Wanafunzi kutoka Chuo cha Mafunzo ya
Ualimu Garissa nchini Kenya wanashinikiza wahamishiwe kwenye vyuo
vingine nchini Kenya kutokana na kuhofia usalama wa maisha yao.
Wanafunzi hao 600 wamegoma kurejea
kwenye chuo hicho kufuatia mauaji ya wanafunzi 148 wa Chuo Kikuu cha
Garissa na wapiganaji wa kundi la al-Shabaab.
Mwenyekiti wa Chuo Mafunzo ya Ualimu
Garissa Bw. Kimani Braizon amesema ni idadi ndogo mno ya wanafunzi wa
eneo hilo wamerejea kwenye taasisi hiyo ya elimu huku wengine wakiapa
kutorudi.
SHAMRA SHAMRA ZA MAANDAMANO YA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI ZILIVYOFANA MJINI MUSOMA
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi mkoani Mara wakijiaanda kuanza maandamano kutoka Hospitali Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mara wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Musoma.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog). Baadhi ya wanafunzi wa shule ya uuguzi wilayani Musoma wakiwa wamekusanyika nje ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya maandamano ya kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa yamefanyika mjini Musoma kwenye viwanja vya Mkendo, mkoani Mara. Pichani juu na chini ni baadhi ya Wakunga kutoka mikoa mbalimbali ya nchini wakijumuika na wenyeji wao kwenye maandamano ya maadhimisho hayo. Baadhi ya Wakunga wakijumuika na wakinama wa mjini Musoma njiani kuelekea kwenye viwanja vya Mkendo wakati maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga duniani burudani ya matarumbeta yaliyokuwa yakishereheshe maandamano hayo. Wakunga wa kiume kutoka wilaya ya Serengeti wakiwa wamejumuika na wenyeji wao kwenye maandamano hayo.
LIGI YA MABINGWA ULAYA, BINGWA MTETEZI REAL MADRID HOI KWA BIBI KIZEE CHA TURIN
Mabingwa
watetezi wa kombe la klabu bingwa barani Ulaya, Real Madrid wamejiweka
pabaya kusonga mbele kuelekea hatua ya fainali ya michuano hiyo, baada
ya usiku wa kuamkia leo kukubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Kibibi
kizee cha Turin, Juventus ya Italia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya
nusu fainali ya ligi hiyo.
Wakicheza ugenini, Real Madrid walijikuta wakifungwa bao la kwanza katika dakika ya nane ya mchezo, bao likifungwa na Alvaro Morata.
Hata hivyo mshambuliaji mwenye kasi na bidii uwanjani, Cristiano Ronaldo aliisawazishia timu yake ya Real Madrid kwa kichwa katika dakika ya 27 kwa kufunga bao safi, na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimefungana bao 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na walikuwa ni Juventus waliopata bao la pili kwa mkwaju wa penati iliyofungwa na mkongwe Carlos Tevez. Timu hizo zitarudiana wiki ijayo mjini Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Hadi mwisho wa mchezo huo, Juventus 2 na Real Madrid 1.
Ronaldo akifunga bao kwa kichwa
Maelfu ya mashabiki wakiwa wamefurika uwanjani
Wakicheza ugenini, Real Madrid walijikuta wakifungwa bao la kwanza katika dakika ya nane ya mchezo, bao likifungwa na Alvaro Morata.
Hata hivyo mshambuliaji mwenye kasi na bidii uwanjani, Cristiano Ronaldo aliisawazishia timu yake ya Real Madrid kwa kichwa katika dakika ya 27 kwa kufunga bao safi, na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimefungana bao 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na walikuwa ni Juventus waliopata bao la pili kwa mkwaju wa penati iliyofungwa na mkongwe Carlos Tevez. Timu hizo zitarudiana wiki ijayo mjini Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Hadi mwisho wa mchezo huo, Juventus 2 na Real Madrid 1.
Ronaldo akifunga bao kwa kichwa
Maelfu ya mashabiki wakiwa wamefurika uwanjani
WAKUNGA WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KUTENGENEZA TAIFA LA KESHO
Rais
wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Feddy Mwanga akimkaribisha Ofisa
Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges
(kulia) kuzungumza na wakunga nchini waliokusanyika kwenye mdahalo wa
siku moja kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakunga
Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Musoma mkoani Mara. Kushoto ni
Kaimu Muuguzi mkuu wa serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk. Ama Kasangala. (Picha zote na Zainul Mzige)
Ofisa
Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances
Ganges akizungumza na Wakunga nchini Tanzania waliohudhuria kwenye
mdahalo wa siku moja uliofanyika kwenye ukumbi wa Mara ofisi za Mkuu wa
mkoa wa Mara mjini Musoma kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho ya
siku ya Wakunga duniani kujadili changamoto zinazowakabili Wakunga
nchini. Katikati ni Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Feddy
Mwanga na Kushoto ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikalim kutoka Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala.
Ofisa
Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances
Ganges akisisitiza jambo wakati akiteta na Wakunga nchini ambapo pia
aliwatia moyo kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwataka kuendeleza moyo huo
bila kuchoka.
Daktari
bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi, Kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa
jamii, Rosina Lipyoga akizungumza katika siku hiyo ya mdahalo wa
wakunga ambapo alisema ni aibu kwa watoto na wazazi kufa kutokana na
huduma hafifu.
MEYA WA KINONDONI, YUSUPH MWENDA ATWAA TUZO YA MEYA BORA AFRIKA
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhiwa Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi
la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala
za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana. Mwingine ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa
Ghasia.
Katibu
Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mbando na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty pamoja na
watendaji wengine wakifuatilia kwa makini wakati wa hafla hiyo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),
Hawa Ghasia akikabidhi cheti cha Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la
Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) kwa Meya wa Manispaa
ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyo zilizotolewa na Jumuiya
ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),
Hawa Ghasia akikabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la
Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na
Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), kwa Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwa amenyanyua Tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),
Hawa Ghasia akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dola za Marekani
100,000 kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda baada ya
kumkabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la
Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala
za Mitaa ya Afrika (UCLGA) kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.Na
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akifuatana na wasaidizi wake alipofika Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini
Zanzibar leo wakati alipofanya ziara ya hafla kutembelea wananchi wa
sehemu hiyo waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua
iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizungumza na wananchi wa Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar
wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea wananchi wa sehemu hiyo
waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua iliyonyesha juzi na
kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.
Hapa
ni Mtaa wa Mwanakwerekwe ambapo pamefanyika shimo kubwa akama
linavyoonekanwa kutokana na mvua iliyonyesha juzi na kupelekea uharifu
ambao fedha nyingi zitatumika kufukia eneo hili pia Rais wa Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
alitembelea wakati alipofanya ziara ya makusudi leo kutembelea maafa
mbali mbali yaliyotokea kutokana na Mvua hiyo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akipata maelezo kutoka kwa Injinia Ramadhan China wa Idara ya Ujenzi
wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe
Mjini Unguja kuangalia maafa mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa
sehemu hiyo kwa kuvunjikiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa
iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili
wa Rais Mohamed Aboud Mohamed leo wakati wakati alipofanya ziara ya
hafla ya kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia maafa
mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa sehemu hiyo kwa kuvunjikiwa na
nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara
mabali mbali (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili
wa Rais Mohamed Aboud Mohamed (kulia) wakati wakati alipofanya ziara ya
hafla ya leo kutembelea Bwawa la Maji la Mwanakwerekwe Mjini Unguja
kuangalia namana lilivyofurika Maji ya mvua kubwa iliyonyesha juzi na
kupelekea hasara mabali mbali kwa Wananchi.
WEZI WA MIFUGO WAIBA MIFUGO NA KUUWA WATU 46 NCHINI KENYA
Watu wapatao 46 wameuwawa hapo jana
na wengine wengi kujeruhiwa na wezi wa mifugo ambao inaaminika kuwa
ni kutoka Turkana katika kijiji cha Nadome katika mpaka wa Turkana
Mashariki.
Mkuu wa Mkoa wa Rift Valley osman
Warfa amethibitisha kutokea kwa vifo 46 usiku wa kuamkia jana.
Warfa amesema idadi isiyojulikana ya
mifugo imeibiwa na kuongeza kuwa kikosi cha KDF na cha jeshi la
polisi Kenya linawasaka wahalifu hao.
JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA LINAWASHIKILIA WATU 37 KWA KOSA LA KUFANYA FUJO
Jeshi la polisi Mkoani Dodoma
linawashikilia watu 37 kwa kosa la kufanya fujo kwa kuzuia watu
wengine kutoa huduma ya usafiri kama Bajaji na magari ya watu binafsi
kwa kuwapiga watu wanaopanda vyombo hivyo vya usafiri, kupiga magari
kwa mawe na kufunga barabara.
Watu hao wamekamatwa kwenye mitaa ya
Nkuhungu katika barabara ya kwenda Singida na Chadulu kwenye barabara
ya Morogoro katika Manispaa ya Dodoma.
Akifafanua kuhusu kukamatwa kwa watu
hao 37 amesema ni wale tu waliokwenda mbali zaidi na kujichukulia
sheria mikononi, ila kwa wale wote walioegesha magari yao kwenye
vituo au pembezoni mwa barabara hawakukamatwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma
David Misime ametoa wito kwa watu wote kwamba ni marufuku watu kuzuia
wengine kutoa huduma, ni marufuku watu kuharibu mali za wengine.
Wanaofanya uharifu huo watakamatwa na kufikishwa mahakamani ili
sheria ichukue mkondo wake.
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI JOHN KERRY AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA NCHINI SOMALIA
John Kerry amefanya ziara ya
kushtukiza nchini Somalia hii leo, maafisa wa Marekani wamesema na
kuweka rekodi ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa kwanza wa taifa hilo
kuzuru taifa hilo la Afrika lenye machafuko.
Kerry alikaa kwa saa chache katika
Jiji la Mogadishu, na hakuruhusiwa kutoka katika uwanja wa ndege
ambapo alikutana na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud oamoja na
Waziri Mkuu Omar Abdirashid Ali Sharmake.
Msemaji wa Wizara yake Marie Harf
amesema katika ziara hiyo ya Somalia Kerry alienda taifa hilo,
kuonyesha kuunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa katika kuisaidia
serikali ya mpito ya Somalia, kuimarisha amani.
MAALIM SEIF AWATEMBELEA WALIOATHIRIKA NA MVUA HUKO MWANAKWEREKWE, JANG'OMBE NA KWAHANI
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana
na Sheha wa Shehia ya Kwahani Bw. Nassir Ali Kombo, baada ya kutembelea
maeneo yaliyoathirika na mvua katika shehia hiyo.
Na: Hassan Hamad (OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameiagiza Idara ya maafa Zanzibar kushirikiana na Wakuu wa Wilaya kufanya utafiti juu ya watu walioathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha, ili waweze kupatiwa misaada ya haraka.
Amesema mvua hiyo imeleta athari kubwa kwa baadhi ya wananchi hasa katika maeneo ya Mjini na Magharibi, na kwamba misaada ya haraka inahitajika kwa waathirika hao.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo wakati akifanya ziara ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo yakiwemo Mwanakwerekwe, Kwahani na Jang’ombe, ambapo baadhi ya nyumba zimeathiriwa kabisa na kupekelea baadhi ya wananchi kukosa makaazi.
Sambamba na hilo Maalim Seif ameeleza haja kwa Baraza la Manispaa na Idara ya Ujenzi kufanya utafiti wa kina juu ya hali ya mitaro katika manispaa ya Zanzibar, ikiwa ni njia moja wapo ya kulitafutia ufumbuzi wa kudumu tatizo la kupita na kutuama kwa maji katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment