David Msangi Mkurugenzi mkuu wa GEPF
Na Christian Gaya majira Mei 6, 2014
Mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF ulianzishwa chini ya sheria ya namba 51 ya mwaka 1942 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Madhumuni ya mfuko hapo awali ilikuwa kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa serikalini kuu ambao utumishi wao si wa masharti ya chini wizara ya fedha mpaka kufikia mwaka 2004 ambapo mfuko ulipata bodi yake menejimenti na kuanza kufanya kazi kama taasisi ya umma inayojitegemea.
Daud Msangi ambaye ndiye
mkurugenzi mkuu wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF anasema dira ya mfuko ni
kujenga mfuko wenye wigo mpana wa wanachama na wenye kutoa huduma zinazokidhi
matarajio ya wanachama wakati dhima ya mfuko ni kutoa kwa wakati mafao bora
yanayokidhi matarajio ya wanachama kwa kutumia teknolojia ya habari na
mawasiliano ya kisasa na watumishi wenye uwezo wa ari ya kujituma
Akielezea hali ya mfuko
kiutendaji, Msangi anasema kwa mwaka 2004 mfuko ulikuwa na jumla ya wanachama
16,131 ambapo mpaka kufikia mwaka wa fedha 2012/2013 mfuko umeweza kuwa na
wanachama wapatao 62,256. Wakati kwa mwaka 2004 mfuko ulikuwa na jumla ya
michango ya wanachama ipatayo bilioni 5.12 kwa fedha za kitanzania hivyo basi
mpaka kufikia mwaka wa fedha 2012/2103 mfuko umeweza kukusanya jumla ya bilioni
37.2 za kitanzania kama michango kutokana na wanachama wake wapatao 62,256. Kwa
upande mwingine ni kwamba kwa mwaka 2004 mfuko uliweza kulipa mwanachama wake
jumla ya mafao ya thamani ya fedha za kitanzania zipatazo bilioni 67.10.
Anasema katika kipindi cha
miaka mitano (5) idadi ya wanachama imeongezeka kutoka wanachama 30,227 mwaka
wa fedha 2008/09 mpaka kufikia wanachama 60,030 kwa mwaka wa fedha 2012/2013
ambapo ilikuwa sawa na ongezeka la asilimia 98.6.
Wakati kwa upande thamani ya
mfuko huu wa mafao ya kustaafu wa GEPF,
mkurugenzi mkuu anasema thamani ya mfuko imeongezeka kutoka bilioni 72.55 za
fedha za kitanzania kwa mwaka wa fedha 2008/09 hadi kufikia bilioni 198.30 za
fedha za kitanzania mpaka kufikia mwaka wa fedha 2012/2013 ambapo sawasawa na
ongezeko la asilimia 173.33.
“Unajua katika mifuko hii ya
mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii moja ya malengo yake ni kuhakikisha kuwa
thamani ya mfuko inaongezeka na hivyo kuwa na afya bora jambo ambalo tumeweza
kulitekeleza kwani mpaka sasa mfuko una thamani ya shilingi bilioni 198.30,”
mkurugenzi mkuu anasema.
Anabainisha ya kuwa kwa
upande wa uwekezaji mapato ya uwekezaji yameweza kuongezeka kutoka bilioni 5.48
ya fedha za kitanzania kwa mwaka wa fedha 2008/2009 mpaka kufikia bilioni 18.25
za kitanzania ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 233.03 mpaka kufikia mwaka
wa fedha 2012/2013
Anasema ongezeko hilo limechangiwa
na kuongezeka kwa wanachama pamoja na uwekezaji katika sekta mbalimbali kama
amana za serikali, makampuni yaliyo orodheshwa kwenye soko la mitaji
(DSE), uwekezaji wa muda maalum kwenye mabenki ya biashara, mikopo, hati
fungani na majengo.
Kwa upande wa mabadiliko ya
mfuko wa uendeshaji kwenda akiba kwenda mpango wa pensheni, mkurugenzi mkuu
anasema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha sheria mpya ya
mfuko wa GEPF ambapo pamoja na mambo mengine unabadili mfumo wa uendeshaji na
kuruhusu GEPF kulipa mafao ya muda mrefu yaani pensheni. Sheria hii imezingatia
sheria ya SSRA sheria namba 5 ya mwaka 2012. Mafao mapya yatakayolipwa na GEPF
ni pamoja na fao la msaada wa mazishi, fao la pensheni, fao la elimu na fao la
kufariki kazini.
Mkurugenzi mkuu akizungumzia
juu ya mpango wa hiari wa kujiwekea akiba ya uzee (VSRS) anasema mpango huu ni
skimu maalumu iliyobuniwa tangia mwaka 2009 ili kutoa fursa kwa watu wote
kuweka akiba ambaye itawasaidia kupatwa na majanga mbalimbali ikiwemo uzee na kwamba
mpango huu ni matokeo mageuzi katika sekta ambayo yanamtaka kila mtu mwenye
uwezo wa kuzalisha kipato aweze kujiunga na hifadhi ya jamii.
“Kupitia skimu hii kila mtu
anaweza kujiunga awe mkulima, mjasiriamali, sekta ya usafiri na makundi mengine
na mafanikia katika skimu ya hiari tangia kuzinduliwa kwake mwaka 2009, usajiri
wa wamachama wake umefikia 18,060 wakati kwa upande wa akiba zao wanachama
zimefikia bilioni 3.1 fedha za kitanzania” Msangi anasema
Akiendelea
kufafanua mkurugenzi mkuu anasema mpaka sasa mfuko una matarajio ya kufikia
jumla ya wanachama 33,226 mpaka kufikia Juni 2014 ili kufanya mfuko kukua
kadiri ya malengo iliyojiwekea. Wakati
kwa upande wa wanachama Mfuko una matarajio ya kupata akiba za wanachama
kufikia bilioni 5.10 fedha za kitanzania.
Mfuko wa mafao ya kustaafu GEPF ambao hapo awali ulijulikana kama mfuko wa akiba wa wafanyakazi serikalini umeundwa kwa sheria Na.8 ya mwaka 2013.sheria hii mpya imefuta sheria Na.51 ya mwaka 1942 ambayo ilikua inaunda mfuko wa akiba ya wafanyakazi serikalini. Mageuzi katika sekta ya hifadhi ya jamii pamoja na mambo mengine yamepelekea kufanya mageuzi ya mfuko huo kutoka mfumo wa akiba na kuingia kwenye mfuko wa pensheni.
Anasema kwa hapo awali mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF uliokuwa unajulikana kama mfuko wa akiba wa wafanyakazi serikalini ulianzishwa mwaka 1942 kama ilivyoainishwa hapo juu na kwa wakati huo malengo yalikua kutoa kinga ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa serikali kuu wanaofanya kazi katika masharti ya mikataba na wale walio katika masharti ya kawaida.
Mfuko ulifanya kazi zake ndani ya wizara za fedha chini ya kitengo cha pensheni mpaka mwaka 2004 ilipoundwa bodi na kuteua menejimenti na hatimaye mfuko kuanza kujiendesha kama taasisi ya serikali inavyojitegemea yenyewe ukiwa chini ya wizara ya fedha kama wizara mama.
Mkurugenzi mkuu anasema sheria ya mdhibiti na msimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA) ya mwaka 2008 ilibadili mwelekeo wa wanachama wa mfuko na hivyo kufungua milango ya kusajili wanachama kutoka sekta zote ikiwemo sekta ya ajira binafsi.
Msangi anasema ili kujenga ushindani ulio sawa, mwaka 2013 Mfuko wa GEPF ulifuta sheria yake ya awali iliyokuwa inafuata mfumo wa akiba na kutungwa kwa sheria mpya iliyobadili mfumo wa sheria mpya iliyobaadili mfumo wa mfuko kuendeshwa kwa utaratibu wa pensheni kama ilivyo mifuko mengine.
“Sheria hii mpya ambayo imeshapitishwa na bunge na kusainiwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete ndiyo imeanza kutumika rasmi” Msangi anakumbusha.
Ili kutimiza matakwa ya kisekta kwa wakati huu wa ushindani, mkurugenzi anasema Mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF kwa sasa una skimu mbili ambazo ni mpango wa uchangiaji kisheria na wa pili ikiwa ni skimu ya hiari ijulikanayo kama mpango wa hiari wa kujiwekea akiba ya uzeeni unaojulikana kwa kifupi kama VSRS.
Anasema kwa upande wa skimu ya uchangiaji wa kisheria skimu hii ni kwa ajili ya wale wote walioajiriwa katika ajira rasmi bila kujali sekta au aina ya mwajiri na wanachama katika skimu hii huchangia kila mwezi kupitia mishahara yao na mwajiri huwajibika huongeza kiasi kingine ili kufikisha 20% ya mshahara wa mfanyakazi na kupeleka katika mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF kwa wakati muafaka.
Kwa upande wa skimu ya hiari anasema kwa sasa sekta ya hifadhi ya jamii imefungua milango kwa watu wote wenye uwezo wa kuzalisha kipato kujiwekea akiba kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii hivyo basi skimu hii ya hiari inasajili wanachama kutoka makundi mawili ambayo ni waajiriwa ambao ni tayari kisheria wanachangia mifuko ya hifadhi ya jamii iliyopo lakini wanaona ni vyema kujiwekea akiba ya zaidi kwa ajili ya baadaye, na kundi la pili ni wale ambao kisheria hawawajibiki kuchangia kwenye mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii kutokana na akiba zao kutotegemea mshahara yaani waliojiajiri wenyewe kupitia skimu hii, kundi hili la pili linapata fursa ya kuweka akiba itakayowafaa wanapokumbwa na majanga mbalimbali kama vile kuumia wakiwa kazini, kuugua, au kustaafu. Skimu hii ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2009 na mpaka sasa imepata mafanikio makubwa kiutendaji.
“Maudhui ya skimu hii yameandaliwa kwa kuzingatia hali halisi ya watanzania katika sekta mbalimbali za kiuchumi, hivyo kumwezesha kila mtu kujiunga na kumudu kuweka akiba kulingana na uwezo wake” Msangi anabainisha.
Anasema kwa kupitia skimu hii wakulima, wafanyabiashara, wavuvi, waajiriwa, wachimba madini wadogowadogo, mama lishe na waendesha bodaboda, teksi, daladala wameweza kujiunga na kujiwekea akiba ya kuwafaa wanapopata majanga mbalimbali kutokana na umri mkubwa.
Mkurugenzi mkuu anasema
katika mfuko huu wa GEPF wanachama wamegawanyika katika makundi mbalimbali
ambayo ni wafanyabiashara 7,480, kilimo na ufugaji 6,545, ujasiriamali 1,683 na
waajiriwa 2,992.
Msangi anabainisha ya kuwa
pamoja na mafanikio hayo ya mfuko bado mfuko unazo changamoto mbalimbali ambazo
ni maeneo ya uwekezaji kuwa finyu, waajiri kutowasilisha michango kwa wakati
muafaka, pamoja na ushindani ambao
umetokana na uhuru wa wafanyakazi wapya kuwa na uhuru wa kuchagua mfuko wa
kujiunga, na ufahamu mdogo wa watu kuhusu elimu ya elimu ya pensheni ya mfuko
wa hifadhi ya jamii.
Mabadiliko ya kutoka mfuko
wa akiba na kuwa mfuko wa pensheni na kwa upande mwingine ni kwamba jina la
mfuko limebadilika kutoka mfuko wa akiba ya wafanyakazi serikalini na kuwa Mfuko
wa mafao ya kustaafu GEPF.
Msangi anasema mabadiliko
haya yana maana ya kwamba sasa mwajiriwa katika masharti yoyote anaweza
kujiunga na Mfuko huu wa mafao ya kustaafu wa GEPF kwa maana sasa mfuko unaweza
kulipa mafao ya muda mrefu na ya muda mfupi tofauti na hapo awali ambapo mafao
ya muda mfupi tu ndio yalikuwa yanalipwa na mfuko huu.
Kwa ujumla Mfuko wa mafao ya
kustaafu wa GEPF umejipanga vizuri kuhudumia wanachama wote katika mazingira
haya mapya kama ilivyokuwa awali kwa wanachama wa mikataba. Ubora wa huduma
zetu umeboreshwa zaidi ili kukidhi matarajio ya wanachama. Hivyo waajiri na
waajiriwa wote mnakaribishwa kujiunga na Mfuko huu wa mafao ya kustaafu wa GEPF
ili kunufaika na mafao mbalimbali pamoja na huduma bora kabisa kwa viwango vya
sekta ya pensheni ya hifadhi ya jamii hapa nchini msangi anasema ambaye ndiye
mkurugenzi mkuu wa GEPF.
Mfuko wa mafao ya pensheni GEPF hapo awali ulikuwa ni mfumo pekee unaoendeshwa kwa utaratibu wa akiba hapa nchini, hivyo ili kukidhi vigezo vya mageuzi katika sekta ikiwemo ushindani ulio sawa imebidi kubadili sheria na kuwa mfuko wa pensheni kama ilivyo mifuko mingine (sheria ya SSRA Na.8 ya mwaka 2008 pamoja na marejeo (R.E 2012) Msangi anasema ambaye ndiye mkurugenzi mkuu wa GEPF.
Hifadhi ya Jamii ni haki
ya kila Mtanzania. Haki hii imeanishwa katika Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Ibara ya 11(1) na Sera ya Taifa ya Hifadhi ya
Jamii ya mwaka 2003.
Hifadhi ya Jamii ni haki ya kila mtu na si kwa wale tu walio katika ajira rasmi. Kulingana na takwimu zilizotolewa mwaka 2012 idadi ya Watanzania ni milioni 44.9 ambao kati yao watu milioni 1.7 tu ndio waliojiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, hii ikiwa ni asilimia 6.5 tu ya Nguvu kazi yote ya watu milioni 23.7.
Hivyo SSRA inasisitiza Wananchi wote wenye umri wa kufanyakazi, miaka 18 mpaka 60 walioajiriwa katika sekta iliyo rasmi au sekta isiyo rasmi (waliojiajiri) kama vile Wakulima, wafanyabiashara ndogondogo, wasusi, vinyozi, mamalishe, mafundi cherehani n.k kuwa wote wanahaki ya kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika mpango wa lazima au mpango wa hiari, kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kama vile wa GEPF na VSRS ambao ni skimu yake ya hiari
“Ili kufikia malengo
yetu kama yalivyoaininshwa katika dira na dhima na maadili yetu na ili kwenda sambamba
na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea duniani pamoja na mabadiliko
ya aina hiyo ndani ya sekta ya hifadhi ya jamii GEPF tumekuwa tukiboresha mara kwa
mara huduma zetu na kushirikiano baina
yetu na wewe ili kutoa kutoa wa Mafao
kwa wakati muafaka, kutoa wa taarifa sahihi na zenye uhakika na kushughulikia
wa malalamiko pamoja na maoni yako kwa wakati”, anafafanua Mkurugenzi mkuu.
No comments:
Post a Comment