Christian Gaya, Majira Aprili 28, 2015
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Bi Fatma Ali Makame akiwa na mtoto
wake mafao ya uzazi baada ya kuufungua mkutano wa kwanza wa Wadau wa ZSSF wa
siku mbili katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja (katikati) Mwenyekiti
wa Bodi ya ZSSF Dkt,Suleiman Rashid.
Kutokana
na kanuni na haki za uzazi na utaratibu wa shirika la kazi duniani (ILO) lengo
la kubwa la kuwa na fao la uzazi ni kuhakikisha kuwa kazi za wanamke haziingiliwi
na hali hatarishi ya afya ya wanamke pamoja na mtoto wake na kwamba shughuli za
kuzaa hazikwamishi shughuli zao za kiuchumi za kila siku pamoja na usalama wa
kazi zao ziwe za kujiajiri au kuajiriwa.
Fao
hili ni la muhimu sana kwa upande wamama kwani husaidia kupunguza vifo vya
watoto na wamama wenyewe. Utafiti unaonesha ya kuwa idadi kubwa ya wamama
wanaokufa kwa sababu ya kukosa huduma wakati wa kujifungua inaongezeka kila
siku hasa kwa nchi zinazoendelea kama vile Tanzania. Na kwamba kati ya
wajawazito kumi wanajifungua akina mama wanne hupoteza maisha pamoja na watoto
wao. Na matukio haya yote hutokea nchi za Kiafrika ikiwemo Tanzania
Takwimu za hivi karibuni hapa nchini zinaonesha
kwamba kwa mwaka, Tanzania inapoteza kina mama 7,900 kutokana na sababu
zitokanazo na ujauzito. Idadi hiyo ni sawa na vifo 22 kwa siku.
Magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo vya wazazi
nchini na mataifa mengine ni kifafa cha mimba, uzazi pingamizi, kupoteza damu
nyingi wakati na baada ya kujifungua na maambukizi baada ya kujifungua.
Na
elementi kuu za kinga za uzazi ni kama kupata likizo ya uzazi, kupata mafao
taslimu ya kuhakikisha kuwa mama anaweza kujikimu yeye pamoja na mtoto wake
wakati akiwa wa likizo ya uzazi, kuhakikisha kuwa anapatiwa matibabu,
kuhakikisha ya kuwa mama mjamzito anapatiwa kinga ya afya ya ujauzito pamoja na
mama anayeyonyesha bila kumsahau mtoto wake kupatiwa kinga kutokana na hali hatarishi
zinazoweza kusababishwa na sehemu za kazi zenyewe. Mama mjamzito au
anayeyonyesha ana haki kupewa kinga ya kutofukuzwa na kubaguliwa na kupewa
kinga ya kwenda kunyonyesha mara tu baada ya kurudi kazini baada ya kurudi
likizo yake ya uzazi
Wanawake
wengi wanakosa fursa ya kupatiwa malipo ya uzazi kabla ya kujifungua na hata
baada ya kujifungua. Na wanawake wengi zaidi wanatishiwa kufukuzwa kazi na hata
kubaguliwa. Lakini pamoja na hayo mazingira ya kazi, biolojia na kifizikia na
kemia mbalimbali za madawa zinazosaidia kuzalishia kazi zinaweza kuleta hali
hatarishi zaidi kwa upande wa uzazi na watoto wanaozaliwa hasa kwa kukosa
mikakati ya uhamasishaji wa elimu ya umma, miongozo na thathimini juu ya kinga
ya mama anategemewa kujifungua au aliyetoka kujifungua.
“Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeendelea kuchukua juhudi kubwa katika kukabiliana
na changamoto hiyo, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya madaktari na wataalamu
wanaotoa huduma za afya kutoka madaktari 3,634 mwaka 2010 hadi kufikia 4,618
mwaka 2015 ambapo kwa mujibu wa madaktari wote wa sasa daktari mmoja anatoa
huduma kwa watu 9,708.
Ingawa
SMZ imekuwa ikitoa taaluma kwa jamii kuhusiana na umuhimu wa akinamama
kujifungua hospitalini sambamba na kuondoa aina zote za malipo kwa akinamama
wanaojifungua kwenye hospitali za Serikali.
“Kuanzishwa
kwa fao la uzazi katika Mfuko wa ZSSF) ni matokeo ya juhudi za Serikali za
kupambana na kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto nchini. Mfuko wa
ZSSF unakwenda sambamba na malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo
katika mwaka 2012 alitangaza rasmi kufuta malipo kwa wajawazito wakati
wanapojifungua katika hospitali zote Unguja na Pemba” Dkt Ali Mohamed Shein
anasema.
Dk. Shein anaeleza ya kuwa utolewaji wa mfao hayo ya uzazi ni faraja kubwa
kwa wanafamilia ambao ni wanachama wa ZSSF kwani kila mmoja anaelewa taabu
wanayopata akina mama katika kipindi cha kabla na wakati wa kujifungua.
“Uamuzi huu wa kutoa fao na uzazi unakwenda sambamba na jitihada
zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali za kuimarisha ustawi wa kinamama
wajawazito pamoja na kupunguza vifo vya watoto ambavyo baadhi ya wakati
husababishwa na umasikini unaopelekea watoto wakiwa tumboni kukosa mahitaji ya
msingi kwa afya zao au huduma muhimu wakati wanapozaliwa na mara baada ya
kuzaliwa”anasema Dkt. Shein.
Makame Mwadini Silima ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSSF anasema
mafao ya uzazi yatalipwa kwa wanachama wanawake waliotimiza vigezo vya
kuchangia kwa muda wa miezi 36, miezi sita iwe mfululizo kutoka tarehe
anayoomba mafao, uthibitisho wa madaktari wenye kutambulika, vielelezo vya
ushahidi wa kuthibitisha madai ya mafao, awe mjamzito ambaye ujauzito wake
umefikia miezi 28, na awe amejifungua mtoto alie hai.
Anasema kuwa kigezo cha malipo hayo ya fao la uzazi ni asilimia 30 ya wastani
wa mshahara wa mwezi wa wanachama wote wa Mfuko. Anasisitiza kuwa Mfuko utatangaza
kiwango cha wastani wa mshahara utakao tumika kukokotoa mafao ya uzazi kila baada
ya kufanyiwa tathmini ya afya ya mfuko.
Mfuko
wa hifadhi ya jamii wa Zanzibar ulianzishwa mwaka 1998 kwa sheria Namba 2. Lengo la kuundwa
kwa mfuko ni kulipa mafao ya muda mrefu na ya muda mfupi kwa wafanyakazi wa
makundi mbalimbali ambao ni wanachama wake baada ya kukoma kwa ajira kutokana
na sababu mbalimbali zinazoainishwa na sheria hiyo.
Christian Gaya ni
mwanzilishi wa Kituo cha HakiPensheni Tanzania, mshauri na mtaalamu wa masuala
ya hakipensheni. Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa barua pepe: gayagmc@yahoo.com Au kwa habari zaidi za
kila siku juu ya HakiPensheni unaweza kutembelea tovuti www.hakipensheni.blogspot.com
Simu namba +255 655 13 13 41
No comments:
Post a Comment