Na Christian Gaya: Majira: Machi 19, 2013
Sheria ya msimamizi na
mdhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii hifadhi
SSRA ilitungwa na kupitishwa na sheria namba 8 ya mwaka 2008 ili kusimamia
na kudhibiti shughuli zote za hifadhi za jamii hapa nchini kwa kuanza na mifuko
yote ya hifadhi ya jamii iliyopo hapa
nchini kwa sasa kama vile mfuko wa
pensheni wa mashirika ya umma yaani Parastatal Pension Fund (PPF) ulioundwa kwa
ajili ya kutoa huduma ya pensheni ya hifadhi ya jamiii kwa wafanyakazi wote wa
mashirika ya umma na wa sekta ya watu binafsi na sekta ilisiyokuwa rasmi. Mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii (NSSF)
wa sheria namba 28 ya mwaka 1997
Mfuko wa pensheni wa serikali za mitaa yaani Local
Authorities Pensions Fund (LAPF) mfuko wa taifa wa bima ya afya yaani National
Health Insurance Fund (NHIF) unaotoa huduma ya bima ya afya kwa watumishi wote
wa serikali. Na mfuko wa akiba ya wafanyakazi kwa watumishi wa serikali yaani Government
Employees Provident Fund (GEPF). Pamoja na mfuko wa pensheni wa watumishi wa
serikali ya Public Service Pensions Fund (PSPF)
Mpaka sasa mdhibiti
na msimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii (SSRA) ameanza kuleta marekebisho ya
baadhi ya vifungu vya sheria kwa awamu
kwa mfano waajiri wote katika utumishi wa umma na sekta binafsi
wanapaswa kuzingatia matakwa ya sheria hii kwa kuwapa fursa watumishi wapya
kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya lazima wanayoitaka. Bado ni
changamoto kubwa sana kwa SSRA kuleta na kufanya marekebisho haya yote. kwani mpaka sasa haya mashirika ya hifadhi ya jamii
kila moja ina wizara yake inayoisimamia na kuwa utaratibu na kanuni tofauti za
uendeshaji wa mifuko hii. Matokeo yake ni kwamba kiwango cha michango, mfumo wa
mafao, na sifa za kupata mafao na hata mipako na vipa umbele vinatofautiana
kabisa kwa kila mfuko.
Mpaka sasa hakuna
utaratibu ulioanzishwa wa kuruhusu haki za mafao ya mwanachama kuhamishwa
kutoka mfuko mmoja hadi mwingine. Matokeo yake wafanyakazi wamekuwa wakipoteza
baadhi ya haki zao za mafao wakati wakihama kutoka sehemu moja ya mwajiri hadi
mwajiri mwingine. Pia hii imechangia sana kuongezeka kwa tabia ya kuondoa
michango ya pensheni kabla haijakomaa.
Kumekuwa hakuna soko huru la hifadhi ya jamii ambalo
linaweza kumruhusu hata taasisi za watu binafsi au sekta za watu binafsi
kuendesha mifuko ya hifadhi ya jamii kwa muda mrefu ingawa kwa sasa wameruhusu
lakini muundo rasmi haujatoka bado kutoka kwa mdhibiti na msimamizi wa hifadhi
ya jamii (SSRA)
Miongozo ya uwekezezaji wa rasilimali za mifuko hii ya
hifadhi ya jamii ingawa imetolewa tayari lakini haijaanza kutumika mpaka sasa. Mapungufu yaliyomo kwenye mfumo huu wa
hifadhi ya jamii ambayo yanahitajika kutatuliwa na sera hii ya hifadhi ya
jamii. Watu waliomo katika mifuko hii ya hifadhi ya jamii ni wale tu
ambao wameajiriwa kwenye sekta iliyo rasmi
Jumla ya idadi ya wanachama wa mifuko hii ya pensheni ya
hifadhi ya jamii kwa Tanzania ni watu 871,000 na imegawanywa kama ifuatavyo
NSSF ni 363,000, PSPF 193,000, na kwa NHIF 180,000, 90,000 PPF, na kwa LAPF
45,000. Hii inawakilisha kama asilimia 85 ya watu wote waliajiriwa kwenye sekta
iliyokuwa rasmi
Imefikia wakati sasa mifuko ya hifadhi ya jamii inahitaji
kubadilika kimtazamo na kidira imefika wakati ambapo mteja huenda akaonekana ni
mfalme. Mifuko ya jamii nchini inahitaji kujua hili ili kujipanga upya na
kuhakikisha ya kuwa inajali wateja wao hasa kwa kutoa huduma bora kwa wanachama
na wastaafu pamoja na washika dau wengine kama vile wamama, wababa na watoto tegemezi. Mashirika
ya hifadhi ya jamii yanahitaji kupokea malalamiko ya wanachama wao na kujibu
kwa muda muafaka ili kuwaridhisha kama wenye wachagiaji wa michango hiyo.
Wanahitaji kutimiza ahadi wanazotoa kwa wanachama kwa wakati muafaka na siyo
vinginevyo.
Wakati umefika wa kubadilisha sheria zilizopitwa na
wakati na ukiritimba, kila mmoja anahitaji kuingia uwanjani kwa kuuza sera zake
ili kumvutia mteja. Waajiri wanahitajika kubadilika juu ya suara hili la
mabadiliko ya marekebisho ya sheria ya hifadhi ya jamii ya kuwaruhusu
wafanyakazi wapya walioajiriwa kutoka sekta iliyokuwa rasmi na isiyo kuwa rasmi
kuchagua mfuko wowote anautaka mfanyakazi kujiunga nao na wale ambao wako
kwenye ajira lakini walikuwa hawajawahi kuijiunga na mfuko wowote hapa nchini
nao pia wapitiwa uhuru huo wa kuchagua siyo kuchaguliwa na mwajiri.
Ingawa kwa upande mwingine ni changamoto kubwa kwa
waajiri hasa kwa kuongezeka kwa gharama kwa kuhakikisha ya kuwa michango yote
ya wafanyakazi wao inapelekwa kwa muda muafaka kwa kila mfuko wa pensheni
ambayo wafanyakazi wake hao wapya wamechagua kujiunga nayo. Lakini ijuilikana
ya kuwa marekebisho haya yanafanyika ili kutimiza matakwa ya kifungu Na. 30 cha
sheria iliyoanzisha Mamlaka ambayo inampa uhuru mfanyakazi na mfuko wowote
ulioanzishwa kwa sheria ya bunge.na kwa upande wa mifuko ya pensheni naamini
wanajua ya kuwa Kwa mujibu wa vifungu vya (29),( 2) na (3) vya Sheria ya
Usimammizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2008 ni kinyume
cha sheria na ni kosa la jinai kwa mfuko
wowote wa pensheni kuandikisha wanachama waliokwisha andikishwa na Mfuko
mwingine; kutoa taarifa zisizo sahihi kwa lengo la kuaminika kwa wadau, waajiri
na waajiriwa; kutoa nyaraka ukijua kuwa nyaraka hiyo ni ya kughushi; na kupata
ridhaa ya wafanyakazi au waajiri kwa njia ya shinikizo au vitisho
Ni makosa makubwa kwa
mfanyakazi mpya kujiunga au kujiandikisha kwenye mifuko zaidi ya mmoja wa
pensheni kwa kufanya hivyo unaweza kupoteza haki yako ya msingi.pamoja na hayo
kwa mujibu wa kifungu cha 30 cha Sheria ya Usimammizi na Udhibiti wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii na Sheria za Mifuko kama zilivyorekebishwa, mfanyakazi ambaye
hajawahi kujiunga na Mfuko wowote wa Pensheni au anayeajiriwa kwa mara ya
kwanza anao uhuru wa kuchagua mfuko wowote kati ya mifuko tajwa hapo juu. Hii
ina maana mfanyakazi anapaswa kuwa mwanachama wa Mfuko mmoja tu wa Pensheni.
Ili kutekeleza kifungu hiki cha kufanya marekebisho SSRA kwa sasa imeanza
kushirikiana pamoja na vyombo mbalimbali
kama kama vile Idara ya Utumishi wa Walimu (TSD), Idara ya Utumishi wa Umma
(CSD), Idara ya Utumishi wa Serikali za Mitaa (LGSD) Idara ya Utumishi wa
zimamoto (FRSD), Idara ya Utumishi Afya (HSD) na kuhakikisha ya kuwa vyama
mbalimbali vya wafanyakazi vinazingatie pia masharti ya Sheria ya Usimamizi na
Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwenye maeneo yao.
No comments:
Post a Comment