Manispaa
ya wilaya ya Kinondoni kushirikiana na Wizara ya Ardhi nyumba na
maendeleo ya makazi wakiwa wameweka tangazo lao katika ukuta wa uzio
wakimaanisha eneo hilo lisitumike kwa maana ya maeneo ya wazi.
Nyumba nyingine eneo hilo nayo ikisubili kubomolewa na manispaa ya Kinondoni.
Ubomoaji ukiendelea.
Familia ya nyumba inayotakiwa kubomolewa na manispaa wakitoa dhamani za ndani ili kupisha ubomoaji.
Ubomoaji ukiendelea katika maeneo ya Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam.
Wazee wa kazi wakiwa katia geti la nyumba inayotakiwa kubomolewa maeneo ya mtaa wa Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam leo.
Ubomoaji wa uzio wa nyumba maeneo ya Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kubisha hodi na kutokufunguliwa.
Uzio umebomolewa na watu wakiwa ndani kwaajili ya ubomoaji wa nyumba hiyo ambayo imejengwa maeneo ambayo ni ya wazi.
Magari yakiwa ndani ya nyumba inatotakiwa kubomolewa.
Magari ya kitolewa nje ili kupisha ubomoaji wa nyumba maeneo ya Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam leo.
Wenyeji wa nyumba ambayo imeanza kubomolewa uzio wakitoa vitu ndani ili kupisha ubomoaji wa nyumba hiyo.

Wakazi wa nyumba nyeupe inayobomolewa wakitoka nje ya nyumba baada ya kuanza kubomolewa na manispaa ya Kinondoni.
Wananchi wakihamisha vitu kupisha bomoabomoa.

Nyumba nyingine eneo hilo nayo ikisubili kubomolewa na manispaa ya Kinondoni.

Ubomoaji ukiendelea.

Wazee wa kazi wakiwa katika geti la nyumba inayotakiwa kubomolewa maeneo ya mtaa wa Libermann Mbezi Beach jijini Dar es Salaam leo.

Wakazi
wa nyumba nyeupe inayobomolewa wakitoka nje ya nyumba baada ya kuanza
kubomolewa na manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Wananchi waangalia jinsi manispaa inavyobomoa nyumba Mbezi bichi jijini Dar es Salaam leo
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
watoto Zahra na Zarina wanaitaji msaada kwa yoyote atakae guswa
Hawa
watoto Zahra na Zarina wamezaliwa pacha walioungana tarehe 16/11/15
mama yao Bi Tausi Hageze akiwa njiani kwenye boda boda akitokea kijiji
cha Nyarurema Tarafa ya Rulenge Wilaya ya Ngara akielekea hopitali ya
misheni Rulenge. Alipopata uchungu wa kuzidi alimuomba bodaboda asimame
akaweza kujifungua kwa shida mbele ya mumewe anaeitwa Hamdani hapo
njiani.
Baada ya
hapo wakapelekwa hospitali ya misheni Rulenge. Mama na watoto wako
salama, kama unavyo ona katika picha wameungana kiunoni.
Msamaria
amekutana na changamoto hii hapo hospitali na kuamua kuwasaidia
kuchangisha iliwapelekwe Mwanza Bugando Hospital walipo hivi sasa.
Inaelezwa na ma daktari hapo wameshauri watoto wapelekwe India kwa upasuji na matibabu zaidi.
Msamaria anaewasaidia Bi Sabra Said Salum wa namba ya simu 0767220099
anaomba yoyote atakae guswa na kadhia hii afikishe mchaango kwake ili
aweze kuwafanyia safari hii muhimu kuokoa maisha ya mapacha hawa.
Baba Hamdani
Sibhoro na mama Tausi Hageze wote ni wakulima wa jembe la mkono hawana
uwezo hata wa kufika Dar. Bi Sabra kachangisha na kuweza kuwafikisha
Bugando, kuwalipia mahitaji ya hapo.
Mungu awabariki
NEC yatoa Taarifa kuhusu upigaji kura kesho
Na Beatrice Lyimo- Maelezo Dar es Salaam
……………………………………………………
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imetoa taarifa kuhusu upigaji kura katika uchaguzi utakaofanyika kesho
tarehe 22 Novemba, 2015 katika majimbo mawili na kata sita ambapo
uchaguzi wake ulihairishwa.
Akitoa taarifa hiyo leo jijini
Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya uchaguzi
Bwa. Emmanuel Kawishe amesema kuwa Tume ilitoa taarifa kwa kuhairishwa
kwa Uchaguzi katika Jimbo ya Lushoto mkoani Tanga, Jimbo la Ulanga
Mashariki mkoani Morogoro, kata ya Muleba, Uyole, Bukene, Msingi,
Bomang’ombe pamoja na kata ya kasulo kutokana na vifo vya wagombea.
“Kesho ni siku ya kupiga kura ya
kuchagua Mbunge katika majimbo mawili na kuchagua Diwani katika kata
sita, natoa rai kwa wale wote mliojiandikisha kama wapiga kura katika
majimbo na kata hizo kujitokeza kwenye vituo mlikojiandikisha ili kuweza
kupiga kura na kuwachagua viongozi mnaowataka bila hofu, woga wasiwasi
au ushawishi” aliongeza Kaimu Mkurugenzi huyo.
Hata hivyo Bwa. Kawishe alisema
kuwa vituo vitafunguliwa kuanzia saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi
jioni na kuwakumbusha wapiga kura kubeba kadi yake ya mpiga kura.
“Kipaumbele kitatolewa kwa
wagonjwa, watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali, wanawake wajawazito au
wenye watoto wachanga na wazee ambao hawatatakiwa kujipanga kwenye
foleni”
“Wakati wote wa kupiga kura na
kuhesabu kura, mawakala wa vyama vya siasa wawepo kwenye vituo na wajibu
wao ni kulinda maslahi ya vyama vyao na wagombea hivyo hawatakiwi
kuingilia masuala ya utendaji ambayo yamekabidhiwa kwa msimamizi wa
kituo” alifafanua Bwa. Kawishe.
Mbali na hayo Tume ya Taifa ya
Uchaguzi amewapongeza wananchi kutoka majimbo na kata zinazofanya
uchaguzi kesho kwa uvumilivu waliouonyesha katika kipindi chote cha
kusubiri siku ya kupiga kura kumchagua Mbunge au Diwani wao.
KONGAMANO LA MABADILIKO YA TABIANCHI LAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO,JIJINI DAR
Mc katika kongaman0 la Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu
Eva
Mageni ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa
mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, akifungua kongamano
la Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alizungumzia kwa kifupi kuhusu mkutano wa COP21 ambao utafanyika Paris Ufaransa hivi karibuni.
Edward
Tunyone kutoka Forum CC akieleza maana zaidi ya Mabadiliko ya Tabianchi
ambapo alielekeza mazungumzo yake katika majanga asilia, mito kupotea
kutokana na shughuli za wanadamu kama kulima jirani na maeneo hayo,
mwisho alisisitiza swala la mabadiliko ya Tabianchi ni jukumu la kila
mtu na taasisi zinazohusika na mamswala hayo tu.
Bi
Mwindiwe makame aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa
Chakula kutoka Zanzibar, akiendelea kueleza maana ya Mabadiliko ya
Tabianchi alisisitiza kutunza mazingira.
Denis Allan kutoka Norwegian Church Aid Actalliance akielezea umuhimu wa kutunza miti.
Kikundi cha Ngonjela wakiendelea Kuburudisha
Kushoto ni Mtaalam wa Mitandao ya kijamii toka Forum CC akitoa maelekezo ya shindano la Instagram
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza
Aliyewahi kuwa Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2012 St.Matha akielezea jambo kuhusiana na mabadiliko ya Tabianchi
Bw. Gambaedya P.M kutoka Tume ya Ardhi akitoa somo juu ya kilimo hifadhi
Bi.Tatu Kayumbu kutoka Wizara ya Kilimo akieleza ushirikiano wa kilimo na utunzaji wa Mazingira
Kundi la Youth can wakiendelea kutumbuiza
Meneja wa Kampeni Haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akitoa mwongozo wa kikao
Mkutano wa Forum CC ukiendelea
Baadhi ya washiriki wakijadili Michoro ambayo walipewa kazi ya kuipitia na kuijadili.
Kushoto
ni Mkurugenzi mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akijumuika na
wananchi wengine katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi
Baadhi ya waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kwa nyakati tofauti wakionesha bidhaa zao

Kushoto
ni mmoja wa washiriki waliohudhulia kongamano la mabadiliko ya
Tabianchi akipokea zawadi ya tsh 100,000 aliyoshinda Steven Albert.
Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi
*******
ASASI za Kiraia nchini zikiwemo Oxfam Tanzania, Forum CC na Norwegian Church Aid Actalliance zafanya kongamano la Kukabiliana na
mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Chakula
nchini.
mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Chakula
nchini.
Akizungumza Afisa Miradi Msaidizi wa
Shirika la Forum CC,Jonathan Sawaya alisema asasi hizo zimeona ni vema
kuwakilisha sauti za wakulima kwa serikali katika kuhakikisha hatua
stahiki zinachukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Shirika la Forum CC,Jonathan Sawaya alisema asasi hizo zimeona ni vema
kuwakilisha sauti za wakulima kwa serikali katika kuhakikisha hatua
stahiki zinachukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Alisema asilimia kubwa ya wakulima wengi hasa wanawake
ambao karibia asilimia 70 wamekuwa wakiathirika na Mabadiliko hayo
wakati wanapolima.
ambao karibia asilimia 70 wamekuwa wakiathirika na Mabadiliko hayo
wakati wanapolima.
Sawaya alisema wananchi wanapaswa kuhifadhi mazingira na
kutunza vyanzo mbalimbali vya maji ili kupunguza athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabia nchi.
kutunza vyanzo mbalimbali vya maji ili kupunguza athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabia nchi.
“Kwa kushirikiana na shirika la Oxfam pamoja na Norwegian
Church Aid tumeamua kufanya kongamano hili ili kupaza sauti za wakulima
na wafugaji katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi na serikali kutilia mkazo katika kusimamia suala hili kwa kuongeza
bajeti,”alisema Sawaya
Church Aid tumeamua kufanya kongamano hili ili kupaza sauti za wakulima
na wafugaji katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi na serikali kutilia mkazo katika kusimamia suala hili kwa kuongeza
bajeti,”alisema Sawaya
Aidha alisema asilimia kubwa ya wanawake wameonyesha juhudi
mbalimbali za kukabiliana na athari hizo kutokana na wao kujihusisha
katika uzalishaji wa chakula.
mbalimbali za kukabiliana na athari hizo kutokana na wao kujihusisha
katika uzalishaji wa chakula.
“Tuwaunge mkono wazalishaji wa chakula wadogo,wafugaji
pamoja na wavuvi katika suala hili kwa kuwaunganisha na masoko na
kuwapa mikopo,”alisema
pamoja na wavuvi katika suala hili kwa kuwaunganisha na masoko na
kuwapa mikopo,”alisema
Aidha Kongamano hili limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo
watendaji wa serikalini,wakulima pamoja na wafugaji katika kuhakikisha
mabadiliko ya tabia nchi yanatokomezwa.
watendaji wa serikalini,wakulima pamoja na wafugaji katika kuhakikisha
mabadiliko ya tabia nchi yanatokomezwa.
“Kongamano hili ni sehemu ya maandalizi ya Mkuu wa 21 wa
Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajia
kufanyika Novemba 30 nchini Ufaransa,”alisema Sewaya
Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajia
kufanyika Novemba 30 nchini Ufaransa,”alisema Sewaya





















No comments:
Post a Comment