Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya askari Polisi
Mfikiwa Pemba
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na askari polisi wa kike waliokuwa wakijiandaa kwa ajili ya
gwaride la maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi Takatifu ya
Zanzibar mara baada ya kuwaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za
makaazi ya askari Polisi Mfikiwa Pemba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed
Hassan Haji wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi
ya askari Polisi Mfikiwa Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
…………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ametembelea na
kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makaazi ya Askari Polisi
Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Makamu wa Rais ambaye yupo Pemba
kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 55 ya
Mapinduzi ambapo jana
tarehe 10 Januari 2019 aliweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Makaazi ya
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar eneo la Pagali Chake Chake Pemba.
Akizungumza mara baada ya kukagua
maendeleo ya ujenzi huo Makamu wa Rais aliwataka Viongozi wa Vikosi
kuongeza nguvu na kuhakikisha usimamizi wa shughuli za ujenzi wa makaazi
ya askari unakamilika kama ulivyopangwa.
“Mwaka jana tarehe 20 Machi 2018
niliweka jiwe la msingi wa ujenzi wa nyumba za makaazi wa askari wetu
hivyo basi lazima lengo litimie kama tulivyozungumza siku ya uwekaji
jiwe la msingi” alisema Makamu wa Rais.
Kwa upande mwingine Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP)
Mohamed Hassani Haji amesema kuwa mipango ya kumalizia ujenzi wa
makaazi bora ya askari polisi bado inaendelea na kuahidi kuikamilisha
kwani ni dhamira ya jeshi la polisi kuhakikisha askari wake wanaishi
sehemu salama.
Pamoja na mambo mengine Makamu wa
Rais aliwasalimia Askari wa Kike waliokuwa kwenye maandalizi ya gwaride
maalum la siku ya maadhimisho ya kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi
Takatifu ya Zanzibar yatakayofanyika kesho kwenye uwanja wa Gombani,
Chake Chake Pemba.
“Mtapanda vyeo kwa jitihada ya kazi si vinginevyo hivyo Askari unatakiwa ufanye kazi kwa bidii sana” aliwahusia Makamu wa Rais.
No comments :
Post a Comment