Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tabora (RPC) Barnabas Mwakalukwa akitoa salama Jeshi hilo jana
wakati wa uzinduzi wa nyumba mpya za makazi mapya ya Askari mjini
Tabora.
Katibu Tawala
Msaidizi Mkoa wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis Linuma akitoa
salamu za Mkoa jana wakati wa sherehe fupi ya uzinduzi wa nyumba mpya
Askari mjini Tabora.
Baadhi ya Maaskati na Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa nyumba mpya za makazi ya askari jana mjini Tabora
Picha na Tiganya Vincent
………………..
NA TIGANYA VINCENT
MAJENGO matatu ya makazi mapya ya
Polisi yamegharimu jumla ya shilingi milioni 254 kukamilika zikiwemo
zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John
Pombe Magufuli na wadau Mkoani Tabora.
Akisoma risala wakati wa uzinduzi
wa majengo hayo Marakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Msabila Kulwa
Bundala alisema kila jengo lina nyumba mbili za makazi ambalo kila moja
limegharimu shilingi milioni 84.6.
Alisema katika kiasi cha fedha cha
shilingi bilioni 10 , Mkoa wa Tabora ulipata shilingi milioni 150
ambapo wadau wa Jeshi hilo walichangia zaidi ya milioni 100.
Bundala alisema michango ya wadau ilijumuisha fedha tasimu , saruji , vifaa vya umeme na maji.
Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa
wa Tabora (Serikali za Mitaa) Nathalis Linuma alitoa wito kwa wakazi wa
Mkoa wa Tabora kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuboresha makazi
ili wawe na mazingira mazuri ya kuishi na kutoa huduma nzuri kwa jamii.
Alisema maendeleo hayana mwisho ni
vema utaratibu wa jamii kushirikiana na Polisi kuboresha mazingira ya
kuishi na kufanyia kazi yakaendelea ili kuwawezesha kuishi sehemu moja
ambayo itakuwa rahisi kuisaidia jamii pindi wanapohitajika.
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tabora Barnabas Mwakalukwa alitoa wito kwa wadau mbalimbali
Mkoani Tabora kusaidia kukamilisha majengo ya Ofisi likiwemo la Asakari
wa Usalama barabarani ambayo yalianza kujengwa mwaka 2015 ambayo
yamesimama.
Alisema uwepo wa Ofisi ya za
kutosha utaongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa kuwa na mazingira mazuri
ya kutoa huduma kwa wananchi mbalimbali.
No comments :
Post a Comment