– Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na
kuwapongeza baadhi ya Wabunge wapya wa bunge la 11, walipokutana kwenye
viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri
Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika
leo Nov 20, 2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge
wa Ilemela, Angelina Mabula kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino
wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe.
Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma.
Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mtoto
Majaliwa mtoto wa Waziri Mkuu mpya kwenye viwanja vya Ikulu ndogo
Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya
Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini
Dodoma. Picha na OMR
Waziri Mkuu mpya wa awamu ya
Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, akimpongezwa na mkewe baada ya
kuapishwa rasmi leo kwenye Viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino mjini
Dodoma, leo Nov 20, 2015.Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Mlata, kwenye viwanja vya Ikulu
ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu
ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015
mjini Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge
wa Peramiho, Mhe Jenister Mhagama, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo
Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya
Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini
Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Magharibi, Asham Abdallah Juma, kwenye
viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri
Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika
leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge
wa Nzega, Hussein Bashe, kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati
wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa
Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na
OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge
wa Shinyanga mjini Stephen Masele , kwenye viwanja vya Ikulu ndogo
Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya
Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini
Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge
Mchengerwa kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za
kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim
Majaliwa zilizofanyika leo Nov 20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mbunge
wa Viti maalum Kaskazini Unguja, Angela Malembeka, kwenye viwanja vya
Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya wa
awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov
20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hizo kwenye viwanja
vya Ikulu ndogo Chamwino wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mpya
wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa zilizofanyika leo Nov
20,2015 mjini Dodoma. Picha na OMR
Arusha yawa mfano katika ukusanyaji kodi kieletroniki
Na Raymond Mushumbusi- Maelezo
Jiji la Arusha limekuwa mfano mzuri wa
kuigwa kutokana na hatua kubwa iliyofikia katika ukusanyaji kodi kwa
halmashauri zake kupitia mfumo mpya wa ukusaanyaji kodi wa kieletroniki.
Hayo yamezungumzwa leo na na msemaji waOfisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bi
Rebecca Kwandu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mfumo
wa kieletroniki wa ukusanyaji wa kodi na tozo mbalimbali za serikali
ulioanzishwa na TAMISEMI kwa lengo la kuboresha makusanyo ya mapato
katika halmashauri zote nchini.
Bi Rebecca amesema jiji la Arusha
limefanikiwa kuongeza mapato yake toka Tsh Billion 5 mwaka 2012/2013
hadi Tsh billion 10.7 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 214
huku mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo yameongezeka toka Tsh
billion 1.2 mwaka 2013/2014 hadi Tsh Billion 4.8 mwaka 2014/2015 sawa
na ongezeko la asilimia 400.
Aidha kwa mwaka 2015/2016 jumla ya Tsh Billion 8.2 zimetengw
a kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za mapato ya ndani sawa na asilimia 63 ya bajeti yote ya mapato ya ndani.
Naye Mwekahazina wa jiji la Arusha Bw. Kessy
Mpakaya amesema mafanikio waliyoyapata ni kutokana na mabadiliko ya
mfumo wa ukusanyaji kodi na tozo za serikali kutoka mfumo wa kulipa kwa
risiti mpaka mfumo wa kieletroniki ambao umewasaidia kuboresha
ukusanyaji wa mapato ya jiji hilo.
“ Mfumo huu umetusaidi kutunza kumbukumbu za
walipa kodi na makusanyo ya kodi kiujumla na pia fedha zilizokusanywa
tumeziweka kwenye ununuzi wa vifaa, ujenzi wa barabara na miradi
mbalimbali ya maendeleo” alisema Bw. Kessy.
Halmashauri nchini zinapaswa kufahamu kuwa
teknolojia pekee ya matumizi ya TEHAMA haiwezi kuleta mabadiliko pasipo
fikra za watumiaji wa mfumo na walipa kodi kubadilika.
ALEX MSAMA AZUNGUMZIA MAANDALIZI YA TAMASHA LA KUSHUKURU DESEMBA 25, WAIMBAJI KUTOKA MAREKANI KUSHIRIKI
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi
zake zilizopo Kinondoni Moroco wakati alipotoa mwelekeo wa maandalizi
ya TAMASHA la Kushukuru linalotarajiwa kufanyika Desemba 25 kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam na kushirikisha waimbaji
mbalimbali wa muziki wa injili kutoka nchini Tanzania na nje ya
Tanzania.
Bw. Alex Msama amesema leongo la
Tamasha hilo la Kushukuru ni kutoa shukura ni kwa mwenyezi mungu
kutokana na kuijalia nchi yetu na kufanya uchaguzi uliokuwa haki na huru
tukiwa salama kwa amani jambo ambalo tunapaswa kumshukuru mungu.
Tumeshuhudia chaguzi katika
nchi mbalimbali zinapitia Chanamoto nyingi zikiwemo Vurugu lakini nchini
kwetu uchaguzi umepita salama na kutuletea kiongozi mchapakazi Rais Dk.
John Pombe Magufuli.
Msama ameongeza kwamba mbali ya
waimbaji kutoka Tanzania kamati yake ya maandalizi iko katika
mazungumzo na waimbaji mbalimbali wa kimataifa kutoka nchini za nje.
Kama vile Afrika Kusini, Marekani na Uingereza, Hii itakuwa ni mara ya
kwanza kwa waimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Marekani
kushirikishwa katika matamasha ambayo Kampuni ya Msama Promotion
imekuwa ikiyaandaa nchini Tanzania.
Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Hamisi Pembe.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion Bw. Alex Msama akisisitza jambo wakati alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tamasha la kushukuru,
Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Hamisi Pembe.
Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya
Maandalizi ya Tamasha hilo, Hamisi Pembe akifafanua zaidi kwa waandishi
wa habari kuhusu maadalizi yaliyokwishafanyika kwenye suala zima la
ulinzi katika tamasha hilo.
Serikali yaboresha Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato
Serikali imeboresha matumizi ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielekitroniki katika mamlaka za serikali za mitaa.
Hayo yamesemwa na msemaji wa
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Bi.
Rebecca Kwandu leo jijini Dar es salaam.
Bi Rebecca amesema kuwa
TAMISEMI imekuwa ikiendelea kwa nyakati tofauti kufanya maboresho
mbalimbali ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii na kuzisaidia
mamlaka hizo katika kuongeza mapato ya ndani na kuondokana na uteuzi wa
ruzuku kutoka Serikali Kuu.
“Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI
iliamua kuanzisha mfuko wa Local Governement Collection Information
System (LGRCIS) baada ya kufanya tafiti mbalimbali kwa nyakati tofauti
na zilionyesha kuwa hakukuwa na mfumo wowote wa kielektroniki
kurahisisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Halmashauri” alifafanua
Bi. Rebecca.
Mbali na hayo Msemaji huyo
alisema kuwa miongoni mwa malengo makuu ya kuanzishwa kwa mfumo wa
LGRCIS ni pamoja na kupata taarifa za walipa kodi wa mamlaka za serikali
za mitaa na kuhifadhiwa kwa usahihi katika kanzi data ya mfumo.
“ Kupata takwimu sahihi ya
vyanzo vya mapato na kufanya usuluhishi kati ya kilichokusanywa na
kilichotarajiwa kukusanywa, kuongeza mapato kwa kasi zaidi kwa kuwa na
uhakika wa makusanyo katika vyanzo vikuu, kuweka uwazi na uwajibikija
katika makusanyo ya mapato,na kuhimarisha ulipaji miamala ya kodi na
tozo itakayofanywa na walipakodi” aliongeza Bi Rebecca.
Pia alisema kuwa matarajio ya
TAMISEMI ni kuwa mfumo wa LGRCIS utaleta mabadiliko makubwa katika
Halmashaurina kuachana na utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali kuu.
Hata hivyo teknolojia pekee ya
matumizi ya TEHAMA haiwezi kuleta mabadiliko pasipo fikra za watumiaji
wa mfumo wa walipakodi kubadili mazoea.
No comments:
Post a Comment