Pages

Monday, September 21, 2015

SERIKALI YAKIRI CHANGAMOTO LICHA YA MAFANIKIO AJIRA KWA VIJANA

IMG_9847
Meza kuu katika warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF. Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Kazi na Ajira kitengo cha Ajira, Joseph Nganga, Mkurugenzi wa Kazi katika Wizara ya Kazi na Ajira, Ally M. Ahmed, Mkuu wa utafiti na machapisho Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Na Mwandishi wetu
PAMOJA na kuwepo na maendeleo ya kuridhisha katika suala la ajira kwa vijana, serikali imekiri kwamba ukosefu wa ajira bado ni tatizo kubwa duniani na kwa taifa kwa ujumla.
Kutokana na hali hiyo suala la ajira kwa vijana limebaki kuwa ajenda kuu nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kazi katika Wizara ya kazi Ally M. Ahmed wakati akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton.
Alifanya ufunguzi huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eric Shitindi.
Alisema Tanzania inaendelea kukabiliana na tatizo la ajira kutokana na wigo mdogo wa fursa za ajira, tatizo la utaalamu na ukosefu wa uzoefu .
Alisema hata hivyo vijana wanaoamua kujiajiri wenyewe wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la mtaji, maeneo ya kufanyia kazi na utaalamu katika ujasiriamali utakaowawezesha kuendesha miradi wanayoibuni.
Alisema kutokana na uwapo wa sera, mipango na miradi ya maendeleo kuhusu ajira kwa vijana inayoendeshwa kitaifa na kimataifa kumekuwepo na dalili njema za kupungua kwa ukosefu wa ajira.
Alisema utafiti wa mwaka 2014 (ILFS) umeonesha kwamba ukosefu wa ajira umepungua kutoka asilimia 11.7 kwa mwaka 2006 hadi kufikia asilimia 10.3 ka mwaka 2014 huku kwa vijana (wenye umri wa miaka 15 hadi 35) ukipungua kutoka asilimia 13.2 kwa mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 kwa mwaka 2014.
IMG_9768
Mkuu wa Utafiti na mchapishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa hotuba ya utangulizi katika warsha ya vijana na ajira iliyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton. Katika hotuba yake ya ufunguzi alitoa wito wa washiriki kuangalia kwa undani tatizo la ajira kwa vijana na kutoa mwelekeo utakaosaidia watunga sera kuwa na sera madhubuti kuhusu ajira kwa vijana.
Alisema mafanikio yaliyopatikana hayaondoi ukweli kuwa kuna tatizo kubwa la ajira miongoni mwa vijana na kutokana na mazingira ya sasa ni vyema wadau wa ajira kuangalia kwa undani tatizo la ajira la sasa ili kutoa ushauri wa kukabiliana nalo kwa kipindi kifupi na kirefu.
Shitindi alisema kwamba serikali inafurahishwa na juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali kutafuta majibu ya tatizo la ajira, majibu ambayo alisema yakifanywa vyema yatasaidia sana wataalamu wa serikali kutengeneza sera na kanuni zitakazo kidhi haja.
Alisema ipo haja kwa wachambuzi (watafiti) kuelekeza nguvu zao katika kutafiti soko la ajira ili kusaidia watengeneza sera kuona mahitaji ya soko katika miaka kadhaa ijayo.
Alisema wakati uchumi wa Tanzania unakua kwa asilimia 7 kwa mwaka kwa miaka kumi iliyopita ajira zimekuwa haziendi sambamba na ukuaji wa uchumi na hivyo kuleta maswali mengi ya sintofahamu.
Alisema serikali kwa sasa inataka kuhakikisha kwamba inaboresha upatikanaji wa ajira lakini hilo linawezekana kama taasisi zake zinazotengeneza sera na kuweka mipango zinatambua tatizo na kuona namna ya kuliangalia.
Alisema watafiti wana wajibu mkubwa wa kusaidia serikali kuwezesha vijana kuwa na kazi zenye staha kama sera ya ajira ya taifa inavyotaka.
IMG_9895
Mkurugenzi wa kazi wizara ya kazi na ajira, Ally Msaki Ahmed, akisoma hotuba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Eric Shitindi katika warsha ya kitaifa ya ajira kwa vijana iliyofanyika hoteli ya Duble Tree by Hilton. Katika hotuba yake aliwataka washiriki kujadili kwa makini matatizo ya vijana na kutoa suluhu itakayosaidia watendaji kutunga sera na kutoa mwelekeo mpya wa kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema kwa kuangalia ukuaji wa kisekta, sekta ambayo sasa hivi inahitaji watu ndio ambayo haina wataalamu wa kutosha na hivyo ukuaji wa sekta hizo kama za mawasiliano hauendi sanjari na utaalamu uliopo katika soko.
Katibu Mkuu huyo alitoa wito kwa watu binafsi na serikali kuhakikisha kwamba wanakabiliana na vikwazo vya ajira kwa kutoa elimu na taaluma ili fursa zionekane na kutumika ipasavyo.
Alisema tija inaweza kuonekana katika ukubwa wa utaalamu, ubunifu na namna mafunzo yanavyowawezesha wanafunzi kuwa na uhakika na kazi wanazotaka.
Alisema ipo haja kwa wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kwamba vijana wanaingizwa katika soko la ajira na tatizo la ajira linapunguzwa.
  IMG_9829
Kiongozi Mpango wa ukuaji na ajira wa taasisi hiyo, Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC), Dk. Arjan de Haan akielezea sababu za taasisi hiyo kuunga mkono tafiti kwa ajili ya kusaidia kupatikana ufumbuzi wa tatizo la ajira katika warsha ya ajira na vijana iliyofanyika Double Tree by Hilton hotel.
Katika moja ya maazimio yaliyotolewa na washiriki vijana, walitaka kuwepo na mabadiliko makubwa katika utoaji elimu, ambapo walisema elimu itolewe kwa Kiswahili lakini pia wanafunzi waandaliwe kuwa wabunifu na kujiajiri.
Aidha wametaka kurejeshwa kwa shule za ufundi na shule maalumu kama ilivyokuwa zamani.
Walisema vijana Wanatakiwa kushiriki katika utengenezaji wa sera na kanuni na si kushirikishwa na kutaka matakwa yao yanastahili kuangaliwa na kuzingatiwa ili mtu ajifunze kila anachoona anaweza kukifanya vyema.
Warsha hiyo ya ajira kwa vijana imewezeshwa na IDRC na kuratibiwa na ESRF na mada mbalimbali ziliwasilishwa ambazo zilichambua masuala ya elimu, elimu ya ufundi, changamoto na fursa za vijana katika ajira.
Aidha kulikuwa na mada za majukumu ya serikali na sera katika kuboresha mchakato wa ajira kwa vijana.
IMG_0011
Mchumi na Mshauri huru Bi. Mahjabeen Haji akiwasilisha mada kuhusu hali ya ajira kwa vijana nchini katika warsha ya vijana na ajira ilyofanyika hoteli ya Double Tree by Hilton, katika mada yake alielezea mazingira ya ajira ambapo elimu katika sekta zinazokua kwa kasi kama Tehama ni kikwazo kikubwa katika kuwezesha ajira kwa vijana.
  IMG_9932
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Utafiti na mchapishi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene wakati warsha hiyo ikiendelea.
IMG_0154
Mkurugenzi wa Salama Foundation, Shadrack John Msuya akiwasilisha mapendekezo ya vijana juu ya namna ambavyo vipaji, elimu na ubunifu vinavyoweza kutengeneza ajira kwenye maeneo ya Sayansi, Teknolojia, Kilimo na Ufugaji.Moja ya azimio ni kuwa na sera mpya ya vijana yenye mpango mkakati na tafiti zinazotekelezeka katika warsha ya vijana na ajira.
IMG_0180
Mshauri mwelekezi katika uanzishwaji na uendelevu wa biashara na maendeleo ya jamii, Gidufana Gafufen akiwasilisha mapendekezo yaliyowasilishwa katika vikundi nini kifanyike ili vijana wapende kilimo katika warsha ya vijana na ajira iliyofanyika katika hoteli ya Double Tree by Hilton.
IMG_9875
Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau pamoja na makundi ya vijana waliohudhuria warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
IMG_9704
IMG_9952
IMG_9944
IMG_0110
Mmoja wa washiriki akitoa maoni kwenye warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
   
 
IMG_0354Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya wadau wa ajira kwa vijana iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa na ESRF.
IMG_0150
Pichani juu na chini ni wadau kutoka Taasisi mbalimbali walioshiriki warsha hiyo wakibadilishana mawazo.
IMG_0130
Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga (kulia) akiteta jambo na baadhi ya washiriki.
IMG_0134
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akifurahi jambo na Mtafiti Mwandamizi ESRF, Dk. Georgina Ole Saibul mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo.

Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga akizungumza wakati akifungua kongamano hilo lililo washirikisha wadau mbalimbali kwa kutoa muhutasari wa Madhara ya Tumbaku. (Picha na Geofrey Adroph). Na Andrew Chale, modewjiblog [Dar es Salaam] Chama cha Afya ya Jamii nchini (TPHA), kimeendesha kongamano maalum kwa wanafunzi wa shule msingi zaidi ya Saba ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kutoa elimu ya madhara yatokanayo na utumiaji wa bidhaa za Tumbaku pamoja na kujikinga na athari zake mbaya baadae. Akielezea katika kongamano hilo, Afisa wa TPHA ambaye pia ni msimamizi na mtaafiti wa masuala ya kupambana na madhara ya Tumbaku, Dk. Bertha Maegga amebainisha kuwa, kwa sasa Chama hicho kinaendesha mradi uliopewa jina la “80 CHILDREN STRONG” ukitoa elimu kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 10-14, hasa wa shule za msingi. Dk. Maegga akihutubia umati wa wanafunzi wa shule hizo saba katika kongamano hilo lililofanyika shule ya Msingi Kijitonyama Visiwani, aliwataka wazazi, walimu, walezi na jamii kuwalinda na kukemea watoto wao kuachana na vitendo vya matumizi ya bidhaa za Tumbaku ikiwemo sigara, ugoro, shisha na Tumbaku yenyewe. Aidha, amebainisha kuwa, wameweza kulenga kundi hilo kutokana na kuwa na changamoto za kiukuaji wa kiakili na kisaikolojia. “Umri huu kuna utundu na utukutu mwingi na akili nazo bado hazijakomaa kuepuka ushawishi wa namna mbalimbali ukiwemo na wa matendo yasiyofaa katika maisha yao ya baadaye. Tukiweza kuwalinda katika umri huo. watabaki salama hadi watakapojitambjua nafsi zao na kuamua mambo ya busara na salama katika maisha yao ya baadae” alibainisha Dk. Maegga.
Mshauri wa masuala ya Afya na Familia, mgeni rasmi Dk. Ali Mzige akizungumza kwa kutoa elimu kwa miongoni mwa watu walio weza kuhudhuria kongamano hilo la uelimishaji kuhusu Tumbaku na matumizi ya yanayotokana na bidhaa za Tumbaku.Kwa upande wake, Dk. Ali Mzige mganga wa hospitali ya kimataifa ya Afya ya uzazi ametoa elimu kwa vijana hao na kubainisha kuwa sigara, tumbaku, shisha, ugoro na kuberi ni hatari kwa afya za mwili huku ikisababisha magonjwa mbalimbali.Miongoni mwa magonjwa hayo yatokanayo na matumizi ya sigara ambapo wanaoathirika zaidi ni vijana kwa sababu ya kufuata mkumbo pamoja na kuhisi kwamba uvutaji wa sigara unaongeza sifa ya kuwa mwanaume kamili kitu ambacho si kweli.Changamoto kubwa ni kwamba serikali imeshindwa kudhibiti watengenezaji wa Sigara kwa sababu wanapata kodi kutoka katika viwanda vya sigara japokuwa mapato ni madogo kuliko madhara. “Sigara ina kemikali 4000 ambazo zina uwezo wa kusababisha magonjwa zaidi ya 40, ambayo ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kisukari, na saratani ya mapafu, saratani ya kinywa na mengine mengi. Tumbaku na Sigara zote zimekuwa na madhara yanayofanana. Tumbaku imekuwa ikitumika hasa maeneo ya vijijini na sigara watumiaji wengi wanatoka mjini” alieleza Dk. Ali Mzige. Kwa upande wao wanaharakati wa kupambana na matumizi ya sigara kutoka chuo cha Tiba Muhimbili, kupitia taasisi yao ya African Fight Cancer, Bernard Temba amewaelezea wannafunzi hao kuwa, ni wakati wa kuepuka vishawishi dhidi ya watu wanaotumia sigara kwani wasipofanya hivyo wataweza kupata madhara makubwa ya kiafya.
Mwalimu Margareth William mshereheshaji katika siku hiyo ya kongamano la uelimishaji vijana kuhusu Tumbaku na madhara yatokanayo na bidhaa zake. Naye Mratibu wa Elimu Kata ya Makumbusho ambaye pia alikuwa mgeni katika kongamano hilo, alitoa wito kwa walimu na wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao ikiwemo kufuatilia nyendo zao mara kwa mara ili kuwakinga na vishawishi hivyo vya matumizi ya bidhaa zitokanazo na tumbaku kwani zina madhara makubwa hasa kwa afya za watoto wadogo. Mradi huo wa ’80 Children Strong’, unaosimamiwa na Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) unafadhiliwa na Shirika dogo la Conquer Cancer Foundation ambalo linahusiana na American Society for Clinical Oncology (ASCO) ya nchini Marekani (Chama cha kitabibu cha masuala ya uchunguzi wa tiba ya saratani. Hata hivyo, TPHA imedhamiria kuwa kila mtoto anapata haki ya kuelimishwa kujikinga na matumizi hayo mabaya ya tumbaku, ambapo kwa darasa la watoto 80, asiwepo hata mmoja atakayeingia kwenye viashiria vibaya vya matumizi ya tumbaku hivyo wataendelea kutoa elimu hiyo sehemu mbalimbali nchini. Kwa upande wa shule hizo zilizohudhuria kongamano hilo ni pamoja Shule ya Msingi Mapambano, Kijitonyama Visiwani, Victoria, Mwananyamala B, Mwananyamala Kisiwani, Mashujaa, Shekilango na Mapambano. Kwa upande wa watoto hao walipata pia wasaha wa kuuliza maswali na kupatiwa majibu huku pia kukifanyika na masuala ya maigizo, ngoma, shahiri na ngonjera zilizokuwa na jumbe mbalimbali za kupambana na matumizi ya tumbaku.
Wanafunzi wakisoma na kuelekezana jarida lililochapishwa mahususi kwa ajili ya kuelimisha matumizi mabaya ya Tumbaku. DSC_0019
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mashirika na vyuo mbalimbali.
Kikundi cha majigambo ya jukwaani (ngonjera) kikitoa ujumbe kwa wageni waalikwa pamoja na wanafunzi wenzao kuhusiana na kupambana na kudhibiti matumizi hatari ya Tumbaku.
Wanafunzi wakionesha vipaji vyao vya kuigiza kwa kuelimisha kuhusiana na na madhara ya Tumbaku na ni namna gani ya kuweza kujikinga.
Bernard Temba kutoka Chuo cha Afya cha Muhimbili akitoa somo kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizohudhuria kongamano hilo lililofanyiaka katika shule ya Msingi ya Kijitonyama Kisiwani
Shairi mahususi likiimbwa na wanafunzi hao likiwa limebeba ujumbe wa kijana jiepushe na matumizi ya Tumbaku na bidhaa zitokanazo na Tumbaku.
Mwanafunzi wa darasa la tano, Tadei Ladislausi kutoka shule ya msingi Shekilango (kulia)akisoma madhara yanayo wakumba watumiaji wa Tumbaku.
Wawili kulia ni wanafunzi kutoka Chuo cha Afya Muhimbili, kushoto ni wanafunzi wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani wakiwa wanasikiliza kwa makini maada zilizo kuwa zikiendelea katika kongamano hilo.
Wanafunzi wakiuliza maswali kwa watoa mada inayo husiana na afya kwa kijana na kuepuka matumizi mabaya ya Tumbaku
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani, Bw. Charles Nombo akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali walioweza kuhudhuria katika kongamano hilo.
Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii Bi. Elizabeth Nchimbi akitoa nasaa kwa vijana walioweza kuhudhuria na wale walioko nje wasiweze kutumia Tumbaku kwani ni hatari kwa afya za binadamu
Waandhishi wa habari wakiwa kazini.
Afisa Elimu kata ya Kijitonyama, Mwalimu Shangwe Temba akifunga kwa kutoa neno kwa vijana kuacha kujiingiza katika makundi mbalimbali kwani ndio yanayo pelekea vijana wengi kuhamasika na kuanza kutumia Tumbaku ambayo huwaletea vijana wengi matatizo hususani kwa wanafunzi kuacha shule kwa kuugua vifua vikuu na magonjwa mengine mengi
Picha ya umoja wa kikundi cha wanafunzi kinacho elimisha matumizi mabaya ya bidhaa zinazotokana na Tumbaku.
HIVI NDIYO MAGUFULI ALIVYOTIKISA CHATO JIONI YA LEO

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha  Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akifafanua jambo kwa msisitizo mkubwa wakati akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika uwanja wa shule ya sekondari Chato mkoani Geita.PICHA NA MUCHUZI JR-CHATO,GEITA.
  Wakazi wa Chato na Vitongoji vyake wakifuatilia na kusikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba ridhaa mbele yao jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari chato mkoani Geita.
 Wakazi wa Chato wakishangilia kuonesha kuwa watampa kura za ushindi Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita. 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mbele ya wakazi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita. 
 Wakazi wa Chato na Vitongoji vyake wakifuatilia na kusikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba ridhaa mbele yao jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari chato mkoani Geita.
 Wakazi wa Chato ilkuwa ni shangwe tu kila kona ya uwanja. 
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita ,Joseph Kasheku almaarufu King Msukuma akiwaomba ridhaa wananchi wa Chato ya kumchagua Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli ili aweze kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano.
 Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia  wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
  Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
 Wakazi wa Chato wakishangilia kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Chato na vitongoji vyake jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato mkoani Geita.
Wakazi wa Chato wakishangilia kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.
 Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano,pichani kati anaeshuhudia ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Chato mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara wa Kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.
 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia  katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu. 
 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu. 
 Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu.
 Mama Janet Magufuli, mke wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia   katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu.
 Sehemu ya maelfu ya wananchi   katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari  mkutano wa kampeni 
Sehemu ya maelfu ya wananchi   katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari  mkutano wa kampeni.
Picha na Ahmad Michuzi Jnr.

No comments:

Post a Comment