Pages

Saturday, September 19, 2015

EAST AFRICAN BUSINESS COUNCIL AND INNOVATION NORWAY SIGN MEMORANDUM OF UNDERSTANDING

Norway’s Minister for Trade and Industry, Ms Monica Maeland, bids farewell to EAC Secretary General, Amb. Dr Richard Sezibera, after the two held talks on cooperation between Norway and the EAC.

The Norwegian Minister for Trade and Industry, Ms Monica Maeland, and the Secretary General of the East African Community, Amb. Dr Richard Sezibera, today witnessed the signing of a Memorandum of Understanding (MoU) between the East African Business Council (EABC) and Innovation Norway at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.

The MoU was signed by Innovation Norway’s Chief Executive Officer, Ms. Anita Krohn Traaseth, while EABC Chairman Denis Karera signed on behalf of his organization.
 

Under the MoU, which will be effective for a period of five years, EABC and Innovation Norway agreed to work together on various agreed upon priority areas including trade facilitation; joint activities that are beneficial to both institutions including conferences, trade missions (both international and regional), and; business to business engagement both in EAC and Norway and the Nordic countries.

Some of the main areas of cooperation will be in the petroleum and education sectors with the latter focusing on the information and communication technology sector. The two parties further agreed to increase market access through information sharing; promote investment in both regions, and; capacity building and technical assistance.

EABC and Innovation Norway also undertake to jointly: work together to advocate for beneficial trade and good investment climate in the two regions; work together to develop business to business engagement to enhance business partnerships and networking, and; exchange information on business opportunities in both regions.

TAARIFA KWA UMMA - ZIARA ZA RAIS NJE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Safari za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Nje ya Nchi.
 

Wizara imesikitishwa na taarifa za uongo zilitolewa katika vyombo vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10 ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano (5).

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki. 


Kwa miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi 25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo.
 

Ifahamike kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano kama ifuatavyo:
 

1. Kundi la Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
 

2. Kundi la Makamu wa Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
 

3. Kundi la Waziri Mkuu wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
 

4. Kundi la Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nje ya nchi wanapotembelea Tanzania; na
 

5. Kundi la Wajumbe Maalum wanaokuja nchini kuleta taarifa muhimu kwa Rais.
 

Makundi yote haya hugaramiwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki kifungu cha Ziara za Viongozi.

Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara chini ya Idara ya Sera na Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama vile Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hupitishwa kila mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi juu ya watu wanaotoa taarifa za uongo kwa madhumuni ya kujenga chuki dhidi ya Serikali. Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi zinazoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.

Wizara inaandaa taarifa ya ndefu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambayo itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi.
 

                                                                                        Imetolewa na:
                                                    Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
                                             Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
                                                                                  17 Septemba 2015

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CHAMA CHA CUF, MAALIM SEIF AUNGURUMA KATIKA MAJIMBO YA AMANI NA MAGOMENI

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika viwanja vya Kwawazee mjini Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwatambulisha na kuwanadi baadhi ya wagombea wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kwa majimbo ya Amani na Magomeni katika viwanja vya Kwawazee mjini Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwatambulisha na kuwanadi baadhi ya wagombea wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kwa majimbo ya Amani na Magomeni katika viwanja vya Kwawazee mjini Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwatambulisha na kuwanadi baadhi ya wagombea wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kwa majimbo ya Amani na Magomeni katika viwanja vya Kwawazee mjini Zanzibar.
Wafuasi wa CUF wakimsikiliza mgombea urais wa Zanzibar kupitia CUF Maalim Seif Sharif Hamad, katika viwanja vya Kwawazee (Picha na Ali Hamad, OMKR) Na: Hassan Hamad, OMKR

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza, ataifungua Zanzibar kiuchumi na biashara.

Amesema Zanzibar inazo rasilimali nyingi za kiuchumi lakini bado hazijatumiwa ipasavyo kuwanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla.

Akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa Chama hicho kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Kwawazee kwa ajili ya majimbo ya Amani na Magomeni, Maalim Seif amesema CUF kina sera imara za kuweza kuleta mabadiliko kwa kipindi kifupi.

Amesema tayari ameanza kukutana na baadhi ya makampuni ya uchimbaji wa mafuta, na kumuahidi kuwa yatashirikiana nae kuhakikisha kuwa azma ya uchimbaji wa mafuta inatimia muda mfupi baada ya serikali mpya itakayoongozwa na CUF kuingia madarakani.

BALOZI SEIF AFUNGUA JENGO JIPYA LA MADARASA MANNE SKULI YA MSINGI MOGA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Moga mara baada ya kuzindua jengo Jipya la Skuli ya Kijiji hicho la madarasa Manne lililojengwa kwa nguvu za wananachi wenyewe.
Balozi Seif akipokea Risala ya Wananchi wa Kijiji cha Moga Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la skuli ya Moja.

                                                                                                Picha na –OMPR – ZNZ.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewahimiza wanafunzi Nchini kuongeza bidii katika kujifunza masomo yote na kutilia mkazo zaidi masomo ya Sayansi na Teknolojia ambayo ndio yenye nafasi kubwa katika harakati za kila siku kwenye karne hii ya Sayansi.

Alisema katika kuhakikisha juhudi hizo zinafanikiwa, walimu nao wana jukumu kubwa la kujiendeleza kwa kuwa tayari kujifunza mambo mbali mbali yanayohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akizungumza na Wazazi, Walimu na Wanafunzi wa Kijiji cha Moga baada ya kulifungua jengo jipya la Madarasa Manne la Skuli ya Msingi Moga iliyopo Wilaya ya Kaskazini “ A ” Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema Walimu wanahitaji kupatgiwa msaada mkubwa kutoka kwa Wazazi pamoja na wadau wa Maendeleo katika Sekta hiyo ili skuli zote za hapa Nchini ziweze kupata mafanikio makubwa zaidi.

WAZIRI MKUU APOKEA MISAADA YA SH. MILIONI 330 KWA SHULE ALIYOSOMA

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepokea misaada ya zaidi ya sh. milioni 330 kwa ajili ya shule ya msingi Kakuni, iliyopo kijiji cha Kibaoni, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi.

HUAWEI na NMB zimetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika shule mpya ya msingi Kakuni ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alianzisha wazo la kuijenga kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo. Waziri Mkuu Pinda alisoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya msaada huo yaliyofanyika leo mchana (Ijumaa, Septemba 18, 2015) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Meneja Uhusiano wa kampuni ya HUAWEI, Bw. Jin Liguo alisema kampuni yake inaamini msaada huo utasaidia kupunguza tofauti za kiteknolojia zilizopo kwenye sekta ya elimu.

“Kampuni ya HUAWEI iko Tanzania tangu 2001 na imedhamiria kufanya kazi na wanajamii kila inapoona imepata fursa ya kufanya hivyo, na hasa katika elimu ambako pia tumelenga kupunguza tofauti za kiteknolojia zinazojitokeza kwenye sekta hiyo,” alisema Bw. Liguo.

Kampuni hiyo imetoa kompyuta za mezani 50, HUAWEI Tablets 100, Laptop tano, Printers mbili, Scanner mbili, Projector mbili, Projector Screens mbili, Power System seti moja na Audio System seti moja vyote vikiwa na thamani ya Dola za Marekani 150,000 (sawa na sh. milioni 300).

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Bw. Waziri Barnabas alisema benki hiyo imelenga kukuza michezo shuleni na ndiyo maana imeamua kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa shule hiyo ya Kakuni.

Benki ya NMB imetoa kompyuta nne; jezi za michezo jozi 192 (soka 72, wavu 40, kikapu 40 na pete 40); mipira 40 (soka 10, wavu 10, kikapu 10 na pete 10). Pia imepanga kuchangia ununuzi wa madawati yenye thamani ya sh. milioni 10 ambayo alisema yapo tayari ila yanasubiri ujenzi wa kituo cha walimu ukamilike. Vifaa hivyo vina thamani ya sh. Milioni 30.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Waziri Mkuu Pinda aliwashukuru wawaklishi wa HUAWEI na Benki ya NMB kwa msaada huo ambao alisema utachangia kwa kiasi kikubwa kuitimiza ndoto yake aliyokuwa nayo ya kuisaidia jamii iliyomsomesha.

“Wazo la ujenzi wa shule mpya ya msingi Kibaoni lilitokana na ukweli kwamba nilisoma na kumaliza kwenye shule hii ya Kakuni. Nikiwa ni mtumishi wa Serikali, ni Mbunge na sasa hivi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nilijiuliza hivi shule hii ninaweza kuiacha hivi hivi? Hakuna jambo ambalo naweza kufanya na kuisaidia jamii ya wanakijiji na kata nzima ya kwetu?,” alisema Waziri Mkuu katika mada fupi aliyoiwasilisha leo mbele ya waandishi wa habari.

“Niliwaza pia kufanya ukarabati lakini nikabaini kuwa eneo la shule halitoshi kwani wanafunzi waliopo ni wengi kuliko eneo la shule hiyo. Hivi sasa shule ina wanafunzi wapatao 800. Madarasa yamechakaa na nyumba za walimu pia zimechakaa,” aliongeza.

Waziri Mkuu alisema alipeleka maombi kwenye Serikali ya Kijiji cha Kibaoni ambayo ilitoa ekari 65 kutoka eneo lililokuwa ni mashamba ya bega kwa bega na kisha akawasilisha ombi maalum kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (wakati huo) ambayo hivi sasa ni Mlele ili kuomba ushauri na usimamizi wa jumla katika kuisimamia ndoto aliyokuwa nayo.

Alisema aliishirikisha Halmashauri kuandaa michoro inayotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na OWM-TAMISEMI, na kuwataka waandae mapendekezo ya bajeti kwa kuzingatia taratibu za kiuhandisi na ujenzi na makisio ya awali yalikuwa sh. bilioni 1.3/-.

Alisema alipeleka barua kuomba michango kwa watu binafsi, mashirika ya umma, taasisi, mabenki na balozi mbalimbali ambao hadi sasa wamekwishamchangia sh. milioni 785 na dola za Marekani 267,834 na kwamba hadi sasa kwenye akaunti ya ujenzi amebakiza kiasi cha sh. milioni 40 na dola za Marekani 117,495.

“Katika kuanza zoezi la kukusanya fedha Aprili 2013, Ubalozi wa China ulikuwa wa kwanza kuitikia maombi yetu na ulitoa Dola za Marekani 200,000 ambazo zilikuwa sawa na sh. milioni 320. Pia ubalozi ukamteua mkandarasi wa barabara ya kutoka Nkasi – Kibaoni – Mpanda asaidie katika ujenzi wa shule ili kupunguza gharama,” alisema.

Hadi sasa majengo yaliyokamilika ni madarasa 14, jengo la utawala lenye ofisi za walimu na maktaba mbili (wanafunzi na walimu), jengo la TEHAMA la wanafunzi lenye darasa moja, ukumbi mdogo na ofisi ya mwalimu na majengo mawili ya vyoo yenye matundu 48. Pia ujenzi wa nyumba sita za walimu uko kwenye hatua za mwisho. Nyumba hizo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Waziri Mkuu aliwaomba Watanzania watakaoguswa na jambo hili wamsaidie kutimiza ndoto yake kwani bado anakabiliwa na kazi ya kuweka umeme, maji, kujenga nyumba 18 za walimu, bwalo na jiko, karakana nne za ufundi, vitabu na TABLETS za wanafunzi, kituo cha walimu cha mafunzo ya muda mfupi na utunzaji taarifa (Resource Centre), viwanja vya michezo vya kisasa vinavyozingatia michezo yote, mfumo wa uvunaji maji ya mvua, mfumo wa maji safi na maji taka, nyumba mbili za walinzi na uzio wa shule.

Alitaja vitu vingine ambavyo bado vinahitaji kuchangiwa ni meza za walimu – za ofisini na darasani, viti vya walimu – vya ofisini na darasani, madawati ya shule ya msingi na ya awali, meza na viti vya maktaba zote mbili, meza na viti vya bwalo – shule ya msingi na shule ya awali. Vyote hivi alisema vitagharimu sh. bilioni 2.18.

RAFIKI WA MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS ASEMA MWANARIADHA HUYO AMEDHOOFIKA

U15 WALIOKWENDA MAZOEZI ORLANDO PIRATES WAREJEA

Kufuatia safari ya vijana watano wa U15 Asaad Ali Juma, Maziku Aman, Issa Abdi, Kelvin Deogratias, Athumani Maulid waliokwenda kufanya mazoezi kwenye klabu ya Orlando Pirates kufuatia mwaliko uliotolewa na TFF na klabu hiyo, safari hiyo ilikamilika na vijana wamerejea nyumbani.

Vijana hawa waliongozana na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi wakiwa Afrika Kusini walifanya mazoezi ya wiki moja kuanzia Septemba Mosi mpaka tarehe 7 Septemba, 2015 chini ya uangalizi wa Augusto Placious ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Orlando Pirates.

Idara ya ufundi ya Orlando Pirates imejiridhisha na kiwango kilichoonyeshwa na vijana hao.

Hatua inayofuata ni mawasiliano kati ya shule wanazosoma hao vijana hapa Tanzania na klabu ya Orlando Pirates ili kutafutiwa nafasi za masomo kwenye shule za Afrika Kusini.

Jambo hili likikamilika vijana hao watakwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya masomo na kufundishwa mpira.

TFF inamshukuru Dr. Irvin Khoza Rais na mmiliki wa klabu ya Orlando Pirates kwa ushirkiano na kutoa nafasi kwa vijana wa U15 Tanzania kwenda kufanya mazoezi kwenye klabu hiyo kongwe nchini Afrik Kusini na kuendelezea

LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA KESHO

Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza kusaka nafasi tatu za juu ili kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

Kundi A, Polisi Dar watakuwa wenyeji wa Friends Rangers kwenye uwanja Mabatini mkoani Pwani, Mjii Mkuu ya Dodoma watapambana na Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.

Kundi B, Polisi Morogoro watacheza na Burkina Faso uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji FC watacheza na Kurugenzi uwanja wa Amani mjini Njombe, Lipuli ya Iringa watawaribisha Kimondo FC uwanja wa Wambi- Iringa na JKT Mlale watakua wenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.

Kundi C, Mbao FC watawakaribisha Geita Gold uwanja wa CCM Kirumba, Rhino Rangers watacheza dhidi ya Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja wa Ushirka mjini Moshi na Polisi Mara watakua wenyeji wa JKT Kanembwa kwenye uwanja wa Karume mkoani Mara.

CROATIA YAFUNGA MIPAKA YAKE SABA KATI YA NANE INAYOPAKANA NA SERBIA KUDHIBITI WAHAMIAJI

KARIBU SHULE ZOTE ZA UMMA NCHINI KENYA, ZINATARAJIWA KUFUNGWA HII LEO

TOTTENHAM, SCHALKE NA BORUSSIA DORTMUND WAANZA KWA USHINDI LIGI YA UROPA

KATIBU MKUU WA FIFA JEROME VALCKE ASIMAMISHWA WADHIFA WAKE

TANZANIA NA NORWAY KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akihutubia katika ufunguzi rasmi wa Semina ya Ushirikiano wa Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Norway iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency ya Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Monica Maeland, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanna-Marie Kaarstad na wadau wengine katika sekta ya biashara na uwekezaji kutoka Norway na hapa nchini.

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Maeland (kulia) akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula na katikati ni Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Kaarstad.
                                                                        Waziri Membe akiendelea kuzungumza

MEMBERS BEGIN FIVE DAY CAPACITY BUILDING WORKSHOP IN ZANZIBAR

                                                                                        Group Photo of the Members
Hon Makongoro Nyerere (left) gestures to Hon Adam Kimbisa as Hon Emmanuel Nengo (right) looks on

Hon Dr Odette Nyiramilimo, Chair of the Committee on General Purpose speaks at a session as Hon Jeremie Ngendakumana, Chair of the Committee on Accounts looks on

UJUMBE WA KAMPUNI YA POLY TECHNOLOGIES INC YA CHINA WAMTEMBELEA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (katikati) akiongea na ujumbe wa Kampuni ya Poly Technologies, Inc. ya China (haupo pichani) uliomtembelea ofisini kwake. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil na na kulia ni Katibu wa Waziri, Nelson Kaminyoge.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akimkaribisha Makamu wa Rais wa Kampuni ya Poly Technologies, Inc. ya China Bw. Huang Geming (mwenye tai) aliyeongoza ujumbe wa Kampuni yake kumtembelea Waziri ofisini kwake.
Ujumbe wa Kampuni ya Poly Technologies, Inc. ya China, ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bw. Huang Geming (wa tatu toka kulia) katika mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (hayupo pichani) ulipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake.

TAMASHA LA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015


MWALIMU HOSEA DANIEL KUTOKA FOLUMA TUITION CENTRE AELEZA UMUHIMU WA MASOMO YA ZIADA.
Pichani ni Mwalimu Hosea Daniel kutoka Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) kiitwacho Foluma Tuition Centre kilichopo Tarime Mkoani Mara akiwa darasani.

Na:Binagi Media Group
Mwl.Daniel anasema kuwa Masomo ya ziada ni mhimu kwa mwanafunzi kwa kuwa husaidia katika kukuza uelewa na ufahamu kwa mwanafunzi na hivyo kuongeza ufaulu kwa mwanafunzi.
Pichani ni Mwalimu Hosea Daniel kutoka Kituo cha Masomo ya Ziada (Tuition) kiitwacho Foluma Tuition Centre kilichopo Tarime Mkoani Mara akiwa darasani.

MO DEWJI ANYAKUA TUZO YA MWAKA YA MFANYABIASHARA ANAYESAIDIA ZAIDI JAMII

IMG_9463
Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker akimkabidhi tuzo ya '2015 Philanthropist of the year-East Africa' Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji katika sherehe zilizofanyika hoteli ya DusitD2 jijini Nairobi.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_9492
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akizungumza kwenye hafla ya tuzo za All Africa Business Leaders Awards 2015 (AABLA). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker.
IMG_9595
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akipozi katika picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker.

MSAFARA WA SUGU WASHAMBULIWA KWA MAWE AKIELEKEA KATIKA KAMPENI ZAKE ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MBEYA

Gari la Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi Sugu likiwa kituo cha Polisi kati jijini Mbeya mara baada ya kushambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM
Sugu akiwa kituo cha Polisi na wafuasi wake.Picha Kenneth Ngelesi Mbeya .
(JAMIIMOJABLOG MBEYA )

                                                                                        Na Emanuel Kahema ,Mbeya
 

MGOMBEA ubunge kupitia chadema jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi leo amejikuta katika wakati mgumu baada ya msafara wake kushambuliwa na mawe na wafuasi wanaosadikiwa kuwa ni wa chama cha mapinduzi CCM na kwamba katika tukio hilo watu wawili wamejeruhiwa akiwemo dereva aliyekuwa akimuendesha mgombea huyo .
 

Tukio hilo la kushambuliwa kwa msafara huo, limetokea majira ya saa 11 za jioni katika eneo la barabarani lililopo katika Kata ya Ghana mtaa wa Mbata jijini hapa ambapo inasemekana mgombea huyo alikuwa katika harakati za kampeni kuomba kura kwa wananchi wa Iziwa ambapo mgombea huyo alikuwa ndani ya gari yake yenye namba za usajili T161 CPP Toyota Land Cruser VX .
 

Awali, wafuasi wa chama cha mapinduzi CCM, walikuwa katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea wao ngazi ya Udiwani katika kata ya Ghana iliyopo ndani ya Jiji la Mbeya, hivyo wakiwa kwenye harakati hizo inasemekana walishangaa kuona msafara wa sugu ukipita katikati ya mkutano huo hivyo kushindwa kuvumilia na kuanza kurusha mawe huku wengine wakishikana mithili ya kutaka kupigana.

Katika vurugu hizo gari aliyokuwa amepanda mgombea huyo lilipasuliwa kioo cha mbele na gari ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mbeya, ikipasuliwa kioo cha mbele .

DK MAGUFULI AWATAKA WANANCHI, VIONGOZI KUDUMISHA AMANI YA NCHI ILI AONGOZE VIZURI

LOWASSA AENDELEA NA ZIARA ZAKE KAMPENI, BARIADI MKOANI SIMIYU

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Bariadi (hawapo pichani) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. Katika ziara hiyo, Mh. Lowassa aliambatana na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye pamoja na Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Vyama vinavyounda UKAWA wa Mkoa wa Simiyu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akihutubia katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Badiadi kupitia CHADEMA, Godwin Simba, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Halmashauri ya WIlaya ya Bariadi, Mkoani Mkoani humo, leo Septemba 17, 2015.

No comments:

Post a Comment