Pages

Tuesday, January 29, 2013

HOTUBA YA KUFUNGA SEMINA YA MAFUNZO NA UKUSANYAJI MAONI YA WAFANYAKAZI WA SEKTA YA MADINI JIJINI MWANZA ILIYOTOLEWA NA MKUU WA MKOA WA MWANZA NDUGU EVARIST NDIKILO TAREHE 11/01/2013


Mhe. Gaudentia Kabaka (MB); Waziri wa Kazi na ajira
Mhe. Dkt. Makongoro Mahanga (MB), Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,
Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Ndugu Irene Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA
Dkt. Akwilina Mayunga , Mkurugenzi mtendaji wa OSHA
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa CMA
Dkt. Aggrey Mlimuka, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE
Ndugu Hezron Kaaya – Naibu Katibu Mkuu, TUCTA
Wawakilishi wa Waajiri- Migodini
Wawakilishi wa TAMICO
Ndugu wawakilishi wa Wafanyakazi - Migodini
Wafanyakazi wa SSRA
Wanahabari
Mabibi na Mabwana
Awali ya yote nichukue fursa hii kukushukuru wewe binafsi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa kunialika kuja kuufunga semina ya mafunzo na ukusanyaji maoni ya wafanyakazi wa sekta ya

madini. Naomba pia nitumie fursa hii KUMPONGEZA Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka na Naibu waziri wa Kazi na Ajira Mh. DKt Milton Makongoro kwakutenga muda wao na kuhudhuria kikamilifu kwasiku zote mbili, kwani kulingana na nafasi yao Kiserikali lazima wameacha majukumu mengi nakukubali kujumuika nasi.Hongereni sana kwa hilo.Na nitumie wakati huu kuwakaribisha wote hapa Mwanza jiji lenye madhali safi na upepo mwanana toka Ziwa Victoria. Ni matumaini yangu mmetumia siku zote mbili mlizokuwa hapa Mwanza na hususani katika semina hii kwa mafanikio yenu binafsi, Waajiri wenu, Migodi mnayoiwakilisha na sekta ya hifadhi ya jamii kwa ujumla.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu, nimeelezwa kuwa mmejifunza mengi juu ya sekta ya hifadhi ya jamii kwa ujumla. Aidha mmepata majibu ya maswali mengi ambayo pengine mmekuwa mkijiuliza juu ya Hifadhi ya Jamii na hata Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta Ya Hifadhi ya Jamii.

Semina kama hizi hutoa fursa kwa wanachama na wadau wa sekta ya hifadhi ya Jamii,kushirikishwa katika kutoa maoni, kutoa mapandekezo na maamuzi mbalimbali ya Mfuko ya Hifadhi ya jamii. Wadau wa Mfuko ya hifadhi ya jamii huweza kuchangia kwenye uendeshaji wa Mifuko yao ya Hifadhi ya Jamii moja kwa moja kwa kutoa ushauri, na mapendekezo juu ya hatua mbalimbali za kuboresha utendaji wa Mifuko, kuboresha Mafao, kuboresha maisha ya wastaafu lakini pia kuongeza idadi ya wale wanaopata huduma na mafao yanayotolewa. Wanachama na wafanyakazi wa Migodini hamna budi kuipongeza SSRA kwa kutambua thamani yenu na kuamua kuandaa semina hii ambayo imewapatia fursa ya kusikia majukumu ya Mamlaka,Ushiriki wa Chama cha waajiri na Chama cha wafanyakazi katika mabadiliko ya sheria, Mafao yatolewayo na kila Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, majukumu ya Baraza la Usululishi wa migogoro mahali pa kazi (CMA),na majukumu ya wakala wa afya na Usalma Mahali pa kazi (OSHA ). Nimeelezwa kuwa ushiriki wa Mikutano hii
3
ni mpana na ambapo wapo wawakilishi wa Waajiri, Wawakilishi wa Wajiriwa,Vyama vya wafanyakazi migodini (TAMIKO) , Wakurugenzi wakuu na wawakilishi wa wakurugenzi wakuu wa mifuko yote ya hifadhi ya Jamii Tanzania Bara na Mfuko wa Bima ya Afya,na viongozi wa vyama vya wafanyakazi. Ushiriki wa namna hii(broad based representation) ni mzuri mno kwa kuwa wote wanaohusika na maamuzi katika taasisi wanachama na zinginezo wanapata nafasi ya kushirikipia umehusisha utatu kwani kuna uwakilishi wa Serikali,Vyama vya Waajiri na Vyama vya Wafanyakazi. Kwa maana hii majibu au ufafanuzi juu ya maswala mbali mbali juu ya utendaji wa Mfuko na sekta ya hifadhi ya jamii kwa ujumla yanapatikana hapa. Aidha hali hii inasaidia pia kurahisisha utekelezaji wa mipango mbalimbali kwa kuwa watekelezaji wamehusishwa katika hatua za kujadili na hata kupanga mikakati ya utekelezaji wenyewe. Nawapongeza sana kwa kubuni njia hii ya kukutana na wanachama/wadau wenu na pia kwa kuwaalika watoa huduma yaani mifuko ya Hifadhi ya Jamii na taasisi za Wizara ya kazi ambazo hugusa maslai ya wafanyakazi.

Aidha mada zilizojadiliwa zimelenga katika kuchangia jitihada za Serikali na Mamlaka za kutafuta njia muafaka za kulinda na kutetea maslai ya mwanahama. Ni imani yangu kuwa Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itatathmini kwa kina ushauri na mapendekezo mliyoyatoa na kuyafanyia kazi na hivyo kuleta ufanisi kwa wadau hasa wastaafu.

Niwaombe Mamlaka kwa kushirikiana na mifuko ya Hifadhi ya jamii kuendelea na hatua hii nzuri ya kutoa elimu kwa wadau wa sekta ya hifadhi ya Jamii na na kuziomba taasisi zingine kuwa wazi katika utendaji wake na kushirikisha wadau katika shughuli zao. Kwa kuboresha mahusiano tunaweza kuleta mabadiliko katika utendaji na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania.

Ndugu Mwenyekiti, sekta ya hifadhi ya jamii inategemea sehemu muhimu katika mapambano dhidi ya umaskini kwa kuwa inamuwezesha mstaafu kuendelea kupata kipato hata baada ya kutoka katika ajira.
Hata hivyo wastaafu hawezi kupata mafao kama mashirika yanayotoa ajira hayazingatii taratibu na wajibu wao wa kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati. Kutowasilisha michango huleta usumbufu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuchelewesha ulipaji wa mafao kwa wafanyakazi pale ajira inapokoma au wanapostaafu.

dugu Mkurugenzi mkuu, naomba nisiwachoshe zaidi baada ya siku mbili za mafunzo,majadiliano, mapendekezo, ufafanuzi na maswali na majibu. Mniruhusu tu kutumia japo muda huu kwa mara nyingine tena kusisitiza umuhimu wa kuzingatia yote mliyojifunza hapa ili kuboresha huduma ya Hifadhi ya jamii nchini na hasa kuwawezesha watakaostaafu kuishi maisha bora zaidi. Aidha niwahakikishie kuwa uongozi wa Mkoa utatoa ushirikiano wa karibu kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya Jamii ili iweze kufanikisha malengo yake hapa mkoani.

Baada ya kusema hayo, naomba sasa nitamke kuwa semina ya mafunzo na ukusanyaji maoni ya wafanyakazi wa sekta ya madini jijini Mwanza Imefungwa
Karibuni tena Mwanza
Nawatakia safari njema.

No comments:

Post a Comment