Pages

Thursday, December 20, 2012

Mgaya; Mifuko ya hifadhi inajinufaisha yenyewe

Na Idda Mushi: 4th November 2012
Maoni
Nicholaus Mgaya

Sera za mifuko mingi ya hifadhi ya jamii nchini, zimewekwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya mifuko hiyo na si kuwanufaisha wafanyakazi .

Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Nicholaus Mgaya kwenye warsha ya viongozi wa juu wa chombo hicho inayofanyika mjini Morogoro.

Alisema sera ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) inasema kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kukidhi mahitaji ya wafanyakazi ni lazima kuwa na mafao yasiyopungua tisa, lakini kwa Tanzania mifuko mingi ina mafao matatu pekee.

Alisema isipokuwa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ndilo pekee lenye mafao saba.

Alisema mifuko inakinzana na mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA ).
Mgaya alilizungumzia fao la kujitoa kuwa ni suluhisho pekee la kumkomboa mfanyakazi kutoka katika umaskini pale anapoachishwa au kufukuzwa kazi .

Katika hatua nyingine, Mwenyekiyi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Dk Diwani Mrutu aliwataka watendaji wakuu wa vyama vya wafanyakazi nchini kuhakikisha wanakusanya michango na ada za vyama vyao ili kusaidia shirikisho hilo kujiendesha lenyewe,

Alisema shirikisho hilo linatakiwa kujiendesha kwa kutegemea michango na ada za wanachama wao.
Aidha aliwaonya viongozi wa wafanyakazi ambao wamegeuka wasaliti wa shirikicho hilo kuacha kufanya hivyo kwani ikibidi watatajwa hadharani na na kupigiwa kura za kuwaondoa madarakani.

No comments:

Post a Comment