Meneja
Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi (kulia)
akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya kuhusu Akaunti
ya Hodari ambayo ni akaunti maalumu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na
wa kati wakiwemo Machinga, Bodaboda, Mama lishe, Wafanyabiashara kwenye
masoko, Mafundi vyerehani, Seremala, Wachimbaji Wadogo wa Madini na
makundi mengine. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja
Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi (kulia)
akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili
kushoto) kuhusu Akaunti ya Hodari ambayo ni akaunti maalumu kwa ajili ya
wajasiriamali wadogo na wa kati wakiwemo Machinga, Bodaboda, Mama
lishe, Wafanyabiashara kwenye masoko, Mafundi vyerehani, Seremala,
Wachimbaji Wadogo wa Madini na makundi mengine.
Meneja
Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi (kulia)
akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa pili
kushoto) kuhusu huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB alipotembelea banda
la CRDB Bank kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya
Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack
kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki
ya CRDB imeshiriki Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa
Shinyanga ambapo imetumia fursa hiyo kuwaomba Wananchi kuchangamkia
fursa ya Akaunti ya Hodari ambayo ni akaunti maalumu kwa ajili ya
wajasiriamali wadogo na wa kati wakiwemo Machinga, Bodaboda, Mama lishe,
Wafanyabiashara kwenye masoko, Mafundi vyerehani, Seremala, Wachimbaji
Wadogo wa Madini na makundi mengine.
Akielezea
kuhusu Akaunti ya Hodari kwa Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani
Manya akitembelea banda la CRDB Bank, Meneja Biashara wa Benki ya CRDB
tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi amezitaja sifa za Akaunti ya Hodari
kuwa ni pamoja na kutokuwa na ada ya mwezi kuendesha akaunti.
"Sifa
kuu za Akaunti ya Hodari ni kwamba kiasi cha kufungulia akaunti ni
shilingi 5,000/=, haina gharama za kuendesha akaunti, haina ada ya
mwezi,haina ada ya kutolea pesa tawini,haina makato ya miamala ya
Simbanking, haina makato ya Internet Banking, haina malipo
yanayopokelewa kupitia LIPA HAPA na haina makato ya kutoa pesa
ATM",ameeleza Mwanahamisi.
Mwanahamisi
ameeleza kuwa Benki ya CRDB inawawezesha Mikopo Wachimbaji Wadogo wa
Madini na Wajasiriamali kwani furaha ya Benki ya CRDB ni kuona
Wachimbaji Wadogo wa Madini na Wajasiriamali wanakua kiuchumi.
Maonesho
ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
yamefunguliwa na Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya kwa niaba
ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa
Jumapili Julai 25,2021.
Prof.
Manya ameipongeza na kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea
kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali na kwa upande wa
Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga wamekuwa
miongoni mwa wadhamini wa maonesho hayo.
Maonesho
ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga
yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga
kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa
tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa
kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
No comments :
Post a Comment