Naibu
Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akizunguza na mwakilishi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Ndugu Fred Kafeero na
msaidizi wa mwakilishi huyo Ndugu Charles Tulahi katika ofisi za shirika
hilo jijini Dar es Salaam
Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimueleza muwakilishi wa FAO nchini mipango ya Serikali ya awamu ya tano katika kuinua kilimo
Ndugu Fred Kafeero akimkabidhi Naibu Waziri wa Kilimo baadhi ya machapisho yanayoonyesha mikakati ya FAO
Naibu
Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa akiagana na msaidizi wa muwakilishi
FAO nchini Ndugu Charles Tulahi mara baada ya kumalizika kwa kikao
Innocent Bashungwa akimsikiliza kwa makini muwakilishi wa Shirika la FAO wakati akimuelezea shughuli za shirika hilo
……………………………..
Shirika
la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limeahidi kuendeleza
ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kuiinua sekta ya kilimo
nchini. Hayo yamesemwa na Ndugu muwakilishi wa Shirika hilo nchini Ndugu
Fred Kafeero alipokutana na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa
katika ofisi za FAO jijini Dar es Salaam.
Katika
kikao hicho Ndugu Kafeero alieleza namna ambavyo shirika hilo limekuwa
mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika kutunga sera na kuandaa
mikakati yenye lengo la
kuhakikisha Tanzania inasonga mbele katika
kilimo. Amesema FAO kwa miaka ya karibuni imefanya kazi kwa ukaribu na
Shirika la Takwimu Tanzania (NBS) kwa kulijengea uwezo wa ndani
unaoisaidia pia serikali katika ufuatiliaji wa bei ya mazao nchini.
Nae
Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashungwa alimueleza muwakilishi huyo
mpango wa Serikali ya awamu ya tano wa kuorodhesha wakulima wote nchini
ili kuweza kupanga vizuri kuhakikisha kila mkulima anapata huduma muhimu
zitakazomsaidia toka hatua za uandaaji shamba mpaka masoko, na kuiomba
FAO kama mdau muhimu wa kilimo kuipa Serikali ushirikiano ambapo Ndugu
Kafeero aliahidi kulifanyia kazi ombi hilo.
Aidha, Naibu Waziri Bashungwa ameomba IFAD (shirika tanzu la FAO) isaidie Serikali kwa kushirikiana na Benki
ya Kilimo nchini kuwapatia wakulima nchini kupata mikopo ya riba nafuu,
kusaidia taasisi za utafiti wa kilimo nchini, kujenga uwezo wa
kuzalisha mbegu za mazao ya kimkakati na mchanganyiko, kujenga maghala
ya kuhifadhi mazao ili kupunguza hasara wakati wa mavuno shambani (post
harvest losses) na kuwajengea uwezo maafisa ugani nchini kufundisha
kilimo cha tija kwa wakulima nchini.
Mwakilishi
wa FAO nchini amekubaliana na Naibu Waziri Bashungwa kufanyika kikao
mwezi Februari 2019 cha Wizara ya Kilimo, FAO na mashirika mengine ya
kimataifa yanayohusika na kilimo nchini kujadili vipaumbele tajwa ili
kuijengea uwezo Wizara wa kuweza kuihudumia sekta ya kilimo nchini ili
iendelee kukua na kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kufikia
uchumi wa kati.
No comments :
Post a Comment