Pages

Tuesday, February 26, 2013

Madhara ya kutoa michango ya pensheni mapema kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii




Approximately 90 per cent of listed voters did not bother to verify their registration details in January as advised by the electoral commission and some 12.9 million voters are at high risk of discovering erroneous entries regarding their registration details on the voting day. FILE/NATION

Na Christian Gaya: Majira 25. 2013
Kwa nchi nyingine kuondoa michango ya pensheni mapema inaruhusiwa kwa kuwepo na sheria kama vile ya Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi wa Serikali (GEPF) ambao kila mwanachama ana akaunti yake ya michango ya pensheni au kama ilivyokuwa NPF yaani shirika la akiba ya taifa la wafanyakazi ambapo bunge la Jamhuri la muungano la Tanzania mwaka 1997 lilipofuta sheria Namba 36 ya NPF ya mwaka 1964 iliyokuwa inaruhusu kutoa michango ya pensheni kabla ya wakati wake na kupitisha sheria ya Namba 28 ya NSSF ya mwaka 1997 kuwa rasmi mfuko kamili wa hifadhi ya jamii unaendesha shughuli zake za pensheni kwa utaratibu wa bima ambapo hauruhusu kutoa michango ya pensheni iliyochangiwa na mwanachama pamoja na mwajiri kabla ya kufikisha umri wa miaka 55 kwa hiyari na miaka 60 ya lazima.

Kunaweza kuleta matatizo makubwa katika kuendesha mifuko hii ya jamii kama itaendelea kuendeshwa kisiasa  badala ya kitaalamu. Na kwa kufanya hivyo itafikia wakati ambapo inaweza kusababisha kuvunjika kwa amani na kuleta hasara kubwa kwa serikali kama mdhamini mkubwa wa mifuko hii ya jamii pale itakaposhidwa kuendesha shughuli zao kama sheria na vifungo vya sheria vilivyopitishwa ndani ya sheria hizo  za NSSF, LAPF, PSPF, LAPF, NHIF, na PPF hasa kwa vizazi vijavyo na wazee wataokuwepo wakati huo hasa hawa wanaochangia kwa sasa kwa ajili ya pale wakapostaafu.

Ingawa baadhi ya wataalamu wanasema kutoa michango mapema kabla ya wakati kisheria kutasaidai kuwamotisha watu wengi kuweka akiba kwa kujiunga  na mifuko ya hifadhi ya jamii zaidi na kwamba hata wanachama hai wanaweza kuwa tayari kuchangia kiwango kikubwa zaidi kama sheria itabadilika na inaweza kusaidia kuwaamusha wengi zaidi kwa wale ambao wako nje ya uwingo huu wa hifadhi ya jamii hasa wamama, vijana pamoja na kundi la watu wengi wenye kipato cha chini kama vile  wamama na wababa na hasa kwa watanzania wote ambao hawana kabisa hifadhi hii ya muhimu ya jamii ambayo ni haki ya kila mtu kupata huduma hii kulingana na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na ya shirika la kazi la dunia yaani ILO ya mwaka 1952

Pamoja na haya yote idadi kubwa ya wananchi hasa wachangiaji wa michango hii ya pensheni wanahitaji kupata michango yao mapema kabla ya wakati wake bila ya kujitambua ya kuwa kwa kufanya hivyo wanapunguza na kujiingiza kwenye mazingira hatarishi hasa wakati atakapofikia kustaafu au kupatwa na janga lolote lile ambalo linaweza kutokea wakati anafanya kazi.

Utafiti umeonyesha kuwa ni watanzania wachache wanaweka akiba kwa ajili ya siku zijazo katika akaunti na benki. Taarifa hiyo inasema kuwa watanzania wengi hupendelea kuweka fedha nyumbani au kutumia kwa ajili ya mavazi, chakula na vinywaji. Wataalamu wanasema kuwa tabia hii ya kutoweka fedha inaashiria tatizo kubwa zaidi, ambalo ni kukukosekana kwa tabia na utamaduni wa kuweka akiba, kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Lakini kwa upande mwingine unaporuhusu kutoa michango ya pensheni mapema kabla ya muda wake kisheria kunaweza kuongezea ugumu mkubwa zaidi kwa upande wa utawala na menejimenti ya mfuko wa hifadhi ya jamii. Ugumu huu wa kazi lazima nao utaongeza gharama za uendeshaji ambapo matokeo yake unaweza kuja kupunguza ukubwa wa chungu cha mfuko wa pensheni au thamani ya mfuko wa pensheni ambacho wawekezaji wachangiaji wa akiba au wanachama baaada ya kustaafu wakipate.   Utafiti unaonyesha kuwa mfanyakazi mwenye afya kamili inayotakiwa katika muda wake wa kuajiriwa inatakiwa afanye kazi kwa muda wa usiozidi miaka 35 ili kupata kunufaika hadi mwisho na fao linalotakiwa katika maisha yake

Unapoamua ni lini unataka kuanza kupata mafao yako, kama mwanachama mchangiaji unahitajika kujua vipengele muhimu pamoja na mahitaji ya haraka ya mapato yako, upatikanaji na kiwango cha rasilimali zingine za kustaafu, na maamuzi mengine kama utaendelea kufanya kazi. Kama huna sababu ya mahitaji ya haraka ya mafao, kwa kuwa itakuwa ni maamuzi ambayo siyo ya busara kabisa kuanza kutumia mafao yako wakati bado unafanya kazi. Madhara makubwa ya kudumu ya kuwahi kustaafu mapema ni kuwepo na kupunguziwa na mafao yako ambayo ungeweza kupata mafao bora zaidi kama ungeamua kuendelea kufanya kazi mpaka unapofikisha umri wa kustaafu, na pengine ni kukatwa kwa kodi ya mapato kwenye mafao ya pensheni yako.

Kwa kufanya hivyo inasababisha kupunguza sana mafao ya pensheni halisi ambayo ulitakiwa uyapate hata kwa wafanyakazi wenye mapato wastani ya mwaka. Hata hivyo unapoteza haki yako ya kupata mafao yako ya muda muda mfupi kama vile matibabu, kulipwa na kupewa viungo bandia unapopata ajali unapokuwa kazini, mafao ya mazishi, na mafao ya uzazi kwa wamama.

Kwa msingi kamili wa fao ni uhakika kuwa mtu atakuwa na utaratibu wa fulani wa kusimamia katika miaka yote atakayokuwa kazini na kuhakikisha kuwa mwajiri wako anapeleka michango yake katika ofisi ya hifadhi ya jamii fulani pale alipo na kuhakikisha kuwa unajua hata jinsi ya kukokotoa pensheni yako na mafao mengine ya muda mfupi. Ni wewe mwenyewe unatakiwa kujua ya kuwa katika hifadhi ya jamii je kuna kustaafu mapema na ukistaafu mapema yaani kabla ya kufikisha mwaka wa kustaafu unaweza kupata pensheni pungufu na kiasi gani na baada ya miaka mingapi. Vile vile lazima ujue kama hayo mafao yako yanakatwa kodi ya makato au hayakatwi. Na kama yanakatwa kodi ya mapato ni kiasi gani yatakuwa yamepunguza mafao ya pensheni yako.

No comments:

Post a Comment