Mr. Radhey Mohan (Vice president –
International Marketing, Apollo Health City, Hyderabad), Dr. Mahesh
Verma (Ministry of Tourism & Civil Aviation), Hon. Sh. Pranab
Mukherjee (Hon. president of India), Ms. Sangita Reddy (Joint Managing
Director, Apollo Hospitals Group) and Mr. Vinod Zutshi (Secretary –
Ministry of Tourism, Govt. of India).
Hon. President of India presenting an Award
for Best Medical Tourism facility to Apollo Health City, Hyderabad. This
is the third consecutive year that Apollo Health City, Hyderabad is
receiving this prestigious award.
Wanawake
wa mkoa wa Mara wameaswa kushirikiana kwa pamoja katika shughuli za
maendeleo bila kuangalia tofauti ya itikadi zao za vyama kwa kufanya
hivyo watajiletea maendeleo yao kama wanawake.
Rai
hiyo imetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea
na wanawake wa mkoa huo katika ukumbi wa mikutano wa Musoma Community
Center (MCC) uliopo mjini Musoma.
Mama
Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM
kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema masuala yanayowahusu wanawake
hayana itikadi za vyama kwani maendeleo ni ya wote, katika mambo ya
msingi waungane na kuwa kitu kimoja wasitenganishwe na watu.
Alisema
ili wanawake waweze kujiletea maendeleo ni lazima washikamane, wafanye
kazi kwa umoja na kutumia fursa zilizopo kwani Serikali inasehemu
yake ya kuwaleta maendeleo lakini maendeleo mengine yanahitaji jitihada
zao binafsi.
“Sisi
kama wanawake tunafanana kwa kila kitu tofauti iliyopo ni wajibu wa
kila mmoja wetu katika jamii yake, shirikini kuchangia shughuli za
maendeleo kama ujenzi wa barabara na shule kwa ajili ya watoto wetu na
kuchangia huduma ya afya ili tuweze kupata huduma bora”.
Msiache
kuzitumia fursa zilizopo wasimamieni watoto wa kike wasome kwani
wakiwa na elimu wataweza kujiajiri au kuajiriwa, wengine watakuwa
viongozi wazuri miaka michache ijayo watawasaidia siku za baadaye”,
alisisitiza Mama Kikwete.
Aidha
Mama Kikwete alitumia nafasi hiyo kuwaaga wanawake hao na kuwashukuru
kwa jinsi walivyokuwa wanamtia moyo katika kipindi chote cha miaka 10 ya
utawala wa mme wake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jambo ambalo
lilimpa ujasiri katika kufanya kazi zake za kuwasaidia wanawake na
watoto wa Tanzania.
Mama
Kikwete alisema, “Kazi yangu ninayoifanya kama mke wa Rais
nimeitekeleza nilisema nitawasomesha watoto wa kike wanaoishi katika
mazingira magumu nimewasomesha, nimejenga shule ya watoto wa kike,
nimewainua wanawake kiuchumi na nimesaidia kuimarisha afya ya mama na
mtoto”, alisema Mama Kikwete.
Katika
mkutano huo wanawake walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali na
kuzitaja kero na changamoto zinazowakabili katika maisha yao kama vile
upatikanaji wa maji, uongozi, uchumi na elimu.
Kwa
upande wake Theresia Chacha ambaye ni mkazi wa Nyamagugu wilaya ya
Rorya alimshukuru Mama Kikwete kwa kumsomesha mtoto wake wa kike aitwaye
Paschazia ambaye yupo kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya
WAMA-Nakayama iliyopo Rufiji Mkoani Pwani.
“Mama
Kikwete anasomesha watoto 15 kutoka mkoa wa Mara katika shule
yake, mwanangu ni mmoja wa watoto hao, anamgharamia kila kitu hata
nauli mama huyu analipa mimi silipo chochote”.
Miaka
yote hiyo sijawahi kumuona ndiyo namuona leo nakushukuru sana Mama,
Mwenyezi Mungu akubariki naomba kiongozi ajaye aige mfano wako wa
kuwasidia wanawake na watoto wa Tanzania”, Mama Chacha alishukuru.
Naye
Anastazia Sangarya mkazi wa kata ya Mwisege ambae ni mjasiriamali
alizitaja changamoto wanazokutana nazo kuwa ni pamoja na kupanda kwa ada
ya ushiriki wa Maonyesho ya kimataifa ya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere maarufu kama sabasaba yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es
Salaam kutoka shilingi 50,000 hadi 100,000.
Mama
Anastazia alisema, “Sisi wanawake wajasiriamali tunaumizwa na ada kubwa
ya ushiriki wa maonyesho ya sabasaba kwani tukishiriki licha ya kulipa
kiingilio bado kuna gharama ya nauli na malazi”.
Kwa
upande wa mikopo tunayokopa benki riba yake ni kubwa na kama ikatokea
umechelewa kurejesha kutokana na matatizo ya kifamilia benki haikuelewi
tunakuomba mama yetu utusaidie kutatua changamoto hizi ambazo
zinarudisha nyuma maendeleo ya wanawake wajasiriamali wa mkoa huu,”.
Mama
Kikwete aliahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazowakabili wanawake hao
na kuwataka viongozi wao kuitisha mikutano ya mara kwa mara
itakayosaidia kutatua kero zinazowakabili.
MGOMBEA
UBUNGE JIMBO LA CHUMBUNI USSI SALUM PONDEZA AMJADI, AWAHUTUBIA WANANCHI
WA JIMBO HILO KATIKA MKUTANO WAKE WA KAMPENI VIWANJA VYA MABANDA YA
NGOMBE CHUMBUNI UNGUJA.
Msoma Utenzi akisoma Utenzi maalum
wakati wa Uzinduzi wa Mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja
uliofanyika katika Viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni Zanzibar.
Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi akiwa
katika viwanja vya mkutano akishangilia na Picha ya Mgombea wake wa
Ubunge kupitia CCM Ndg. Ussi Salum Pondeza AMJADI wakati wa mkutano huo
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakiwa
katika viwanja vya mkutano wa Kampeni ya Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo
hilo uliofanyika viwanja vya Mabanda ya Ngombe Chumbuni Unguja.
Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani
wakiwapungia mikono Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kampeni wakati
msoma utenzi akitaja majina ya Wagombea.
Wanachama wa CCM wa Tawi la Masumbani
Jimbo la Chumbuni wakifuatilia mkutano huo wa kampeni uliofanyika
viwanja vya mabanda ya ngombe chumbuni Unguja
Mgombea Ubunge Jimbo la Mfenesini Kanali
Mstaaf Masoud akimtunza msoma Utenzi wakati wa mkutano wa Uzinduzi wa
Jimbo la Chumbuni Unguja.
Katibu wa CCM Jimbo la Chumbuni akisoma utaratibu wa mkutano huo wa kampeni wa jimbo hilo.
Aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la
Chumbuni Unguja Mhe Machano Othman, akiwasalimia Wananchi wa Jimbo hilo
na kuwaombea Kura Wagombea wote wa CCM wanaogombea katika Jimbo la
Chumbuni kuazi Mbunge Mwakilishi na Madiwani kuwa kura ya Ndio kuendelea
maendeleo katika jimbo hilo walioyawacha wao.kwa sasa anagombea Jimbo
la Mfenesini nafasi ya Uwakilishi
Mgombea Ubunge Jimbo la Mfenesini Kanal
Mstaaf Masaud, akiwasalimia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa
Mkutano wa Kampeni ya Uzinduzi ya Jimbo zilizofanyika katika viwanja vya
mpira mabanda ya ngombe chumbuni Unguja.
Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Kusini
Unguja Mhe Haji Ameir akizungua mkutano wa Kampeni wa Jimbo la Chumbuni
Unguja uliofanyika katika viwanja vya mpira mabanda ya ngombe chumbuni
na Kuwatambulisha Wagombea wa CCM wa Jimbo hilo.na kuwaombea Kura siku
ya Uchaguzi Mkuu kwa kura ya Ndio, pamoja na Rais wa Zanzibar Dk Shein,
na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya Kampeni wakishangilia na Vipeperushi vya wagombea wa Jimbo la Chumbuni Unguja.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Kusini Unguja Mhe Haji Ameir akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Chumbuni Ussi Salum Pondeza AMJADI, wakati wa mkutano wa Kampeni wa
Jimbo la Chumbuni uliofanyika katika viwanja vya Mabanda ya Ngombe
Chumbuni.
Mgombea Ubunge Jimbo la Chumbuni Ussi
Salum Pondeza AMJADI akiwataka Wananchi wa Jimbo la Chumbuni kujiandaa
na Maendeleo katika Jimbo hilo katika kipindi chake cha miaka mitano
kuweza kulibandilisha Jimbo hilo katika maendeleo kwa Vijana na Wazee
katika sekta mbalimbali zikiwemo za Elimu, Maji, Kujiajiri Wenyewe na
Afya. amewataka kumpigia Kura ya Ndio kuweza kuwaletea maendeleo hayo.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni
akimwaga Serazake kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakati wa mkutano
wake wa kampeni katika viwanja vya mpira mabanda ya ngombe chumbuni
Unguja.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja
Wanachama wa CCM
wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Jimbo la Chumbuni Unguja
wakati akihutubia Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Ussi Salum Pondeza
AMJADI, uliofanyika viwanja vya mabanda ya ngombe chumbuni Unguja.
Wananchi wa Jimbo la Chumbuni wakifuatilia Mkutano wa Kampeni wa Jimbo hilo uliofanyika viwanja vya mabanda ya ngombe chumbuni.
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Chumbuni
Miraj Kwaza akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Chumbuni Unguja wakati wa
mkutano wa kampeni wa Jimbo hilo na kusoma baadhi ya vipengele vya Ilani
ya Uchaguzi ya CCM jinsi itakavyotekelezwa katika kipindi cha miaka
mitano ijayo ya Dk Shein.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Jimbo la Chumbuni Unguja
Msanii wa Bendi ya Yamoto, akitowa burudani kwa Wanachama wa CCM wa Jimbo la Chumbuni wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Jimbo hilo.
Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano huo wa Kampeni ya Jimbo la Chumbuni Unguja
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Kusini Unguja Mhe Haji Ameir, akimtambulisha Mgombea Udiwani wa Wadi ya
Chumbuni, Ndg. Mussa Haji Idrisa kwa Wananchi wa Jimbo hilo
Mgombea Udiwani Wadi ya Chumbuni Ndg Mussa Haji Idrisa. akiwasalimia Wananchi wakati akitambulishwa na kuomba Kura.
Mgombea Udiwani Wadi ya MuembemakundiNdg Haji Juma, akiwasalimia Wananchi wakati akitambulishwa na kuomba Kura.Mgombea Udiwani Wadi ya MuembemakundiNdg.Haji Juma. akiwasalimia Wananchi wakati akitambulishwa na kuomba Kura


No comments:
Post a Comment