Pages

Thursday, April 30, 2015

MAFUNDI WANUSURIKA KIFO BAADA YA JENGO LA GHOROFA TATU KUANGUKA KENYA

MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MH. SUBIRA MGALU AZINDUA RASMI SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 KIJIJI CHA KISANGA

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga kata ya Masaki Wilayani Kisarawe Bwana Mohamed Shomoi Mlembe akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu kuzundua Rasmi Shindano la mama shujaa wa chakula 2015 msimu mpya , pamoja na wageni wote waliofika katika sherehe Hizo.
Mgeni Rasmi katika Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizundua Rasmi Shindano hilo, na kuwasihi wakinamama wa Kisarawe wachukue fomu za kushiriki kwa wingi, pia aliwashukuru Shirika la Oxfam kwa kukichagua kijiji cha Kisanga kuwa wenyeji wa Mashindano hayo.
Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea Historia na Madhumuni ya shindano la Mama shujaa wa Chakula
Kikundi cha sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani ya Shairi wakati Sherehe hizo zikiendelea ambapo maudhui makubwa yalikuwa ni Ushiriki wa mwanamke katika kumiliki Ardhi na Haki zake
Diwani wa wa kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akishukuru shindano la Mama Shujaa wa Chakula kufanyika katika kijiji cha kisanga na kuwahakikishia washiriki wote kuwa kijiji kipo salama na watashirikiana pamoja kwa mambo yote wakati wa shindano hilo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA DHARURA WA VIONGOZI WA NCHI NA SERIKALI WANACHAMA WA SADC KUHUSU UENDELEZAJI VIWANDA, HARARE ZIMBABWE.

AD1
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Hoteli ya Rainbow, jijini Harare, Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini unaojadili kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR AD2 AD3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake katika Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini Harare, Zimbabwe, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR AD4
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akihutubia mkutano huo. AD5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba ya Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, wakati akifungua rasmi Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. Picha na OMR
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani Ruvuma.
unnamed
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge wa uhuru leo mjini Songea katika Uwanja wa Majimaji ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2015.
3
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi ulifanywa leo mjini Songea na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea.
4
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwa mwaka 2015 Juma Khatibu Chum(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kulia) Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.

                                                Picha na Frank Shija na Tiganya Vincent, Songea

MAYWEATHER AMBEZA PACQUIAO KWA KUINGIZA MKWANJA MDOGO

UJIO WA RAIS OBAMA KENYA MAAFISA USALAMA WA MAREKANI WAANZA KUWASILI

MATAIFA YAONYESHA HASIRA BAADA YA KUUWAWA RAIA WAO NCHINI INDONESIA

KIONGOZI WA KOREA KASKAZINI AAGIZA KUUWAWA WATU 15 KATIKA MWAKA HUU

WAZIRI MKUU AAGANA NA BALOZI WA BRAZILI

1 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Brazil nchini, Fransisco Carlos Soares Luz amabaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 29, 2015 kuaga.
2
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Brazil nchini, Fransisco Carlos Soares Luz amabaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 29, 2015 kuaga.( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu ).

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekutana na Balozi wa Brazili nchini Tanzania, Bw. Fransisco Luz na kujadiliana mambo kadhaa kuhusu maendeleo na mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza na Balozi Luz ofisini Magogoni jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumatano, Aprili 29, 2015), Waziri Mkuu alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano ambao ameutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi cha miaka sita ambacho amekuwa akiiwakilisha nchi yake hapa nchini.

Balozi Luz ambaye amepangiwa kwenda Jordan kwenye kituo kipya, alisema anaondoka nchini akiamini kwamba mtu atakayekuja kumpokea ataendelea mambo aliyoyaanzisha ikiwemo mradi wa kufadhili utafiti na uendelezaji wa zao la pamba kwenye kituo cha utafiti wa kilimo cha Ukiriguru, Mwanza.

Balozi Luz ambaye alifika kumuaga Waziri Mkuu, alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu kwamba ubalozi huo umefanikiwa kupeleka Watanzania wawili kusomea kozi za Uzamili (Masters’ Programme) kwenye vyuo vikuu vya Brazil.

“Wanafunzi hawa wawili waliondoka Februari mwaka huu, ni kati ya wanafunzi saba waliofuzu lakini wengine watano walikosa ufadhili kutoka kwenye taasisi zao. Mmoja anasomea Geo-Physics na mwingine Oil Engineering,” alisema Balozi Luz.

Balozi Luz ambaye anatarajia kuondoka nchini mapema mwezi ujao, amepangiwa kituo kingine ambapo ataenda kuiwakilisha nchi yake nchini Jordan.
 
E ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA

WASAFIRSHA DAWA ZA KULEVYA WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI NCHINI INDONESIA

MABONDIA MANNY PACQUIAO NA FLOYD MAYWEATHER WAWASILI LAS VEGAS KWA MBWEMBWE

MAFURIKO YALETA MAAFA NAROK NCHINI KENYA

BALOZI WA UMOJA WA AFRIKA AMINA SALUM ALI ATOA RAMBI RAMBI KWA KIFO CHA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA


Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
 
Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.
 
Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.
 
Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika Mungu amlaze pema peponi, Amin.
 
Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania.

TANZANITE YAKOSA SOKO HAPA NCHINI KUTOKANA NA WATANZANIA KUTOKUVAA MADINI HAYO

SAM_2162
Kulia Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine Gibson A.Kilala akitoa maelezo kwa Waziri wa nishati na madini George Simbachawene hivikaribuni jijini Arusha mara baada ya Waziri huyo kutembelea banda lao katika maonyesho ya nne ya madini na vito yaliyofanyika katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha.
(Habari na Picha kwa hisani ya Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_2156
Baadhi ya madini
SAM_2163
Mkurugenzi wa kampuni ya madini ya Moreshine Gibson A.Kilala akimuonyesha Waziri baadhi ya madini yanayopatikana katika kampuni yao
SAM_2160
Waziri wa nishati na madini George Simbachawene kushoto akipata maelezo mafupi kutoka kwa mfanyakazi wa Moreshine Bw.William Simba
SAM_2161
Waziri wa nishati na madini George Simbachawene akiangalia madini.
SAM_2159
Waziri wa nishati na madini George Simbachawene akiangalia baadhi ya madini yanayopatikana katika banda la Moreshine kushoto ni mkurugenzi wa kampuni hiyo Gibson A.Kilala na kulia ni William Simba mfanyakazi wa Moreshine

DK. SHEIN:MATIBABU YA UBONGO NA UTI WA MGONGO NI HATUA MUHIMU YA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe wa Watalaamu Mabingwa wa Magonjwa ya Kichwa, Uti wa Mgongo na Matibabu ya Maumivu kutoka nchi za Afrika Mashariki ukiongozwa na Dk.Mahmoud Qureshi pia Makamu wa Rais wa Taasisi ya Maendeleo ya Mafunzo Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana,

                                                                                           [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuanza kwa huduma ya matibabu ya ubongo na uti wa mgongo katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ni hatua muhimu katika kufikia lengo la Mpango wa Serikali wa kuifanya hospitali hiyo kuwa hospitali kamili ya rufaa.
 

Akizungumza na ujumbe wa wataalamu wa magonjwa ya kichwa na uti wa mgongo kutoka nchi za Afrika Mashariki Ikulu jana, Dk. Shein alisema amefurahishwa na namna Kituo cha Matibabu ya Ubongo na Uti wa Mgongo katika hospitali ya Mnazi Mmoja kilivyopata mafanikio ya haraka katika kipindi kifupi tangu kilipoanzishwa.
 

Aliupongeza uongozi wa Wizara ya Afya kwa kuitumia vyema fursa iliyopata Zanzibar ya msaada wa kuanzisha kituo hicho ambacho ni cha pekee nchini Tanzania.
 

Aidha Dk. Shein aliipongeza taasisi inayoshughulikia matibabu ya uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kutoka Hispania (Neurosurgical Education Foundation-NED) kwa msaada wake hadi kufanikisha ujenzi na kituo kicho.
 

Dk. Shein aliueleza ujumbe huo ambao ulifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali na Mnazi Mmoja Dk. Jamala Adam Taibu kuwa anapata faraja kuona hatua kwa hatua malengo ya Serikali ya kuimarisha huduma za rufaa katika hospitali hiyo yanatekelezwa.
 

Alifafanua kuwa wakati akifungua kikao cha kwanza cha Baraza la Wawakilishi mara baada ya kuunda Serikali mwaka 2010 aliahidi kuanzisha huduma tatu kuu nchini ambazo ni upasuaji wa moyo, matibabu ya njia ya chakula, na maradhi ya njia ya mkojo na figo.
 

Alibainisha kuwa kati ya huduma hizo ni huduma ya upasuaji moyo ndio maandalizi yake hayajakamilika lakini mengine maandalizi yamekamilika na utekelezaji wake uko katika hatua mbalimbali na za kutia moyo sana.
 

Ni jambo la kujivunia aliueleza ujumbe huo kuona sasa kituo cha Matibabu ya Ubongo na Uti wa Mgongo katika hospitali hiyo kinaweza kuvutia wataalamu kutoka nchi za nje hivyo kutoa fursa kwa madaktari nchini kujifunza kutoka wataalamu hao.
 

Kwa hivyo alitoa wito kwa madaktari vijana kuhakikisha wanaitumia fursa hiyo ipasavyo kujifunza na kupata utaalamu hadi kuwa mabingwa katika fani hiyo.
 

Aliukumbusha tena uongozi wa hospitatli hiyo kuzingatia mambo makuu ya hospitali ya rufaa ambayo ni kutoa huduma, kutoa mafunzo na kufanya tafiti na kusisitiza kuwa kwa kuzingatia hayo hospitali itakuwa imetimiza majukumu yake ipasavyo.
 

Katika maelezo yake kwa Mheshimiwa Rais, Dk. Jamala alieleza Kituo cha Matibabu ya Ubongo na Uti wa Mgongo cha hospitali ya Mnazi Mmoja kilikuwa mwenyeji wa semina ya siku mbili ya Watalaamu Mabingwa wa Magonjwa ya Kichwa, Uti wa Mgongo na Matibabu ya Maumivu kutoka nchi za Afrika Mashariki iliyofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 25 Aprili, 2015.

BORUSSIA DORTUMND YAITUPA NJE BAYERN MUNICH KOMBE LA UJERUMANI

Timu ya soka ya Bayern Munich imeshindwa katika harakati zake za kuendelea kukusanya vikombe nchini Ujerumani, baada ya kushuhudia usiku wa kuamkia leo ikitupwa nje ya kombe la Ujerumani na Borussia Dortmund katika mchezo wa nusu fainali ya kombe hilo uliomalizika kwa mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penati. 

Dakika 90 zilishuhudia timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, bao la Bayern Munich likifungwa na Lewandowski katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza, bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. 

Kipindi cha pili Borussia Dortmund walisawazisha bao hilo kupitia kwa Aubameyang katika dakika ya 75. 

Katika upigaji wa penati, Bayern Munich ilishuhudia ikikosea penati nne na Borussia Dortmund ikitumbukiza penati mbili hivyo kufuzu kucheza fainali ya kombe hilo. 
Pamoja na kushindwa kufuzu kwa hatua ya fainali ya kombe la Ujerumani, Bayern Munich tayari ni mabingwa wa ligi kuu nchini humo msimu huu.Kocha mkuu wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp akishangilia baada ya timu yake kupata tiketi ya kucheza fainali ya kombe la Ujerumani.
Wachezaji wa Borussia Dortmund wakifurahia kufuzu kucheza fainali ya kombe la Ujerumani baada ya kuifunga Bayern Munich kwa mikwaju ya penati usiku wa kuamkia leo

FANYENI REDIO ZENU ZITAMANIKE, WAMILIKI REDIO JAMII WAAMBIWA

DSC_0088
Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya masoko na mpango biashara kwa viongozi wa redio jamii nchini wakati kuhitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ambayo imefanyika katika kituo cha Redio jamii Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0219
Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana kwenye kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0229
 Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa akiuliza swali kwa mkufunzi wa warsha ya mafunzo ya masoko na mpango biashara (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha warsha ya awamu ya kwanza inayofadhiliwa na mradi wa SIDA kwa kushirikiana na UNESCO iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii cha Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.
DSC_0067
Pichani juu na chini ni Viongozi wa Redio Jamii nchini walioshiriki mafunzo ya masoko na mpango biashara yanayofadhiliwa na mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ikiwa ni hitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi huo yaliyofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.

SKYLIGHT BAND KUANZA WEEK END ALHAMIS HII NDANI YA MZALENDO PUB


LIGI KUU UINGEREZA, LIVERPOOL HOI KWA HULL CITY

Mshambuliaji wa Hull City Michael Dawson akiwa ameruka juu na kuupiga kichwa mpira uliomshinda mlinda mlango wa Liverpool, Simon Mignolet na kujaa moja kwa moja wavuni.
Timu ya soka ya Liverpool imeendelea kujiweka pabaya kushindwa kuingia nne bora, baada ya jana usiku kukubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa Hull City katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza. 

Katika mchezo huo, bao la wenyeji lilifungwa na Michael Dawson kwa kichwa kunako dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza. 

Kwa matokeo hayo Liverpool wamesimama katika nafasi ya tano wakiwa na jumla ya pointi 58 huku Hull wakiwa katika nafasi ya 15 wakiwa na pointi 34.

SHEREHE ZA MUUNGANO ZILIVYOFANYIKA WASHINGTON SEATTLE

Mayor wa Seattle Amin (kushoto akiwa na Bwana Ubwa Jas katika sherehe ya Muungano iliyofanyika siku ya Jumamosi April 25, 2015 Seattle jimbo la Washington.
Bi Ubwa akiwa kwenye sherehe ya Muungano iliyofanyika siku ya Jumamosi April 25, 2015 Seattle jimbo la Washington.
Wadau wakiwa kwenye sherehe ya Muungano Seattle.
Nick akiwa na mama mwenye nyumba wake Edith
                                                            Jimmy na mama mwenye nyumba wake Fatma

Zaham Brothers

No comments:

Post a Comment