Ujenzi daraja la Kigamboni wanukia
21st November 2011
B-pepe
Chapa
Maoni
Wakandarasi
saba ambao wamefanikiwa kupita katika mchakato wa awali wa kumpata
mkandarasi atakayeshinda zabuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni tayari
wamefanya ukaguzi katika eneo hilo.
Akizungumza
na NIPASHE jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Msemaji wa Wizara ya
Ujenzi, Martini Ntemo, alisema wakandarasi hao wametembelea eneo hilo
mapema wiki hii kwa ajili ya kufanya tathmini ya ujenzi.
Alisema
kabla ya mchakato huo wa kuwapata wazabuni walijitokeza wakandarasi 16
walichambuliwa na ndipo walipopatikana hao saba ambao wanashindanishwa.
Ntemo
alisema lengo la ziara hiyo ni kuwapatia maelezo ya kitaalam
wakandarasi hao kuhusu maudhui ya mradi husika na changamoto zake kabla
ya kuwasilisha makisio yao kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.
Alisema
ujenzi wa daraja hilo unatarajia kuanza mwanzoni mwa mwaka 2012 na
kwamba tayari zimeshatengwa bilioni 130 kwa ajili ya zoezi hilo.
Hata
hivyo, alisema daraja hilo ambalo ni la kisasa zaidi kujengwa hapa
nchini ambapo litakuwa na barabara tatu kila upande yaani kuwa na uwezo
wa kuruhusu magari sita kupita kwa wakati mmoja.
“Daraja
hilo linatarajiwa kuwa na urefu wa mita 600 na litakapokamilika
litakuwa ni kiungo muhimu kati ya Jiji la Dar es Salaam na Kigamboni na
pia litachangia kupunguza msongamano wa magari hapa jijini," alisema
Ntemo
Alisema
Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF tayari limeshatoa Sh bilioni 100
kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa daraja hilo kwa kushirikiana na Wizara
hiyo ambapo watachangia asilimia 40.
Aidha,
alisema mchango huo wa NSSF ni moja ya maagizo ambayo aliyatoa Waziri
wa Ujenzi, Dk John Magufuli Mwezi Machi mwaka huu ambapo aliwataka
kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni mapema iwezekanavyo ili kuhakikisha
kuwa usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Kigamboni unaimarishwa na hivyo
kuondoa kero ya usafiri.
Ntemo alisema NSSF itachangia asilimia 60 na Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itachangia asilimia 40 zilizobakia.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment