank Shija,WHVUM.
Picha na Frank Shija,WHVUM.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel akizungumza na Vijana wa Tanzania walioshiriki
mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile (hawapo
pichani) uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 6 – 14 Novemba 2015
ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya ngao kutoka kwa Bibi. Dorice
Assenga (katikati) kwa niaba ya Vijana kutoka Tanzania walioshiriki
mkutano wa tatu wa Vijana kutoka nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika
nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16 Novemba 2015 ukiwa na lengo la
kubadilishana uzoefu kutoka nchi washiriki. Kulia ni Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Baadhi
ya vijana wa Tanzania walioshiriki mkutano wa tatu wa Vijana kutoka
nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika nchini Misri kuanzia tarehe 9 – 16
Novemba 2015.Kutoka kushoto ni Baraka Chedego, Paul Simango na Rwihula
Daniel
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN, AKUTANA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA ULINGO TANZANIA (UMOJA WA WANAWAKE WANASIASA).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Wanawake Wanasiasa
kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania walio katika Mtandao wa
Ulingo, wakati alipokutana nao katika kikao kilichoandaliwa na
Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye
Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na baadhi ya Wanawake wanaounda Umoja wa Wanawake Wanasiasa
kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania walio katika Mtandao wa
Ulingo, wakati alipokutana nao katika kikao kilichoandaliwa na
Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye
Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
Baadhi
ya Wanawake Wanaulingo wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwahutubia kwenye
katika kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya
kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo
Nov 26, 2015. Picha na OMR
Balozi Getrude Mongela, akichangia moja ya kati ya mada zilizokuwa zikizungumziwa katika kikao hicho leo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na baadhi ya Wanaulingo alipokuwa akipokelewa alipowasili
kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015 kwa ajili ya
kuhudhuria kwenye Kikao maalum kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania
kwa ajili ya kumpongeza . Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano kwa wanawake wakati wa
kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya
kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo
Nov 26, 2015. Picha na OM
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akishiriki kuimba wimbo maalum wa mshikamano kwa wanawake wakati wa
kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya
kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo
Nov 26, 2015. Picha na OM
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipokea zawadi ya ‘Dua’ kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar na
Katibu wa Ulingo Tanzania, Salama Aboud Talib, baada ya kumalizika kwa
kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya
kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo
Nov 26, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipokea zawadi ya picha baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa
na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika
kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akifurahia jambo na Balozi Getrude Mongela baada ya kumalizika kwa kikao
kilichoandaliwa na Wanaulingo Tanzania maalum kwa ajili ya kumpongeza
kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26,
2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo
Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya
Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na
Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye
Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo
Tanzania, wanaounda Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya
Siasa Tanzania, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na
Wanaulingo hao maalum kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye
Ukumbi wa BOT jijini Dar es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiagana na baadhi ya Viongozi wa Mtandao wa Ulingo Tanzania, wanaounda
Umoja wa wanawake Wanasiasa wa Vyama mbalimbali vya Siasa Tanzania,
baada ya kumalizika kwa kikao kilichoandaliwa na Wanaulingo hao maalum
kwa ajili ya kumpongeza kilichofanyika kwenye Ukumbi wa BOT jijini Dar
es Salaam,leo Nov 26, 2015. Picha na OMR
Wahamiaji haramu wakamatwa Tabata Segerea
Na Shamimu Nyaki-Maelezo
Jeshi la polisi kanda
maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wahamiaji haramu 105 raia wa
Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa
wanasafirishwa kwenda nchi nyingine za Afrika.
Akizungumza na waandishi
wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya
Dar es Salaamu Kamishna Suleiman Kova amesema wahamiaji hao ambao wote
ni wanaume wamekamatwa kutokana na ushirikiano wa wasamaria wema
wanaoshi eneo hilo la Tabata Segerea.
Ameongeza kuwa wahamiaji
hao waliingia nchini ya usimamizi wa mwanamke mmoja anaeitwa Zainabu
Umwiza (25) anaesemekana ni raia wa nchi ya Burundi ambae anajihusisha
na biashara hiyo ya usafirishaji haramu wa binadamu ambao ni kosa la
jinai tayari kuwapeleka nchi nyingine na hivyo amemuomba ajisalimishe
“ Bi Zainabu Umwiza
mwenye asili ya Burundi tunamwomba ajisalimishe maana yeye ni
mfanyabiashara wa usafirishaji wa binaadamu kutoka nchi za Afrika
kwenda Ulaya” kamanda Kova alisisitiza.
Aidha kamanda Kova
ameeleza kuwa polisi walifanya upekuzi katika nyumba ya mwanamke huyo
ndipo walipowakuta wahamiaji hao ambapo uchunguzi wa awali unaonyesha
kwamba, usafirishaji wa binadamu kutoka Afrika kwenda bara la Ulaya
unaofanywa na mwanamke huyo, ambao hufanyika kwa malipo ya Dolla 1000
kwa mtu mmoja.
Kamanda Kova ameongeza
kuwa watuhumiwa hao walipohojiwa kujua kwamba wana kibali chochote cha
kuingia nchini waligunduliwa kuwa hawana na kueleza kuwa waliingia
kupitia njia za panya na mbinu nyingine ambazo bado zinachunguzwa na
kwamba wamewajulisha idara ya Uhamiaji na watashirikiana nao katika
upelelezi ili hatimaye sheria ichukue mkondo wake.
Hata hivyo amewataka
wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kundoa na
kuzuia tatizo la wahamiaji haramu ambao wamekua tishio katika usalama wa
maisha ya wananchi na mali zao.
Zoezi la Usafi wa Mazingira Kuwa Endelevu Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Said Meck Sadiki
akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) ofisini kwake leo
alipokuwa akizungumzia zoezi la usafi na namna mkoa ulivyojipanga
kutekeleza zoezi hilo siku ya 9 Disemba.
Waandishi wa habari
wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam juu ya usafi wa mazingira siku ya 9 Disemba.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kulia)
akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki
(Kushoto) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)
kuhusu utekelezaji wa agizo la Mhe Rais la kufanya usafi wa mazingira
katika maadhimisho ya sherehe za uhuru wa Tanzania Bara.
(Picha zote na Raymond Mushumbusi – Maelezo )
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Lilian Lundo-MAELEZO
Mkuu wa Mkoa Dar es
Salaam, Mhe. Said Meck Sadiki amesema zoezi la usafi wa mazingira
litakalofanyika siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9
Desemba, litakuwa ni endelevu kwa mkoa wa Dar es Salaam hata baada ya
kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tano. Mhe. Dkt John Pombe Joseph
Magufuli aliagiza kuwa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara
mwaka huu yatumike kwa kufanya usafi wa Mazingira kote nchini badala ya
kufanya sherehe za gwaride la askari wa vikosi vya Ulinzi na Usalama.
Akiongea na vyombo vya
habari leo Mhe. Sadiki alianza kwa kumpongeza Mhe. Rais kwa uamuzi
aliouchukua wa kubadilisha sherehe za uhuru kuwa ni siku ya kufanya kazi
badala ya kwenda uwanjani na kuangalia gwaride na halaiki mbalimbali
kama ilivyokuwa ikifanyika miaka iliyopita.
“Mhe. Rais katurejesha
kule tulipotoka ambako kauli mbiu ya sherehe za uhuru ilikuwa ni uhuru
na kazi au uhuru ni kazi wakati watanzania walikuwa wakiungana na
kufanya kazi kwa umoja na kushirikiana,” alisema, Mhe. Sadiki.
Aidha, Mhe Sadiki
alisema, zoezi la usafi kwa mkoa wa Dar es Salaam litaanza rasmi
tarehe 1 Disemba mwaka huu na kumalizikia 9 Disemba mwaka huu siku ya
kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru na kuongeza kuwa zoezi hilo
litakuwa endelevu.
Mhe. Sadiki aliongeza kwa
kusema kuwa, uongozi wa mkoa umewaomba wadau kujitokeza kwa kuchangia
fedha au vifaa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo na amewataka
watendaji kushawishi wananchi wa maeneo yao kutafuta vifaa badala ya
kusubiri kuletewa na Halmashauri.
Pia, Mhe Sadiki
amewahimiza watendaji wa mitaa na kata kutimiza wajibu wao wa
kuhakikisha maeneo wanayoyasimamia yanakuwa katika hali ya usafi muda
wote ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko na pale inakapobainika eneo
fulani lipo katika mazingira ya uchafu basi mtendaji wa eneo hilo
atawajibishwa kwa kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kosa la
kutotimiza wajibu wake.
Vilevile ametoa wito kwa
wananchi kuzingatia usafi kwa kuacha tabia za kutupa taka ovyo hasa
wanapokuwa katika vyombo vya usafiri na kutokujisaidia katika mitaro au
vichaka ili kuepukana na uchafuzi wa mazingira kunakopelekea kutokea
kwa magonjwa ya mlipuko .
LEAT WATOA MIZINGA 350 KWA VIKUNDI VYA UFUGAJI NYUKI
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akikabidhi moja ya mizinga 175 kwa mfugaji nyuki kutoka Kiwel
…………………………………………………………………………………….
NA DENIS MLOWE, MUFINDI
TIMU ya
Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na
Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) umetoa jumla ya mizinga ya
kufugia nyuki 350, kwa vikundi 16 vya wilaya ya Mufindi na Iringa
vilivyoko katika mkoa wa Iringa.
Akizungumza
wakati wa ugawaji wa mizinga hiyo iliyofanyika katika kata ya Sadan
wilayani Mufindi juzi, Afisa mradi wa LEAT kutoka Mufindi Jamal Juma
alisema lengo la mradi huo ni kuimarisha uhifadhi wa mazingira na
kuongeza kipato cha jamii kwa njia ya kufuga nyuki na kupanda miti.
Alisema kuwa
malengo mengine mahususi ya mradi huo ni kuleta ufanisi wa kulinda,
kutunza na kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na kuongeza
kipato cha mwananchi mjasiriamali mara baada ya mauzo ya asali
iliyovunwa kupitia mizinga hiyo.
Alisema kuwa
Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache yenye utajiri mkubwa wa
rasilimali za asili mathalani misitu na wanyapori hivyo kuwa chanzo
kikubwa cha mapato kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Juma alisema
kuwa kutokana na hali hiyo kuna changamoto mbalimbali za usimamizi na
uhifadhi zikiambatana na uchomaji moto ovyo, kuchoma mkaa,ukataji miti
uliokithiri na ujangiri mambo ambayo inasababisha hasara kwa taifa.
Alisema kuwa
kutokana na changamoto hizo husababisha umaskini, kukauka kwa vyanzo vya
maji kutoweka kwa uoto wa asili na kuongezeka kwa athari za mabadiliko
ya tabia nchi.
“ Mradi huu
utasaidia sana jamii ya watu wa wilaya ya Mufindi walioko katika vikundi
vya ufugaji nyuki kuhakikisha unaboresha kipato kwa kuendesha mafunzo
ya ufugaji nyuki na uvunaji, upandaji miti,kusaidia jamii kwa kuzipatia
vitendea kazi vya ufugaji nyuki kama hivi ambavyo leat imetoa kwa
kusaidiana na USAID utasaidia kuondokana na changamoto zote hizo endapo
utafanyiwa kazi kwa umakini. “ alisema
RAIS WA ZANZIBAR AKABIDHIWA TUNZO
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akipokea Tunzo ya dhahabu iliyopewa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kutoka kwa Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana na Watoto Bibi
Zainab Omar Mohamed ( Gold Future Policy Award ) kwa mwaka 2015) ambayo imetolewa na Taasisi ya kimataifa ya World Future Council katika
Mji wa Geneva Uswizi tarehe 20 Oktoba, 2015 baada ya Sheria ya Watoto
ya Zanzibar ya Mwaka 2011 kuzishinda sheria za Nchi nyingine zaidi ya 20
kwa kukidhi vigezo vilivyoshindaniwa,hafla ya makabidhiano hayo
ilifanyika leo Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiiangalia Tunzo ya dhahabu iliyopewa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana
na Watoto Bibi Zainab Omar Mohamed ( Gold Future Policy Award ) kwa mwaka 2015) ambayo imetolewa na Taasisi ya kimataifa ya World Future Council katika
Mji wa Geneva Uswizi tarehe 20 Oktoba, 2015 baada ya Sheria ya Watoto
ya Zanzibar ya Mwaka 2011 kuzishinda sheria za Nchi nyingine zaidi ya 20
kwa kukidhi vigezo vilivyoshindaniwa,hafla ya makabidhiano hayo
ilifanyika leo Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA JESHI LA POLISI
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto),
akipokelewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Chuo cha Polisi
Kilwa Road, kufungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Jeshi hilo,
jijni Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati),
akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi wakati wa
kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi
uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Polisi, Kilwa road, jijini Dar es
Salaam.
Washiriki
wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakishiriki
kuimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi, wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi Kilwa Road jijini Dar
es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akifungua
mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi kilichofanyika Chuo
cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar es Salaam.
Washiriki
wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Polisi wakiwa katika
mkutano Baraza hilo uliofanyika Chuo cha Polisi, Kilwa Road jijini Dar
es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Chama cha Wakulima Tanzania (AFP) chapongeza hotuba ya Rais dk. John Pombe Magufuli
Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Chama cha Wakulima Tanzania (AFP)
kimepongeza hotuba ya Rais wa awamu ya Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli aliyoisoma wakati wa ufunguzi wa
Bunge la 11, Novemba 20 mwaka huu mjini Dodoma.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mahusiano wa Makundi Maalum wa AFP Bw. Peter Sarungi ameeleza kuwa hotuba hiyo imesimama katika mambo ya msingi na yenye kuleta mabadiliko ya kuijenga Tanzania mpya.
Aidha Sarungi aliongeza kwa kusema anaamini kupitia kauli mbiu ya hapa kazi tu uchumi wa nchi utakua na kuboresha huduma za afya,upatikanaji wa elimu kwa watu wote ,kupanda kwa thamani ya shilingi ya Tanzania,kuongeza heshima ya uchumi nje na ndani ya na kuwa na viongozi wawajibikaji.
“kwa kweli hotuba ya rais imegusa nyanja zote muhimu ikiwemo namna ya kukabiliana na kuondokana na rushwa,upatikanaji wa vituo vya afya bora,elimu na mimi naunga mkono jitihada hizi zenye tija ya kuleta mabadiliko ” alisema Sarungi.
Sarungi amekemea vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na baadhi ya wabunge ikiwemo matumizi mabaya ya lugha za kejeli na kuzomea hali ambayo inaharibu utendaji wa kazi za Bunge na kuleta mgawanyiko baina yao .
“Kuna umuhimu wa kuziangalia upya kanuni za kudumu za bunge kwa kuongezwa vifungu vya kuzuia na kutoa adhabu kali kwa mtu yeyote ndani ya ukumbi wa bunge kutumia maneno ya vijembe, kejeli, misemo ya mafumbo na lugha za kuudhi ziwekewe msisitizo wa kuzikomesha ikiwemo kutoa adhabu kali ya kutandikwa viboko” alisema Sarungi.
Mwisho alitoa rai kwa wabunge kuzingatia mambo ya muhimu yaliyowapeleka bungeni ikiwemo kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi na kujenga umoja na upendo bila kujali itikadi za vyama vyao ili kujenga Tanzania mpya.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mahusiano wa Makundi Maalum wa AFP Bw. Peter Sarungi ameeleza kuwa hotuba hiyo imesimama katika mambo ya msingi na yenye kuleta mabadiliko ya kuijenga Tanzania mpya.
Aidha Sarungi aliongeza kwa kusema anaamini kupitia kauli mbiu ya hapa kazi tu uchumi wa nchi utakua na kuboresha huduma za afya,upatikanaji wa elimu kwa watu wote ,kupanda kwa thamani ya shilingi ya Tanzania,kuongeza heshima ya uchumi nje na ndani ya na kuwa na viongozi wawajibikaji.
“kwa kweli hotuba ya rais imegusa nyanja zote muhimu ikiwemo namna ya kukabiliana na kuondokana na rushwa,upatikanaji wa vituo vya afya bora,elimu na mimi naunga mkono jitihada hizi zenye tija ya kuleta mabadiliko ” alisema Sarungi.
Sarungi amekemea vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na baadhi ya wabunge ikiwemo matumizi mabaya ya lugha za kejeli na kuzomea hali ambayo inaharibu utendaji wa kazi za Bunge na kuleta mgawanyiko baina yao .
“Kuna umuhimu wa kuziangalia upya kanuni za kudumu za bunge kwa kuongezwa vifungu vya kuzuia na kutoa adhabu kali kwa mtu yeyote ndani ya ukumbi wa bunge kutumia maneno ya vijembe, kejeli, misemo ya mafumbo na lugha za kuudhi ziwekewe msisitizo wa kuzikomesha ikiwemo kutoa adhabu kali ya kutandikwa viboko” alisema Sarungi.
Mwisho alitoa rai kwa wabunge kuzingatia mambo ya muhimu yaliyowapeleka bungeni ikiwemo kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi na kujenga umoja na upendo bila kujali itikadi za vyama vyao ili kujenga Tanzania mpya.
Muhimbili Yapokea Mashine ya kusaidia wagonjwa kupumua
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akipokea
mashine ya ventilator ya kusaidia wagonjwa kupumua endapo wamezidiwa
baada ya kuugua. Kushoto ni Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na
Afrika, Qasem Sumrein akikabidhi mashine hiyo leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akitoa
ufafanuzi baada ya kupokea mashine hiyo
Daktari Bingwa wa Magonjwa
Mahututi na Uzingizi, Moa Kalunga katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa mashine hiyo kwa
wagonjwa.
Meneja Mauzo barani Afrika,
Gordon Blair akimalizia kufunga mashine ya ventilator ambayo
imekabidhiwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
…………………………………………………………………………………………..
Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) imepokea msaada wa mashine mojaya Ventilator ya kumsaidia mgonjwa
kupumua yenye thamani ya Dola za Kimarekani 36,000 sawa na Shilingi
milioni 80.
Msaada huo umetolewa leo na Kituo cha kitabibu cha Halmiton chenye makao yake makuu nchini Switzerland .
Akikabidhi mashine hiyo mpya na
kisasa , Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika kutoka
Halmiton , Qasem Sumrein amesema pamoja na kutoa msaada huo wataendelea
kutembela MHN ili kutoa mafunzo jinsi ya kuitumia pamoja kufanya
matengenezo endapo itahitajika kwa kuwa mashine hiyo ina waranti ya
miaka miwili.
Akipokea msaada huo Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MHN, Profesa Lawrence Mseru ameshukuru msaada huo
ambao una lenga kuboresha huduma za afya na kueleza kwamba hospitali
hiyo inahitaji kutengeneza ICU nyingine ikiwamo ya mama na mtoto hivyo
bado zinahitajika mashine 120 kwa sababu MHN inapokea wagonjwa wengi.
Akielezea kuhusu mashine hiyo
Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Usingizi Moa Kalunga amesema
mashine hiyo itamsaidia mgonjwa aliye mahututi kupumua na hivyo kuokoa
maisha yake na mgonjwa akirejea katika hali ya kawaida mashine hiyo
inaonyesha .
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
MTU MMOJA MKAZI WA MWANJELWA WILAYANI
MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ADENI EZEKIA [25] ALIFARIKI DUNIA
WAKATI AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA YA
KUSHAMBULIWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA
KUTUHUMIWA WIZI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 25.11.2015 MAJIRA YA SAA 19:30 USIKU HUKO MWANJELWA, WILAYA YA MBEYA MJINI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI MPAKA SASA HAIFAHAMIKI ALIIBA NINI NA SEHEMU GANI.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 25.11.2015 MAJIRA YA SAA 19:30 USIKU HUKO MWANJELWA, WILAYA YA MBEYA MJINI NA MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI MPAKA SASA HAIFAHAMIKI ALIIBA NINI NA SEHEMU GANI.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 14 MKAZI WA KITONGOJI CHA IHEWA, ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHRISTINA S/O YUSTI, ALIUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 25.11.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO IHEWA KATA NA TARAFA YA IGAMBA WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAO TANGU TAREHE 24.11.2015 MCHANA. MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI NA BIBI YAKE DAINES MPELWA NA SIKU HIYO YA TAREHE 24.11.2015 KWENDA SOKONI KUUZA MBOGA NA HAKURUDI/HAKUONEKANA HADI MWILI WAKE NJIANI TAREHE 25.11.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA.
TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA KABLA YA KUUAWA MAREHEMU ALIBAKWA NA KUZIBWA PUA HIVYO KUKOSA HEWA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NJIANI UMBALI WA MITA 174 KUTOKA NYUMBANI KWAO HUKU UKIWA NA MICHUBUKO.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 14 MKAZI WA KITONGOJI CHA IHEWA, ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CHRISTINA S/O YUSTI, ALIUAWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 25.11.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO IHEWA KATA NA TARAFA YA IGAMBA WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAO TANGU TAREHE 24.11.2015 MCHANA. MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI NA BIBI YAKE DAINES MPELWA NA SIKU HIYO YA TAREHE 24.11.2015 KWENDA SOKONI KUUZA MBOGA NA HAKURUDI/HAKUONEKANA HADI MWILI WAKE NJIANI TAREHE 25.11.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA.
TAARIFA ZA AWALI ZINADAI KUWA KABLA YA KUUAWA MAREHEMU ALIBAKWA NA KUZIBWA PUA HIVYO KUKOSA HEWA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NJIANI UMBALI WA MITA 174 KUTOKA NYUMBANI KWAO HUKU UKIWA NA MICHUBUKO.
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Airtel Tanzania yapiga ‘tafu’ Taswa SC
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akimkabidhi vifaa vya
michezo Mwenyekiti wa timu ya waandishi wa habari za michezo nchini
(Taswa SC) Majuto Omary kwa ajili ya kutumika katika mechi zao.
……………………………………………………………………………………………
Kampuni ya Airtel Tanzania
imeiipiga ‘tafu’ timu ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za
michezo nchini, Taswa SC kwa kuwapatia vifaa vya michezo.
Akizungumza katika makabidhiano
hayo jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema
kuwa kampuni yao inatambua mchango wa waandishi wa habari za michezo
nchini katika kuendeleza michezo na kuamua kutoa vifaa vya michezo
ambazo ni seti mbili za jezi na mipira.
Mmbando alisema kuwa mbali ya kuwa wadau wakubwa wa michezo, msaada huo ni moja ya muendelezo wao katika shughuli za kijamii.
“Airtel Tanzania ni wadau wakubwa
wa michezo na burudani, tumeshiriki katika shughuli mbali mbali ikiwa
kuendesha michezo ya Airtel Rising Stars, tumeamua kuunga mkono juhudi
za timu ya waandishi wa habari za
michezo kuwakutanisha wana-habari
na kushiriki katika mazoezi na mechi kwa ajili ya kuhamasisha vipaji na
afya zao,” alisema Mmbando.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo ambao umetokana na maombi yao kwa kampuni hiyo.
Majuto alisema kuwa Taswa SC kwa
kujua wadau wake, waliamua kuomba msaada wa vifaa hivyo na Airtel
Tanzania kuwajali na kuchukua juhudi za haraka kutoa mchango wao.
“Tumeomba kwa kampuni nyingi,
bado hatujapata majibu ya kukubaliwa au la, Airtel Tanzania imeonyesha
mfano kwa kutusaidia kwa haraka sana, ni faraja kwetu, tunawaomba
wengine waige mfano wao,” alisema Majuto.
Alisema kuwa Taswa SC bado
inakabiliwa na changamoto ya vifaa vingine kama viatu kwa timu zake za
soka na netiboli na kuwaomba wadau wafikirie kuwasaidia. “ Tupo tayari
kupokea vifaa vingine, timu
inatakiwa kuwa na vifaa vya
kutosha, jezi za aina mbalimbali, mipira ya mazoezi na mechi, hivyo kama
kuna wadau wanataka kutusaidia, wasisite kufanya hivyo,” alisisitiza
Majuto.
COMPACT PLUS SUBSCRIBERS SCORE A FESTIVE EPL SEASON ON SUPERSPORT 3 – PLUS NEW SUPERSPORT 5 CHANNEL
ng
football fans on Compact Plus tidings of great joy! The Barclays
Premier League (English Premier League) currently in mid-season will
return to SuperSport 3. Hence, Compact Plus subscribers will be
delighted to know that from 01 December 2015, they will be able to
access the bulk of the EPL action for the rest of the football season
which ends in May 2016!
As part of MultiChoice Africa’s
commitment to ensuring that DStv subscribers have a bumper Festive
season this year, all active Compact Plus subscribers will get the EPL
experience on SuperSport 3 while SuperSport 5 will be made available to
provide coverage of the La Liga.
This move will ensure all the
subscribers have a fantastic holiday season with a wide range of added
entertainment for the whole family which includes the various holiday
pop-up channels including the Nigerian Festivals, Hoolee, the Pope’s
Kenya Visit alongside new channels like M-Net Family, Vuzu and Emmanuel
TV!
“We understand that our
subscribers are experiencing tough economic conditions at the moment and
want to ensure we go the extra mile for our valued subscribers. The
DStv festive season will give you 100% and more great family sport, kids
programming, news and entertainment!,” said COUNTRY GM.
The Barclays Premier League is the
sporting world’s most riveting soap opera, filled with larger than life
characters who thrill, infuriate, spread joy and despair in equal
measure.
From an unfortunate slip to losing
grip of the title, to grabbing it via a stoppage time winner no other
league in the football world comes close to delivering such amazing
drama.
Featuring the cream of the
Football Management crop who can always be depended upon for a
newsworthy soundbite, to some of the beautiful games’ greatest players
who regularly turn on the flair and style, the Premier League will keep
fans across the globe on the edge of their seats, talking and tweeting
non-stop from one match week to the next.
DStv Compact Plus subscribers will
get to experience the unpredictability of the league that has been
demonstrated this season. So far, this has been one of the most open
football seasons in years with the likes of Leicester City competing
with the big names for a top 4 slot, while champions Chelsea lag close
to the drop zone.
This festive season will dish up
its fair share of mouth-watering fixtures for subscribers to look
forward to, including the following blockbusters:
• Arsenal v Man City – December 21, 2015
• Man Utd v Chelsea – December 28, 2015
• Everton v Tottenham – January 2, 2016
• Liverpool v Arsenal – January 13, 2016
• Man City v Everton – January 13, 2016
• Chelsea v Everton – January 16, 2016
• Liverpool v Man Utd – January 17, 2016
• Arsenal v Chelsea – January 24, 2016
• Man Utd v Chelsea – December 28, 2015
• Everton v Tottenham – January 2, 2016
• Liverpool v Arsenal – January 13, 2016
• Man City v Everton – January 13, 2016
• Chelsea v Everton – January 16, 2016
• Liverpool v Man Utd – January 17, 2016
• Arsenal v Chelsea – January 24, 2016
So, can the reigning champ Chelsea
survive relegation? Will Mourinho be fired? Who will make up the top 4
for Champions league qualification? Can Klopp revive Liverpool? Catch
all this football drama on SuperSport 3 from 1 December 2015!
For more sports news and live match fixtures on SS3 and SS5, please visit www.supersport.com.
KAMPUNI YA MEGATRADE INVESTMENT LTD YAVIPIGA JEKI CHUKO KIKUU CHA USHIRIKA NA BIASHARA,MOSHI PAMOJA NA CHAMA CHA SOKA CHA MKOA WA KILIMANJARO
![]() |
| Mweka hazina wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,Kusianga Kiata,akitizama hundi iliyotolewa na kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha. |
![]() |
| Baadhi ya wadau wa soka waliofika kushuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo jengo la Voda House. |
![]() |
| Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha,Edmund Rutaraka akizungumza jambo mara baada ya kukabidhi hundi kwa mkuu huyo wa chuo. |
![]() |
| Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika na Bashara (MOCU) Profesa Faustine Bee akizungumza mara naada ya kukabidhiwa hundi hiyo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. |
BALOZI SEIF ALI IDI ATOA MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU HALI YA KISIASA ZANZIBAR
Seif
Ali Idi ameimabia RFI Kiswahili kuwa, viongozi wa kisiasa kutoka
serikali na upinzani wamekubaliana uchaguzi Mkuu kurudiwa tena.
Hata hivyo, Makamu huyo wa pili
amedokeza kuwa hadi sasa haijaafikiwa ikiwa tume ya sasa ya Uchaguzi
inayoongozwa na Mwenyekiti Salim Jecha Salim aliyefuta matokeo hayo
itakubaliwa kusimamia uchaguzi mpya.
Katika hatua nyingine, kiongozi huyo ameeleza kuwa rais Ali Mohamed Shein anaendelea kuwa uongozini kikatiba.
Wananchi wa Zanzibar wanasubiri uamuzi wa viongozi wa kisiasa kuhusu mvutano huu wa kisiasa katIka visiwa hivyo.
WAKAZI WA MIKOA YA MANYARA,ARUSHA NA KILIMANJARO WAJITOKEZA UZINDUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.
![]() |
| Brass Band ya Chuo cha Polisi Moshi ikiongoza maandamano ya uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini . |
![]() |
| Wanafunzi wa kozi ya awali ya Askari Polisi kutoka shule ya Polisi Tanania wakiwa katika manda,ano ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini. |
![]() |
| Maanda,mano ya lipita maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi. |
![]() |
| Maandamano hayo yakipita eneo la kituo kuu cha Mabasi cha mjini Moshi yakieekea katia viwanja vya kituo hicho ambako uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini . |
![]() |
| Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisikiliza malezo kutoka katika banda la shirika la NAFGEM linalopambana na vitendo vya Ukeketaji. |
![]() |
| Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akisikiiza maelezo kutoka TAWREF ambao pia wameshiriki katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. |
SHIWATA kugawa nyumba 14 Mkuranga, yampongeza Dkt. Magufuli kumteua Majaliwa Waziri Mkuu
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania
(SHIWATA)umeandaa mkutano wa wanachama wake Jumamosi kutangaza majina ya
wanachama watakaokabidhiwa nyumba 13 na misingi ya nyumba 14 katika
kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim
Taalib alisema jana Dar es Salaam jana kuwa mkutano huoutakaofanyika
Ilala, Bungoni Dar es Salaam kuanzia saa 4 pia watatangazwa viongozi
watakaoshika nafasi za uongozi zilizo wazi.
Nafasi za uongozi zilizo wazi ni
Makamu Mwenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Marehemu Kepteni John
Komba,Katibu ambayo ilikuwa inashikiliwana Selemani Pembe ambaye yupo
India kikazi na Mweka Hazina ambaye Flowin Nyoni ambaye ni Mhadhiri wa
Chuko Kikuu cha Dodoma.
Katika hatua nyingine SHIWATA
imeupongeza uongozi wa Rais John Pombe Magufuli kumteua Mkufunzi wa
Mpira wa Miguu wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Majaliwa Kassim
Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
Alisema medani ya michezo
inahitaji msukumo wa viongozi wanaojua michezo hivyo ni kipindi cha
kujiandaa kuiletea sifa Tanzania kupitia michezo ya soka, ndondi,
riadha,netiboli na mingine katika michezo ya Afrika Mashariki,Michezo ya
Afrika, michezo ya madola na michezo ya dunia.
Taalib alisema ili kuonesha
viongozi wetu wapya ni wapenda michezo hivi karibuni Rais Magufuli
alikubali kuwa mgeni rasmi katika pambano la kuwania kucheza kombe la
dunia kati ya Stars na Algeria kwenye uwanja wa Taifa ambapo alimtuma
Makamu wa Rais, Suluhu Samia Hassan kumwakilisha hiyo inaonesha Tanzania
imepata viongozi wapenda michezo.
Alisema wasanii na wanamichezo
watapiga hatua kubwa mbele kwenye uongozi wa Dkt. Magufuli kwani kuna
kila dalili kuwa kazi zao zitathaminiwa na kupewa kipaumbele.
Taalib alisema mtandao wa SHIWATA
ambao unajumuisha wanamichezo, wasanii, waigizaji, waandishi wa habari
na wasanii wa kazi za mikono wamemkubali Dkt. Magufuli kwa kasi
aliyoanza nayo ya kufuatilia mambo hasa kuondoa kero za wanyonge ambao
kwa kipindi kirefu wamekuwa hawapati huduma muhimu za kijamii za elimu
na afya.
Alisema wasanii wanaimani kubwa na
Dkt. Magufuli kwani ni mchapakazi na mtu asiyependa wananchi wake
wadhulumike wakiwemo wasanii ambao walizunguka nchi nzima kwenye kampeni
zake na kujionea shida za wananchi zinazowakabili wakiomba mahitaji
mbalimbali katika nchi yao yenye rasilimali lukuki.
SHIWATA yenye wanachama zaidi ya
8,000 nchini inamiliki hekari 300 za kujenga nyumba za makazi wa bei
nafuu ambako nyumba 120 zimekwisha jengwa katika kijiji cha Mwanzega
Mkuranga na hekari 500 zilizotengwa kwa ajili ya kilimo zimelimwa na
kupanda mazao mbalimbali katika kijiji cha Ngarambe Mkuranga.





















No comments:
Post a Comment