Watanzania
wamekuwa wakipambana kila siku ili kijikwamua kutoka katika umasikini
uliokithili wa kukosa hata milo mitatu na mahitaji muhimu kama afya ,
maji , malazi , mavazi na elimu. Serikali ya awamu ya nne ikiongozwa na
Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ilipambana vilivyo kuhakikisha
inasaidia watanzania hasa wale walioko katika kaya masikini sana
Tanzania kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kujikwamua katika
hilo.
TASAF ni Mfuko wa Jamii, ambao Serikali inausimamia na kuutengea fedha pamoja na kupata ufadhili kutoka kwa wadau wa maendeleo, miongoni mwa wadauwa maendeleo ni Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Shirika la Maendeleo la Serikali ya Marekani (USAID) na Serikali ya Uhispania (Spain)
Mufuko wa maendeleo ya jamii(TASAF) umeanzishwa kwa dhumuni la kufadhili na kuwezesha shughuli mbalimbali za kimaendeleo nchini Tanzania. Makala hii imejikita katika kuchanganua na kuelezea kwa jinsi gani mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) ulivyosaidia kaya masikini Tanzania.
Lengo kuu la mfuko huu ni kuwezesha jamii zenye kipato cha chini kuinua hali yao ya kimaisha kwa kuanzisha shughuli zitakazo inua uchumi wao kwa kupitia taasisi zao wenyewe. Taasisi hizi zitaundwa na wao wenyewe kwa kuanzia ngazi ya kikundi na hatimae vikundi vitaunda jumuiya na hata kuunda shirikisho la kuwakomboa wao wenyewe.
Malengo mahususi ni pamoja na kuwezesha uundaji wa hiari wa vikundi vyenye mwelekeo mmoja na kuanzisha ushirikiano baina ya vikundi na taasisi zingine za maendeleo ili kukuza mitaji, stadi za kazi na ujuzi, Kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwao, Kuwezesha vikundi vyenye ari vya watu maskini kutekeleza shughuli za kuzalisha mali, kusaidia shughuli za uwekezaji kwenye miradi midogomidogo inayotekelezwa na watu maskini ili kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi na Kujenga uwezo wa wanakikundi na taasisi zao za kijamii, kama vile Halmashauri za vijiji nk
Mfuko huu umekuwa na awamu kuu tatu mpaka sasa za kuwezesha kaya masikini Tanzania kujikwamua kiuchumi. Baada ya kukamilika kwaAwamu ya I na ya II , TASAF imeleta mafanikio makubwa kwa pande zote mbili za nchi yetu ya Tanzania ( Zanzibar na Tanzania Bara.) kwa kuwa jamii maskini zimewezeshwa kutekeleza miradi zaidi ya13,954 ( kawa awamu ya Kwanza miradi iliyotekelezwa na kukamilika ni 1,704 na wakati wa Awamu ya Pili jumla ya miradi 12,250 ilikamilika).

DUCE yaadhimisha maadhimisho ya miaka 10.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Jumuiya ya Chuo Kikuu Kishiriki
cha Dar es salaam (DUCE) imeaswa kuendelea kushiriki katika shughuli za
kijamii kwa wanapanga siku moja kila mwaka ya kutoa huduma za kijamii
ili kuwa kitovu cha nidhamu bora na chachu ya maendeleo nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es salaam upande wa Taaluma Prof. Florens
Luoga wakati wa kufungaji wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya chuo
cha DUCE leo jijini Dar es salaam.
“Nawashukuru sana waliojitokeza
kwenda kutoa misaada hospitalini, kushiriki kuchangia damu, kupanda
miti na kwenda shule mbalimbali kuhamasisha masuala anuai ya kielimu kwa
wanafunzi pamoja na walimu wao ili elimu iwe na tija na ufanisi kwa
Watanzania wa sasa na baadaye” alisema Prof. Luoga.
Akitoa hotuba ya kufunga
sherehe hizo, Prof. Luoga aliupongeza uongozi wa chuo cha DUCE kwa kuwa
sehemu ya jamii ya Watanzania na kusisitiza kuwa ni wajibu wa chuo kikuu
chochote duniani kutoa mchango kwa jamii katika elimu na kuwaletea
maendeleo wananchi na taifa kwa ujumla.
Prof. Luoga alisisitiza kuwa
ushiriki katika shughuli za kijamii utaendelea kusaidia chuo hicho
kujitangaza na kujenga mahusiano mema miongoni mwa wanajamii ambao ndiyo
chuo kimekuwa kikiwahudumia kwenye utoaji huduma mbalimbali.
Naye Mkuu wa chuo cha DUCE
Prof. William Anangisye alisema kuwa zaidi ya kutoa taaluma katika elimu
ya juu, wanajukumu pia la kujali suala la maadili kwa wanachuo.
Kwa upande mwingine Prof.
Anangisye amesema kuwa chuo chake kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
katika kutoa taaluma na huduma bora kwa wanachuo ambazo ni pamoja na
upungufu wa wahadhiri wa ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu na uwezo
mdogo wa mabweni ya kulala ya wanachuo.
Chngamoto nyingine ni uhaba wa
vyumba vya kutosha vya madarasa na kumbi za kuendeshea semina wakati wa
masomo ikizingatiwa chuo hicho kimerithi majengo na miundo mbinu mingine
kutoka kilichokuwa chuo cha ualimu cha Chang’ombe pamoja.
Aidha, katika maadhimisho hayo
yaliyofanyika kwa wiki moja kuanzia Novema 16 hadi 20 mwaka huu,
yamefanyika mashindano ya michezo mbalimbali ikiwemo soka, mpira wa
pete, kuvuta kamba, kufukuza kuku, kukimbia kwa magunia, riadha na
uvaaji wa mavazi yenye staha kwa wanachuo wa kike na wa kiume.
Katika shindano hilo la mavazi
yenye staha, mshindi kwa upande wanaume alikuwa John Paul mwanafunzi wa
mwaka wa pili na Ruth Mtata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa upande wa
wanawake.
Washindi hao walisema kuwa
wanafurahia maisha yao wakati wote wakiwa chuoni na hata wakiwa nyumbani
kwani wao ni walimu na wakiwa katika mavazi yenye heshima ni rahisi
kuwafundisha wanachuo wengine na jamii kwa ujumla kuvaa mavazi kulingana
na mila na desturi za kitanzania ambapo waliwaasa wanachuo wengine
kuvaa nguo ambazo hazitoi maswali kwa wanafunzi wanaowafundisha na jamii
kwa ujumla.
KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU ANOGESHA MAHAFALI YA 10 YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE DAR ES SALAAM LEO
Mkurugenzi
wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Thomas Katebalilwe akihutubia kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, aliyekuwa mgeni
rasmi katika mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila akielezea mafanikio ya chuo.
Mkurugenzi
wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Thomas Katebalilwe (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa
Sifuni Mchome, mwanafunzi, Benard Nyoni, aliyefanya vizuri katika masomo
yake wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere (MNMA), Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa
chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila na Kaimu Mwenyekiti ya Bodi ya
chuo, Evelyne Makalla.
Mkurugenzi
wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Thomas Katebalilwe (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti kwa
niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa
Sifuni Mchome, mwanafunzi, Godfrey Nchimbi aliyefanya vizuri katika
masomo yake wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu
ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kushoto ni
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila, Kaimu Mwenyekiti ya Bodi
ya chuo, Evelyne Makalla na Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MASO), Elias
Kumanya.
Wahitimu
wa ngazi ya cheti, stashahada na shahada ya kwanza waliofanya vizuri
katika masomo yao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa
vyeti na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, wakati wa
sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
(MNMA)
Meza kuu ilivyokuwa ikionekana kwenye mahafali hayo.
Mkurugenzi
wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Thomas Katebalilwe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu
wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto), na Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya chuo, Evelyne Makalla katika mahafali hayo.
Brass Bendi ya Magereza ikiongoza maandamano wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi na viongozi wengine wakiongoza maandamano kuelekea eneo la sherehe.
Wahitimu
wa ngazi ya cheti, stashahada na shahada ya kwanza wakiwa katika
sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
(MNMA), yaliyofanyika Dar es Salaam.
Wanafunzi wenzao wakiwapongeza watangulizi wao kwa kuhitimu.
Brass Bendi ya Magereza ikitoa burudani katika mahafali hayo.
Wahadhiri wa chuo hicho wakiwa katika mahafali hayo.
Wageni waalikwa wakijumuika katika sherehe hiyo.
Hapa ni kazi tu
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu waliofanya vizuri masomo yao wakiwa katika icha ya pamoja na meza kuu.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.
Hiyo ni furaha tupu ya kuhitimu
DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA DISEMBA 15
Kalenda ya dirisha la usajili kwa
vilabu vya Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja
la Pili (SDL) lilofunguliwa Novemba 15, litafungwa Disemba 15 mwaka huu.
Vilabu vinavyoshiriki ligi hizo
zilizopo chini ya Shirikisho Mpira wa Miguu (TFF) vinaombwa kufanya
usajili katika muda uliopangwa ili kuepukana na kuchelewa, na kufungwa
kwa dirisha hilo.
Usajili wa dirisha dogo ni kwa
vilabu ambavyo havijajaza idadi ya wachezaji 30 katika usajili
uliofanyika wakati wa dirisha kubwa la usajili (Juni – Agosti 2015),
usajili huo wa wachezaji unafanyika katika tovuti ya TFF, www.tff.or.tz kisha kwenye link ya Club Registration.
KILIMANJARO STARS YAWASILI ETHIOPIA
Kikosi
cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ tayari
kimewasili Addis Ababa nchini Ethiopia leo alfajiri kikiwa na wachezaji
18 pamoja na vinogozi tayari kwa mashindano ya Kombe la Chalenji
yatakayoanza kutimua vumbi kesho Jumamosi nchini humo.
Kilimanjaro Stars inayonolewa na
kocha mkuu Abdallah Kibadeni, akisaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda,
imepangwa katika kundi A, ikiwa na wenyeji timu ya taifa ya Ethiopia,
Rwanda, pamoja na Somalia.
Wachezaji waliosafiri na timu
hiyo ni magolikipa Ally Mustafa na Aishi Manula, walinzi Shomari
Kapombe, Kessy Radmahani, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Ishaka,
Salim Mbonde na Kelvin Yondani.
Wengine ni viungo Himid Mao,
Salum Abubakar, Jonas Mkude, Salum Telela na Said Ndemla, huku safu ya
ushambuliaji ikiongozwa na Malimi Busungu, Elias Maguri, Saimon Msuva,
Deus Kaseke na nahodha John Bocco.
Stars itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Somalia siku ya Jumapili katika uwanja wa Addis Ababa.
NAIBU KAMISHNA MKUU WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) NA UJUMBE WAKE WATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Uongozi wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi ukiwa katika kikao na Ujumbe wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) uliotembelea Wizara hiyo. Wa
pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
John Mngodo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo akizungumza na ujumbe wa Shrika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) (haupo pichani)
uliotembelea Wizara hiyo ambapo masuala mbalimbali kuhusiana na
wakimbizi yalijadiliwa. Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazohifadhi
wakimbizi, hasa kutoka Ukanda wa Maziwa Makuu.
Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bi. Kelly Clements
akizungumza katika kikao na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
(haupo pichani) wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi. Katikati ni Mkurugenzi wa UNHCR, Kanda ya Afrika
na kushoto ni Mtendaji Msaidizi wa Naibu Kamishna Mkuu wa UNHCR, Bi.
Geraldine Salducci.
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi
katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke akizungumza
katika kikao cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na ujumbe wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wakati ujumbe huo
ulipotembelea Wizara. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
BASATA YAWAPIGA MSASA VIONGOZI WA VYAMA VYA WASANII
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Utamaduni anayeshughulikia Lugha kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bi. Shani Kitoga (Kulia) akizungumza na viongozi wa
vyama vya wasanii wa Mkoa wa Dar es Salaam (Hawako pichani)
waliohudhuria mafunzo ya kujengewa uwezo yaliyoandaliwa na Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kushoto ni Kurugenzi wa Idara
ya Ukuzaji Sanaa BASATA Bi. Vivian Nsao Shalua.
Katibu Mtendaji wa Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (Kulia) akisisitiza jambo
wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya wasanii
yaliyoandaliwa na Baraza hilo mapema wiki hii. Kulia kwake ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Utamaduni anayeshughulikia Lugha kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Shani Kitoga
………………………………………………………………………………………………
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
limewapa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo katika maeneo mbalimbali
viongozi wa vyama na taasisi zinazojihusisha na wasanii ili kujenga
ufanisi zaidi katika sekta ya Sanaa.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia Jumanne hadi Alhamisi ya wiki hii yalijikita katika kuwajengea uwezo Wasanii kwenye maeneo ya uandaaji bajeti, uandaaji wa mipango mikakati na sheria ya hakimiliki na hakishiriki na mikataba kwenye kazi za Sanaa.
Akizungumza kwenye hafla ya kuyafunga mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alisema kwamba ana matumaini makubwa kwamba mafunzo haya kwa viongozi wa wasanii yataamsha ari katika utawala na utendaji wa sekta ya Sanaa na kufanikisha kupiga hatua kwa sekta hii muhimu.
“Nina imani katika mafunzo haya tutawaona viongozi wa wasanii mnakuwa na mipango ya muda mrefu, wa kati na mfupi maana hakuna jinsi tunaweza kuwaongoza wasanii bila kuwa na mipango” alisisitiza Mngereza.
Kuhusu suala la hakimiliki, hakishiriki na mikataba kwenye kazi za Sanaa alisema kuwa ni tatizo linalowakumba wasanii wengi hivyo imani ya BASATA ni kuona viongozi hawa waliopatiwa mafunzo wanakuwa msaada kwa wasanii walio chini ya vyama vyao.
“Suala la hakimiliki linamgusa kila msanii, naamini kwenye suala hili mmejifunza vya kutosha. Aidha, mmejifunza suala la mikataba katika kazi za Sanaa, nawaomba muwe mabalozi katika kuwaelimisha wasanii umuhimu wa mikataba katika kazi wanazozifanya” Aliongeza Mngereza.
Awali akiongea kabla ya kukabidhi vyeti kwa washiriki, mgeni rasmi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Shani Kitoga aliwataka viongozi hao kuzingatia mafunzo waliyoyapata na kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa mabadiliko kwenye sekta ya Sanaa.
“Sanaa tunasema ni kazi hivyo lazima mafunzo haya mliyoyapata myatafsiri katika vitendo kwa kuonesha utendaji kazi ulio bora na unaozingatia mipango” alisema Bi. Kitoga.
Akiongea kwa niaba ya viongozi wa wasanii zaidi ya arobaini (40) waliohudhuria mafunzo hayo, Msanii mkongwe wa Sanaa za Maonesho Kassim Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala alilipongeza BASATA kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwaeleza wasanii kuwa sasa hakuna sababu ya kulalamika bali kuyafanyia kazi yale waliyojifunza.
Mafunzo haya ambayo ni sehemu ya kutekeleza mpango mkakati wa BASATA yaliwezeshwa na wakufunzi Rashid Masimbi ambaye ni mtaalam wa kuandaa mipango mikakati, Mrisho Mtumwa ambaye ni mtaalam wa kuandaa bajeti na John Kitime ambaye ni Msanii na mtaalam wa masuala ya hakimiliki na hakishiriki.

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA SHEREHE ZA KUMWAPISHA WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA
Rais John Magufuli akiwa katika
picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary
Majaliwa baada ya kumwapisha Waziri Mkuu kwenye ikulu ndogo ya
Chamwinomjini Dodoma Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa kassim
Majaliwa akipongezwa na Mbunge wa Isimani, William Lukuvi baada ya
kuapishwa kwenye ikulu ya Chamwino mjini Dodoma Novemba 20, 2015. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akipongezwa na Mbunge wa Buchosa, Dkt.Charles Tizeba baada ya
Waziri Mkuu, Majaliwa kassim Majaliwa kuapishwa kwenye ikulu ya
Chamwino Dodoma Novemba 20, 2015. (picha na Ofisi ya Maziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary
Majaliwa akipongezwa na Mbunge wa Buchosa, Dkt.Charles Tizeba baada ya
Waziri Mkuu, Majaliwa kassim Majaliwa kuapishwa kwenye ikulu ya
Chamwino Dodoma Novemba 20, 2015. (picha na Ofisi ya Maziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa kassim
Majaliwa akipongezwa na Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe baada
ya kuapishwa kwenye ikulu ya Chamwino mjini Dodoma Novemba 20, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa akipongezwa na Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za
kuapishwa kwake kwenye ikulu ndogo ya Cahamwino jijini Dar es salaam
Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majliwa akipongezwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Sheikh Mtopa
baada ya kuapishwa kwenye ikulu ndogo ya Chamwino jijini Dar es salaam
Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa akipongezwa na Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za
kuapishwa kwake kwenye ikulu ndogo ya Cahamwino jijini Dar es salaam
Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim
Majaliwa akipongezwa na Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za
kuapishwa kwake kwenye ikulu ndogo ya Cahamwino jijini Dar es salaam
Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment