Pages

Sunday, June 29, 2014

PPF na maonesho ya biashara 2014

 Banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF, lililoko kwenye viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam. PPF inashiriki maonyesho ya 38 ya biashara ya mwaka huu 2014 na inawakaribisha wananchi wote kujonea na kupata taarifa ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo
 Afisa Michango wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Gloria Maboya, (Kulia), akiwapatia taarifa za michango, wanachama wa PPF, waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyeshjo ya 38 ya biashara ya kimagtaifa kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Afisa Michango wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Gloria Maboya, (Kushoto), akitoa elimu kuhusu Mfuko huo, kwa mwanachama huyu aliyetembelea banda la PPF lililoko viwanja vya Maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (Kushoto), akimkabidhi Mwnanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, taarifa yake ya michango alipotembelea banda ya PPF, kwenye siku ya pili ya Maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
Mratibu wa Kanda za Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mbaruku Magawa (Kushoto), akimfafanulia Mwanachama wa Mfuko huo, kuhusiana na michango yake, alipotembelea banda la PPF, kwenye siku ya pili ya Maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment