Kwa ufupi
Orodha ya leo imefanya idadi ya Mawaziri hao
walioteuliwa kufikia Mawaziri 16 huku wananchi wakiendelea kusubiri
nafasi mbili kwani awali Rais Kenyatta aliutangazi umma kuwa baraza
lake la mawaziri litakuwa na watu 18 tu.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akishirikiana na
Makamu wa Rais William Ruto leo ametangaza kwa mara ya pili majina 12 ya
Mawaziri watakaounda Baraza jipya.
Orodha ya leo imefanya idadi ya Mawaziri hao
walioteuliwa kufikia Mawaziri 16 huku wananchi wakiendelea kusubiri
nafasi mbili kwani awali Rais Kenyatta aliutangazi umma kuwa baraza
lake la mawaziri litakuwa na watu 18 tu.
Miongoni mwa mawaziri walioteuliwa leo na wizara
zao zikiwa kwenye mabano ni Najib Balala( Madini ), Charity Ngilu
(Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya mijini ), Adan Mohamed ambaye kabla ya
uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Baclays Afrika
(Viwanda na Maendeleo ya Biashara).
Wengine ni Anne Waiguru(Maendeleo ya wananchi na
Mipango), Felix Tarus Kosgey(Kilimo, Mifugo na Uvuvi), Judy Wahungu(Maji
na Maliasili), Hassan Wario(Michezo na Utamaduni), Jacob Kaimenyi
(Elimu) Francis Kimemia (Katibu wa Baraza la Mawaziri) na Lawrence
Lenayapa (Mnadhimu wa Ikulu).
Kwa habari zaidi ungana nasi baadaye
No comments:
Post a Comment