Na Christian Gaya: Majira 01 January 2012
Mfumo
wa pensheni wa hifadhi ya jamii mpaka sasa una wanachama ambao wako chini ya
milioni 45 ya watanzania wote. Ambapo idadi ya nguvu kazi ya watanzania wote
inakisiwa kuwa ni milioni 20.94 kati ya hawa ni asilimia 6.5 ya nguvu kazi
ndiyo wako chini ya mpango wa hifadhi ya jamii nchini. Na kila mfuko wa
pensheni wa hifadhi ya jamii uko chini ya wizara tofauti mfano Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lipo chini ya wizara ya kazi na maendeleo ya vijana,
shirika la pensheni kwa ajili ya mashirika ya umma (PPF), Mfuko wa Pensheni wa
hifadhi ya jamii kwa ajili ya Watumishi wa Umma (PSPF) na Mfuko wa Akiba ya
Wafanyakazi wa Serikali (GEPF) yote mitatu ipo chini ya Wizara ya Fedha na
Mipango.
Wakati
Mfuko wa Bima wa Taifa yaani (NHIF) upo chini ya Wizara ya Afya na wakati huo
huo mfuko wa pensheni ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya wafanyakazi wa
serikali za mitaa yaani (LAPF) wenyewe upo chini ya
wizara ya Serikali za Mitaa. Na kabla ya ya mwaka 2008 hayakuwa na chombo
chochote cha kusimamia na wala kudhibiti
mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii kama yanavyosimamiwa na SSRA yaani
msimamizi na mdhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Mashaka
na wasiwasi ulikuwa mwingi sana juu ya uendelefu wa mashirika haya ya hifadhi
ya jamii hasa juu ya mgawanyo wa masoko kulingana na sheria tofauti
zilizotungwa.
Hapakuwa
na usawa wa mgawanyo wa soko huru wa wateja kama inavyoonyesha hapo juu mfano
kila mfuko ulipangiwa sekta yake ya kuwahudumia
kisheria na hii ilifanya baadhi ya mifuko kuwa na wateja wachache na
hivyo kupungua kwa mapato yatokanayo na michango ya wafanyakazi wachagiaji ya
kuendeshea mifuko na kuweza kulipa mafao ya muda mfupi na ya muda mrefu.
Na
kila mfuko wa hifadhi ya jamii unatoa mafao yake tofauti, na hata kama
yanafanana kila moja ina taratibu na kanuni zake. Hivyo hayafuati utaratibu wa
mafao kama yalivyoainishwa na shirika la kazi la dunia (ILO) chini ya kifungu
cha 102 cha mwaka 1952. Ambapo imeanisha mafao yafuatayo: pensheni ya uzee,
pensheni ya ulemavu, pensheni ya urithi, haya ni yakiwa kama mafao ya muda
mrefu na mafao ya muda mfupi ni kama vile uzazi, bima ya afya, msaada wa
mazishi, kuumia kazini na magonjwa yatokanayo na kazi, mafao ya uzazi, mafao ya
wasiokuwa na kazi, na msaada wa kujikimu kwa wale wenye watoto chini ya umri wa
miaka 18 kisheria.
Malipo
ya mafao kwa wanachama hayaendi na mfumuko wa bei. Inakuwa nafuu kupata
shilingi ya leo kuliko shilingi ya kesho. Kwa sababu kama ulitakiwa kupata
mifuko ishirini ya saruji unapata mifuko kumi tu kwa sababu thamani ya fedha
ambayo ndiyo mafao yako yanakuwa yameliwa na mfumuko wa bei wa wakati huo.
Hata
riba inayotolewa na mifuko hii ni ndogo sana ukilinganisha na michango
mwanachama anayochangia. Wakati huo huo michango ya mwanachama huo ndiyo
inayowekezwa kwenye vitega uchumi mbalimbali kama vile kwenye hisa, vipande, na
hatifungani. Na baadhi ya idadi kubwa ya michango huwekezwa kwenye miradi ya
nyumba na makazi mbalimbali na faida inayopatikana ndiyo mwanachama hugawiwa
kwenye akaunti ya kila mwanachama.
Na
changamoto nyingine ni pale mifuko wanapokosa sehemu endelefu za uwekezaji hasa
kwenye sehemu za muda mfupi na za muda mrefu kama vile kwenye majengo, hisa,
vipande, na hatifungani
Kumekuweko na ongezeko kidogo sana la kuelewa juu ya
mfumo wa hifadhi ya jamii hasa juu ya mafao yanayotolewa, jinsi ya kujiunga
kuwa wanachama, vitega uchumi na shughuli mbalimbali za sekta.
Taasisi za hifadhi ya
jamii ya jamii nchini Tanzania zimekuwa zikiwekeza orodha ya fedha kwa faida
kwenye mikopo, nyumba za kupangisha, hatifunganishi, kuweka akiba benki zote
hizi zimechangia maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii.
Kumekuweko na ongezeko kidogo sana la kuelewa juu ya
mfumo wa hifadhi ya jamii hasa juu ya mafao yanayotolewa, haki na wajibu wa
mwanachama jinsi ya kujiunga kuwa wanachama, vitega uchumi na shughuli
mbalimbali za sekta hii ya hifadhi jamii.
Sekta ya hifadhi ya jamii isiyo kuwa rasmi hasa kwa
makundi ya kusaidiana yamekuwa yakijipanga vizuri zaidi kwa sasa ukilinganisha
na hapo siku za nyuma.
Mapungufu yaliyomo kwenye
mfumo huu wa hifadhi ya jamii ambayo yanahitajika kutatuliwa na sera hii ya
hifadhi ya jamii yakisimamiwa na mdhitibi na msimamizi wa hifadhi ya jamii
(SSRA). Idadi kubwa ya watu waliomo katika mifuko hii ya
hifadhi ya jamii ni wale tu ambao wameajiriwa kwenye sekta iliyo rasmi, ambapo
takwimu zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya watu kutoka katika sekta isiyokuwa kuwa
rasmi inazidi kupungua kila siku kuwa wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii
badala ya kuongezeka.
Na hata wafanyakazi kutoka katika sekta isiyo rasmi
wakiandikishwa kuwa wanachama wa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii inakuwa
ni vigumu sana hasa jinsi ya kuwapata, kuwaandikisha, kukusanya michango, jinsi
ya kuwahamasisha na kuwaelemisha juu ya mafao yatolewayo na faida zake pamoja
na haki na wajibu wa mwanachama. Na idadi kubwa ya watu ambao wako sekta rasmi
hawana utamaduni wa kuweka akiba.
Hata hivyo inaonyesha kuwa
idadi kubwa ya mafao yanayotolewa na mifuko hii ya hifadhi ya jamii nchini
Tanzania yako chini ya kiwango cha shirika la kazi la dunia (ILO) yaani kwa
idadi ya mafao, ubora wa
mafao, na kutokwenda na ukali wa maisha ya kila siku.
Hivyo mpaka sasa haya
mashirika ya hifadhi ya jamii kila moja ina wizara yake inayoisimamia na kuwa
utaratibu na kanuni tofauti za uendeshaji wa mifuko hii. Matokeo yake ni kwamba
kiwango cha michango, mfumo wa mafao, na sifa za kupata mafao na hata mipango
na vipa umbele vinatofautiana kabisa kwa kila mfuko.
Mpaka sasa hakuna utaratibu ulioanzishwa wa kuruhusu
haki za mafao ya mwanachama kuhamishwa kutoka mfuko mmoja hadi mwingine.
Matokeo yake wafanyakazi wamekuwa wakipoteza baadhi ya haki zao za mafao wakati
wakihama kutoka sehemu moja ya mwajiri hadi mwajiri mwingine. Pia hii
imechangia sana kuongezeka kwa tabia ya kuondoa michango ya pensheni kabla
haijakomaa kiwango cha kuwa tayari kama mafao ya kustaafu.
Huduma za wanachama zimekuwa haziridhishi kwa
wateja. Mwanachama anaonekana kama siyo mfalme wa mifuko hii ya hifadhi ya
jamii. Imekuwa ikichukua muda mrefu mwanachama kupata mafao yake. Mara nyingi
malalamiko ya wanachama yamekuwa hayasikilizwi ipasavyo. Mafao yamekuwa
yakilipwa pungufu. Na ushirikishwaji wa wanachama kama wabia wao kwenye
mikakati, mipango na miradi umekuwa ukisua sua sana.
No comments:
Post a Comment