Kwa ufupi
Kama tulivyosema hapo juu, Serikali haionekani
kufurahia utaratibu uliowekwa kwa shinikizo la wafadhili la kuweka wazi
ripoti hizi za CAG. Ndiyo maana imeushinikiza Uongozi wa Bunge kufuta
utaratibu uliokuwapo wa Bunge kujadili ripoti hizo moja kwa moja na
kuiwajibisha Serikali.
Moja ya mafanikio ambayo yametokana na ripoti za
kila mwaka za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ni
wananchi kutambua kwamba mhujumu mkuu wa uchumi wa nchi yetu siyo
mwingine bali ni Serikali. Pamoja na Serikali kubuni mbinu mbalimbali
ili wananchi wasizijadili kwa undani na kuweza kutambua chanzo cha
kukwama kwa uchumi wa nchi yao, vyombo vya habari vimehakikisha mambo
muhimu yaliyo katika ripoti hizo yanawafikia wananchi.
Hivyo, miezi miwili au mitatu hivi ijayo vyombo
vya habari makini vitaendeleza utamaduni huo wa uwajibikaji kwa wananchi
kwa kuhakikisha wananchi wanafahamu mambo muhimu yaliyomo katika Ripoti
ya CAG kwa mwaka wa fedha uliopita. Ripoti hiyo iliwekwa wazi na CAG,
Ludovick Utouh alipokutana na waandishi wa habari mjini Dodoma juzi,
ambapo ilianika ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na udhaifu katika
usimamizi wa mikataba na ukusanyaji kodi.
Kama ilivyokuwa huko nyuma, ambapo ripoti hizo
ziliwawezesha wananchi kupata mwamko wa jinsi Serikali na taasisi zake
zinavyodumaza uchumi kwa vitendo vya ubadhirifu na ufujaji wa fedha za
umma, Ripoti ya CAG iliyozinduliwa katikati ya wiki itawapa tena fursa
ya kushuhudia kujirudia kwa vitendo hivyo ndani ya Serikali na taasisi
zake.
Kama tulivyosema hapo juu, Serikali haionekani
kufurahia utaratibu uliowekwa kwa shinikizo la wafadhili la kuweka wazi
ripoti hizi za CAG. Ndiyo maana imeushinikiza Uongozi wa Bunge kufuta
utaratibu uliokuwapo wa Bunge kujadili ripoti hizo moja kwa moja na
kuiwajibisha Serikali.
Jambo ambalo wananchi watajifunza baada ya kujua
kilichomo katika Ripoti ya CAG iliyozinduliwa katikati ya wiki ni ukweli
kwamba kimsingi Serikali haijakubali kubadilika na kufuata njia nyoofu
ya uadilifu na uwajibikaji.
Bado watumishi wake katika ngazi za juu wanafuja
fedha mithili ya mabaharia walevi na imekataa katakata kuzingatia
ushauri ambao CAG alikuwa akitoa kupitia ripoti zake za kila mwaka.
Kwa mfano, CAG amegundua kwamba Serikali imepuuza
kabisa ushauri wake wa kuitaka ipunguze misamaha ya kodi isiyo ya
lazima. Ripoti ya sasa inasema misamaha hiyo bada
Ni ushahidi kwamba baadhi ya viongozi serikalini
wanafaidika na misamaha hiyo. Ebu fikiria mantiki ya Serikali kusamehe
makampuni ya madini Sh140 bilioni au sababu za kusamehe kampuni na watu
binafsi kodi ya Sh304 bilioni.
CAG alipendekeza wabunge wasiwe wajumbe wa bodi za
mashirika ya umma, lakini idadi yao katika mashirika hayo ndiyo kwanza
inazidi kuongezeka. Wakiwa katika bodi hizo hawawezi kuyasimamia
mashirika yake ipasavyo kwa sababu ya wao kuwa na masilahi binafsi. Kwa
mfano, Ripoti ya sasa ya CAG imegundua kwamba Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Serikali Kuu (PSPF) umepata hasara ya Sh6.487 trilioni.
Kwa mshangao wa CAG, Uongozi wa Bunge pengine kwa
shinikizo la Serikali umevunja Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma
(POAC) na kuunganisha shughuli zake na Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu
(PAC).
CAG ameonya, na tunafikiri yuko sahihi kwamba PAC
itazidiwa na haitaweza kumudu majukumu ya kusimamia mashirika ya umma
zaidi ya 300, wizara zote na taasisi zake.
No comments:
Post a Comment