Pages

Wednesday, June 17, 2015

BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA SUDAN NCHINI

MKURUGENZI WA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WA MAMBO YA NJE AAGANA NA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA UNDP NCHINI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA RASMI MATANGAZO YA TELEVISHENI YA MFUMO WA ANALOJIA.

5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za Ukomo wa matangazo ya Televisheni ya Analojia, zilizofanyika leo Juni 17, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibofya kitufye cha Lap Top kuashiria kufunga rasmi Matangazo ya Televisheni ya Analojia, baada ya kufikia ukomo rasmi hii leo Juni 17, 2015 baada ya kufanikiwa kuzima mitambo ya Analojia kwa nchi nzima. Sherehe hizo za ukomo zimefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara.
7
                                                                                          Wadau wa masiliano.

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY NCHINI

Picha na Reginald Philip.

RATIBA YA BARCLAYS PREMIER LEAGUE HADHARANI, KUANZA KUTIMUA VUMBI AUGUST 08' 2015

                                                Mabingwa wa ligi kuu England 2014/2015, Cheslea
Shirikisho la soka nchini England ( FA ) limetoa ratiba ya msimu mpya wa ligi kuu nchini humo ambayo imepangwa kuanza kutimua vumbi August 08' 2015 katika viwanja kumi tofauti. 

BALOZI SEIF AWATAKA WAZAZI KUWAPOKEA WATOTO WAO WALIOACHANA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA


                                                                                                    Picha na – OPMR – ZNZ.

Wazazi wameaswa kuwa tayari kuwapokea Vijana au watoto wao walioamua kuacha matumizi ya dawa za kulevya ili kuwalinda na vishawishi vinavyoweza kutoa nafasi ya kuwarejesha tena kwenye matumizi ya Dawa hizo pamoja pombe haramu.

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi ametoa wosia huo wakati wa kuwapokea Vijana Sita wa Kijiji cha Fujoni walioamua kuacha kutumia Dawa za kulevya na kupata mafunzo watakayoyatumia kuwasomesha wenzao kuachana na Dawa hizo hapo katika Skuli ya Fujoni Wilaya ya Kaskazini “ B “.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema wapo Wazazi na Familia Nchini ambao bado wanaendelea na tabia ya kuwatenga Vijana wao walioathirika na Dawa za kulevya kwa kuchelea kufanyiwa matendo ya maudhi kama wizi.

KATIBU MKUU BALOZI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA BALOZI MTEULE WA QATAR NCHINI

KOREA KASKAZINI IMESEMA INAKABILIWA NA UKAME MBAYA KUWAHI KUTOKEA KATIKA KARNE

MAHAKAMA YA NCHINI MISRI IMEUNGA MKONO ADHABU YA KIFO KWA MOHAMMED MORSI

Mahakama ya nchini Misri imeunga mkono adhabu ya kifo iliyotolewa kwa rais aliyeng'olewa madarakani wa nchi hiyo Mohammed Morsi, kwa kosa la kusababisha kutoroka kwa wafungwa wengi.

Hukumu hiyo ilitolewa awali mwezi Mei, sasa imethibitishwa baada ya majadiliano na viongozi wa kidini wa juu wa Misri pamoja na Mufti Mkuu.

Hukumu ya kifo kwa viongozi wakuu wa chama cha Muslim Brotherhood, akiwemo kiongozi wao mkuu Mohammed Badie, pia nayo imeridhiwa kutekelezwa.
ECUADOR ZAANZISHA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA

TANAPA WAKABIDHI MRADI WA UJENZI WA DARAJA KATIKA VIJIJI VYA SINGANA SUNGU WILAYA YA MOSHI VIJIJINI.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI ,ANGELA KAIRUKI ATEMBELEA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)MKOA WA KILIMANJARO

NIAMBIE LIVE SHOW....FATHER'S DAY SPECIAL

KINANA ASAFIRI KWA BODABODA KWENDA KUKIOKOA KIJIJI CHA ILYAMCHELE KISICHOKUWA NA SHULE WILAYANI BUKOMBE

DKT. MAGUFULI AWASILI ZANZIBAR KUTAFUTA WADHAMINI

Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mchakato wa uhakiki wa kadi za wanachama wa CCM Wilaya ya Mfenesini Kisiwani Zanzibar waliojitokeza kumdhamini.
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Mussa Haji Katibu wa CCM Wilaya ya Mfenesini Kisiwani Zanzibar
Dkt. Magufuli akifurahia mara baada ya kukabidhiwa fomu za Wadhamini kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ya Kaskazini B-Unguja.
Dkt. John Magufuli akisomewa dua katika Wilaya ya Wete Pemba mara baada ya kumaliza zoezi la kupata wadhamini katika katika kisiwa cha Pemba. Dkt. Magufuli amepata Wadhamini katika mikoa mitano kisiwani Zanzibar, Mitatu Unguja na Miwili Pemba

WAZIRI MKUU APATA WADHAMINI 9,141 KATAVI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wanaCCM waliofika kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya Kibaoni kumdhamini katika nia yake ya kuwania uteuzi wa CCM katika kugombea nafasi ya urais Juni 15, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimian na baadhi ya wananchi wa Mpanda waliofika kwenye ofisi ya CCM ya Wilaya ya Mpanda kushuhudia na kumdhamini ilia pate sifa za kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Juni 15, 2015.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AFANYA ZIARA KATIKA MKOA WA LINDI KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

11
Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu akimpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani humo kuanza ziara ya siku mbili.
1
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na watendaji wa NHC mara baada ya kuwasili Mkoani humo kuanza ziara ya siku mbili.
3
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Mwantumu Mahiza akitoa taarifa fupi ya Mkoa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani humo kuanza ziara ya siku mbili kutatua migogoro ya Ardhi. Mh. Mahiza alielezea ushirikiano uliopo kati ya Mkoa na NHC wa kuwezesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za watumishi wa Mkoa huo.
4
Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu akitoa taarifa ya Mkoa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi mara baada ya kuwasili Mkoani humo kuanza ziara ya siku mbili kutatua migogoro ya Ardhi.

No comments:

Post a Comment