Pages

Sunday, November 22, 2015

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kufanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo

images 

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atafanya ziara katika Hospitali ya Taifa Mhimbili Kesho Jumatatu (23 Novemba, 2015) kuanzia majira ya saa nne asubuhi.
Ziara hiyo ni kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyeagiza fedha zilizochangwa ajili ya hafla ya wabunge zitumike kununulia vitanda vya wagonjwa katika hospitali hiyo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasilino, IKULU
20 Novemba, 2015

MWAKALEBELA AKANUSHA KUFUTWA KWA KESI YAKE DHIDI YA MCHUNGAJI PETTER MSIGWA NA MKURUGEZI WA MANISPAA YA IRINGA.


 FREDRICK MWAKALEBELA AKIWA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM  WILAYA YA IRINGA MJINI WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
 BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOANI IRINGA WALIPOKUWA WANAWASIKILIZA FREDRICK MWAKALEBELA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM WILAYA YA IRINGA MJINI.
Chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa mjini
kimekanusha kufutwa kwa kesi yao dhidi ya mkurungenzi wa manispaa hii pamoja na
mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji PETTER MSINGWA.
 
Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa CCM
wilaya ya iringa mjini ELISHA MWAMPASHE amesema kuwa taarifa zilizosambaa
sehemu mbalimbali sio za kweli.
 
“Nimekuwa nikipigiwa simu nyingi toka jana nikipewa
taarifa kuwa kesi yetu imetupiliwa mbali na imeenea sana kwenye mitandao ya
kijamii na maeneo mbalimbali ukweli ni kwamba kesi ya uchaguzi namba tano ya
2015 haijafutwa”alisema Elisha mwampashe.
 
Mwampashe ameongeza kuwa kesi hiyo bado haijapangiwa
siku ya kusikilizwa wala kupangiwa jaji wa kuendesha kesi hiyo hivyo anashangaa
kuaona taarifa zinazendelea kuenena mitaani
 
“Ifahamike kuwa mahakamani kuna shauri la
msingi  ambalo lilikuwa na kupinga
matokeo na kuna  shauri dogo  namba 28 la mwaka 2015 ndio lilikuwa
likizungumziwa jana kwa lengo la kuomba kupunguziwa dhamana kutokana na sheria
kuruhusu kufanya hivyo” alisema Elisha Mwampashe.
 
Mwampashe amemalizia kwa kuwataka wananchi  na wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea
kuwa na subra kwa kuwa haki yao ya msingi itapatikana mahakani na kuwasii
wananchi wanaopotosha taarifa hizi.
 
 Kwa upande
wake Fredrick Mwakalebela aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la iringa mjini
amesema kuwa shauri lilofutwa ni la kuomba kupunguziwa pesa ya dhamana.
 
“Nilikuwa kimya kutokana na kufatilia swala hili
kimya kimya kwa lengo la kupata haki yangu ya msingi ambayo nimenyang’anywa na mkurugezi
wa manispaa ya iringa pamoja na mchungaji petter msingwa” alisema Fredrick
mwakalebela 
 
Mwakalebela amemalizia  kwa kusema kuwa kesi hiyo inaendeshwa naye
pamoja na chama cha mapinduzi kwa kuwa chama ndio kilichompa nafasi ya kugombea
ndio maana kila kitu anachokifanya chma lazima kijue juu ya kesi hivyo. 
Ilitolewa
aarifa Kuhusu kutupiliwa mbali kwa shauri ya dhamana ya kesi ya ubunge Iringa
Mjini Msajiri wa Mahakama kuu Iringa Bi Ruth Masamu amesema kesi ya aliyekuwa
mgombea ubunge Jimbo La Iringa Mjini Fredrick Mwakalebela alitoa ombi la kuomba
kupunguziwa dhamana kutoka milioni kumi na kushuka angalau kwa kiasi kidogo.
Hii ni
kutokana na vifungu vya sheria kuruhusu kuomba ombi hilo na mahakama kulikataa
na kumtaka aongeze mtuhumiwa ambaye ni mwanasheria wa serikali kwenye kesi yake
kwa gharama hiyohiyo.
Hivyo uvumi
uliotolewa jana kwamba kesi imefutwa si kweli kwa sababu mpaka sasa kesi bado
haijapangwa wala kuanza kusikilizwa.

Wakazi wa Arusha sasa kufurahia Intaneti ya kasi zaidi ya 4G LTE kutoka TIGO

Mshereheshaji wa hafla MC Taji Liundi akitoa maelekezo jinsi intaneti ya kasi zaidi kutoka Tigo katika  hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE   iliyofanyika jijini Arusha  mwishoni wa wiki iliyopita  
Wadau Husni na Benedict Mponzi wakiwa katika pozi katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE   iliyofanyika jijini Arusha  mwishoni wa wiki iliyopita  
Watoa huduma wa Tigo wakiwa katika pozi tayari kutoa msaada na maelekezo jinsi gani wateja wa TIgo wa jijini Arusha na maeneo ya jirani watakavyofurahia intaneti ya kasi  hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE   iliyofanyika jijini Arusha  mwishoni wa wiki iliyopita  
Mkuu wa kitengo cha biashara wa Tigo  Bw, Shavkat Berdiev akitoa hotuba fupi katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE   iliyofanyika jijini Arusha  mwishoni wa wiki iliyopita
Wageni rasmi wakipiga ngoma kama kuashiria uzinduzi rasmi w a Intaneti ya kasi zaidi nchini ya TIGO 4G lte katika hafla ya uzinduzi huo  iliyofanyika jijini Arusha  mwishoni wa wiki iliyopita  
Watoa huduma wa Tigo mkoani Arusha wakiwa katika pozi na tayari kutoa huduma na maelekezo jinsi huduma ya Tigo 4G lte itakavyowanufaisha wakazi wa jiji la Arusha na maeneo ya jirani katika hafla iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita 
Mtaalamu wa mitandao ya kijamii wa Tigo , Bi Samira Baamar akiwa na washindi wa zawadi za vifaa vya intanet vinavyotumia teknolojia ya 4g lte  (MODEM NA ROUTER ) waliofanikiwa kujishindia katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE   iliyofanyika jijini Arusha  mwishoni wa wiki iliyopita  
Mgeni rasmi Wilson E Nkambaku , mkuu wa wilaya  Arumeru akitoa hotuba fupi katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE   iliyofanyika jijini Arusha  mwishoni wa wiki iliyopita  
Umati wa wakazi wa jiji la Arusha wakifurahia jambo katika katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE   iliyofanyika jijini Arusha  mwishoni wa wiki iliyopita 
 
………………………………………………………………………………….
Arusha,
Novemba 18 2015.
Wateja wa Tigo waishio Arusha
sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia
upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo
kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano
zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.
‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana
katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es
Salaam kuanzia mapema mwaka huu’’, amesema Mkuu wa Kitengo cha Internet
David Zacharia.
Akizungumza  na waandishi wa
habari jijini Arusha, Zacharia amesema: “ni kielelezo cha jinsi ambavyo Tigo
imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya dijitali katika maisha
ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia teknolojia ya
kisasa na kibunifu nchini Tanzania.”
Mtandao wa 4G LTE una kasi kubwa zaidi katika kuperuzi
na kupakua kwa rahisi kutoka kwenye mtandao wa
intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma
hii p
ia inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora hali ya juu na kufanya
mikutano kwa njia ya mtandao. 
 
“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waishio Arusha kwamba sasa
wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na Intaneti
yenye kasi zaidi,” Gutierrez amesema. Arusha ni makao makuu ya taasisi nyingi
za kimataifa ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki na kitovu cha utalii nchini.
Wateja wote wa Tigo 4G LTE watanufaika na
promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi  elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama
bonasí.
Ametaja miji mingine katika mikoa sita ambapo 4G itaanza
kupatikana hivi karibuni kuwa ni Arusha, Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza
na Tanga, “jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G
nchini Tanzania.” Lengo kuu ni kufkisha huduma ya 4G katika kila kona za
nchi ifikapo mwaka ujao, Zacharia ameongeza kusema. 

No comments:

Post a Comment