Pages

Wednesday, May 29, 2013

Ushirikishwaji wa wadau na mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii



http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/03/Page-12.jpg
Wajibu wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii ni kuhakikisha ya kuwa inawashirikisha wadau wake wote wakuu hasa waajiri, serikali na bila kusahau wanachama na familia zao ambapo makundi hayo matatu yanaunda kitu kinachoitwa utatu hawa wote  wanaunda utatu. wananchi lazima mtambue kuwa wawekezaji wa mifuko hii ni waajiri na wafanyakazi pale wanapojiandikisha na kuwa wanachama wachangiaji kwa kukatwa asilimia fulani kutoka katika mishahara yao na mwajiri na yeye kuchangia kiasi hicho hicho au zaidi kwa ajili ya mfanyakazi wake kwa makubaliano ya kupata huduma mbalimbali za muda mfupi na za muda mrefu kutoka katika kwa hiyo mifuko.


Hivyo uwakilishi wao lazima uwemo ndani ya utawala wa mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii mara kwa mara kwa vitendo. Vile vile inatambulika kuwa hata serikali ina kazi kubwa juu ya mifuko hii ya hifadhi ya jamii  hasa zaidi kwa kuangalia na kusimamia kiwango cha kinga juu ya majanga wanayokumbana nayo jamii yetu hapa nchini pamoja na kuangalia mchango wa mifuko hii kwa upande wa uchumi wa nchi yetu  na serikali kama mdhamini mkuu wa mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii. Serikali kuwa mdhamini hii ina maana ya kuwa mfuko wowote ukifirisika serikali ndiye atayewajibika kuwalipa wanachama wa mfuko huo michango na pensheni zao na madeni mengineyo bila kuteteleka. 


Hapa kinachoshindikana ni utekelezaji ingawa utaratibu na kanuni zote za uhusiano wa utatu uliopo kati ya mwajiri, mfanyakazi na serikali na jinsi ya kuwashirikisha. Huenda ugumu unaokuja ni jinsi ya kupata taasisi na au mtu sahihi ambaye anaweza kuwa mwakilishi wa kutosha wa wachangiaji, wategemezi pamoja na wadau wengine wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Mfuko wa hifadhi ya jamii unaweza kuwa na wanachama wengi na kukawa na taasisi nyingi zinazowakilisha waajiri na wafanyakazi wakati baadhi ya wanachama wengine wakawa hawana mtu yeyote wa kuwakilisha mambo yao. Lakini kwa upande mwingine mfuko unaweza kuwa na wigo mdogo wa wanachama  na idadi kubwa ya wanachama hao hao wakawa na uelewo mdogo wa dhana ya hifadhi ya jamii pamoja na kutojua hata utawala wa vitendo wa mfuko wa pensheni ya hifadhi ya jamii na wakawa hata umoja wao wa wafanyakazi kuwa mdogo kiasi cha kwamba ukawa hata uwakilishi wao kutokuwa na nguvu yeyote. Hivyo kuna haja ya kuangalia mgawanyo wa majukumu na kati ya serikali na bodi, mgawanyo wa majukumu kati ya bodi na wawakilishi  na mwisho mgawayo wa majukumu kati ya bodi na mkurugenzi makuu. Hii mara nyingi mambo mengi yanakuja kuingiliwa na hali ya kiasi iliyopo nchini. Kwa sababu unakuta mkurungezi mkuu wa mfuko wa pensheni ya hifadhi ya jamii anachanguliwa na rais wa nchi.  


Na kwa upande mwingine wajumbe wa bodi kuchanguliwa wa wizara mama, mfano mfuko wa pensheni wa mashirika ya umma yaani Parastatal Pension Fund (PPF) wenyewe uko chini ya wizara ya fedha,  Mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) wizara ya kazi na ajira, Mfuko wa pensheni wa serikali za mitaa yaani Local Authorities Pensions Fund (LAPF) wizara ya serikali za mitaa, mfuko wa taifa wa bima ya afya yaani National Health Insurance Fund (NHIF) wizara ya afya. Na mfuko wa akiba ya wafanyakazi kwa watumishi wa serikali yaani Government Employees Provident Fund (GEPF) wizara ya fedha . Pamoja na mfuko wa pensheni wa watumishi wa serikali ya Public Service Pensions Fund (PSPF) ambao nao upo chini ya wizara ya fedha ingawa kwa sasa yote inasimamiwa na mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA). Mifuko ya hifadhi ya jamii, wanachama, wafanyakazi, waajiri. Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii iliundwa kwa sheria Na 8 ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2008 kwa lengo la kusimamia na kudhibiti sekta ya hifadhi ya jamii kwa manufaa ya wanachama na kwa taifa kwa ujumla. Mamlaka ilianza kazi rasmi mwaka 2010.


Mamlaka ina jukumu la kusimamia shughuli zote za hifadhi ya jamii nchini ikiwa ni pamoja na mifuko yote ya hifadhi ya jamii iliyo anzishwa kwa sheria ya bunge ambayo ni mifuko ya pensheni,mifuko ya akiba .mifuko ya bima ya afya na mifuko ya hiari na kuhakikisha kwamba mifuko inakuwa endelevu ,inaendeshwa kwa kufuata kanuni na taratibu za kisheria, wanachama wanapata taarifa za mifuko yao ,mafao yanaboreshwa na serikari inapunguziwa mzigo.
Kwa hiyo wawakilishi wote wa bodi idadi yao kubwa wanatoka serikali, na mara nyingi katiba za mifuko ya hifadhi ya jamii inaeleza wazi sifa za hao wajumbe wa bodi au bodi ya wadhamini ambazo hata kidogo hazifuatwi badala yake kuchaguliwa kwa kujuana na matokeo yake anaishia kumsikiliza mkurugenzi mkuu bila kuhoji chochote kwa muda wote wa miaka mitatu na mwaka wa mwisho huenda ndipo anapoweza kuanza kuelewa baadhi za taarifa za mahesabu lakini mwanzoni anaishia kuitikia kwa sababu ya kutokuwa na upewa wa kutosha juu ya mambo ya hifadhi ya jamii. Kwa hiyo mzigo wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii unabaki chini ya serikali yenyewe kwa sababu utawala na usimamizi wote wa mifuko hii upo chini ya usimamizi na uthibiti wa chombo cha serikali hivyo hata kesho mfuko wowote ukafilisika atayebeba mzigo wa kulipa mafao au pensheni  na na madeni itakuwa serikali yenyewe kama mdhamini wa mifuko yote hapa nchini

No comments:

Post a Comment