Na Christian Gaya: Majira 15 Januari 2013
Mafao ya hifadhi ya jamii ni ya
muhimu sana kwa
mtu yeyote anayetegemea kustaafu kazi kutokana na kazi ya kuajiliwa au kujiajili
mwenyewe. Ni mtu mwenyewe anaweza kusimamia sababu zinazoweza kujenga au
kuharibu utaratibu wa mafao ya hifadhi ya jamii
Kwa msingi kamili wa fao ni
uhakika kuwa mtu atakuwa na utaratibu wa fulani wa kusimamia katika miaka yote
atakayokuwa kazini na kuhakikisha kuwa mwajiri wake anapeleka michango yake
katika ofisi ya hifadhi ya jamii fulani pale alipo na kuhakikisha kuwa anajua
hata jinsi ya kukokotoa pensheni yake na mafao mengine ya muda mfupi. Ni mtu
mwenyewe anatakiwa kujua ya kuwa katika hifadhi ya jamii je kuna kustaafu
mapema na ukistaafu mapema yaani kabla ya kufikisha mwaka wa kustaafu unaweza
kupata pensheni pungufu na kiasi gani na baada ya miaka mingapi. Vile vile
lazima ujue kama hayo mafao yako yanakatwa
kodi ya makato au hayakatwi. Na kama yanakatwa
kodi ya mapato ni kiasi gani yatakuwa yamepunguza mafao ya pensheni yako.
Utafiti unaonyesha kuwa
mfanyakazi mwenye afya kamili inayotakiwa katika muda wake wa kuajiriwa
inatakiwa afanye kazi kwa muda wa usiozidi miaka 35 ili kupata kunufaika hadi
mwisho na fao linalotakiwa katika maisha yake
Unapoamua ni lini unataka
kuanza kupata mafao yako, kama mwanachama mchangiaji unahitajika kujua
vipengele muhimu pamoja na mahitaji ya haraka ya mapato yako, upatikanaji na
kiwango cha rasilimali zingine za kustaafu, na maamuzi mengine kama utaendelea kufanya kazi
Kama huna
sababu ya mahitaji ya haraka ya mafao, kwa kuwa itakuwa ni maamuzi ambayo siyo
ya busara kabisa kuanza kutumia mafao yako wakati bado unafanya kazi. Madhara
makubwa ya kudumu ya kuwahi kustaafu mapema ni kuwepo na kupunguziwa na mafao
yako ambayo ungeweza kupata mafao bora zaidi kama
ungeamua kuendelea kufanya kazi mpaka unapofikisha umri wa kustaafu, na pengine
ni kukatwa kwa kodi ya mapato kwenye mafao ya pensheni yako.
Kwa kufanya hivyo inasababisha
kupunguza sana
mafao ya pensheni halisi ambayo ulitakiwa uyapate hata kwa wafanyakazi wenye
mapato wastani ya mwaka. Hata hivyo unapoteza haki yako ya kupata mafao yako ya
muda muda mfupi kama vile matibabu, kulipwa na
kupewa viungo bandia unapopata ajali unapokuwa kazini, mafao ya mazishi, na
mafao ya uzazi kwa wamama. Mchanganuo wa wastani wa matarajio ya muda wa kuishi
unasema kuwa mtu mwenye miaka chini ya wastani wa matarajio ya kuishi au wenye
kiwango cha juu cha mapunguzo ya mafao ya pensheni ni bora akaanza mapema
kuchukuwa mafao yake. Na mtu mwenye matarajio ya kuishi maisha mengi zaidi ya
wastani ya miaka ya kuishi anatakiwa kuahirisha mafao yake
Mpango wa kustaafu ni
uthibitisho ambao unatatanisha, uliyojaa vitu vyenye mashaka na visivyotabirika na kuaminika juu
ya kiasi gani cha fedha kitachohitajika wakati wa kustaafu na mambo mengine
kama vile jinsi ya kujua kiwango cha kuchangia kwenye mfuko wa akiba wa hifadhi
ya jamii au kwenye mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii , na kiasi gani cha rasilimali ya kustaafu
kinatakiwa kuwekezwa, na kiasi gani cha michango au mafao kinachotakiwa kutoa
kutoka katika rasilimali ya kustaafu au kutoa kabla ya kufikisha miaka ya
kustaafu kulingana na mujibu wa sheria.
Matokeo ya kufanya maamuzi
mabaya inapunguza rasilimali za kustaafu na kusababisha kiwango cha kuishi au
kuhitajika kuchelewesha muda wa kustaafu ili kukusanya rasilimali ya ziada.
Kimsingi ni muhimu kutoa maamuzi yenye busara ili kupata njia nzuri ya kujua
mchanganyiko huu wa hifadhi ya jamii, pensheni za mwajiri, mpangagilio wa
rasilimali za mtu binafsi, hatifungani, hesabu ya soko la fedha, na jinsi ya
kumiliki nyumba vinaingiliana na jinsi ya kuamua juu ya rasilimali iliyopo na
matumizi ya pensheni za kustaafu.
Baadhi ya maswali ya msingi
ambayo wafanyakazi vijana wanaweza kuwa nayo hasa pale wanapokaribia kustaafu
ni kama vile; ni lini ninatakiwa kuanza
kupokea mafao ya hifadhi ya jamii? Ni thamani ya kiasi gani cha pensheni kwa
kila mwaka mmoja unaongezeka kuendelea kufanya kazi na kuchangia michango baada
ya kuzidisha mwaka wa lazima wa kustaafu? Ninahitaji kufanya kazi na wakati huo
huo na kupokea mafao ya hifadhi ya jamii?
Kwa kiwango cha chini uchambuzi
wowote unahitaji kufikiria nyongeza ya mafao ya muda wa kustaafu ukilinganisha
na kodi ya mapato na kusahau ongezeko la kiasi cha pensheni kinachoongezeka
baada ya mwaka wa lazima wa kustaafu. Kumbuka ya kuwa kila mwaka mmoja unaozidi
mwaka wa kustaafu wa lazima yaani miaka 60 huenda unaweza kuvutia kukuongezea
pensheni ya asilimia 1.5 ya wastani ya mapato yako ya kila mwezi. Na unapoamua
kutoa michango mapema kabla ya kufikia muda wa lazima wa kustaafu yaani miaka
55 unaweza kupunguza asilimia 1 ya wastani ya mapato yako ya pensheni ya kila
mwezi. Kuna haja ya kuchambua sababu zinazoadhiri mafao yako na maamuzi kamili
ya kuanza lini kutumia mafao ya hifadhi ya jamii hasa kwa kupata ushauri wa
uhakika kutoka kwa wataalamu wa fani hii ya hifadhi ya jamii kabla hajaamua.
No comments:
Post a Comment