Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Habib Ali Shariff akitoa maelezo kuhusu Mfumo
mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa jinsi unavyofanyakazi zake kwa
haraka, katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt
Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Shirika la John Snow Incorporated (JSI) nchini, Deo Kimera akitoa
nasaha zake kwa Viongozi na Maafisa wa Afya waliopata elimu juu ya
matumizi ya mfumo mpya wa Ugavi wa madawa wa kielektroniki walioshiriki
katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika Park Hyatt Hotel
Shangani Mjini Zanzibar.
Mshauri
Mwandamizi kutoka Shirika la Misaada la Marekani USAID Kelly Hamblin
akitoa shukran zake kwa Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kwa mashirikiano yao ya kufanikisha Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi
wa madawa nchini, katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo. Uliofanyika
Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri
wa Afya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akitoa shukrani zake kwa Shirika
la John Snow Incorporated (JSI) kutokana na juhudi zao za kuwawezesha
maafisa wa Afya wa Zanzibar kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa Ugavi wa
madawa kwa njia ya kielektroniki katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo
uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Mfamasia
kutoka Bohari Kuu Zanzibar Bi. Khadija Ali Shehe akielezea changamoto
walizokumbana nazo wakati wa kutumuia mfumo wa Karatasi katika
Usambazaji wa Madawa vituoni kabla ya kuzinduliwa Mfumo mpya wa
kielectroniki hii leo
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Gombani Pemba Abdalla Mbaruk Saleh akitoa
ushuhuda wa namna Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi wa madawa
unavyofanya kazi zake kwa haraka na ufanisi, katika hafla ya uzinduzi wa
mfumo huo. Uliofanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna katikati
akizindua Mfumo mpya wa Kielectroniki wa Ugavi na Usambazaji wa Madawa
kwa niaba ya Makamu wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idd. Kulia kwake ni
Msimamizi wa taaluma kutoka Shirika la John Snow Incorporated (JSI)
Anselm Namala ,na kushoto ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman. Hafla
ya uzinduzi wa mfumo huo imefanyika Park Hyatt Hotel Shangani Mjini
Zanzibar.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna kushoto
akihutubia mara baada ya uzinduzi wa Mfumo mpya wa Kielectroniki wa
Ugavi na Usambazaji wa Madawa kwa niaba ya Makamu wa Pili wa rais Balozi
Seif Ali Idd. Hafla ya uzinduzi wa mfumo huo imefanyika Park Hyatt
Hotel Shangani Mjini Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo
Zanzibar.
Kwa hisani ya ZanziNews
LOWASSA AWASILI MAKAO MAKUU YA CHADEMA KUCHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS NDANI YA CHAMA HICHO
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward
Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya
chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua
fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa
amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha
CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es
Salaam.
Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama
Regina Lowassa akiwasili ofisi za Makao makuu ya CHADEMA yaliyopo
Kinondoni jijini Dar,akiwa ameambatana na Mh Lowassa (hayupo
pichani),kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama
hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA
kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi
karibu,jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward
Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama
cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina
akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini
Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia
chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na
UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi
karibu,jijini Dar es Salaam.
Rabsha za hapa na pale zilikuwepo
kama uonavyo pichani wakati Mh.Lowassa akiwasili Makao Makuu ya
CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua fomu ya
kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho.
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward
Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama
cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina
akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini
Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia
chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na
UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi
karibu,jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward
Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya
chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde,kuchukua
fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa
amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA kupitia chama cha
CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi karibu,jijini Dar es
Salaam.
WAHAMIAJI WAANGUSHA UZIO KUWAHI KUPANDA TRENI KUZAMIA UINGEREZA
Mamia ya wahamiaji wameangusha uzio
wa fensi kuelekea katika njia ya reli usiku wa jana wakati wakikatiza
kujaribu kuwahi kupanda treni kuelekwa Kent katika safari
iliyobatizwa jina la kuingia Uingereza ama kifo.
Wabunge waandamizi wa Uingereza
wamesema jeshi la Uingereza linapaswa kupelekwa kuwadhibiti wahamiaji
hao kwa kuwa inaonekana mamlaka za Ufaransa zimezidiwa na kushindwa
kuwazuia.
Hali hiyo imechangia maafisa polisi
wa kutuliza ghasia wa Ufaransa 120 kupelekwa katika eneo hilo, ili
kusaidiana na askari kanzu 250 walipo katika eneo hilo, hata hivyo
idadi hiyo inasemekana haitoshi.
Wahamiaji wanawake wakikatiza juu ya uzio
Mhamiaji akipenya kwenye tundu katika uzio huo
No comments:
Post a Comment