Pages

Tuesday, May 6, 2014

Saccos nchini kunufaika na mikopo ya NSSF

 
 Mmoja wa wafanyakazi waandamizi wa mradi huo, ambaye hakutaka jina lake kuandikwa kwenye gazeti, alisema kuwa kasi ya ujenzi imepungua kutokana na fedha kidogo zinazotolewa kwa ajili ya uendelezaji.PICHA|MAKTABA

Na Fina Lyimo Mwananchi.
Kwa ufupi
Masaki alisema mbali na kupatiwa mikopo kwa wanachama, pia watatibiwa bure na tegemezi wao bila kulipa chochote.


Siha. Shirika la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeanza kuingia kwenye vyama vya kuweka na kukopa (Saccos).


Kwa mujibu wa mfuko huo, sasa imeziasa Saccos kushawishi wanachama wao wajiunge na NSSF ili wapate fursa zinazotolewa na mfuko huo.

Meneja wa NSSF, Mkoa wa Kilimanjaro, Delfina Masaki, alisema hayo jana kwenye mkutano maalumu wa wanachama wa Saccos ya Ivueny iliyopo Siha mkoani Kilimanjaro. Alisema wanachama wa Saccos wakijiunga na mfuko huo watapewa mkopo kwa riba nafuu.

Masaki alisema kupitia Saccos wanachama wa NSSF wanapatiwa mikopo yenye riba ndogo, hali itakakayowafanya watumie mikopo hiyo kwa kufanya biasara na kuinua kipato cha kwa ujumla.
Masaki alisema mbali na kupatiwa mikopo kwa wanachama, pia watatibiwa bure na tegemezi wao bila kulipa chochote.

Meneja huyo alisema mfuko huo huwa unachukua riba ya asilimia 9.2 kwa wanachama wanaokopeshwa kuanzia Sh50 milioni na kuendelea. Kwa upande wake Mweneykiti wa Saccos ya Ivaeny Rodrick Maimu, alipongeza uongozi wa NSSF kwa kuwahamasisha na kuweza kupata fursa ambazo zinatolewa na mfuko huo. Alisema wanafanya linalowezekana kuimarisha uhusiano baina yao kwa lengo la kuleta tija kila upande.

No comments:

Post a Comment