Mahakama ya Wilaya ya Dodoma jana
ilimwachia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson
Minja kuendelea na dhamana yake baada ya kujiridhisha kuwa hakuvunja
masharti ya dhamana yake tangu aliapoachiwa kwa dhamana Januari 28
mwaka huu.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya
Wilaya ya Dodoma, Rhoda Ngimilanga alisema kuwa ameridhishwa na
upande wa utetezi kuwa mshtakiwa hajawahi kuvunja masharti ya dhamana
yake tangu alipoachiwa kwa dhamana Januari 28 mwaka huu.
Awali mwendesha mashtaka mwandamizi
wa serikali, Rose Shio aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo
umeshakamilika ambapo April 9 itaanza kusikilizwa kwa usikilizwaji wa
awali.
Hata hivyo aliiomba mahakama hiyo
kuendelea kuzuia dhamana ya Mshtakiwa kwa kuwa bado hapakuwa na
utulivu wa amani nje kutokana na wafanyabiashara kuendeleza migomo ya
kufungua maduka yao pamoja na kugoma kuendelea kutumia mashine za
kieletroniki za Efds.
MUHAMMADU BUHARI AJIPONGEZA KWA USHINDI NA KUSEMA NI KURA YA MABADILIKO
Mshindi wa urais katika uchaguzi wa
Nigeria Muhammadu Buhari, amepongeza ushindi wake kuwa ni wa kura ya
mabadiliko na uthibitisho kukua kwa demokrasia nchini humo.
Buhari pia amempongeza rais
anayeondoka madarakani Goodluck Jonathan kama mpinzani wa kweli,
ambaye ameridhia kuachia madaraka kwa njia ya amani.
Buhari ambaye ni Jenerali wa zamani
wa jeshi la Nigeria amemshinda Jonathan kwa kura milioni 15.4 dhidi
ya milioni 13.3.
No comments:
Post a Comment