Balozi Seif aitaka NSSF kuongeza wanachama
3rd February 2012
B-pepe
Chapa
Maoni
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd
Changamoto
hiyo ilitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali
Idd, katika sherehe za ufunguzi wa kongamano la pili la wadau wa mfuko
huo wa kimataifa.
Balozi
Idd alisema NSSF na mifuko mingine imeelekeza nguvu zake kwa kupata
wanachama kutoka sekta rasmi tu na ndio maana wanachama waliopo hawafiki
milioni moja.
Alisema
hiyo ni kasoro kubwa inayohitajika kurekebishwa mara moja na kuna haja
kwa uongozi wake kuchukua juhudi za makusudi kuongeza wanachama kutoka
sekta kama kilimo ambayo Watanzania wengi zaidi wanajishughulisha nayo
kuliko sekta nyingine.
Alisema
zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanajishughulisha na kilimo na kundi
hilo ni muhimu sana kwa mfuko huo kama sekta hiyo itaandaliwa utaratibu
mzuri.
Alisema
mafanikio yaliyofikiwa na NSSF ni makubwa katika uwekezaji wa vitega
uchumi vya ndani ya nchi, kwa misingi hiyo mafanikio hayo yanapaswa
kwenda sambamba na kuyafanya mafao ya wanachama wake kuwa bora zaidi na
makubwa zaidi.
Pia
alitoa changamoto kwa mifuko yote ya hifadhi za jamii nchini kujitahidi
kuyafanya mafao na malipo mengine kwa wanachama wao kuwa mazuri zaidi.
Balozi
Idd aliisifu NSSF kuwa na mradi wa nyumba za bei nafuu jijini Dar es
Salaam na kusema kuwa mradi huo unapaswa kuendelezwa nchini kote kwani
gharama za ujenzi za nyumba kwa wanachama wa kawaida au hata mtu wa
kawaida ni kubwa mno.
Alisema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pia inao mpango wa aina hiyo kutokana
na hali hiyo inaialika NSSF kwenda Zanzibar kushirikiana na ZSSF
kuwekeza katika mpango huo.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau, alisema mafaniko mengi
ya mfuko huo nchini ni kwa kubuni miradi mingi ya maendeleo na kuongeza
kiwango cha pensheni ambacho kimepanda kutoka Sh. 52,000 hadi Sh.
80,000.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment