Tuesday, May 21, 2019

Rais Magufuli Atoa Maagizo Mazito kwa Mashirika Yasiyotoa Gawio kwa Serikali

Rais Magufuli ameyataka mashirika na Taasisi zinazotakiwa kutoa gawio kulingana na sheria kuhakikisha hadi kufikia mwei Julai mwaka huu wawe wameshakamilisha zoezi hilo.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 21 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza katika hafla ya kukabidhi gawio kwa serikali kutoka shirika la masiliano Tanzania TTCL ambapo ameagiza mashirika hayo kuchukuliwa sheria iwapo watashindwa kutekeleza agizo hilo.

“Mashirika ambayo hayatoi gawio kila siku ni hasara tu itabidi kutumia sheria na ikishindikana yaondoke maana haiwezekani wao wanaangalia wenzao wakati walipewa mashirika hayo sawa na bure hivyo kabla ya mwezi Julai mashirika yote 253 yanatakiwa yawe yameshafanya hivyo ” amesema.

“Fedha hizi ni ndizo zinazosaidia katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile ujenzi wa barabara, hospitali shule hivyo kwa wale wote wanaotakiwa kutoa gawio kulingana na sheria wanapaswa kufanya hivyo,” amesema.

Aidha ametoa wito kwa watanzania kuendela kuliunga mkono shirika la TTCL kwa kusema kuwa ni la nyumbani lakini pia mapato na faida zitakazopatikana zitatumika kuwasaidia watanzania na kwamba ndio nembo pekee ya kumkumbuka baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.

No comments :

Post a Comment