Pages

Thursday, November 19, 2015

PSPF, NHIF wazindua fao la matibabu kwa wanachama wa mpango wa uchangiaji hiari



Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, SSRA, Omar Kahlfan, (katikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Neema Muro, (wa pili kushoto), Meneja wa Mpango wa Uchagiaji wa Hiari wa PSPF,Mwanjaa Sembe, (wa kwanza kushoto) na maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, (kulia waliosimama), wakishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, wakitia saini makubaliano ambayo yatawezesha taasisi hizo mbili kushirikiana ambapo Wanachama wa PSPF wa mpango wa Uchangiaji wa Hiari, watadhaminiwa na Mfuko huo ili waweze kuingizwa kwenye utaratibu wa kupatia bima ya afya kutoka NHIF.
Na Christian Gaya Majira Ijumaa Novemba 20, 2015
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wameingia makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu bure kwenye hospitali zote zenye mkataba na NHIF.

Makubaliano hayo yalitiwa saini Novemba 18, 2015, kati ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando na kufuatiwa na uzinduzi rasmi ambapo wanachama wa kwanza zaidi ya 10 wamepatiwa kadi za Bima ya Afya.

Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya PSPF, jingo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu alisema, uamuzi huo wa PSPF kushirikiana na NHIF, ni utekelezaji wa malengo na ahadi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dtk. John Pombe Magufuli, ambaye aliwaahidi Watanzania wote wanapata huduma za afya zilizo bora. “  Katika kuhakikisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais inaaanza kutimizwa: PSPF kwa kushirikiana na wenzetu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya tutatoa huduma za afya kwa wanachama wa Mpango wa Uchangaji wa Hiari wa PSPF.” Alisema Bw. Mayingu katika hotuba yake.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pensheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha. wajasiriamali wadogo ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla
Kwa kutoa kinga ya huduma ya bima ya afya kwa wanachama wake na familia zao PSPF inatambua kwamba wananchi walio na afya bora ni nguvukazi na raslimali kubwa katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini. Kwa kutoa mafao ya huduma ya bima ya afya PSPF itaisaidia serikali katika kuinua hali ya afya ya wananchi wote na hasa wale walioko na wanaofanya kazi kwenye sehemu hatari zaidi, kwa kutoa mafao ya huduma za afya PSPF itachangia serikali katika kukidhi mahitaji ya wananchi na kuongeza umri wa kuishi wa watanzania.
Tangu kuzinduliwa kwake mapema Machi mwaka 2013 tayari wanachama zaidi ya 5,000 wamejiunga na mpango huo wa hiari ambapo makundi zaidi ya 25 yamejiunga na mfuko huu kutokana na ubora wa mafao yake na mikopo inayotolewa kwa wanachama waliojiunga na mfuko huo kwa miaka mitano

No comments:

Post a Comment