Pages

Sunday, May 31, 2015

EDWARD LOWASSA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA TANZANIA, JANA JIJINI ARUSHA

 

 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SOURCE:http://issamichuzi.blogspot.com/
 Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).
 Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
 Mh. Lowassa akiwapungia wananchi.
 Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akihutubia katika mkutano wa hadhawa wa kutangaza nia yake hiyo,  kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.
Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa wakati wa mkutano uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Mh. Edward Lowassa akipongezwa na baadhi ya Wabunge waliohudhulia mkutano huo, baada hotuba yake.

Ujumbe wa M

PITIA VICHWA VYA MAGAZETI-MEI 31,2015

1 2
5
6
8
7
10
9
3 4

FLAVIANA MATATA FOR NYANDCOMPANY

MWANAMITINDO AFANYAYE KAZI ZAKE ZA UANAMITINDO ALIYEJIKITA MAREKANI FLAVIANA MATATA AMEKUWA AKIFANYA KAZI MBALI MBALI ZA KUONESHA MAVAZI JUKWAANI SAMBAMBA NA HIZI ZA MATANGAZO YA KIBIASHARA  YA MAVAZI NA SAFARI HII AMEFANYA NA KAMPUNI YA NEWYORK AND COMPANY KWA AJILI YA MAVAZI YA MAJIRA YA JOTO
FullSizeRender IMG_6387 IMG_6388 IMG_6389
aofisa wa Umoja wa Benki za Akiba Duniani Kanda ya Afrika Wakitembelea Zanzibar
Meneja wa Tawi la Benki ya Posta Zanzibar Ndg Justin S.Nandonde akisalimiana na kumkaribisha wageni wake walipotembelea Tawi hilo Zanzibar kujionea utendaji wa Benki ya Posta Tawi la Zanzibar wakiwa katika ziara yao Zenj.
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg. Sabasaba Moshingi, akitowa maelezo ya
Ujumbe wa Maofisa wa Benki wa Umija wa Mabenki Duniani Kanda ya Afrika,
walipotembelea Benki ya Posta tawi la Zanzibar.
Wajumbe wa Mkutano wa Wanachama wa Umoja wa Mabenki Duniani na Kanda ya Afrika wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania wakati walipofika Tawi la Benki ya Posta Zanzibar,
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg. Sabasaba Moshingi, akitowa maelezo ya
Ujumbe wa Maofisa wa Benki wa Umija wa Mabenki Duniani Kanda ya Afrika,
walipotembelea Benki ya Posta tawi la Zanzibar
Mkurugenzi wa Tekohama na Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Jema Msuya akitowa maelezo ya kiufundi kwa ujumbe huo.walipotembelea Benki ya Posta Tawi la Zanzibar Mchangani  
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Zanzibar Ndg. Justin SNdandonde akitowa maelezo kwa ujumbe huo ulipotembelea Tawi hilo na kuagalia ufanisi wa huduma za Benki hiyo kwa wateja wao
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi akiwa na wakeni wake wakitoka katika moja ya sehemu ya historia ya Kanisa la Mkunazi Zanzibar.  
Mtembeza Watalii katika Mji Mkongwe seif Ali akitowa maelezo kwa Ujumbe huwa sehemu za historia za Mji Mkongwe wa Zanzibar. 
Maofisa wa Umoja wa Benki za Akiba Duniani Kanda ya Afrika wakiwa katika ziara yao katika mji mkongwe na kupata kuonja Ubuyu wa Kwaissa sokomuhugo Zenj wakiwa katika ziara ya siku mbili Zanzibar baada ya kumaliza Mkutano wao Dar.
Mtembeza Watalii Zenj akitowa maelezo kwa Ujumbe huo wa Maofisa wa Mabenki ya Akiba wakiwa katika ziara yao kutembelea sehemu za historia za mji Mkongwe Zanzibar wakipata maelezo ya Mlango wa Zanzibar

JAMBO LEO YAICHABANGA BODABODA FC TAMASHA LA BODABODA UKONGA

 Wachezaji wa timu ya Gazeti la Jambo Leo, wakifanya mazoezi ya kupasha mwili muda mfupi kabla ya kuvaana na timu ya Bodaboda FC ya Wilaya ya Ilala, wakati wa Tamasha la Bodaboda kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam leo. Katika mechi hiyo, Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
 Kikosi cha timu ya Gazeti la Jambo Leo kilichopambana na Bodaboda FC
 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (wa pili kulia), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Gazeti la Jambo Leo, muda mfupi kabla ya timu hiyo kukipiga na timu ya Bodaboda FC ya Wilaya ya Ilala, wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam jana.Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bodaboda FC , muda mfupi kabla ya timu hiyo kukipiga na timu ya Gazeti la Jambo Leo, wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam
 Silaa akitoa mawaidha kwa timu hizo kabla ya mechi kuanza
 Mchezaji wa timu ya Jambo Leo,  Frank Balile (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Bodaboda, Sharif Mohamed
 Mlinda mlango Maganga Benjamin wa timu ya Bodaboda Wilaya ya Ilala, akiudaka mpira katikati ya wachezaji wa timu ya Jambo Leo ‘Wagumu Stars’ Zahoro Mlanzi (kushoto) na Ali Salum wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam. Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa. Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
 Moja ya kizazaa langoni mwa Bodaboda FC iliyosababishwa na washambuliaji wa Jambo Leo
 Mshambuliaji wa timu ya Gazeti la Jambo Leo, Ali Salum (katikati) akifunga bao la kwanza dhidi ya Bodaboda FC,wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika tamasha hilo alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa.Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
 
Slaa akiwasalimia wachezaji wa timu hizo mbili

SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI BINAFSI KWENYE SEKTA YA UCHUKUZI

uc1
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2015/2016 bungeni mjini Dodoma leo.
uc2
 Mbunge wa Kisarawe (CCM) Bw. Suleiman Jafo akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya uchukuzi leo bungeni mjini Dodoma.
…………………………………………………………….
Na Fatma Salum – Maelezo
Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imesema inakaribisha wawekezaji binafsi kwenye miradi mbalimbali ili kuboresha sekta za uchukuzi na hali ya hewa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge zilizowasilishwa kwenye mjadala wa bajeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma.
“Serikali inawakaribisha wawekezaji binafsi kuwekeza kwenye miradi ya kuboresha miundombinu ya uchukuzi na hali ya hewa kwa kuwa Serikali peke yake haiwezi kukamilisha miradi yote bila ya ushirikiano na wengine”
Dkt. Tizeba alisema Serikali ina mipango madhubuti ya kuboresha miundombinu nchini ikiwemo reli, bandari na barabara na kupitia dhana ya ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (Public Private Partnership) itaweza kufanikisha mipango hiyo kwa ufanisi na kwa wakati.
Aidha Dkt. Tizeba aliongeza kuwa kupitia juhudi za Serikali baadhi ya miradi ipo katika hatua za awali ikiwemo uboreshaji wa viwanja vya ndege 11 kwenye mikoa mbalimbali nchini ambapo wataalamu wameshafanya upembuzi yakinifu (Feasibility Study) na fedha zikipatikana vitafanyiwa matengenezo mara moja.
Akizungumzia upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Dkt. Tizeba alibainisha kuwa taratibu za kumpata mzabuni zinaendelea na akipatikana ujenzi wa gati namba 13 na 14 za bandari hiyo utaanza.
Leo Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta aliwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2015/2016 ambapo bunge lilikubali kupitisha zaidi ya shilingi bilioni 452.9.

MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UDIWANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA SONGEA MKOANI RUVUMA

Mwandishi wa Habari mwandamizi Bi. Celesencia Kapinga akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakata alipotangaza nia ya kugombea udiwani kata ya NDILIMALITEMBO Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa pamoja na Mwandishi wa Habari wa gazeti la Majira ambaye ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilimalitembo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) . Habari na picha na Demasho.com.
……………………………………………………..
WAKATI watu mbalimbali wameanza kujitokeza
kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia vyama vya siasa
mwandishi wa habari  Mwandamizi,  Mkoani
Cresensia Kapinga ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Ndilima
litembo manispaa ya Songea  Ruvuma.
 
Mwandishi huyo ametangaza nia yeke ya
kuwania nafasi ya udiwani  mbele ya
waandishi wa habari  kwenye ofisi za
chama cha waandishi wa habari  Mkoa wa
Ruvuma  zilizopo mtaa soko kuu
mkoani  humo.
Amesema kuwa  kabla ya kutangaza nia amejipima na kujiona
anaweza kuongoza kata baada ya kuwa
aligombea nafasi hiyo kupitia viti masalumu mwaka 2010 ambapo kura
hazikutosha.
 
Akijibu masawali mbalimbali ya Waandishi wa
habari amesema kuwa ameamua kugombea nafasi hiyo baaada ya kuona Changamoto
mbalimbali zinazowakabaili Wananchi Katika Kata hiyo iliyokonje kidogo ya
Manispaa  ya songea hazijafanyiwa kazi. 
 
‘Ziko Changamoto nyingi zinazowakabili
Wananchi  wa Kata ya Ndilimalitembo bado
hazijafanyiwa kazi,baadhi zikiwa ni Ukosefu wa Zahanati,Shule kukosa Vyoo na
Wananchi kukosa soko la uhakika la kuuza mazao yao ambazo naamini  nikipata
nafasi ya kuwa Mwakilishi wao nitazishughulikia’anasema Bi. Cresensia
Kapinga.
 
Anasema kuwa kuwa kutokana na  na taaluma yake ya uandishi wa habari ana
uwezo wa kuingia Ofisi yoyote katika Manispaa ya Songea  na kuwasemea Wananchi wa  Kata hiyo hivyo anasema ni fursa  pekee ya Wananchi hao kumpa Fursa ya kuongoza
Kata hiyo.
Kwa upande wa Waandishi wa habari amesema
kuwa  kwa kuwa yeye ni Mwanahabari
atajitahidi kuwasema kwenye Baraza la
Madiwani  akiamini yapo mambo
mengi yanashindwa kushughulikiwa ikiwemo posho zao.
 
Kwa upande wao Waandishi wa Habari
wamepongeza hatua hiyo  na kutaka
Waandishi wengine wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa
Waandishi wamekuwa  wakinadi watu wengine
wakati wapo baadhi yao wana uwezo wa kuongoza.
Mmmoja wa Waandishi hao Julius Konala
anasema hatua hiyo ni ya kupongeza sana kwa kuwa imefunguia njia kwa Wanahabari
wengine kugombea zaidi  na kuwata
Wananchi  na Wanaccm kumuunga mkono  katika
azma yake ya kutaka kuwa  Diwani
wa Kata ya Ndilimalitembo.

EDINORI LINGERIE NA MALI MPYA

unnamed (3)
Duka kubwa Na kisasa underwear Na bra za kisasa kwa kina mama Na kina Dada limefunguliwa mizigo mpya kabisa kutoka uingereza , uturuki Na Italy. Karibuni sana bei ni nafuu sana .duka Lipo tabata bima kwenye Fremu mpya juu ya duka la Hussein pamba Kali. Karibuni nyooote karibuni sana.

KAMATI YA UTENDAJI YA COASTAL UNION KUHUSU KUWAACHA WACHEZAJI WALIOMALIZA MIKATABA YAO NA WENGINE KUENDELEA KUBAKI.

download (3)NA MWANDISHI WETU,TANGA.
Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Coastal Union ambacho kimeketi
katikati ya wiki hii chini ya Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union,
Steven Mguto kimeazimia kuwaacha baadhi ya wachezaji ambao muda wao
ulikuwa umemalizika huku wengine wakiongezewa mikataba ya kuendelea
kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.
Kimsingi wachezaji hao wameachwa na sasa wapo huru kutumikia timu
nyengine ambazo zitahitaji huduma zao
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa Coastal
Union,Oscar Assenga amesema
kuwa maamuzi hayo yalifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya
klabu hiyo ambacho kilifanyika juzi mkoani hapa.
Amesema kuwa kimsingi katika kikao hicho kiliridhia kuwaacha wachezaji
waliomaliza mikataba yao ikiwemo Shabani Kado,Keneth Masumbuko,Yayo
Kato Lutimba, Seleimani Kibuta,Bakari,Razack Khalfani,Itubu Imbem na
Othumani Tamimu.
Aidha amesema kuwa wachezaji wengine ambao klabu imeamua kuwaacha ni
Hussein Sued, Mansour Alawi, Amani Juma, Mohamedi Mtindi na Mohamed
Hassani.
Hata hivyo amesema wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao ambao klabu
ipo kwenye mazungumzo nao kwa ajili ya msimu ujao ni Bakari Mtama,Rama
Salim, Godfrey Wambura na Joseph Mahundi.
Wakati huo huo, uongozi wa Coastal Union umewapandisha timu wachezaji
wanne kutoka timu ya vijana kucheza timu ya wakubwa ambao ni Mtenje
Albano, Tumaini Karim, Mohamed Twaha Shekue “Djong”, Fikirini
Suleiman“Mapara”

CITY LOUNGE – CATERING & EVENT PLANNING

unnamed (2)

MH. LOWASSA KUANZA “SAFARI YA MATUMAINI” MCHANA WA LEO

Gari iliyombeba Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid, jijini Arusha mapema leo asubuhi wakati akielekea kwenye Ofisi za CCM Mkoa. Mh. Lowassa anatarajia kulihutubia taifa mchana wa leo kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid, ikiwa ni sehmu ya kutangaza kwake nia yake ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha.Kulia ni Mkewe Mama Regina Lowassa.
Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.
Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole (hayupo pichani).

CCM WASHINDA NAFASI YA UENYEKITI MJI MDOGO WA HIMO.

Msimamizi wa Uchaguzi na mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akizungumza wakati wa
kutangaza matokeo katika uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti wa mji mdogo
wa Himo.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika
uchaguzi huo kutoka vyama mbalimbali vya siasa.
Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himo Hussein
Jamal akizungumzamara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo
katika uchaguzi huo uliofanyika katika shule ya walemavu wa usikivu
eneo la njia Panda.
Baadhi ya viongozi waliofika kushuhudia
Uchaguzi huo.
Mkurugenzi wa wilaya ya Moshi,Fulgence
Mponji akitoa ufafanuzi katika uchaguzi huo.
Baadhi ya madiwani walioshiriki uchaguzi
huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya
Moshi,Moris Makoi akisalimia mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi
huo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga
akizungumza wakati wa kufunga kikao cha uchaguzi huo.
Dc Makunga akipeana mkono na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Moris Makoi mara baada ya kuzungumza
katika uchaguzi huo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya
Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

MRATIBU MKAZI WA UN NCHINI NA WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI WATEMBELEA ENEO LA MAPOKEZI YA MUDA KWA WAKIMBIZI MJINI KIGOMA

IMG_0495Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) akiongozana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa tatu kushot0) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya huduma za Wakimbizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke (katikati), Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kulia), Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kulia) mara tu baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma, eneo ambalo Wakimbizi wanapokelewa na kupewa huduma ya kwanza kabla ya kuelekea katika eneo maalum ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
……………………………………………………………………
Na Modewjiblog team
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe katikati ya wiki wametembelea eneo la mapokezi ya Wakimbizi kutoka Burundi lililopo katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Walipofika katika eneo hilo la mapokezi waliojionea huduma mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Shirika la Kimataifa Ia Uhamiaji (I.O.M), Shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chakula duniani (WFP), Shirika la afya duniani (WHO) pamoja na Shirika la UNFPA linaloshughulikia mahitaji ya wanawake hasa wale waliokuwa wajawazito.
Wakimbizi wengi waliofika eneo hilo walikuwa na afya dhoofu kutokana na kusafiri kwa umbali mrefu.
Kutokana na hali hiyo baadhi yao ilibidi wapatiwe huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya makazi yaliyotengwa kwa Wakimbizi ikiwemo kambi ya Nyarugusu iliyopo katika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Hata hivyo kambi hiyo ya Nyarugusu ina uwezo wa kuchukua sio zaidi ya Wakimbizi 50,000 lakini sasa ina Wakimbizi zaidi ya 48,000 kutoka Burundi na 60,000 kutoka Jamuhuri ya watu wa Congo.
Aidha Waziri Chikawe alisema kuwa Serikali imetenga eneo maalum ambalo litajengwa kambi mpya itakayojulikana kama Nyarugusu B ambayo itakuwa ni mahususi kwa Wakimbizi kutoka Burundi.
Mh. Chikawe alisema kuwa kambi hiyo itakamilika ndani ya miezi mitatu kutoka hivi sasa, ili kuwatenganisha Wakimbizi kutoka Congo na Burundi.
IMG_0457Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akizungumza na wafanyakazi wa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaoandikisha Wakimbizi wanaowasili kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kabla ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0468Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Kasulu, Kigoma, Amah Assiama-Hillgartner (kushoto) akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa tatu kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wa pili kushoto) walipotembelea uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0504Mmoja wa watoa huduma kwenye kituo cha muda cha Wakimbizi katika viwanja vya Lake Tanganyika akipuliza dawa ya kuua wadudu kwenye mifereji inayozunguka uwanja huo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ya milipuko ikiwemo Kipindupindu.
IMG_0512Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi waliokuwa kwenye foleni ya kupanda mabasi kuelekea kambi ya Nyarugusu kwenye makazi maalum yaliyotengwa na Serikali ya Tanzania yanayohudumiwa na Shirika linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengi ya Umoja wa mataifa. Wanne kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
IMG_0440Foleni ya Wakimbizi kutoka Burundi kuelekea kwenye mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la IOM kuwapeleka kwenye eneo maalum la kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0524Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kulia) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakishuhudia baadhi ya Wakimbizi wakipakia kwenye mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la IOM tayari kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.
IMG_0525
IMG_0544
IMG_0550Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (aliyeipa mgongo kamera kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe (wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakiagana na baadhi ya Wakimbizi wanaoelekea kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma kutokea katika kituo cha muda cha mapokezi na huduma za afya kilichopo katika viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0475Baadhi ya wakina mama na watoto zao wakiwa wamejipumzisha ndani ya viwanja vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0523Wahudumu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wakiwapulizia dawa maalum kwenye mikono na miguu kwa ajili ya kuua bakteria kabla ya kuingia ndani ya mabasi na kuelekea katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0531
IMG_0536
IMG_0563Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) wakielekea kutembelea mabanda mbalimbali ya huduma za afya yaliyopo kwenye viwanja vya Lake Tanganyika yanayotoa huduma kwa Wakimbizi wanaowasili kabla ya kupekwa kambini.
IMG_0559Pichani juu ni baadhi ya watoto wakipatiwa matibabu ndani ya kituo cha muda kabla ya kuelekea kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0568Wazazi na watoto wakiwa kwenye hema maalum, huku nwengine wakiwa kwenye dripu za kuongezewa maji mwilini.
IMG_0558
IMG_0569Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari wakisafisha mikono yao na kupuliziwa dawa maalum katika viatu mara baada ya kutembelea mahema yenye wagonjwa mbalimbali Wakimbizi kutoka Burundi wanaopatiwa matibabu kwenye kituo cha muda kilichopo kwenye viwanja vya Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0578Baadhi ya watoto wakijiliwa na kujifaraji kwa kucheza mpira katika kituo maalum cha kupokelea Wakimbi wanaotafuta hifadhi nchini Tanzania wakitokea nchini Burundi katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
IMG_0581Pichani juu na chini ni familia za Wakimbi wakiwa wamejipumzisha kwenye kituo cha muda katika viwanja vya Lake Tanganyika huku wakisubiri safari ya kuelekea katika kambi ya Nyarugusi iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
IMG_0583
IMG_0500Sehemu ya eneo la uwanja wa Lake Tanganyika.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI NIGERIA

NI1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania wanaoishi Nchini Nigeria katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Abuja Nigeria leo May 29,2015.
NI2
Baadhi ya Watanzania wanaoishi Nchini Nigeria wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akizungumza nao leo May 29,2015  katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Abuja Nigeria leo May 30,2015.
NI3
Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Mhe. Danniel Ole Njolai akimkabidhi zawadi ya saa iliyotolewa na Watanzania wanaoishi Nchini Nigeria Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, baada ya kuzungumza na Watanzania hao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Abuja Nigeria leo May 29,2015.
NI4
NI5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Nchini Nigeria Baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Abuja Nigeria leo May 29,2015. (Picha na OMR)
NI6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Nchini Nigeria Baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Abuja Nigeria leo May 29,2015. (Picha na OMR)

MWENGE WA UHURU WAKIMBIZWA WILAYA YA KINONDONI MKUU WA WILAYA ATANGAZA AJIRA YA PAPO KWA PAPO

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa ameubeba mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda baada ya kumaliza mbio zake wilayani humo Dar es Salaam leo leo asubuhi. Mwenge huo ulianza mbio zake Wilaya ya Ilala na kuzindua miradi mbalimbali.
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum (kulia), akisalimia na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda.
 Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kinondoni wakiwa wamejipanga foleni wakisubiri kuupokea mwenge wa Uhuru kabla ya kuanza mbio zake wilayani humo.
 Wakimbiza mwenge kitaifa.
 Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
  Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ya mradi wa maji Mburahati Barafu na Kisiwani uliofadhiliwa na Jumuia ya Ulaya, Serikali ya Ubelgiji na Serikali ya Tanzania  wakati wa ukimbizaji wa mwenge huo Wilaya ya Kinondoni humo.
  Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ya baabara tatu katika Shule ya Sekondari ya Makulumla. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Beatrice Mhina.
 Mwanafunzi Noel Mwita wa Shule ya Sekondari ya Makulumla, akiekeza namna ya kuchanganya madawa wakati kiongozi huyo wa mwenge, Juma Chum (wa nne kushoto), alipoweka jiwe la msingi za maabara katika shule hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Beatrice Mhina, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
 Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.
  Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.
 Wananchi wa Mburahati wakiupokea mwenge huo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika eneo hilo.
 Vijana wa hamasa wakipamba hafla hiyo kwa kuonesha matukio mbalimbali.
 Mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoacha matumzizi ya dawa ya kulevya mbe ya Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kituo cha vijana walioathiriwa na dawa hizo katika Hospitali ya Mwananyamala.
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum, akimkabidhi Amina Mshana chandarua kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Wakimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa,  Delina Simfukwe (kushoto) na Bakia Abdallah wakiteta jambo na mwanamuziki RehemaChalamila ‘Ray C baada ya kutoa ushuhuda kuhusu matumizi ya dawa za kulevya.
…………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ametoa ajira ya moja kwa moja kwa kijana Yusuf Mzitto mtaalamu wa masuala ya kompyuta ambaye alikuwa ameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya  wa wilaya hiyo.
Makonda alitoa ajira kwa kijana huyo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu. Juma Khatibu Mchum wakati wa uzinduzi wa kituo cha vijana walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya kilichozinduliwa na kiongozi huyo wa mbio za mwenge katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi.
“Kijana huyu mwenye elimu ya juu ya masuala ya kompyuta alikuwa ameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya hivyo baada ya kuacha kutumia dawa hizo tumempa ajira katika ofisi yangu ili aweze kufanyakazi badala ya ujuzi wake kupotea bure” alisema Makonda.
Makonda alisema kuwa katika kuwawezesha vijana walioathiriwa na dawa hizo wamepatana na viongozi wa manispaa hiyo kuwa kila kampuni inayofanya shughuli za kijamii katika wilaya hiyo ili iweze kupata tenda ya kufanya kazi yoyote ni lazima itoe mchanganuo  kwanza wa utoaji wa nafasi ya ajira kwa vijana wa wilaya hiyo.
Alisema wamechukua hatua hiyo ili kutoa fursa ya ajira kwa vijana waliohamua kuachana na matumzi ya dawa za kulevya ambao hawana kazi hivyo kupitia  kakampuni hizo ziweze kuwasaidia vijana hao baada ya kupatiwa tenda na manispaa hiyo.
Alisema ili kuunga jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kupambana na uingizaji wa dawa za kulevya ameanzisha mpango wa kukutana mara moja kila mwezi na vijana walioathiriwa na dawa hizo ili kubadilishana mawazo badala ya kuwatenga.
Makonda alisema vijana hao wengi wao ni wataalamu wa masula mbalimbali akimtolea mfano kijana aliyepewa ajira katika ofisi yake ambaye atawasaidia katika mambo mengine.
Akizungumzia mbio za mwenge katika wilaya yake kwa mwaka huu alisema umezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi saba yenye jumla ya sh.5,079,153,972 ambapo kati ya fedha hizo sh.14,802,200 ni fedha kutoka serikali kuu, sh.2,672,992 kutoka katika Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, sh.913,800,780 ni mchango wa wahisani na sh.1,477,978,000 ni michango ya wananchi.
Alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa maji, ujenzi wa barabara, ujenzi wa baabara, ujenzi wa shule za Sekondari, ujenzi wa jengo la wazazi, ujenzi wa ofisi ya Kata na ujenzi wa nyumba ya walimu.
Alisema mwenge huo ulipata fursa ya kukagua miradi endelevu wa ugawaji wa vyandarua, mradi wa wanawake wajasiriamali, mradi wa vijana wajasiriamali watunzaji wa mazingira na mradi wa huduma za ukimwi.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Juma Khatibu Chum aliwataka watanzania wote bila ya kujali itikadi za vyama vyao kudumisha amani na utulivu wa nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.
Alisema amani ya nchi tusipo kuwa makini inaweza kuharibiwa kwa siku moja wakati imetafutwa kwa miaka mingi na aliwata vijana kuacha kutumia dawa za kulevya na kujikinga ma malaria ambayo yame kuwa yakiua watu wengi kuliko ukimwi. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

NEC YAKAMILISHA MAANDALIZI UBORESHWAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA KWA MIKOA 4

Maandalizi ugawaji wa mashine kwa ajili ya kuandikisha wanchi katika daftari la wapiga kura kwa Kanda ya 5 Tano kati ya Sita yamekamilika leo Mei 29, 2015 zaidi ya Biometric Voter Registration (BVR) zipatazo 1492 zinaanza kusambazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kuanzia mapema Alfajiri Kanda ya Tano ni Mikoa ya Mara, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA MAGEREZA KOZI NA. 27 CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA ZAFANA, MKOANI MBEYA

mag
Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani) leo Mei 29, 2015 katika Chuo cha Magereza, Kiwira Kilichopo Mkoani Mbeya.
mag1
Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani) leo Mei 29, 2015 katika Chuo cha Magereza, Kiwira Kilichopo Mkoani Mbeya.
mag2
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza leo Mei 29, 2015 Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya.
mag3
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akipokea Salaam ya heshima akiwa jukwaan kabla ya kukagua Gwaride Maalum katika sherehe za kufunga Mafunzo ya Uaskari Magereza, Kiwira Mbeya(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stanford Ntirundura.
mag4
Katibu Mkuu akikabidhi zawadi kwa Mhitimu wa Kozi Na. 27 ya Uaskari Magereza ambaye amefanya vizuri katika Somo la Gwaride na Ukakamavu Askari Mhitimu, Ezra Kapesa leo katika sherehe za kufunga Mafunzo hayo Mkoani Mbeya(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
mag5
Gadi ya Askari wa Kike ambao ni Wahitimu wa Kozi ya Awali ya Uaskari Magereza wakila Kiapo cha Utii kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi(hayupo pichani) katika sherehe za ufungaji Mafunzo hayo.
mag6
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akimuongoza Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(katikati) kuelekea kwenye Ukumbi wa Mihadhara kwa ajili ya kufunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza leo Mei 29, 2015(kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stanford Ntirundura.
mag7
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aweze kutoka hotuba ya kufunga rasmi Mafunzo ya Uaskari Magereza katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mkoani Mbeya(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

BONDIA FRANSIC CHEKA KUZIPIGA KESHO MAY 30 UKUMBI WA P.T.A SABASABA

Mabondia Francis Cheka kushoto na Kiatchai Singwancha wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa May 30 utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba 
PICHA NA SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Francis Cheka kushoto na Kiatchai Singwancha wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumamosi ya May 30 utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba 

Simbachawene aitaka Australia kuimarisha uwekezaji nchini

sim1
Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene (Kulia) akimkaribisha Naibu  Waziri Mkuu  ambaye pia ni Waziri wa Afya na Utalii kutoka  Australia Magharibi Kim Hames (kushoto) mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mikutano wa  Wizara  ya Nishati na Madini kabla ya kuanza kwa kikao. Hames alifanya ziara yenye lengo la  kubaini  fursa za uwekezaji nchini.
sim2
Naibu  Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Afya na Utalii kutoka  Australia Magharibi   Kim Hames (kushoto) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene (Kulia) maeneo ambayo  nchi ya  Australia ingependa kuwekeza.
cha2
Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene (Kulia) akimshukuru  Naibu  Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Afya na Utalii kutoka  Australia Magharibi Kim Hames (kushoto) mara baada ya kumkabidhi   zawadi. Wengine ni ujumbe  ulioambatana na Naibu Waziri Mkuu huyo.
cha3
Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene ( wa pili kutoka kulia) Naibu  Waziri Mkuu  ambaye pia ni Waziri wa Afya na Utalii kutoka  Australia Magharibi   Kim Hames ( wa tatu kutoka kulia) wakiwa  katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka  Australia  uliohudhuria kikao hicho.
…………………………………………………………………………………….
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini, George  Simbachawene  ameitaka nchi ya Australia  kuimarisha  uwekezaji   katika sekta za nishati na madini nchini  ili ziweze kuchangia  ukuaji wa uchumi wa nchi
Simbachawene aliyasema hayo katika  kikao chake na Naibu Waziri Mkuu wa Australia Magharibi,  Kim Hames na ujumbe wake  aliyemtembelea ofisini kwake kwa ajili  ya kupata  taarifa za maeneo yanayohitaji uwekezaji nchini.
 Alisema  uhusiano  kati ya  Tanzania na Australia ni wa muda mrefu, ambapo  Australia imekuwa  ikiwekeza nchini kupitia sekta ya  madini  kupitia makampuni yake  ya madini na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
Aliendelea kusema kuwa kupitia makampuni ya madini ya Australia, huduma za jamii kama vile miundombinu, elimu na afya zimeboreshwa.
Wakati huo huo Afisa Mtendaji kutoka   Wakala wa Jiolojia   Tanzania (GST) Prof. Abdulkarim Mruma  akielezea ushirikiano kati ya  wakala  huo na  Australia, alisema kuwa nchi ya  Australia kupitia chuo chake cha  Cuten ilishirikiana na GST katika kufanya utafiti wa madini katika ukanda wa  dhahabu  ulioko  kusini mwa Dodoma  uliopelekea kugundulika kwa madini ya  dhahabu na almasi.
Aliongeza kuwa kupitia utafiti wa  madini katika ukanda wa dhahabu  ulioko  Dodoma  watumishi wawili kutoka  wakala  huo walifanikiwa kupata shahada za uzamifu (PhD) katika Chuo Kikuu  cha Cuten.
Aliongeza kuwa, nchi ya Australia imekuwa ikitoa ufadhili kwa watumishi wake  kusomea katika musala ya  uchenjuaji madini na maabara katika ngazi za shahada na uzamifu.
Profesa Mruma aliiomba  nchi ya Australia kuendelea kusaidia Wakala huo  kwa vifaa vya kisasa vya jiofizikia na kemia  pamoja na mafunzo yanayohusu madini katika ngazi mbalimbali.
Naye Mkuu wa Chuo cha Madini, Sudian  Chiragwile aliongeza kuwa, chuo kilikabidhiwa mgodi wa  Resolute uliokuwa unamilikiwa na kampuni ya  Golden Pride ya Australia ambapo wamekuwa wakiutumia kwa ajili ya mafunzo ya  vitendo kwa wanafunzi.
Alisema mgodi  wa Resolute ulioachwa bado una eneo  kubwa linaloweza kuchimbwa madini na kuwataka  wawekezaji kutoka  Australia kujitokeza na kuwekeza kwenye  shughuli za madini.
Naibu  Waziri Mkuu wa Australia  ambaye pia ni Waziri wa Afya na Utalii kutoka  Australia  Kim Hames alisema kuwa, nchi ya  Australia ipo  tayari kushirikiana na  Tanzania katika  uwekezaji  hususan katika sekta za nishati na madini na kuongeza kuwa katika kuboresha sekta ya madini, kutakuwa na programu  za kubadilishana utaalam na uzoefu kwa wataalam kutoka  Tanzania na  Australia.
Hames alisisitiza kuwa Tanzania  imebarikiwa  kuwa na  rasilimali nyingi za madini na kuahidi kushirikiana  na  Serikali  ya  Tanzania katika kuinua  sekta ya madini nchini.

UMOJA WA WATANZANIA WALIOSOMA NCHINI AUSTRALIA WAZINDULIWA RASMI

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (aliyesimama) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) jijini Dar es Salaam leo. 
ha02
Waziri wa Afya na Utalii wa Australia Mh. Dkt. Kim Hames akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) jijini Dar es Salaam leo.
ha3
Baadhi ya Watanzania  waliosoma nchini Australia wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) leo jijini Dar es Salaam.
ha4
Baadhi ya Watanzania  waliosoma nchini Australia wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) leo jijini Dar es Salaam.
ha5
Rais wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) Bw. Francis Mhimbila akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
ha6
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza na waandishi  habari baada ya kuzindua Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) leo  jijini Dar es Salaam.

ZIARA YA MHESHIMIWA ALI HASSAN MWINYI JIJINI TEHRAN TAREHE 24 – 27 MEI 2015


ANDIKENI WOSIA KUEPUSHA MIGOGORO – WAZIRI MKUU

ta2
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza wakati alipozindua Uandishi wa Wosia katiak sherehe za miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wananwake (TAWLA0 kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015.Kushoto ni balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelaker.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania wote nchini wajenge tabia ya kuandika wosia ili kuondoa matatizo ya mirathi pindi mume anapoaga dunia
Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Mei 29, 2015) wakati akizindua kampeni ya kuandika wosia kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam
Akizungumza mara baada ya kushuhudia uandishi wa wosia mbele ya wakili, Waziri Mkuu alisema uandishi wa wosia ni suluhisho la migogoro mingi inayosababishwa na wanandigu ambao wakati mwingine wala hawakushiriki kuchuma mali wanayogombea
“Kuandika wosia siyo uchuro kama ambavyo watu wengi wanadhani… ninatoa kwa Watanzania kuandoak wosia mapema kwani inasaidia kuondoa matatizo ya mirathi baada ya mmoja wao kuondoka duniani,” alisema.
“Mtua anapaswa kutamka mali nilizonazo ni kadhaa na endapo nitakufa mali hii apewe fulani, na hii fulani na nyingine fulani. Hati hii inapaswa kutunzwa kwa mwanasheria, benki au kwa Kabidhi Wasii. Tusipolifanya hili, matatizo yataendelea kuwakumba wajane na watoto walioachwa na marehemu,” alisema.
Aliipongeza TAWLA kwa kuchukua jukumu la kuhamasisha umma kuhusu suala la uandishi wa wosia lakini pia akawataka wanachama wa TAWLA wajikite zaidi kwenye kutetea haki za makundi maalum kama walemavu wa ngozi, vikongwe na watu kutoka makabila madogodogo. “Haya makundi yana shida zao ambazo hazifanani na watu wengine. Nendeni vijijini, mkatoe elimu, jueni changamoto wanazokabiliana nazo, wasikilizeni shida zao na muone ni njia gani mnaweza kuwasaidia,” alisema.
Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema katika kipindi cha miaka nane kuanzia mwaka 2006 hadi 2014, jumla ya vikongwe 2,219 waliuawa katika mikoa ya Geita, Simiyu, Mara, Kagera na Mwanza ambayo alisema yote iko Kanda ya Ziwa. “Mauaji haya yanasababishwa na imani potofu za kishirikina; jamii kuwa na uelewa mdogo wa sheria; ukosefu wa imani za kiroho; ukosefu wa elimu; na waganga wa kienyeji kupiga ramli,” alisema.
Alisema makabila madogo yanakabiliwa na matatizo ya ardhi ambayo ndiyo tegemeo lao kuu, vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi wanatishiwa usalama wa maisha yao bila sababu yoyote. “Nendeni mkatoe elimu zaidi kwa watu hawa ili tuwalinde wazee wetu, makabila madogo kama Wahadzabe na Wasandawe pamoja na ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi,” alisisitiza.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa TAWLA, Bi. Aisha Bade alisema chama hicho kimetumia wanasheria wanawake zaidi ya 200 na wasaidizi wa kisheria 400 (paralegals) kutoa msaada wa kisheria kwa watu mbalimbali ambao hawana uwezo kumudu gharama za kesi.
“Katika mwaka 2014, tumetoa msaada wa kisheria kwa watu zaidi ya 10,000 ambao hawana uwezo kumudu gharama za kesi kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini,” aliongeza.
Naye Balozi wa Sweden nchini, Bw. Lennarth Hjelmaker, akizungumza kwa niaba ya wadau wa maendeleo nchini alisema Serikali ya nchi hiyo ilitenga kiasi cha sh. bilioni 4 kusaidia mpango wa miaka minne wa chama hicho wa kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na usawa wa kijinsia.
“Hadi sasa tumekwishatoa sh. bilioni 3.5 ambazo kati ya hizo, sh. bilioni 1.1 zimetumika kusaidia wanawake wapatiwe haki zao; sh. milioni 500 zimetumika kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya ili watoe huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana na sh. milioni 700 zimetumika kutoa mafunzo kwa viongozi wa ngazi ya chini wanaohusika kutoa maamuzi. Kiasi cha sh. bilioni 1.2 kimetumika kuendeleza shughuli za chama,” alifafanua.
Pamoja na kutoa elimu kwa jamii na kutetea haki za akinamama na wasichana, Balozi huyo wa Sweden alisema kuna haja ya kuweka mkazo ili kuwafikia wanaume na wavulana wengi zaidi ili waweze kujirekebisha na kubadili tabia na mitazamo yao dhidi ya wanawake na wasichana.

Maadhimisho ya SIKU YA AFRIKA yafanyika Washington DC

Balozi wa Misri nchini Marekani Mhe. Mohamed Tawfik akiongea kufungua sherehe ya African Union iliyofanyika siku ya Alhamisi May 28, 2015 katika hotel ya JW Marriott, Washington DC
Balozi wa Morocco nchini Marekani Mhe. Rashad Bouhlal akiongea machache.
Msemaji mkuu wa sherehe ya siku ya Afrika Mhe. Donald Tetelbaum.
Mchungaji Jesse Jackson akiongea kwenye sherehe ya siku ya Afrika.
Maureen Umeh mfanyakazi wa kituo cha luninga cha Fox News DC akisherehesha sherehe ya siku ya Afrika.
Mambalozi wa Afrika nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba.
Mkuu wa Utawala na Fedha mama Lily Munanka akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Githae.

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA WIZARA YA USHIRIKIANO AFRIKA MASHARIKI ZALENGA KUBORESHA UHUSIANO WA TANZANIA KIMATAIFA

be1
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Bernard Membe akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2015/2016 bungeni leo mjini Dodoma.
be2
Mabalozi wa Tanzania kwenye nchi mbalimbali duniani wakifuatilia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2015/2016 iliyowasilishwa leo bungeni mjini Dodoma.
be3
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Harrison Mwakyembe akimsikiliza kwa makini mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kushoto) nje ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma. Kulia ni mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. ShyRose Bhanji.
be4
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju (kulia) akisisitiza jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma jana.
be5
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kushoto) na Mhe. ShyRose Bhanji (kulia) mara baada ya kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2015/2016  leo bungeni mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA FATMA SALUM – MAELEZO

WANAHABARI MKOA WA IRINGA NA POLISI WAKUTANA KATIKA KIKAO CHA MAHUSIANO MEMA

Baadhi ya wanahabari  mkoa  wa Iringa  wakiwa katika picha  ya pamoja na viongozi  wa  jeshi la polisi mkoa wa Iringa mara baada ya  kumalizika  kikao  chao cha mahusiano mema na kutambulishana kati ya wanahabari na viongozi wapya wa  jeshi  la Polisi waliokaa ni kamanda wa polisi Ramadhan Mungi wa tatu  kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard na katibu wa IPC Francis Godwin na maofisa wengine wa polisi mkoa
Baadhi ya askari polisi wakiwa ktk kikao cha pamoja na wanahabari leo
Wanahabari Mkoa wa Iringa wakiwa ktk kikao cha pamoja na maofisa wa jeshi la Polisi
Wanahabari  wakiwa katika kikao na jeshi la polisi
Kamanda wa  polisi mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi akitoa mafunzo mafupi kwa  wanahabari kati ya utendaji kazi wa  jeshi la polisi na vyombo vya habari
 
 Na FGBLOG
Wanahabari wa mkoa wa Iringa
leo wamekutana na kamanda wa polisi na maofisa wa jeshi la polisi Mkoani
hapa ili kuendelea kufanya Kazi kwa ushirikiano kwa faida ya Mkoa wa
Iringa.
Katika kikao hicho kilichoambatana na semina fupi ya kukumbushana wajibu wa Kazi za wanahabari na askari.
Akitoa
mafunzo hayo kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amesema
kuwa ili kuufanya Mkoa wa Iringa uweze kufanikiwa ni lazima wabahabari
na polisi kufanya Kazi zao kwa kuzingatia maadili na kutofanya upendeleo
katika utendaji wao.
 
Mungi alisema kuwa mbali ya kazi kubwa ambazo vyombo vya habari mkoani hapa
vinafanywa bado jeshi lake limeamua kukutana na wanahabari hao ili
kizidi kuufanya Mkoa kuwa na taswira nzuri ktk mahusiano Kati ya pande
hizo mbili kama njia ya kuwatumikia wananchi.
 
Alisemakwa Mkoa wa Iringa vyombo vya habari vimeonyesha mchango mkubwa zaidi
zaidi na kutaka mchango huo na jitihada hizo kuendelea zaidi .
 
Kamanda Mungi amesema kuna haja ya wanahabari na askari polisi kuendelea
kujenga mahusiano kwa kukutana na viongozi wao kabla ya kufanya
mapambano yasiyo na tija.
 
Alisema kuwa wao kama jeshi la polisi wanatambua kuwa vyombo vya habari ni
muhimu kwa jamii hivyo lazima kujenga mahusiano mema na kuwa askari
polisi hawanasababu ya kuendeleza mivutano 
 
Alisema kuwa kuna wakati mwingine ajali imetokea na Kazi ya mwanahabari ni
kuhabarisha umma na polisi kuokoa hivyo lazima kufanya Kazi kwa karibu
na kutoa majibu stahiki kwa wanahabari na wanahabari kutotumia jazba
katika utendaji Kazi zao 
 
Akizungumza katika mafunzo hayo  mwenyekiti wa chama cha  waandishi  wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard  alisema  kuwa hatua ya  jeshi la polisi mkoa wa Iringa kuandaa kikao  hicho cha kufahamiana na mafunzo mafupi kwa wanahabari ni ya kupongezwa zaidi hasa kwa wakati  huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu .
 
Alisema  kuwa tofauti baina ya badhi ya askari na wanahabari  ilikuwa ikijitokeza kutokana na pande  hizo  mbili zinazofanya kazi za kijamii kutoatambuana vilivyo hivyo kila upande  kuonyesha chuki dhidi ya mwingine jambo ambalo halijengi bali hubomoa.
 
Leonard  alisema kikao  hicho  kina umuhimu mkubwa kwa wanahabari  hasa  wakati  huu  wa kuelekea  uchaguzi mkuu ambao baadhi ya askari  walikuwa  wakiwachukia wanahabari na  wanahabari  kuwachukia polisi hasa kutokana na matukio ya nyuma kabla ya Mungi  kuwa kamanda wa  polisi wa mkoa huo wa Iringa.
 
Katika  hatua  nyingine mwenyekiti  huyo aliomba  jeshi la polisi  kuwa  na utaratibu wa kukutana na  wanahabari japo kwa  mwezi mara moja  ili  kujitathimini  utendaji kazi wao na  pale  penye tofauti  basi  kuweza kuzimaliza kwa njia  sahihi kuliko kila mmoja kutumia nguvu zisizo na tija.

MAHAFALI YA KWANZA YA CHUO CHA UALIMU RUNGEMBA MUFINDI


Baadhi ya  wanahabari  wakiwa katika picha ya pamoja na mhitimu katika mahafali  hiyo kutoka kushoto ni Neema Msafiri , Flora Kamaghe na kulia ni Clement Sanga
Kamati ya mandalizi ya  mahafali  hiyo
Viogozi  mbali mbali  wakiwa katika chuo  hicho mara baada ya mahafali
  Mgeni  rasmi katika mahafali ya kwanza  ya  chuo cha ualimu  Rungemba
wilayani Mufindi mkoani Iringa Bw Exaud Kigahe kutoka  wizara  ya
viwanda na biashara makao makuu (  wa nane kutoka  kulia) akiwa fuatiwa
na mkurugenzi wa chuo hicho Askofu Mulilege  Mkombo pamoja na viongozi
wengine wa  chuo  hicho serikali na  chama tawala wakati wakiwa katika
picha ya pamoja na  wahitimu hao
 ………………………………………………………………………………………………………………..
        Na FGBLOG
KATIKA
kuhakikisha watoto  wanaotoka katika familia  na uwezo  wakiwemo yatima
,kanisa la House of Prayer shield of Faith Cristian Fellowship Church
(HOPS) lenye makao makuu yake mkoani Dar es Salaam  limeanzisha chuo cha
ualimu kitakachotoamafunzo ya  ualimu kwa gharama nafuu kwa  wanafunzi
wake kama njia ya  kutekeleza mpango wake  wa  elimu kwanza.
 
MKurugenzi
mkuu  wa  chuo  hicho askofu Mulilege  Mkombo aliyasema hayo jana
wakati  wa mahafali ya  kwanza  ya  chuo  hicho yaliyofanyika katika
viwanja  vya  chuo cha  Ualimu Rungemba wilaya  Mufindi  mkoani Iringa .
Alisema
kuwa hatua  ya  kanisa lake  kuanzisha utaratibu  wa kujenga chuo
hicho na shule  mbai mbali za Sekondari  nchini  ni  kuisaidia  serikali
katika kusaidia  familia  maskini na  yatima  kuweza  kunufaika na
elimu ya gharama nafuu  kama  njia  ya kupunguza ujinga miongoni mwa
jamii ya  kitanzania hasa  ile  isiyo na uwezo  wa kusoma katika shule
za  sekondari na vyuo ambavyo ada yake ni  kubwa .
Nilipewa maoni ya  kuanzisha  chuo  hicho na Mungu  na Waumini  wa
kanisa na  HOPS kwa  kutambua umuhimu  wa  elimu waliweza  kujitolea
michango  yao mbali mbali ya kuanzisha  ujenzi  wa  chuo   hicho na
mwaka 2013 chuo  hicho  kilianzishwa kwa  kuwa na wanafunzi 8 pekee ila
kwa  sasa ni  wanafunzi 43 ndio  walioweza  kuhitimu kwa mwaka wa kwanza
katika  chuo hicho….Yesu Kristo alinielekeza niwahudumie watu katika
Afya  na Elimu ” alisema askafu Mkombo
Kuwa moja kati ya kazi  kubwa  za kanisa  hilo ni kuwafanya  watu  wote
wamjue Mungu na  kuwarudisha  vijana waliovamiwa na nguvu  za giza
katika maisha yanayompendeza  Mungu , kuwaponya walioathirika na
utumiaji  wa madawa ya kulevya ,kuzuia mauwaji ya kikatili na ugaidi
ili  kumrudisha mwanadamu katika utu  wa haki na kweli ,kurekebisha
maadili yaliyoporomoka na kuwa huduma  hizo  zinatolewa kwa watu  wote
bila kujali imani  zao ,
 
AskofuMkombo alisema katika  huduma za  kijami lengo la kanisa  hilo ni
kuendelea  kujenga shule  za msingi ,sekondari na vyuo pamoja na
kusaidia  kuanzisha Zahanati katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
 
Hata hivyo  alisema  kuwa sababu  kubwa ya  kutoa elimu kwa ada  ndogo ni
moja kati ya mkakati wa kanisa hilo katika kuthamini sekta ya  elimu na
kuamini  kuwa elimu ndio  dira  peke ya  mtanzania huku  likiamini  kuwa
uwekezaji muhimu ni katika  sekta ya  elimu  na  sio mijini pekee bali
hata vijijini ambako siku zote  wamekosa fursa 
 
Akielezea
mkakati  wa wilaya ya  Mufindi katika  eneo hilo la chuo cha ualimu
Rungemba alisema ni kuona  eneo hilo linajengwa shule ya msingi na
sekondari kwa ajili ya mazoezi kwa  wanafunzi wa  chuo   hicho ambacho
kwa sasa kinatoa mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya cheti ,Diploma peke
japo  baadae ni kujenga majengo  zaidi kwa ajili ya kuanza  kutoa Digrii
ya kwanza na ya pili na kuwa  waumini  wapo tayari  kujenga majengo
hayo  ila  wanasubiri  serikali ya  kijiji  kuwaongezea eneo la ardhi
zaidi.
Pia askofu Mkombo alisema kuwa malengo ya kanisa ni kuona kila wilaya na
mkoa wa Tanzania wanajenga  shule ,chuo ,zahanati au  Hospitali  ili
kila mtanzania  aweze  kupata elimu na huduma za afya kwa gharama nafuu
zaidi .
Alisemakuwa moja kati ya changamoto katika  chuo  hicho ni  wanachuo badhi
kupata  shida ya malazi  kutokana na uchache wa mabweni ,pia  nyumba
za  walimu  pia  kukosekana kwa Hospitali ama  zahanati katika kijiji
hicho  cha Rungemba .
 
Akizungumzakatika mahafali  yao  mgeni  rasmi Bw Exaud kigahe kutoka  wizara ya
viwanda  mbali ya  kupongeza  kanisa  hilo kwa kuanzisha  chuo  hicho
katika  wilaya ya Mufindi bado  alisema akiwa kama mdau wa elimu katika
wilaya ya  Mufindi ataungana mkono  na jitihada za  kanisa  hilo katika
kukiendeleza  chuo  hicho na kuchangia kiasi cha Tsh milioni 1 kwa
ajili ya kusaidia ujenzi  wa mabweni .
 
Bw Kigahe  alisema  kuwa yeye ni mkazi wa kijiji cha Nundwe wilaya ya
Mufindi ila amesikitishwa  zaidi  katika  zoezi la uandikishwaji katika
daftari la kudumu la wapiga  kura   kuona  sehemu  kubwa ya  vijana
ambao  wapo chini ya miaka 40  kushindwa  kujua kusoma na kuandika
katika  wilaya  hiyo ya  Mufindi na  kutaka   chuo  hicho  kuendelea
kutoa furasa  zaidi kwa wilaya  hiyo .
 

PINDA AHUTUBIA SHEREHE ZA MIAKA 25 WA TAWLA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi Mwanaidi Maajar baada ya kuhutubia katika sherehe za siku ya Wanasheria Wananwakde Tanzania Tawla , kwenye viwanja vya  Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ta4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) baada ya kuhutubia katika sherehe za miaka 25 ya chama hicho kwenye viwanja vya  Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015. Aliyekaa wapili kulia ni balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelaker.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ta2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza wakati alipozindua Uandishi wa Wosia katiak sherehe za miaka 25 ya Chama cha Wanasheria Wananwake (TAWLA0 kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Mei 30, 2015.Kushoto ni balozi wa Sweden nchini, Lennarth Hjelaker.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA KUAPISHWA RAIS WA NIGERIA LEO

bi1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiteremka kwenye Ndege walipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Asha Bilal, wakiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na mtoto Ernest Nkayala alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea shada la maua kutoka kwa Mtoto Elin Mwandobo alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
bi6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ngoma za kabila la Kinigeria alipowasili Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nnamdi Azikiwe Abuja kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Mohammadu Buhari iliyofanyika leo May 29,2015 katika Uwanja wa Ego Squar mjini Abuja Nigeria.
(Picha na OMR)

ASILIMIA 42% YA WATOTO WAMEDUMAA TANZANIA

download (1)
Na Gladness Mushi ,Arusha
Asilimia 42 ya watoto wamedumaa nchini Tanzania hali inayosababishwa
na kukosekana kwa lishe bora yenye virutubisho hivyo hivyo kusababisha
udumavu na kuathiri afya ya akili.
Profesa Joyce Kinabo wa Chuo Kikuu cha Sokoine kilichopo mkoani
Morogoro amesema kuwa kukosekana kwa lishe bora kumekua kukiathiri
maendeleo ya taaluma kwa watoto na kuzorotesha maendeleo ya jamii kwa
ujumla.
Joyce akizungumza katika mkutano wa wa masuala ya Lishe uliondaliwa na
taasisi ya kimataifa ya chakula na lishe (FANUS), uliofanyika jijini
Arusha amesema kuwa kati ya watoto 100 watoto 42 wanakabiliwa na
tatizo la udumavu hivyo ameitaka jamii na serikali kutilia mkazo suala
la lishe bora na virutubisho ili kuondokana na tatizo hilo.
“Serikali na watunga sera wanapaswa kutambua uhusiano ulioko kati ya
lishe bora na maendeleo ya taifa,elimu ya lishe na virutubisho itolewe
kuanzia ngazi ya familia,jamii hadi kitaifa na pia mashuleni somo la
lishe lirudishwe ili kuchochea ustawi bora wa jamii na taifa” Alisema
Joyce
Amesema kuwa jamii ya wafugaji hususani wamasai wanakabiliwa na tatizo
la udumavu ,ukondefu na upungufu wa damu mwilini kwa kukosa kutumia
mboga mboga na matunda na vyakula vingine  kwani jamii hiyo hupendelea
maziwa na nyama.
“Asilimia 16% wana kimo kisicholingana na umri wao yote haya
yanasababishwa na lishe duni kwa baadhi ya watu” Alisema Profesa
Profesa Tola Atinmo wa chuo kikuu cha Ibadan nchini Nigeria kitengo
cha Virutubisho vya binadamu amesema kuwa haki ya kupata lishe na
virutubisho ni haki ya msingi ya kila binadamu kama ilivyoainishwa
kwenye mkataba wa haki za binadamu wa kimataifa wa mwaka 1948.
Ameishauri serikali kuhakikisha kuwa inaboresha masuala ya lishe,afya
na usalama wa chakula kwa raia wake .
Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa mkutano huo
unatoa fursa kwa wataalamu wa masuala ya lishe nchini na viongozi
kujifunza masuala hayo muhimu katika maendeleo ya jamii.

Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati- Mhe William Lukuvi

1
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali mkoani Tabora leo kuhusiana na masuala yanayohusu sekta ya ardhi mkoani humo katika ukumbni wa mikutano wa Isike. Kulia ni mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua
4
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi akizungumza na Wananchi wa Eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora, kuhusiana na mgogoro wa Ardhi unaowakabili wananchi hao ambao unaotokana na Manisapaa kutowalipa fidia ya maeneo yao.
5
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh Suleiman Kumchaya akijadiliana jambo wakati Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh William Lukuvu alipotembelea eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora kusikiliza matatizo ya Ardhi yanayo wakabili wananchi wa eneo hilo leo.
……………………………………………………………
Na Clarence Nanyaro
Kuanzia mwaka ujao wa fedha,serikali itapunguza gharama mbalimbali za upimaji ardhi kwa zaidi ya nusu ili kuwezesha wananchi wengi kupima maeneo yao na kupata hati miliki ili kupunguza migogoro ya ardhi ambayo imekithiri hapa nchini.
Akizungumza na watendaji wa sekta mbalimbali wa mkoa wa Tabora,Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mh William Lukuvi alisema Wizara itapunguza kwa zaidi ya nusu gharama za upimaji ardhi ili kila mwananchi aweze kupima eneo lake na kupata hati suala ambalo litapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa inatokea.
Aidha Mh Lukuvi aliongeza kuwa sambamba na kupunguza migogoro ya ardhi, serikali pia itaweza kukusanya bkwa wingi kodi ya pango la ardhi na hivyo kuongeza mapato amabayo yataisiaidia serikali katika kufanikisha shughuli za maendeleo.
Hata hivyo pamoja na kupunguza gharama hizo Wazrizi Lukuvi aliwaonya Maafisa ardhi,kuacha tabia ya kuendesha shughuli za serikali kwa kukiuka taratibu,akitolea mfano wa maafisa hao kupima viwanja juu ya viwanja suala ambalo limekuwa linaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi.
“Maafisa ardhi lazima wafanye kazi kwa kuzingatia taratibu ili kuepusha migogoro ambayo inatokea miongoni mwa wananchi na kuwasababisha kuichukia serikali yao” alisema Mh Lukuvi na kuongeza kuwa atakayebainika kukiuka taratibu atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu.
Waziri Lukuvi yuko mkoani Tabora kwa shughuli za kikazi,ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa anatafuta suluhu ya migogoro ya ardhi katika manispaa ya Tabora ambapo alikutana na wananchi wa maeneo ya Malabi,Uledi,Malolo na Kizigo ambako kumekuwa na migogoro ya ardhi kutokana na baadhi ya wananchi wa maeneo hayo kutolipwa fidia baada ya Manispaa ya Tabora kupima viwanja katika maeneo hayo.
Akiwa katika eneo la Malabi,Waziri Lukuvi aliiagiza Manispaa ya Tabora kupima upya eneo hilo na kulipatia kanisa la African Inland Church (AIC) ekari kumi na ekari 28 zipimwe kwa ajili ya Wananchi ili kumaliza mgogoro huo na kmujongeza kuwa kila atayepata hati lazima ahakikishe kuwa analipa kodi ya pango la ardhi.
Awali,Katibu tawala wa mkoa wa Tabora Bi Kudra Mwinyimvua aliweleza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa kwa sasa Mkoa wa Tabora ndio wenyewe eneo kubwa na hivyo juhudi na nguvu kubwa inatakiwa ili kupima maeneo mengi kuepusha migogor ya ardhi. Tayari Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeidhinisha shilingi milioni 142 kusaidia manispaa ya Tabora kupima maeneo yake.

No comments:

Post a Comment